Pages
(Move to ...)
Home
▼
Wednesday, January 20, 2016
RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA BALOZI WA ISRAEL NCHINI IKULU JIJINI DAR LEO.
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Balozi wa Israeli nchini Mhe Yahel Vilan
alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo January 19, 2016.
SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LATOA MSAADA KWA KITUO CHA WATOTO JINJA, UGANDA.
Wanachama wa mpango wa kujitolea wa "i-Volunteer" wa shirika la ndege la Etihad wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wa kituo cha kulea watoto cha “Whisper Children’s Home” kilichopo Jinja-Uganda walipotembelea kituo hicho kutoa msaada mwishoni mwa juma.
RAIS DKT.MAGUFULI AKUTANA NA BALOZI SEIF ALI IDD LEO.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Idd amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa hali ya Zanzibar ni shwari na Wazanzibar wanasubiri kutangaziwa tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi.
www.shaabanmpalule.blogspot.com
SERIKALI YAOMBWA KUCHANGIA CHAKULA CHA WATOTO WAKIWA SHULENI.
SERIKALI yaombwa kuchangia chakula cha watoto wakiwa shule ili kuwasaidia kusoma wakiwa wameshiba kwani watoto hawawezi kusoma wakiwa na matumbo hayana chakula.
Hayo yamesemwa na
Shule kuu ya Elimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Joviter Katabaro wakati akichangia maada katika mkutano wa kujadili masuala ya elimu katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyrere jijini Dar es Salaam leo.
Nae Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Haki Elimu, John Kalage kuwa wamependekeza Lugha ya Kiswahili na Kiingereza iwe lugha ya kufundishia na kujifunzia kwa ngazi zote ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.
Pia ametoa wito kwa serikali kuwa kutoa elimumsingi bure sabamba na kupunguza michango ya wazazi mashuleni.
Aidha Karage amesema kuwa ili kuhakikisha ubora mashuleni, shule, taasisi na vyuo vinapaswa kufanyiwa ukaguzi kuhusu ufundishaji na ujifunzania pamoja na mazingira kuwa mazuri.
Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Bashiru Ally akizungumza na wadau wa elimu leo jijini Dar es Salaam wakati wakijadiliana kuhusiana na masuala mbalimbali ya elimu kwa watoto waliotolewa fedha na Serikali kwaajili ya kutolewa elimu bure kwa elimu ya Sekondari na Shule za msingi. Kulia ni Profesa Mshiriki wa chuo kikuu cha Dodoma, Profesa Willy Komba.
ANGALIA MVUA ZILIVYOITIKISA DAR ES SALAAM, NA HAPA NI HALI YA KIWANJA CHA JANGWANI JIJINI DAR ES SALAAM HII LEO.
WANAYANGA NA WADAU WA TIMU HIYO WAHIMIZWA KUTUMIA KADI ZA ATM ZA BENKI YA POSTA TPB · JK AHANI MSIBA WA ALIYEKUWA MKURUGENZI WA TAA, MHANDISI SULEIMAN SAID SULEIMAN · ASKARI WA JWTZ ABAKWA NA MWENDESHA BODABODA · KESI YA KUPINGA MATOKEO JIMBO LA TARIME VIJIJINI YARINDIMA MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA. · MWILI WA MBUNGE LETICIA NYERERE WAWASILI JIJINI DAR ES SALAAM MAZISHI YAKE KUFANYIKA BUTIHAMA MKOANI MARA KESHO KUTWA · SHEIKH SALMAN ATEMBELEA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO · SERIKALI KUFUNGUA VIWANDA VYA NGOZI DAR, GEITA NA SHINYANGA – WAZIRI MKUU · UCHAGUZI WA VIONGOZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA NEW YORK JUMAMOSI, FEBRUARY 13, 2016.
·
·
Hello Ladies and Gentlemen
·
KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI, MEJA JENERALI RWEGASIRA ALITAKA JESHI LA ZIMAMOTO KUONGEZA KASI KUKUSANYA MAPATO
·
KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI NA UTALII AKUTANA NA KUNDI LA WASHIRIKA WA MAENDELEO KATIKA SEKTA YA MAZINGIRA, MALIASILI NA MABADILIKO YA TABIA NCHI (DPG-E)
·
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA MPANGO MKAKATI WA WAFANYABIASHARA DUNIANI
·
BABY SHOWER
·
KICHUPA CHA LEO BILAL MASHAUZI Ft. AT - DALALI[Official VIDEO]
·
UKISHIKWA SHIKAMANA
·
WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA BAADA YA KUKUTWA WAKIWA NA DAWA ZA KULEVYA
·
RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA BALOZI WA ISRAEL NCHINI IKULU LEO
·
Wananchi Wachomewa Moto Nyumba Zao
·
Wahariri wa Mawio wajisalimisha Polisi
·
Ofisi za ZEC zapigwa komeo
·
KATIBU MKUU AONGEA NA MENEJIMENTI YA OFISI W A MAKAMU WA RAIS.
