Pages

Tuesday, February 17, 2015

Rais Kikwete amewaongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya chifu Abdul Adam Sapi Mkwawa.

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dokta Jakaya Mrisho Kikwete juzi amewaongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya chifu wa kabila la Wahehe marehemu Abdul Adam Sapi Mkwawa kijijini kwao kalenga na kushuhudia kiapo cha chifu mpya wa kabila hilo chifu Adam wa pili aliyetawazwa katika kiti hicho cha uchifu baada ya kifo cha baba yake.
Mazishi hayo ya chifu Abdul Adam Sapi Mkwawa yalitanguliwa na kiapo cha kumsimika chifu mpya wa wahehe kilichoongozwa na wazee wa mila kutoka kabila hilo na baadae shughuli ya mazishi ikaendelea kwa kutanguliwa na ibada ya mazishi iliyoongozwa na sheikhe wa wilaya ya Iringa Issa Ngwele.
 
Alhaji Abdul Mkwawa aliaga dunia jumamosi iliyopita katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa alikokuwa anapatiwa matibabu
Chifu Adam wa pili ni mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Highland iliyopo manispaa ya Iringa na kwa kuwa hajafikisha umri wa miaka 20 kazi ya uchifu itashikiliwa na baba yake mdogo Hassan Mkwawa.

No comments:

Post a Comment