Pages

Wednesday, February 18, 2015

FAINALI DARAJA LA KWANZA KUCHEZWA JUMAPILI


indexTimu za African Sports ya Tanga na Mwadui FC ya Shinyanga zinatrajiwa kucheza mchezo wa fainali ya kusaka Bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) siku ya jumapili katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
African Sports waliibuka washindi wa kwanza katika Kundi A, na Mwadui FC washindi wa kwanza Kundi B watacheza mchezo huo wa fainali ambapo Bingwa atapewa zawadi ya Kombe na medali, hali kadhalika kwa msindi wa pili.
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ilimalizika mwishoni mwa wiki kwa timu nne kupanda Ligi Kuu kwa kila kundi kutoa timu mbili, Kundi A ni African Sports na Majimaji FC, Kundi B ni timu za Mwadui FC na Toto African

No comments:

Post a Comment