·
WABUNGE WA CCM WAENDELEA NA KIKAO MJINI DODOMA
·
Mambo sita kutikisa Bunge
·
DONDOO ZA MAGAZETI
WANAYANGA NA WADAU WA TIMU HIYO WAHIMIZWA KUTUMIA KADI ZA ATM ZA BENKI YA POSTA TPB
Posted: 19 Jan 2016 01:48 PM PST
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Grace Majige akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa wadau wa Yanga kutumia kadi za ATM za Yanga. Mkutano huo na wanahabari ulifanyika kwenye ofisi za benki hiyo tawi la Kariakoo jijini Dar es Salaam, Januari 19, 2016. Wengine pichani kushoto ni Mkuu wa Masoko wa benki hiyo, Omary Kaya, na Afisa Habari na Mawasiliano wa beki hiyo, Timotheo Mwakifulefule.
Tuesday, January 19, 2016
WADAU WA ELIMU WA MKOA WA MBEYA NA KATAVI WAKUTANA KUJADILI JINSI YA KUONGEZA IDADI YA UFAULU WA WANAFUNZI WA DARASA LA SABA MKOA WA MBEYA.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh:Abbas Kandoro akizungumza na Waandishi wa Habari hawapo Pichani nje ya Ukumbi wa Mkapa uliopo Sokomatola Jijini Mbeya katika Semina ya Wadau wa Elimu wa Mkoa wa Mbeya na Mkowa wa Katavi ambao wamekutana leo kuzungumzia juu ya Mbinu ambazo wanazitumia Mkoa wa Katavi kufanikiwa kufaulisha Wanafunzi kwa Asilimia kubwa kulinganisha na Mkowa wa Mbeya na Mikoa mingine.
WANAFUNZI 686 WA CHUO KIKUU CHA ELIMU CHA KUMBU KUMBU YA DR. ABDULRAHMAN AL – SUMAIT WATUNUKIWA VYETI VYAO LEO ZANZIBAR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiambatana pamoja na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kumbu ya Dr. Abdulrahman Al – Sumait wakiingia kwenye uwanja kwa ajili ya Mahfali ya 15 ya chuo hicho hapo Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Kulia ya Balozi Seif ambae alimuwakilisha Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein kwenye Mahafali hayo ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Hicho Dr. Abdulrahman Al - Muhailan na kushoto ya Balozi Seif ni Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho Profesa Hamed Rashid Hikmany.
USALAMA WA AFYA KWA WAFANYAKAZI
TAARIFA ZA UPOTOSHWAJI ZA GAZETI LA MWANAHALISI KUHUSIANA NA UCHAGUZI WA UBUNGE JIMBO LA KIJITOUPELE
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
KUHUSU UPOTOSHWAJI WA TAARIFA ZILIZOANDIKWA NA GAZETI LA MWANAHALISI KUHUSIANA NA UCHAGUZI WA UBUNGE JIMBO LA KIJITOUPELE
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), inapenda kutaarifu Umma na Watanzania kwa ujumla kuwa Jimbo la Kijitoupele lililoko Zanzibar ni miongoni mwa Majimbo hamsini(50) ambayo yalitegemewa kufanya uchaguzi mkuu tarehe 25, oktoba,2015.
Hata hivyo Jimbo hilo halikufanya uchaguzi wake wa Mbunge kutokana na hitilafu katika karatasi za kupigia kura badala Wapiga kura walishiriki katika kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Tume imefikia uamuzi wa kutoa ufafanuzi huu kutokana na taarifa iliyochapishwa na gazeti la MwanaHalisi toleo l Na.322 la Januari 18, 2016 katika ukurasa wake wa mbele likidai “ NEC YAIBUA MAPYA” Habari hii si sahihi na inalenga kuupotosha umma na kuleta uchochezi miongoni mwa Wananchi.
