Pages

Sunday, September 21, 2014

SIMBA SC YATULIZWA 2-2 NA WAGOSI WA KAYA….YAYO KATO AZIMA NDOTO ZA KIDEDEA

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
WEKUNDU wa Msimbazi, Simba wamelazimisha sare ya mabao 2-2- na Wagosi wa Kaya, Coastal Union katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu soka Tanzania bara uliomalizika jioni hii uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Simba chini ya kocha Patrick Phiri walianza mpira wakilishambulia mara kadhaa lango la Coastal na katika dakika ya 7 ya kipindi cha kwanza Mnyama aliandika bao la kuongoza kupitia mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na kiungo mkongwe, Shaaban Kisiga ‘Malone’.

No comments:

Post a Comment