Analog Clock

TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, January 31, 2012

TWIGA STARS , NAMIBIA ZAINGIZA MIL 38/-


Mechi ya marudiano ya raundi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Nane za Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Namibia (Brave Gladiators) imeingiza sh. 38,220,000.
Kiasi hicho ni kutokana na watazamaji 16,334 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa juzi (Januari 29 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Twiga Stars kuibuka na ushindi wa mabao 5-2.
Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 1,000 (watoto), sh. 2,000 (viti vya kijani na bluu), sh. 3,000 (viti vya rangi ya chungwa), sh. 5,000 (VIP C na B) na sh. 10,000 kwa VIP A.
Watoto waliokata tiketi kuingia uwanja ni 634, viti vya rangi ya kijani na bluu 13,238, viti vya rangi ya chungwa 1,040, VIP B na C 1,246 na VIP A watazamaji 176.
Vilevile Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawashukuru washabiki na wadau wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine kufanikisha mechi hiyo kati ya Twiga Stars na Namibia.

KATIBU WA ORGANAIZESHENI WA CCM TAIFA BI ASHA ABDALLA JUMA BAADA YA KUFANYIWA MATIBABU

KATIBU WA ORGANAIZESHENI WA CCM TAIFA BI ASHA ABDALLA JUMA BAADA YA KUFANYIWA MATIBABU YA MGUU WAKE HUKO CHENNAI INDIA ,KAAMA ANAVYOONEKANA PICHANI AKIWA NA WAUGUZI WALIOKUWA WAKIMPATIA HUDUMA KATIKA HOSPITALI YA MIOT INDIA.
KATIBU WA ORGANAIZESHENI WA CCM TAIFA BI ASHA ABDALLA JUMA AKIWA NA PROF MOHANDAS MKUU WA HOSPITALI HIYO YA MIOT NCHINI INDIA.

BASATA KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI SASA KUDHIBITI UHARAMIA KWENYE SANAA


Na Mwandishi Wetu
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na Jeshi la Polisi nchini wameunda kikosikazi maalum kitakachokuwa kikifuatilia uharamia na maovu mbalimbali katika shughuli za Sanaa na Burudani. 
Kikosikazi hicho kimeundwa baada ya Jeshi la Polisi nchini kutumia Sanaa shirikishi katika kutoa elimu kwa wadau wa Sanaa kuhusu dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila wiki makao makuu ya BASATA Ilala Sharif Shamba.
Akizungumza kuhusu kikosikazi hicho, Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa, BASATA Bi. Vivian Shalua alisema kuwa, kazi kubwa ya kikosi hiki itakuwa ni kufuatilia maonesho yasiyokuwa na vibali, uharamia kwenye kazi za wasanii na wasanii kutoka nje wanaoingia nchini kinyume cha sheria.
Aliyataja majukumu mengine ya kikosikazi hicho kuwa ni pamoja na kudhibiti maonesho yanayodhalilisha utu na maadili ya mtanzania, kusimamia utoaji vibali kwa wasanii wa kitanzania wanaoenda kufanya maonesho nje ya nchi na majukumu mengine yatakayojitokeza.
“Kikosikazi hiki kitakuwa tayari kufuatilia taarifa yoyote ya uharamia kwenye kazi za wasanii, maonesho yanayodhalilisha utu na maadili ya mtanzania na wasanii wanaoingia ndani ya nchi na kufanya maonesho bila vibali” alisisitiza Shalua. 
Kikosikazi hicho kinaundwa na Shani Kitogo (Afisa Utamaduni Ilala), Tatia Ramadhan (Polisi, TAZARA), Afande Jeremiah (Polisi Kati), Koplo Juma Mashauri (Polisi Airport), Michael Kagondela (Idara ya Utamaduni), Afande Deus Matoro (Reli) na Afande Swai (Traffic),
Wengine ni Vivian Shalua (BASATA), Jonathan Abel na Tatu Burhan (Uhamiaji), Deus Kessy (Polisi Reli), Koplo Josephat Syllively (Polisi – Maji), Masanja Nyalali (Polisi – Airport) na PC Mwakajaby (Polisi – TAZARA)
Akizungumza kwenye Jukwaa hilo la Sanaa, Asp Edson Kasekwa kutoka Polisi Makao Makuu Kitengo maalum cha Operesheni uzuiaji uhalifu,alisema kuwa, Jeshi la Polisi linawategemea wadau wa Sanaa wakiwemo wasanii katika kutoa taarifa juu ya matukio ya uharamia na uhalifu kwa ajili ya ufuatiliaji na udhibiti.
“Ni vema Wasanii na wadau wa Sanaa kwa ujumla wakaonesha ushirikiano kwa Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa na kudhibiti uharamia na maovu kupitia sekta ya Sanaa. Hii ndiyo maana ya dhana hii ya polisi jamii na ulinzi shirikishi ya polisi kushirikiana na jamii” alisema Afande Kasekwa.
Kikosikazi hiki kimeundwa huku kukiwa na taarifa za uwepo wa vikundi mbalimbali vinavyofanya maonesho yenye kudhalilisha utu na maadili ya mtanzania huku uharamia kwenye kazi za Sanaa ukizidi kushika kasi.