Kwa ujumla maelezo yote yaliyopo katika taarifa hiyo yanaeleza kwamba, Tume imeanzisha Jimbio jipya, kwa mujibu wa taarifa ya gazeti husika ni Jimbo la Kijitoupele – Zanzibar.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda inasisitiza kuwa taarifa zilizotolewa na Gazeti la MwanaHALISI siyo za kweli, ni za uongo, uzushi, uzandiki na uchochezi. Kufuatia taarifa hiyo,Tume inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:
• Tarehe 13 Julai, 2015 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari ikionesha Orodha ya Majimbo yatakayofanya uchaguzi wa Mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na Jimbo la Kijitoupele lipo katika Orodha hiyo. Taarifa hii ipo katika tovuti ya Tume.
• Katika Taarifa hiyo, Tume ilieleza wazi kuwa Majimbo ya Zanzibar yataendelea kuwa hamsini (50), ingawaje Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imeongeza majimbo manne na kuwa Hamsini na Nne (54).
• Tulieza sababu ya kubaki na Majimbo hamsini (50) ni kutokana na matakwa ya Ibara ya 98 (1) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo ili kuongeza idadi ya wabunge kutoka Zanzibar inahitaji theluthi mbili ya Wabunge kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya Wabunge kutoka Zanzibar kuunga mkono mabadiliko hayo.
• Tulieza kuwa, kipindi hicho Tume isingeweza kuandaa na kuwasilisha Muswada Bungeni kwa kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilikuwa linamaliza muda.
• Katika taarifa hiyo, ilifafanuliwa kuwa, ili kubaki na majimbo Hamsini (50), kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, majimbo manne yaliunganishwa kwa ajili ya Uchaguzi wa Wabuge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaotoka Zanzibar.
• Majimbo yaliyounganishwa ni:
1. Jimbo la Bububu liliunganishwa na Jimbo la Mtoni, likaitwa jimbo la Bububu
2. Jimbo la Mwera liliunganishwa na Mto pepo likaitwa jimbo la Mwera
3. Jimbo la Kiembesamaki liliunganishwa na Chukwani likaitwa jimbo la Kiembesamaki
4. Jimbo la Pangawe liliunganishwa Kijitoupele likaitwa Kijitoupele
• Kwa mantiki hiyo Jimbo la Kijitoupele ni mojawapo ya Majimbo hayo (50) ambayo Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilisimamia na kuratibu Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wabunge.
• Tarehe 28 Oktoba, 2015 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitoa taarifa kwa Umma kuwa, ilishapokea Matokeo ya Kura za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa kutoka Majimbo yote ya Zanzibar na siyo “siyo Matokeo ya Ubunge”
• Tarehe 19 Desemba, 2015 Tume ilitoa orodha ya Majimbo ambayo hayajafanya Uchaguzi wa Wabunge tarehe 25 Oktoba, 2015 kutokana na hililafu mbalimbali, mojawapo ya majimbo hayo nane (8), jimbo la Kijitoupele - Zanzibar ni miongoni.
Ni vema wananchi wakafahamu kwamba, Tume ya Taifa ya Uchaguzi haianzishi na haijaanzisha Jimbo jipya la Uchaguzi baada ya Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015.
Hii inaonesha ni kiasi gani Mhariri wa Gazeti la MwanaHALISI alivyodhamiria kuupotosha Umma kwani katika Makala/Taarifa hiyo hiyo ambayo anadai hakuna Jimbo la Kijitoupele (Unguja); anaeleza kuwa tarehe 25 Oktoba 2015 wapiga Kura wa Jimbo la Kijitoupele walikosa fursa ya kumchagua Mbunge. Amemtaja Mhariri wa Gazeti la MwanaHALISI kuwa ni Wapiga Kura wa Jimbo la Kijitoupele, ambalo anadai eti Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeliibua miezi mitatu baada ya Uchaguzi. Huu ni uongo na upotoshwaji wa makusudi kabisa.
Tume inapenda wananchi waelewe kuwa, hata kabla Tume ya Uchaguzi haijafuta matokeo wa Zanzibar, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilikuwa imesha tangaza kuahirisha Uchaguzi katika Majimbo nane (8) likiwemo la Kijitoupele kwa sababu za Vifo vya Wagombea na hitilafu mbalimbali.
