MPALULEBLOG:

Pages

▼

Sunday, June 19, 2016

UTALII WA NDANI WAZIDI KUPATA MASHIKO ,WASOMI CHUO KIKUU SMMUCo WATEMBELEA HIFADHI YA NGORO NGORO


Simba dume akiwa anaunguruma
Simba jike akiwa amepumzika kwenye nyasi

Na Dickson Mulashani

Suala la utalii wa ndani limeonekana kupata mashiko baada ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Stefano Moshi Memorial University College (SMMUCo) kuhamsika na kuamua kutembelea hifadhi ya taifa ya Ngoro ngoro ili kujionea vivutio vya kipekee vinavyopatikana humo.
Wanafunzi hao wakiwa katika geti la kuingia hifadhi ya Ngoro ngoro

Akizungumzia safari hiyo mmoja wa wanafunzi hao Emmanuel Kalenzi amesema waliguswa kupanga ziara hiyo kuunga mkono wadau mbali mbali wanaohamasisha utalii wa ndani ili kuweza kuwa mabalozi kwa wengine. “Sisi kama wasomi ndio tunapaswa kuwa mabalozi kwa jamii inayotuzunguka na ili uwe balozi mzuri basi uwe umashajionea kwa macho” alisema.

Nyati dume mwenye umri mkubwa ambaye tayari ametengwa na kundi lake
Ndege aina ya Cranes nao wanapatikana katika eneo la crater
Nyumbu akiwa amepumzika mara baada ya kula nyasi
Unknown at 11:26 AM
Share

No comments:

Post a Comment

‹
›
Home
View web version

About Me

Unknown
View my complete profile
Powered by Blogger.