MKUTANO WA CHADEMA WA KUZINDUA OPERATION HAMSHAPOPO KATA YA SINZA -

 Kamanda wa Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),kata ya Sinza, Patodi Gwakisa (kushoto), akifuatilia kwa makini tukio hilo
Mkazi wa Dar es Salaam, akiinua juu Kadi yake ya Uanachama muda mfupi baada ya kujiunga juzi

SHULE YA MSINGI MGABE YAPATIWA MSAADA WA MADAWATI NA BENKI YA KCB WENYE THAMANI YA MILIONI 6 NA LAKI 5Benki  ya KCB Tanzania imetoa ime kabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya shule kwa shule ya Msingi Mugabe,Sinza Maalum na Shule ya Uhuru mchanganyiko wenye thamani ya zaidi ya  sh. Milioni 18.4.
Akikabidhi msaada huo mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo Dokta Edmund Mndolwa alitaja miongoni mwa vifaa hivyo ni madawati,vywakula ,vifaa vya michezo na vinginevyo.

Dkt.Mndolwa allisema  nsaada huo unaonesha ni kwa jinsi gani benki yake inazingatia wajibu wake wa kusaidia jamii inayoizunguka kupitia sekta ya elimu,afya ,mazingira na maafa mbalimbali ili kupunguza umasikini nchini.
Amewataka kutunza vifaa hivyo ili viweze kudumu kwani ni vya gharama na viweze kutumika na wanafunzi wengine kwa manufaa ya jamii nzima.
“Napenda kuchukua fursa hii kuwafahamnisha kwamba Benki ya KCB inatoa huduma mbalimbali kwa wananchi 

wanoizunguka,tunaamini kuwa jamii inayotuzunguka nayo itatuunga mkono kwa kuchangamkia huduma zetu ambazo ni pamoja na kufungua akaunti,kuchukua mikopo ya nyumba na biashara”alisema .
Akizungumza kwa niaba ya wanajumuiya ya Mugabe shule ya Msingi, Mwalimu Mkuu  wa Shule hiyo ya Sinza Maalum Bw.Asafu Mahelele alisema  pamoja na msaada huo bado wanakabiliwa na changamoto ya vifaa vya kufundishia ikiwemo Vitabu vya Kiada, Uchakavu wa
Mapaa ya Majengo ya Shule na ubovu wa Miundombinu ya vyoo vya Walimu na Wanafunzi na kudai kuwa watayatunza ili yaweze kutumiwa kwa muda mrefu.
"Tunashukuru kwa msaada huu mdogo kutoka benki hii ya KCB,bado tuna changamoto nyingi zinazotukabili ikiwemo  ukosefu mkubwa wa vitabu vya kiada ,uchakavu wa mapaa ya majengo ya shule  yetu na ubovu wa miundombinu ya vyoo vya walimu na wanafunzi"alisema Bw.Mkiramwene.
KCB Tanzania ndiyo benki kongwe kuliko zote Afrika Mashariki ikiwa iliyoanza kuanzishwa Zanzibar mwaka 1896 na badae kusambaa Mombasa ,Nairobi, na kurudi nchini mwaka 1997.
Baadhi ya Walimu wa Mugabe, Wanafunzi pamoja na Wafanyakazi wa KCB Benki wakiwa kwenye Moja ya Madawati yaliyokabidhiwa leo.
Viongozi mbalimbali wa Serikali, wanafunzi wa shule ya Mugabe na Maafisa wa Benki ya KCB katika picha ya pamoja.