Jimbo la Kijitoupele la Zanzibar ni miongoni mwa majimbo nane (8) ambayo yaliahirishwa kufanya uchaguzi wa Wabunge tarehe 25 Oktoba, 2015, ambapo majimbo sita (6) ambayo ni Lushoto, Ulanga Mashariki, Masasi Mjini, Ludewa, Handeni Mjini na Arusha Mjini yaliahirishwa kutokana na vifo vya wagombea na majimbo mawili (2) ya Kijitoupele - Zanzibar na Jimbo la Lulindi – Masasi yaliahirishwa kutokana na hitilafu mbalimbali.
Hoja nyingine iliyotolewa na gazeti hilo ilihusu uteuzi wa Uteuzi wa Wabunge wa Viti Maalum. Ifahamike kwamba katika maamuzi yake kuhusiana na viti maalum, Tume imezingatia matakwa ya Ibara ya 78 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inayoeleza kuwa, ili chama kilichoshiriki Uchaguzi Mkuu kipate Viti Maalum ni lazima kiwe kimepata angalau asilimia tano (5%) ya Kura zote halali za Ubunge. Hivyo, Viti Maalum vilivyobaki haviwezi kugawanywa hadi hapo Jimbo la Kijitoupele litakapofanya Uchaguzi katika tarehe ambayo itaitangazwa
na
Tume hapo baadaye.
Mhariri wa Gazeti la MwanaHALISI alipaswa kufanya uchunguzi na uchambuzi wa kina kuhusu habari aliyoiachapisha ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Viongozi wa Tume ya Uchaguzi ili wapate ufafanuzi wa Majimbo ya Uchaguzi na siyo kutoa Taarifa za uongo, uchochezi na upotoshaji kama walivyofanya.
Mhariri wa Gazeti la MwanaHALISI atambue uandishi wa habari ni zaidi ya kushika kalamu na kuandika, unahusisha uwezo wa kutafuta habari pande zote mbili ili kupata mizania ya habari anayoiandika, kufanya utafiti, kujiridhisha pasipo shaka kuwa habari anayoitoa ni sahihi.
Kwa kuwa Mhariri wa Gazeti la MwanaHALISI alikusudia kuupotosha umma kwa sababu anazozifahamu yeye mwenyewe kwa kutoa Taarifa zisizo sahihi, za uongo na uchochezi Tume ya Taifa ya Uchaguzi inamtaka Mhariri wa MwanaHALISI KUIOMBA RADHI TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI, UKURASA WA MBELE WA TOLEO LIJALO KAMA ALIVYOFANYA KATIKA GAZETI HILO.
Kama wasipofanya hivyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi italichukulia Gazeti la MwanaHALISI hatua za Kisheria.
Imetolewa na
Kailima,R.K
www.shaabanmpalule.blogspot.com
WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA KULIOMBEA TAIFA.
Mwenyekiti wa Good News for All Ministry, Askofu Charles Gadi akizungumza na waaandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu mkutano wa maombi siku ya Jumatano ya tarehe 20 Januari mwaka huu katika eneo la Soko la Samaki Feri ili kuomba Mungu kuepusha ongezeko la joto nchini kushoto ni Katibu wa Good News For All Ministry Mchungaji Palemo Massawe.
Picha na Beatrice Lyimo Maelezo
Na Beatrice Lyimo- Maelezo
MWENYEKITI wa Good News for All Ministry, Askofu Charles Gadi ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kumuomba Mungu dhidi ya hali ya hewa ya joto kali nchini.
Askfou huyo ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar e s Salaam mara baada ya Mamlaka ya hali ya hewa kuonyesha hali ya joto kufika nyuzi joto 35°C.
Askofu Gadi ameongeza kuwa, wanatarajia kufanya mkutano wa maombi siku ya Jumatano ya tarehe 20 Januari mwaka huu katika eneo la Soko la Samaki maarufu kama Feri ili kuomba Mungu kuepusha ongezeko la joto nchini.
“Joto limesambaa katika maeneo ya pwani hususani Dar es Salaam, Tanga, na visiwa vya Zanzibar, hivyo kwa hali hii tumeona tufanye mkutano wa maombi mafupi katika eneo la Soko la samaki la feri siku ya Jumatano kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 6 mchana,
“Mungu amenipa nafasi ya kuomba dhidi ya majanga ya kimazingira kama haya hivyo tunawakaribisha watu wote wa Dar es Salaam tuje tumlilie Mungu kwa pamoja ili tuondokane na janga hili la joto na madhara ya Elnino” alifafanua Askofu Gadi.
