Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye akimkabidhi cheti mhitimu wa kidato cha sita, Burilo Busagi,
katika mahafali ya kidato cha sita shule ya Sekondari Nsumba, Mwanza.
Jumla ya wahitimu 374 wa kidato hicho walipewa vyeti. Kushoto ni Mkuu
wa shule hiyo Josephat Zakeyo.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
akimkabidhi cheti mhitimu wa kidato cha sita, Tifugundulwa Tumbika
katika mahafali ya kidato cha sita shule ya Sekondari Nsumba, Mwanza.
Tumbika alikabidhiwa cheti hicho kwa kuibuka mwanafunzi bora katika
kuzungumza Kiingereza. Wapili kulia ni Mkuu wa shule hiyo Josephat
Zakeo.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye akizungumza na mwanafunzi aliyesoma shule ya sekondari ya
Nsumba, Mwanza, kati ya mwaka 1954 na 1957 (darasa la nane na kumi)
Damas Ngoma, wakati wa mahafali ya kidato cha sita ya shule hiyo leo.
Nape ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo alisoma pia katika
shule hiyo hadi kidato cha nne mwaka ambako alimaliza mwaka 97. Watatu
ni Mkuu wa shule hiyo Josephat Zakeo.(Picha zote na Bashir Nkoromo).
Na Zahira Bilal Maelezo Zanzibar
Waziri
wa kazi uwezeshaji wananchi kiuchumi na ushirika Haroun Ali Suleiman
amesema kuwa idadi ya vyama vya ushirika vinavyoaandikishwa imekuwa
ikiongezeka na kwamba vyama hivyo vimekuwa vikiongezewa nguvu ya
usimamizi na utaalamu.
Hayo
aliyasema leo wakati akijibu swala la Mwakilishi wa nafasi za
wanawake Salma Mussa Bilali alietaka kujua hatua zinazochukuliwa na
wizara katika kuimarisha vyama vya ushirika wilayani huko katika ukumbi
wa baraza la wakilishi chukwani
Waziri
Haroun alisema kuwa zoezi la kukusanya takwimu za vyama
litakapokamilika litasaidia kujua mahitaji ya wataalamu na watendaji
kwa ujumla
Aidha
alisema wizara yake inajitahidi kujipanga ili kuweza kuimarisha
utendaji wilayani na katika vitengo maalumu vya idara ya ushirika pia
kusimamia mpango wa mafunzo kwa maofisa wa ushirika wa ngazi mbali
mbali ili kuongeza utaalamu na uwezo wao wa kuhudumia vyama vya
ushirika kwa ufanisi zaidi
Alisema
wizara yake inampango wa kuanzisha vituo vya stadi maalumu kwa ajili
ya kutoa elimu kwa washirika na kuweza kuimarisha vyama vya ushirika
kwa kila wilaya
Alisema
kufanya hivyo inaweza kuondoa usumbufu wa tatizo la ucheleweshaji
wa usajili wa vyama vya ushirika na kuongeza kasi ya kukagua na
kupewa usajili kwa haraka
Sambamba
na hayo alisema kufanya hivyo ni kuwawasaidia wananchi wa mijini na
vijijini kupata ajira na kuwaondoshea umasikini na ndio malengo ya
wizara hiyo
Father Alphonse M.Sammot
wa kanisa katoliki nchini Malta akitoa mada yake juu ya mambo muhimu ya
historia ya Kikristo yaliyoko nchini Uturuki ambapo amewasihi
watanzania Wakristo kutembelea nchini Uturuki na kuijua historia hiyo
ikiwa ni pamoja na kufanya ibada maalum huko, Father Alphonse M.Sammot
amehudumu muda mrefu huko Uturuki amezungumza hayo katika warsha
iliyokutanisha wadau na mawakala wa tiketi za ndege pamoja na viongozi
wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo, Warsha hiyo imefanyika
kwenye Hoteli ya Hyyat Regency Dar es salaam ya jijini Dar es salaam na
imeandaliwa na shirika la ndege la Turkish Airlines la Uturuki.
Bw. Emim Cakmak Mwenyekiti wa Baraza la Maendeleo ya Utalii na afya Uturuki (Turkish Hearth care and Tourism Development)akizungumza
katika warsha ya siku moja iliyokutanisha makampuni ya mawakala wa
kuuza tiketi za ndege na baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristo, Warsha
hiyo ilikuwa ikizungumzia maeneo mbalimbali yenye historia ya Ukristo
ambayo wakristo wanaweza kutembelea na kujionea kumbukumbu hizo na
imefanyika leo katika hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam jijini Dar es salaam
Mustafa
Ozkahraman Meneja wa Turkish Airline Tanzania akitoa mada katika warsha
hiyo juu ya mambo mbalimbali na ubora wa huduma za usafiri wa anga wa
shirika hilo, kushoto ni Bw. Emim Cakmak Mwenyekiti wa Baraza la Maendeleo ya Utalii na afya Uturuki (Turkish Hearth care and Tourism Development).
Baadhi ya masista pia wamehudhuria katika warsha hiyo iliyoandaliwa na shirika la ndege la Turkish Airlines.
Kutoka kushoto ni )Bw. Emim Cakmak Mwenyekiti wa Baraza la Maendeleo ya Utalii na afya Uturuki(Turkish Hearth care and Tourism Development),
Mustafa Ozkahraman Meneja wa Turkishh Airline Tanzania na Victoria
Carmak Meneja Huduma wa Hello Tourism Travel Agency wakiwa katika picha
ya pamoja leo.
Baadhi
ya viongozi wa dini madhehebu ya Kikristo wakiwa katika warsha hiyo
iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es salaam leo.
Kulia
ni Warda Saad wa shirika la ndege la Turkish Airlines na kushoto ni
Bahati Chando kutoka kampuni ya R$R ya jijini Dar es salaam wakiwa
katika warsha hiyo.

No comments:
Post a Comment