Pages

Thursday, December 31, 2015

TTCL YATOA ZAWADI YA MWAKA MPYA KWA VITUO VYA YATIMA DAR ES SALAAM.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura akikabidhi sehemu ya msaada kwa baadhi ya watoto kutoka Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kiwohede kilichopo Buguruni Malapa cha jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa leo na Kampuni ya TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. 

JESHI LA POLISI LAWATAHADHARISHA WANANCHI KUHUSU MKESHA WA MWAKA MPYA.








WADAU WA UJENZI WATAKIWA KULITUMIA BARAZA LA TAIFA LA UJENZI ILI KUEPUKA MIGOGORO.


Na: Jovina Bujulu - MAELEZO.

Wadau wa Ujenzi wameshauriwa kutumia huduma za kitalaam zinazotolewa na Baraza la Taifa la Ujenzi ili kuepuka migogoro inayojitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi nchini.

Wito huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza hilo Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu majukumu ya baraza hilo katika utatuzi wa migogoro inayotokea katika maeneo mbalimbali.

Mhandisi Chamuriho amesema kuwa migogoro ya miradi ya ujenzi inayojitokeza mara kwa mara baina ya wadau husika hutokana na kukosekana kwa ushirikiano baina yao.

" Wadau wanatakiwa kushirikiana kulingana na makubaliano yao ili mradi husika ukamilike"  Alisema na kuongeza kuwa tofauti kati ya wadau wa miradi ya ujenzi hujitokeza kutokana na ukubwa na ugumu wake.

Aidha, Dkt. Chamuriho amesema kwamba migogoro ya ujenzi isiposuluhishwa mapema hugharimu pesa nyingi, muda wa wadau na fursa za matokeo ya miradi inayojengwa.

"Ninajua njia mahususi ya utatuzi wa migogoro inayoajitokeza nchini ni kutumia mahakama ambayo mashauri yake huchukua muda mrefu, ili kuokoa muda huu, utatuzi mbadala katika ujenzi ni kulitumia Baraza la Ujenzi" alisisitiza  Mhandisi Dkt. Chamuriho.

Akitaja majukumu mengine ya Baraza hilo amesema kuwa ni kutoa huduma za ushauri , usuluhisi wa migogoro, mafunzo, ukaguzi wa kiufundi, utafiti na kutoa machapisho ya kiufundi.

Alisema kuwa Baraza la Taifa la Ujenzi lilianzishwa kwa mujibu wa sheria ya Bunge na 20 ya mwaka 1976 na kuanza kutekeleza majukumu yake.

ONYO KALI MKESHA WA MWAKA OLE WAO WATAKAOFANYA FUJO.


AFISA BIASHARA WA HALMASHAURI YA DODOMA ASIMAMISHWA KAZI