RC SAID MWAMBUNGU WA RUVUMA AHIMIZA KILIMO CHA KISASA

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu (mwenye kaunda suti nyeusi) akisikiliza maelezo ya kilimo kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Songea Thomas Sabaya (kulia) wakati wa ziara ya kukagua usambazaji wa pembejeo kijiji cha Lugagara wilaya ya Songea
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akiongea na watendaji wa vijiji vya Magagula.Muungano Zomba na Lugagara wilaya ya Songea jana alipotembelea kuhamasisha wakulima kuzalisha mahindi kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo.Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Thomas Sabaya(kulia) na mwenyekiti wa Halmashauri ya Songea Rajab Mtiula(Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma)
Wakulima wa kijiji cha Magagula wilaya ya Songea wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu (hayupo pichani) jana alipofanya ziara ya kukagua shughuli za kilimo Revocatus A.Kassimba
Afisa Habari
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma
Serikali imewataka wakulima mkoani Ruvuma kulima kwa wingi mahindi katika msimu huu kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo licha ya changamoto za soko lililowakabiri msimu wa kilimo uliopita.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu wakati wa ziara yake katika vijiji vya Magagula, Lugagala na Muungano Zomba vilivyopo wilaya ya Songea .
Mwambungu aliwaeleza wananchi kuwa serikali inatambua kero ya ununuzi wa mahindi iliyotokea msimu wa 2011/2012 ambapo wakulima wengi walichelewa kupokea fedha zao kutoka Wakala wa Hifadhi za Chakula (NFRA).
Aliongeza kusema kuwa changamoto ya fedha za wakulima hazitajitokeza tena msimu ujao kwani tayari serikali imejiandaa kwa kutengwa fedha katika bajeti ili kuhakikisha mahindi yote yatanunuliwa kwa wakati.
“Limeni kuliko mwaka jana kwani serikali imejipanga kununua kwa wakati na kuhakikisha kuwa hakuna mkulima atakayecheleweshewa malipo na serikali” alisema Mwambungu na kuongeza kuwa hakuna mkulima sasa anayeidai serikali wote wamelipwa.
Mkuu wa mkoa Mwambungu alisisitiza kuwa serikali inafanya kila linalowezekana kuondoa kero ya kukopa mahindi ya wakulima hivyo ni vema wakulima wakaendelea kuunga mkono juhudi hizi za serikali kwa kuongeza uzalishaji.
Katika msimu 2011/2012 wa kilimo kwa mujibu wa taarifa za Wakala wa Hifadhi ya Chakula jumla ya tani 50,018 za mahindi zimenunuliwa kutoka kwa wakulima mkoani Ruvuma zenye thamani ya shilingi bilioni 17.5 ambapo kilo ilinunuliwa kwa shilingi 350.
Mkuu wa Mkoa alitumia fursa hiyo kuwapongeza wakulima wa vijiji hivyo alivyovitembelea kwa kutumia vema pembejeo za ruzuku kwa mfumo wa vocha kwani wameongeza uzalishaji wa mahindi na kuifanya wilaya ya Songea kuongoza katika kuzalisha mahindi mkoani.
Ziara ya Mkuu wa mkoa ilihusisha pia kukagua zoezi la ugawaji wa vocha za pembejeo ambapo kwa mujibu wa taarifa ya iliyotolewa na Mkuu wa wilaya ya Songea Thomas Sabaya alisema wilaya imepata mgao wa vocha 64,417 ambazo zimesambazwa kwa wakulima.
Sabaya alisema vocha hizo zinahusisha mbegu bora za mahindi, mbolea ya kupandia na mbolea ya kukuzia ambapo bei ya mfuko wa mbolea ya kupandia (DAP) inauzwa shilingi 80,000/=huku mkulima akichangia shilingi 52,000/=.
Kuhusu mbolea ya kukuzia (UREA) mfuko unauzwa shilingi 72,000/= na mkulima anachangia shilingi 52,000/= huku serikali ikilipia zinazobaki na kwa mbegu bora mfuko unauzwa shilingi 40,000/= huku mkulima akichangia 20,000/= na serikali zinazobakia.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa kijiji cha Lugagara Bi Taifa Mahundi katika risala yake alisema wakulima wana changamoto kubwa ya upungufu wa vocha za ruzuku hivyo akaiomba serikali kuongeza mgao kwa kijiji.
Mkuu wa mkoa akijibu hoja hiyo aliwafahamisha wananchi kuwa vocha zinazotolewa ni vigumu kufanana na idadi ya wakulima kwani hiyo ni ruzuku itolewayo na serikali kuwasaidia wakulima kujenga uwezo wa kujitegemea.
Katika msimu huu wa kilimo mkoa wa Ruvuma umepatiwa vocha za ruzuku ya pembejeo za kilimo 192,000 ambapo kwa mwaka uliopita ulipatiwa vocha 204,000 hivyo kuwa na upungufu wa vocha 12,000/=.
Mkoa wa Ruvuma ni kati ya mikoa sita maarufu kwa uzalishaji wa mahindi nchini ambapo mikoa mingine ni Iringa, Mbeya, Rukwa, Kigoma na Morogoro.

