Pages

Wednesday, January 9, 2013

IBF YAAWAALIKA WAFANYABISHARA WA KITANZANIA BERLIN, UJERUMANI

 


Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati linawaalika wafanyabishara wa kitanzania kuhudhuria mkutano wa mwaka wa IBF/USBA utakaofanyika katika jiji la Berlin nchini Ujerumani kuanzia tarehe Mei 21-25th, 2013.
 Katika mkutano huo wanachama zaidi ya 3000 wa IBF/USBA kutoka nchi zaidi ya 200 duniani watahudhuria.
 Hii ni fursa pekee kwa wafanyabishara wa Kitanzania kuweza kutumia mkutano huu kutangaza biashara zao katika sekta mbalimbali hususan sekta ya Kitalii, TEHAMA, usafirishaji wa bidhaa za kitanzania nje ya nchi pamoja na uwekezaji katika sekta mbalimbali nchini.
 Mkutano wa mwaka wa IBF/USBA huwakutanisha wafanyabishara waliowekeza katika sekta mbalimbaki za kiuchumi na hutoa fursa kubwa kwa wafanyabishara kujenga mitandao mzuri wa biashara.
 Rais wa Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi anawahimiza Watanzania kuchangamkia fursa hizi ili waweze kufaidika kiuchumi,
 Aidha, Ngowi anawahamasisha wakuzaji wa mchezo wa ngumi pamoja na wale wanaofanya shughuli za Branding (kukuza biashara) kuhudhuria mkutano huu na kujipatia fursa mbalimbali za biashara.
 Ngowi ataongoza ujumbe nzito kutoka bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati wakiwamo Mawaziri wa Michezo kadhaa kutoka nchi zilizo katika ukanda huu.
 

No comments:

Post a Comment