MPALULEBLOG:

Pages

▼

Wednesday, December 30, 2015

KESI YA WAFANYAKAZI WA TRA KUSIKILIZWA JANUARI 13 MWAKANI


download (17)

Na Nyakongo Manyama-Maelezo
Kesi inayowakabili wafanyakazi wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) inatarajiwa kusikilizwa
tena January 13, 2016
Akizungumza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini dar es salaam Wakili wa Serikali Bi.Dianna Lukondo amesema kuwa kwa leo Kesi ilikuja kwa ajili ya kusikilizwa na kutoa dhamana kwa washtakiwa na hivyo imeshindikana kusikilizwa kutokana na upelelezi kutokamilika.

“Upelelezi haujakamilika hivyo kesi itasikilizwa tena Januari mwakani ” alisema Dianna.Kesi hiyo inawakabili aliyekuwa Naibu Kamishna TRA Tiagi Masamaki, meneja wa kitengo Huduma kwa Wateja Habibu Mponezya, na wengine ni Khamis Omary, Eliaichi Mrema, Burton Kaisi, Harun Mpande na Raymond Louis.

Washtakiwa hao wanatuhumiwa kwa kosa la uhujumu uchumi, wakidaiwa kuhusika na upotevu wa makontena 329 katika Bandari ya Dar es Salaam yaliosababisha ukwepaji wa ushuru zaidi ya sh. Bilioni 80.
Unknown at 4:36 AM
Share

No comments:

Post a Comment

‹
›
Home
View web version

About Me

Unknown
View my complete profile
Powered by Blogger.