Pages

Friday, November 7, 2014

DC MUFINDI AIPONGEZA SHULE YA SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA KWA KUONGOZA MTIHANI WA DARASA LA SABA

DC Mufindi Evarita Kalalu Na matukiodaima.co.tz SERIKALI wilayani Mufindi mkoani Iringa imeipongeza shule binafsi ya Southern Highlands Mafinga kwa kuongoza kiwilaya na kuwa shule ya 8 kimkoa katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa darasa la saba mwaka 2014 . Akitoa pongezi hizo hizo mkuu wa wilaya ya Mufindi Evarista Kalalu alisema kuwa shule hiyo imeendelea kuipa heshima kubwa wilaya ya Mufindi kutokana na kuendelea kufanya vema katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba kwa miaka 13 mfululizo sasa na kuwa imefanikiwa kupanda kutoka nafasi ya tatu mwaka jana hadi kushika nafasi ya kwanza mwaka huu katika wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kufaulisha wanafunzi wote darasani.

No comments:

Post a Comment