Monday, January 30, 2012

PAZI YAJIPANGA BAADA YA KUFUNGWA NA JKT

Timu ya Mpira wa Kikapu PAZI ya jijini Dar es Salaam, hivi sasa ipo kwenye uwanja wake wa nyumbani inajifua vilivyo ikiwa ni baada ya kupoteza mchezo wake wa jana dhidi ya timu ya JKT mchezo uliyofanyika katika Uwanja wa Ndani wa Taifa(IN-NDOOR) Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Timu hiyo, Kalemaa, pamoja na wadau mbalimbali wa timu hiyo maarufu kama wazee wa chama wapo muda huu katika uwanja wa Tanesco Drive in kwa lengo la kupanga mikakati ya kufanikisha ushindi katika michezo mingine iliyosalia.
"timu yetu ni nzuri sana na tumefanya mabadiliko makubwa kwenye usajili wetu safari hii isipikuwa kufungwa ni moja ya mchezo na tutahakikisha tunapigana kufa na kupona hadi tufanikiwe kutwa ubingwa kwa mwaka huu"alisema Kalemaa
kwa mujibu wa kalemaa timu hiyo ilipoteza mchezo huo wa jana kutokana na wachezaji wake wengi kuwa majeruhi.


Wakulima zao la Karafuu Kisiwani Pemba watakiwa kutohifadhi Karafuu zao Majumbani

Na:- Marzuku Khamis Maelezo Pemba.
Wakulima wa zao la Karafuu Kisiwani Pemba wametakiwa kutohifadhi Karafuu zao Majumbani na badala yake waziopeleke katika vituo vya ununuzi vya Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC) kwa ajili ya kuziuza badala ya kuzirundikiza Majumbani mwao kama inavyojitokeza hivi sasa
Wamesema kufanya hivyo kutawaepushia na vitendo vya Wizi na pia kuweza kupata uzito mkubwa wa Karafuu zao zitakazowapatia pato zuri zaidi
Wakuu wa vituo mbali mbali vya ZSTC vya unuzi wa karafuu waliyasema hayo wakati walipotembelewa na kamati ya kitaifa yakudhibiti zao la Karafuu Zanzibar wakati walikpokuwa wakitembelea vituo mbali mbali vya ununuzi wa karafuu pamoja na vikosi vya ulinzi wa zao hilo kisiwami Pemba.
Wamesema kuwa ukweli hivi sasa Msimu wa Uchumaji wa Karafuu upo ukingoni lakini kilichobainika kuwa bado Karafuu zimo Katika majumba mbali mbali ya wakulima hivyo ni wajibu wa kila mkulima hivi hivi sasa kuzipeleka kwenye vituo vya ZSTC kwa kuziuza jambo ambalo litakuwa ni faida kubwa kwao na serikali kwa jumla.
Wakizungumzia juu ya suala la malipo ya Wakulima wanaouza karafuu zao humo vituoni wamesema kuwa hakuna hata Mkulima mmoja aneidai ZSTC na mtu yoyote anaekwenda kuuza Karafuu zake mara tu baada yakuuza anapewa malipo yake yote.
Aidha wakuu hao wa vituo wamesema kuwa kwa ujumla kazi ya ununuzi wa Karafuu imekwenda vizuri na mashirikiano kutoka kwa wauza karafuu pia yalikuwa mazuri na makubwa na kutowa wito kwa Wakulima kuharakisha kuzipeleka Karafuu zao Kuziuza hivi sasa Katika vituo vya ZSTC kwani wasije kupata usumbufu pale ZSTC itakapoamuwa kupunguza vituo hivyo Vijijini na kuvibakisha vituo vya Mijini.
Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Mustafa Mohamed Ibrahim ambae ni mjumbe wa kamati ya kitaifa ya kudhibiti zao la karafuu Zanzibar amesema kuwa amefarajika sana na kazi nzuri inayoendelea kufanyika katika utekelezaji wa kazi za ununuzi wa Karafuu na kuwataka Wakuu hao kuendelea kutoa Mashirikiano kwa Wakulima wa zao la Karafuu kwa kuwakumbusha kuzipeleka kuuza karafuu zao haraka kwenye vituo hivyo vya ZSTC na kutozihifadhi majumbani.
Katika ziara hiyo wajumbe wa kamati ya kudhibiti zao la Karafuu Zanzibar ambayo ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa Kusini UngujaMustafa Mohamed Ibrahim ilitembelea Ghala kuu la kuhifadhia karafuu lilioko Mkoani, Kituo cha ununuzi wa Karafuu cha Kiwani,Chanjaani,Bwagamoyo, Raha,Mgogoni,Kisiwani, Mtambile na Chumbageni Wambaa.
Pia Wajumbe wa kamati hiyo walitembelea kambi za Vikosi vya Kudhibiti Magendo vya Chaanjaani na Mkuumbuu.

