Pages

Tuesday, March 11, 2014

MBEYA CITY FC: RICHARD PETER KUWAKOSA JKT RUVU KUTOKANA NA MAJERUHI, YEYA KAMILI GADO MECHI IJAYO!!

mbeya cityNa Baraka Mpenja 

WAGONGA nyundo wa Mbeya, klabu ya Mbeya City wanaendelea kujinoa makali yao kuelekea mchezo ujao machi 16 dhidi ya Maafande wa Jeshi la  kujenga Taifa, JKT Ruvu katika dimba la Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Afisa habari wa klabu hiyo, Freddy Jackson amesema wachezaji wapo wapo katika hali nzuri na uimara mkubwa wa kufanya vizuri mechi ijayo.
“Maandalizi yetu ni mazuri sana na tunaendelea kujiandaa vyema ili kuhakikisha kuwa tunaibuka na pointi tatu muhimu katika mchezo huo ambazo zitatuweka katika nafasi nzuri zaidi kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara”. Alisema Freddy.

No comments:

Post a Comment