Pages

Friday, December 11, 2015

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YAFUTA VYAMA VYA KIJAMII 1,268



Katika ufutwaji wa vyama hivyo chama kimojawapo kilichofutwa ni chama cha wapiga picha nchini ambacho kimeshindwa kukidhi vigezo vya uendeshaji na kushindwa hata kuendesha vikao vyake.
Nantanga amesema kuwa vyama vingine 1,406 vimepewa kusudio la kufutwa na baada siku 21 kuanzia leo, kama havitatoa kusudio la kujitetea basi navyo vitafutwa.
Amesema kufuatana na kanuni ya vyama inayoundwa na kifungu cha 38 cha sheria ya vyama vyote vya kijamii vinapaswa kulipa ada ya kila mwaka.
Aidha, amesema kanuni ya 6 za vyama za kijamii inayosomwa pamoja na kifungu cha 22 cha sheria ya vyama inavitaka vyama vya kijamii kuwasilisha taarifa za kila mwaka za hesabu zilizokaguliwa za mapato na matumizi ya vyama kwa msajili wa vyama.
Aliongeza kuwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inatoa angalizo kwa vyama vyote vya kijamii kuendesha shughuli zake kwa kufuatana na sheria zilizoanzisha vyama hivyo.

No comments:

Post a Comment