BAYPORT KUTOA MSAADA WA VITABU KIBONDO

Bayport Manager masoko na uhusiano (aliyekaa kulia) Bwana Ngula Cheyo na bayport branch manager (aliyesimama kushoto) bwana Imani Mtewele katika uzinduzi rasmi wa huduma za jamii iitwayo ” Bayport books for schools’ katika shule ya msingi Boma iliyoko wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma
Taasisi ya kifedha ya Bayport ,katika kampeni yake ya huduma za jamii iitwayo ” Bayport books for schools “ kutoa vitabu kwenye shule 20 katika wilaya 20 Tanzania bara sasa imezindua rasmi kampeni yake na kutoa vitabu vya darasa la kwanza katika shule ya msingi Boma iliyoko wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma. Katika hafra hiyo mgeni ramsi alikuwa ndg Ndunduguru kwa niaba ya mkuregenzi wa halmashauri ya wilaya Kibondo. Manager masoko na uhusiano bwana Ngula Cheyo alisema Bayport iliaamua kutoa msaada wa vitabu darasa kwanza na kidato cha kwanza kwa kuwa tunaamini kumpa mtoto mwamko wa elimu ni lazima kumjengea msingi madhubuti mapema katika elimu yake ya chini yaani darasa la kwanza na kidato cha kwanza. Bayport itatoa vitabu 120 kwa kila shule za msingi ambavyo ni kwa masomo ya Sayansi,Hisabati Na kingereza pia vitabu 80 kwa kila shule za sekondari kwa masomo ya Sayansi,Hisabati na atlasi 2 Wakati huo huo Bayport ilizindua rasmi tawi Kibondo ambalo ni tawi la 60 miongoni mwa matawi yake Tanzania. Manager wa tawi la kibondo Bwana Imani Mtewele alisema kwamba amefurahi sana kwani sasa wateja wa kibondo wanapata huduma zao kwa uhakika na ukaribu zaidi.

Vodacom yatangaza promosheni ya punguzo la gharama

Wateja kupiga simu kwa robo shilingi. Kutuma SMS kwa 25/-
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imetangaza promosheni ya aina yake ya punguzo la gharama za simu kupiga na kutuma ujumbe mfupi wa maneno- SMS itakayowahusisha wateja wa kampuni hiyo ambao sasa watapiga simu kwa gharama ya ROBO SHILINGI kwa sekunde.
Promosheni hiyo ya siku saba kuanzia Jumatatu Januari 30, 2012 inahusu kupiga simu za ndani ya mtandao wa Vodacom yaani kupiga Vodacom kwenda Vodacom kati ya Saa nne usiku na saa moja asubuhi kila siku kwa wateja wote wa malipo ya kabla
Aidha sanjari na ofa hiyo kamambe Vodacom imetoa pia punguzo la gharama ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno hadi shilingi 25/- kwa ujumbe wakati wote wa siku kwenda mtandao wowote wa simu ya mkononi nchini kwa kipindi cha siku saba nayo pia kuanzia leo Jumatau Januari 30, 2012.
Akitangaza promosheni hizo mbili Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza amesema ni imani yake kwamba katika kipindi chote cha siku saba cha promosheni hiyo wateja watafurahia kwa kufanikishiwa mawasiliano ya biashara, familia, kazi na mengineyo kwa gharama nafuu zaidi.
“Wateja wa Vodacom wakati wote wanafurahia huduma bora, nzuri na zenye kukidhi mahitaji halisi, ni wazi kipindi hiki cha siku saba cha promosheni hii ya punguzo la gharama za upigaji wa simu na utumaji SMS kitawapatia wakati mwengine bora wa kufurahia kuwa wateja wa kampuni inayoongoza soko”Alisema Bw. Rene.
Promosoheni hii inakwenda sawa na azma ya Vodacom ya kutoa fursa ya watanzania kuunganishwa kimawasiliano na kubadili maisha.
Ili mteja wa Vodacom aweze kufurahia promoheni hii ya punguzo la gharama za mawasiliano anapaswa kwanza kujiunga kwa kupiga *100# na kuanzia hapo atakuwa na uwezo wa kufurahia mawasiliano nafuu zaidi nchini miongoni mwa mitandaso ya simu za mkononi.
“Ni fursa nzuri kwa wateja wetu, tunawaomba waitumie ikiwa ya kiwango cha chini zaidi kuwahi kutokea katika soko la mawasiliano ya simu za mkononi nchini na Vodacom itaendeleza utamaduni wa kuwa kinara wa kubuni na kuleta sokoni promosheni pamoja na huduma zenye thamani na mantiki halisi ya wateja wetu na jamii nzima nchini.” Aliongeza Bw. Rene
Rene aliongeza kwa kusema “Tunapoangalia katika utaratibu wetu wa kawaida wa mfumo wa maisha tanagundua kuwa muda wa kati ya saa nne usiku na saa moja asubuhi ndio wanafamilia hukaa pamoja na kufanya mawasiliano yenye lengo la kupashana habari za familia na hata kazi na biashara baada ya majukumu ya kutwa nzima au kabla ya kuanza siku mpya, hivyo ni imani yetu tumewapa wateja kitu chenye thamani na kinachoweza kutumika vema na kumnufaisha kila mteja.”Aliongeza
Vodacom ikiwa na wateja zadi ya milioni kumi nchini ni wazi promosheni ya aina hii itatoa faida kubwa kwa jamii kwa kuwawezesha kutumia sehemu ya punguzo la gharama ambazo wangengia kupiga na kutuma ujumbe mfupi wa maneno kuelekeza sasa fungu hilo katika matumizi ya mahitaji mengine

