Wasimamizi wa Uchaguzi wakielekeza namna ya 
kupiga kura wapiga kura walijitokeza kupiga kra mkoani Katavi Uchaguzi 
wa Seriklali za Mitaa.
(Picha zote na Kibada Kibada –Katavi)
………………………………………………………………………………..
Na Kibada Kibada -Katavi 
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 
Katika Mkoa wa Katavi umekamilika kwa wananchi kujitokeza kupiga kura 
kwa kufuata taratibu kanuni na sheria zinazoongoza uchaguzi wa serikali 
za Mitaa ingawa kulikuwa na changamoto cha hapa na pale kama kuchelewa 
kufika kwa karatasi za kupigia kura na vituo vingine uchaguzi 
kuahirishwa dakika za mwisho kutokana na Mgombea kukosa Sifa ya kugombea
 .
Akizungumzia kuahirishwa kwa 
uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nsanda Kata ya Ugalla kwa kile 
kilichoelezwa kuwa Mgombea kukosa Sifa ya kugombea baada ya kuwa kuwa 
amehukumiwa kifogo cha mwaka mmoja jela siku moja kabla ya uchaguzi 
hivyo kukosa sifa ya kuweza kugombea na nafasi hiyo kubaki wazi hadi 
hapo itakapotangazwa tena na mamlaka husika ya uchaguzi wa serikali za 
mitaa.
Afisa uchaguzi wa Halmashauri ya
 Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi Betwel Ruhega ameeleza kuwa kwa mjibu wa
 taratibu mgombea anapokuwa amepatikana na kosa la jinai na kuhukumiwa 
kifugo tena cha mwaka mmoja hivyo  anakuwa amepoteza sifa za kugombea 
uongozi  hivyo hafai kuwa kiongozi tena kwa mjibu wa taratibu.
Ruhega akaeleza kuwa aliyekuwa 
Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Kitogoji cha Nsanda amekosa sifa 
baada ya kufugwa na siku moja kabla ya uchaguzi hivyo nafasi hiyo kuwa 
wazi,kwa mjibu wa utaratibu inabidi kuahirisha ili kutoa nafasi kwa 
chama kupendekeza na kuteua jina la mgombea mwingine wa nafasi hiyo ya 
mwenyekiti.hivyo uchaguzi umeahirishwa hadi utakapotangazwa tena kwa 
mjibu wa Kanuni taratibu na sheria za uchaguzi.sitanislau makungu 
chadema
A kaongeza kuwa maeneo mengine 
mambo yameenda kama yalivyopangwa na wananchi wamejitokeza kwa wingi 
kupiga kura na hivi wanasubiria matokeo.
Na taarifa zilizopatikana kutoka
 Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Kata ya Mpandandogo wagombea nafasi ya 
Uenyekiti wa Kitongoji Igagala B’ wamegongana kura hivyo inabidi 
uchaguzi huo urudiwe upya.
Kwa Mjibu wa Afisa Uchaguzi wa 
Halmashauri ya Mpanda Charles Linda amesema wagombea wa Nafasi ya 
Mwenyekiti wa Kitongoji  cha Igagala C Kijiji cha Igalala Kata ya Mpnda 
Ndogo wamegona kwa kupata kura sawa hivyo inabidi uchaguzi urudiwe upya .
Linda amewataja waliolingana 
kura kuwa ni  Mgombea wa Nafasi ya Mwenyekiti kuptia tiketi ya CCM Isaya
 Daud  na Stanslaus Makungu kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na 
Maendeleo.
Katika hatua nyingine wapiga 
kura wa kituo cha kupigia kura Mnyagala walilazimika kusubiri kuanza 
kupiga kura majira ya saa nane mchana baada ya kuchelewa kuwafikia 
karatasi za kupigia kura  hivyo kurazimika kusubiri hadi zilipo fika 
karatasi hizo wakaanza kupiga kura.
Kwa Mjibu wa Msimamizi wa Kituo 
cha kupigia kura Steven  Msomi alieleza kuwa wananchi walijitokeza tangu
 asubuhi kusubilia kupiga kura na hawakuchoka na hamasi ilikuwa kubwa 
hasa akina mama na vjiana wengi wamehamasika na kujitokeza kwa wingi.na hali ya usalama ni shwari.
Katika maeneo mengine Mkoani 
humo uchaguzi umeendeshwa kwa amani na usalama hadi kufungwa kwa vituo 
vya kupigia kura kullikuwa hakuna taarifa zozote zilizoripotiwa 
zinazohusiana na uvunjifu wa amani.
No comments:
Post a Comment