Pages

Saturday, March 8, 2014

AIRTEL YAIPIGA JEKI POLISI

unnamedAfisa mnadhimu wa Polisi Kinondoni SSP Bibie Juma akikabidhiwa msaada wa samani za Ofisi na afisa usiano na matukio wa kampuni ya  mawasiliano ya airtel Dangio Kaniki.
………………………………………………………………………………
Na Abdallah  Selemani wa Jeshi la Polisi.
Kampuni ya mawasiliano ya simu  airtel Tanzania imetoa msaada wa samani za ofisi,vikiwemo viti sita na  meza sita kwa jeshi la polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni.
Msaada huo ni kwa ajili ya matumizi ya  ofisi za kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Kinondoni ambazo zitapelekea  kuwaongezea ufanisi askari  wa usalama barabarani .

Akikabidhi samani hizo machi 5 katika viwanja vya polisi oysterbay  afisa usiano na matukio wa kampuni ya  mawasiliano ya airtel Dangio Kaniki alisema wamekabithi misaada  kwa lengo la kukuza ushirikiano kati ya jeshi la polisi na kampuni ya airtel.
Dangio kwa niaba ya  airtel  ameidi kuendelea kutoa misaada kwa jeshi la polisi kadri wawezavyo.
Akizungumza  kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni afisa mnadhimu wa polisi kinondoni(SSP) Bibie juma athumani  alisema anaishukuru kampuni ya airtel kwa msaada waliotoa na kuahidi kutunza samani hizo na kutoa wito kwa makampuni mengine ya mawasiliano kulisaidia  jeshi la polisi.

No comments:

Post a Comment