MCHUNGAJI VOMO-:CHANGAMOTO ZA MWAKA 2011 ZISIWAFANYE MKATEE TAMAA


NA GLADNESS MUSHI  -ARUSHA
IMEELEZWA kuwa pamoja na nchi kukabiliwa na majanga na changamoto mbalimbali hasa kwa mwaka 2011 wakristo hawapaswi kukata tamaa juu ya changamoto hizo bali wanatakiwa kuangalia imani na mahitaji ya Mungu Kwa mwanadamu ili aweze kupunguza na kuondoa changamoto hizo.
Hayo yameelezwa mjini hapa na mchungaji Simion Vomo wakati akiongea na waumini wa kanisa la T.A.G Christian All Nation Church lilopo katika manispaa ya mji wa arusha mapema wiki hii.
Aidha mchungaji Vomo alisema kuwa katika mwaka 2011 mambo mengi sana yalijitokeza hali ambayo iliwapelekea baadhi ya waumini kukata tamaa lakini katika mwaka huu mpya wa 2012 wanapaswa kumuangalia mungu zaidi kuliko matatizo yao binasi.
Alibainisha kuwa hata katika matatizo mungu yupo na kwa hali hiyo kila mwanadamu anapaswa kuangalia mpango na mikakati mbalimbali ya mungu na kuachana na tabia ya kuona wameshindwa mbele ya Macho ya wanadamu
Awali alisema kuwa nao waliofanikiwa wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatangaza zaidi utukufu wa mungu kuliko mafanikio yao kwa kuwa ndicho chanzo pekee cha kufanikiwa katika maitaji mbalimbali ambayo yanamzunguka mwanadamu wa leo.
Alibainisha kuwa endapo kama wataweza kufanya hivyo ni wazi kuwa mafanikio yatakuwa ni makubwa sana ukilinganisha na mafanikio ambayo hayana utukufu wowote hapa duniani.
Alimalizia kwa kusema kuwa kwa wale ambao hawajafanikiwa kwa msimu wa mwaka uliopita wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanaongeza kiwango cha imani katika maisha yao kwa kuwa Pia Mungu anapenda na kuthamini zaidi Mtu mwenye Imani.

TIMU YA OLDUVAI KIDS YAIBUKA KIDEDEA KOMBE LA KUHAMASISHA UPIMAJI VVU


Na.Ashura Mohamed -Arusha
Timu ya mpira wa miguu ya Olduvai Kids iliyopo mkoani hapa imeibuka mshindi katika fainali za kombe la kuhamasisha vijana kupima virusi vya ukimwi kwa kuichapa timu ya kaloleni B Magoli 2-0 mechi iliyochezwa jana katika viwanja vya kumbukumbu vya sheikh Amri Abeid mjini arusha.
Akiongea mara baada ya kumalizika kwa mechi hiyo mratibu wa tamasha hilo Samweli Mpenzu amesema kuwa lengo la tamasha hilo ni kuwawezesha vijana kuwa pamoja kupitia michezo pamoja na kutambua afya kwa kuwa michezo ni afya ili kijana anapogundulika kuwa na virusi vya ukumwi basi aweze kufuata ushauri nasaha.
Mpenzu amesema kuwa kupitia tamasha hilo vijana wameweza kuwa pamoja kupitia michezo hiyo pia wamepata fursa nyingine ya kupima virusi vya ukimwi ili kujua afya zao na jinsi ya kujikinga ambapo huduma hiyo pia ilikuwa inapatikana katika viwanja hivyo.
Pia amewashukuru vijana wote waliojitokeza pamoja na timu zote kumi kwa kuwa bila wao tamasha hilo lisingekuwa na ushindani ambapo amesema tamasha hilo pia litafanyika tena mwezi wa pili ambapo safari hii itakuwa ni upande wa wanawake.
Naye mgeni rasmi katika tamasha hilo katibu wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Arusha Zakayo Mjema amesema kuwa tamasha hilo liliandaliwa na YES Tanzania pamoja Tackle Afrika ambapo amewataka wadhamini hao kufanya liwe endelevu.
Mjema amesema kupitia nafasi yake wapo tayari kushirikiana na wadau wa michezo mkoani hapa ili kuwafanya vijana kuwa bise kuliko kukaa bila shughuli maalum ya kufanya pamoja na kuinua soka la mkoa wa Arusha.
Mshindi wa pili katika tamasha hilo ni timu ya Kaloleni B,mshindi wa tatu ni timu ya Intersports na timu zilizoshiriki ni CIDT,Younglife,Caroline Ranges,Arusha Talent, na Young Kids ambapo mshindi wa kwanza aliondoka na kombe na timu zote zilipata hati ya ushiriki.

