Pages

Tuesday, February 17, 2015

TFF YAZIPONGEZA AFRICAN SPORTS, MWADUI, MAJIMAJI NA TOTO

  Majimaji(2)
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini – TFF Bw. Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Wenyekiti wa klabu ya African Sports (Tanga) , Majimaji (Ruvuma),  Mwadui (Shinyanga) na Toto Africans ya Mwanza kwa timu zao kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
Katika salamu zake Bw. Malinzi amesema vilabu hivyo vinapaswa kujipanga na kufanya maandalizi kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom 2015/2016, kwani VPL ni ngumu kutokana na timu zote kuwa na ushindani mkubwa wa kutafuta matokeo mazuri kuepeuka kushuka daraja.
Kwa niaba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini -TFF, familia ya mpira na watanzania kwa ujumla wanawapa pongezi timu za African Sports, Majimaji, Mwadui na Toto Africans kwa kupanda Ligi Kuu ya Vodacom na kuwatakia maandalizi mema ya VPL 2015/2016.

No comments:

Post a Comment