JIJI LA DAR ES SALAAM LATIKISWA NA MUONEKANO MPYA WA DHAHABU WA BIA YA SERENGETI LAGER

Meneja wa kinwaji cha Serengeti Lager kutoka kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Allan Chonjo anayeendesha gari pamoja na Kanji ambaye pia ni mfanyakazi wa kampuni hiyo wakiongoza msafara wakati ulipopita mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es salaam leo, kuutambulisha muonekano mpya wa nembo ya bia ya Serengeti Lager huku ikiwa na ubora na viwango vilevile.

Kamalade Ali Choki na mkundi lake la Extra Bongo wakifanya vitu vyao kwenye jukwaa la gari maalum.
Mpiga gitaa la bass wa Extra Bongo akipiga gitaa huku mnenguaji wa bendi hiyo akicheza mbele yake wakati msafara huo ulipopita katika barabara ya Uhuru leo.
Extra Bongo wacharuka na kumwaga mauno barabarani wakati msafara wa promosheni ya Muonekano Mpya wa Dhahabu ukiendelea katika mitaa mbalimbali jijini Dar es salaam leo.
Muonekano mpya wa Dhahabu wa Serengeti Lager akipita maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam Msafara akupita katika maeneo ya BP katika baranbara ya Bandari ukitokea Chang'ombe Kiwandani na kuelekea maeneo ya Kariakoo jijini Dar es salaam.

Dk. Shein akutana na Mwakilishi Mkaazi wa UNDP nchini

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mwakilishi Mkaazi wa UNDP nchini Tanzania Dk. Alberic Kacou,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar jana.(Picha na Ramadhan Othman Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Mwakilishi Mkaazi wa UNDP nchini Tanzania Dk. Alberic Kacou,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar jana.(Picha na Ramadhan Othman Ikulu)
 

DK. JAKAYA KIKWETE HANDS OVER ALMA CHAIR TO PRESIDENT ELLEN JOHNSON SIRLEAF OF LIBERIA

A cross section of African Leaders Malaria Alliance (ALMA) leaders at the working session luncheon at the Africa Union Summit during which out-going Chairman President Jakaya Mrisho Kikwete handed over the ALMA chair to President Ellen Johnson Sirleaf in the side-lines of the AU Summit in Addis Ababa, Ethiopia. ALMA is an alliance of African Heads of State and Government working to end malaria-related deaths. This body was founded by African Heads of State to utilize their individual and collective power across country and regional borders:
President Jakaya Kikwete makes his opening speech and give the status of Malaria. Others from left is the new AU Chairman President of Benin, the Executive Secretary of ALMA, Ms Joy Phumaphi , new ALMA Chair and President of Liberia Madame Ellen Johnson Sirleaf, and newly elected ALMA Vice Chair and President of Mozambique, Mr Armando Guebuza STATE HOUSE PHOTOS

DAR LIVE KWAWAKA MOTO, MAPACHA WATATU, TID, SUPER SHINE, MR BLU WAFANYA KUFURU

WASANII wa muziki wa kizazi kipya na dansi Bongo, Khaleed Mohamed ‘TID’, Herry Samir ‘Mr Blu’, wakiwa na kundi la Mapacha Watatu ambalo linaongozwa na Khaleed Chuma ‘Chokoraa’, Junior Kalala ‘Kalala Junior’, na Joseph Michael ‘Jose Mara’, na kundi la muziki wa mwambao la Super Shine, usiku wa kuamkia leo wamefanya kufuru ndani ya ukumbi wa kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam. Wanamuziki hao walivunja rekodi ya mashabiki wengi waliowahi kushuhudia makamuzi kama hayo katika kituo hicho cha burudani nchini.
Shoo hiyo pia ilisindikizwa na makundi mengine kama Wakali Dancers, na wasaniii wengine wa Bongo Fleva wakiwemo Zuhura na Dogo Mfaume na Hejos Band. Watoto wakiserebuka ukumbini.
Msanii wa kucheza na kuigiza, Mpella Shaa ‘Kidevu cha Kuku’ akiwa amekaa juu ya chupa jukwaani hapo.
Mr Blue akitoa burudani kwa kila mtu.
Bosi wa TOP Bandi, mwanamuziki TID, akiwajibika.
Kundi la Wakali Dancers likitesa jukwaani.(Na: Mwandishi Wetu)

TWIGA STARS YAISASAMBUA NAMIBIA KITITA CHA MAGOLI 5-2 UWANJA WA TAIFA

Timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania(TWIGA STARS) Jana imefanikiwa kuifunga Timu ya Namibia kwa jumla ya magoli 5-2 katika mchezo wa Kimataifa Kufuvu fainali za Afrika uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Twiga yalifungwa na Mwanahamisi Omar katika dakika 21, Asha Rashid 'Mwalala', bao la pili dakika 46, bao la tatu Etoe Mlenzi, dakika ya 84, Asha Rashid,bao la nne dakika ya 88, na bao la tano, likifungwa tena na Mwanahamis, dakika ya 90. Mabao ya Namibia mawili ya yamefungwa na Beki wa Twiga, Etoe, aliyejifunga dakika ya 29 na bao la pili likifungwa na Juliana Skrywer, dakika 73.
Kwa matokeo hayo sasa Twiga Stars inatarajia kukutana na mshindi kati ya Misri au Ethiopia ambapo Misri ilikuwa inaongoza kwa mabao 4-2 dhidi ya Ethiopia.
Twiga iliwakilishwa na Fatuma Omary, Fatuma Bashiri, Pulkaria Charaji, Fatuma Khatibu, Sophia Mwasikili, Mwapewa Mtumwa, Mwanahamisi Omari, Etoo Mlezi, Fatuma Mstafa, Asha Rashid,Fadhila Hamad,  na wachezaji wa Akiba walikuwa ni Maimuna Saidi, Mwajuma Abdallah, Siajabu Hassan, Aziza Mwadini, Zena Khamis, Semen Abeid, Rukia Khamisi na Mwanaidi Khamis.
Namibia iliwakilishwa na Susanna Eises, Uerikondjera Kasaona, Lovisa Mulunga, Esther Amukwaya, Stacey Naris, Alberta Dakies, Shirley Cloete, Lethicia Manga, Thomalina Adams, Elmarie Fredericks, Lydia Eixas na wachezaji wa Akiba ni Novata Paulus, Veweziwd Kotjipati, Mangulukeni Hamata, Mariana Gaebusi, Lena Noreses, Lonaine Jossob na Juliana Skrywer.
Mchezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania Twiga Stars Asha Rashid akimtoka beki wa timu ya taifa ya Namibia ya wanawakeLovisa Mulunga, katika mchezo wa kuwania fainali za kombe la dunia kwa wanawake unaochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jioni hii,
Wachezaji wa Twiga Stars wakishagilia mara baada ya mchezaji wa timu hiyo Asha Rashid kufunga goli la pili katika kipindi cha pili.
Mashabiki wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza kwa mpambano huo kwenye uwanja wa Taifa.

Mchezaji Mwanahamisi Omari a.k.a Gaucho akihojiwa na mwandishi wa habari wa BBC Eric David Nampesya baada ya kumalizika kwa mpira kati ya Twiga Stars na Namibia , Mwanahamis Omari 'Gaucho' ni mfungaji pekee wa mabao 2 kati ya 5 ya Twiga, katika mchezo wa kutafuta kufuzu kwa fainali za Afrika kwa Wanawake, zinazotarajia kufanyika mwezi Juni mwaka huu. (Na: Mwandishi Wetu).

 

Sunday, January 29, 2012

CHAMA CHA KIJAMII CCK CHAPATA USAJILI


 Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini John Tendwa, akiwa tayari kukabidhi Cheti cha Usajili wa Kudumu kwa Chama cha Chama Cha Kijamii (CCK) Ofisini kwake jana,
Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini John Tendwa, akikabidhi Cheti cha Usajili wa Kudumu kwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Chama Cha Kijamii (CCK) Constantine Akitanda, hafla iliyofanyika katika Ofisi za Msajili.
 Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini John Tendwa,wa tatu kushoto akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa  Chama cha Chama Cha Kijamii (CCK).
 Mwandishi wa Habari akifuatilia kwa Makini Makabidhiano hayo
Vijana wakiwa wamebeba Bango la Chama hicho
Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini John Tendwa,akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Kijamii (CCK).Mara bada ya kukabidhiwa Cheti hicho.