Kwa upande wake katibu wa Good News For All Ministry Mchungaji Palemo Massawe amewataka Wananchi kuchukua hatua ili kujikinga dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu kwa kufanya usafi katika mazingira yanayowazunguka.
www.shaabanmpalule.blogspot.com
Meneja wa Mradi wa Kansa ya Shingo ya Kizazi wa UMMATI, Jeremiah Makula akizungumza wakati wa utoaji tuzo kwa wadau wa mradi wa kansa ya Shingo ya Kizazi iliyofanywa, PSI Tanzania, Marie Stopes pamoja na UMATI iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
MWANAMKE AKUTWA KWENYE PAA LA JENGO LA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO JIJINI DAR ES SALAAM LEO.
Manamke ambaye jinalake halikupatikana mara moja akiwa amekaa juu ya paa la majengo ya Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam leo.
Mwanamke huyo akizungumza na watu waliokusanyika ikiwa alikuwa hasikiki vizuri maneno aliyokua akiongea kutokana na wananchi waliokusanyika kumuuliza maswali mengi kwa wakati mmoja.
TANESCO YATOLEA UFAFANUZI MADAI YA WAKAZI WA KIJIJI CHA SESEKO, MKOANI SHINYANGA.
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
SHIRIKA la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) limetolea ufafanuzi kuhusu malalamiko ya Wakazi wa kijiji cha Seseko Kata ya Mwamalili mkoani Shinyanga.
Ufafanuzi huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, Bw. Lusajo Mwakabuku wakati akiongea na Idara ya Habari mara baada ya kuhojiwa kuhusu madai ya wakazi wa kijiji hicho kuhusu kufyekwa kwa mazao yao bila ya kulipwa fidia na Shirika hilo.
Mwakabuku amefafanua kuwa madai ya wakazi wa eneo hilo yamekuwa yakijirudia mara kwa mara licha ya TANESCO kuwalipa fidia kwa wakazi hao tangu mwaka 1999.
Mwakabuku amefafanua kuwa, Madai hayo yanatokana na njia ya msongo wa Umeme wa kilovoti 220 ambayo ni njia inayotokea Shinyanga kuelekea Mwanza na inaonekana hawa wanaolalamika kufyekewa mazao yao ni wale ambao wamevamia ama wameweka makazi yao hivi karibuni katika maeneo hayo kwasababu Shirika la TANESCO lilishawalipa wakazi ambao walipitiwa na nguzo hizo tangu mwaka 1999.
Aidha, Bwana Mwakabuku aliongeza kuwa, TANESCO kabla ya kupitisha nguzo katika maeneo ya makazi ama mashamba ya wananchi huwa wanawasiliana na uongozi wa eneo husika na kukubaliana na wananchi wenyewe ili waruhusiwe kupitisha ama kutopitisha nguzo za umeme, na ilipotokea wanakubaliwa basi fidia inalipwa kwa wakati na kwa kufuata utaratibu ikiwemo kufanya tathmini ya kutosha na kisha kuwalipa kwa wakati kulingana na matakwa ya Sheria.
‘’Wakati mwingine baadhi ya wananchi wamekuwa wasikivu kwa kukubali na kuruhusu kupitisha nguzo za umeme katika maeneo yao na tumekuwa tukiwalipa fidia, lakini kuna wengine wamekuwa wakifanya shughuli za kibinadamu ikiwemo ulimaji mazao chini ya laini za umeme kwa makusudi ili walipwe fidia pindi yakifyekwa, hawa wanakuwa wanavunja utaratibu ambao umewekwa na TANESCO kuwa, ndani ya mita thelathini kwa pande zote mbili ambazo laini zinapita hakutakiwi kufanyika shughuli yoyote ya makazi au maendeleo, hivyo katika ukaguzi wetu tunapofika na kukuta wamekiuka taratibu hizo tunazuia uendelezaji wa shughuli hizo na hasa kubwa likiwa ni suala la usalama wa mali na maisha yao wenyewe wananchi.’’, alisema Mwakabuku.
Amewahasa wakazi nchini kote kuzingatia Sheria ya mita 60 kwa kutofanya shughuli zozote za kibinadamu chini ya nguzo za umeme kwa ajili ya usalama wa maisha yao kwani umeme upitao unakuwa ni wa msongo mkubwa hivyo unaweza kuhatarisha maisha yao endapo wanakaidi kufanya hivyo.
www.shaabanmpalule.blogspot.com
POLISI MKOANI MWANZA YAKANUSHA KUHUSIKA NA UHALIFU
JESHI la Polisi mkoani Mwanza imekanusha kuhusika na uhalifu kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini.
Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Justus Kamugisha alipokuwa akizungumza ofisini kwake kuhusu tuhuma zilizotolewa juu ya Jeshi la Polisi mkoani humo kuhusika na Uhalifu.
Kamanda Justus Kamugisha amesema kuwa kuna taarifa zimekuwa zikitolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Jeshi la polisi mkoani humo linajihusisha na masuala ya uhalifu ikiwemo baadhi ya maofisa wao kushirikiana na wahalifu katika uuzaji wa dawa za kulevya pamoja na kushirikiana na majambazi kupora mali za wananchi .
“Ni habari za uongo na za kulichafua Jeshi la Polisi na mimi kama Kamanda wa Polisi nimelipokea suala hili kwa masikitiko na natoa onyo kwa vyombo vya habari na jamii kwa ujumla kuacha tabia ya kueneza habari sizizokuwa za kweli” Amesema Kamanda Kamugisha.
Aidha Kamanda Kamugisha amesema kuna malalamiko yanayotolewa kuhusu Jeshi la Polisi mkoani hapo kujihusisha na ulanguzi wa bidhaa zinazouzwa kwenye kanteeni za Polisi, taarifa hizo ni za uongo kwani Serikali imeshafuta msamaha wa kodi katika bidhaa hizo ambazo zilikuwa na bei tofauti na zile zilizopo katika maduka ya kiraia.
www.shaabanmpalule.blogspot.com
PESA ZA MAENDELEO YA ELIMU NJOMBE POLISI YAAGIZWA KUSIMAMIWA
Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dr Rehema Nchimbi akiongea na askari wa Mkoa wa Njombe.
WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA DAWA ZA KULEVYA
Madawa ya kulevya yaliyokamatwa mkoani Mbeya.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
www.shaabanmpalule.blogspot.com
WENGI WAJITOKEZA MAZISHI YA ALIYEKUWA MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA
Monday, January 18, 2016
Maoni: 0
Mwili ukiwasili katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazishi.
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa
aliyekuwa Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi, Suleiman Suleiman kabla ya mazishi yake.
TANZIA- TAARIFA YA MSIBA DMV SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA FAMILIA YA SEBO KUTOKA KWA BALOZI LIBERATA MULAMULA MAZISHI YA ALIYEKUWA MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA YAFANYIKA KATIKA MAKABURI YA KISUTU LLEO Shule ya Chipu wajisaidia porini TECNO OWN THE STAGE EPISODE 10 MBUNGE WA JIMBO LA LINDI AENDELEA KUTIMIZA AHADI ZAKE JIMBONI KWAKE MISA YA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU LETICIA NYERERE JAPAN YASAINI MIKATABA YENYE THAMANI YA DOLA 204,300 KWA AJILI YA KUSAIDIA MAENDELEO YA JAMII TANZANIA Tusingempeleka shule asingesombwa na mafuriko-Mama HISTORIA FUPI YA HAYATI PADRI CALISTI NYAMBO ALIYEFARIKI NCHINI MAREKANI AKIFANYA SHUGHULI ZA UTUME UKISHIKWA SHIKAMANA BALOZI MLIMA AKUTANA NA KAIMU BALOZI WA CHINA WEMA SEPETU AWAFUNDA WABUNIFU WA MAVAZI CHIPUKIZI WATAKAOPAMBA LADY IN RED FASHION SHOW 2016 PAPASO WITH DIAMOND PLUTNUMZ PART THREE PAPASO WITH DIAMOND PLATNUMZ PART TWO PAPASO WITH DIAMOND PLUTNUMZ PART ONE WAZIRI SIMBACHAWENE ASIMAMISHA KAZI WAKURUGENZI KATAVI NA KIGOMA Kichupa cha leo John rodgers_MAMA [Official video] LONGA NA VIJIMAMBOBLOG NA DR CRISPIN SEMAKULA PART ONE AND TWO TANZIA: GEORGE SEBO MWENYEKITI WA CCM DMV HATUNAE TENA BREAKING NEWS: WANANCHI WA BONDE LA MKWAJUNI WAFUNGA BARABARA NA KUFANYA FUJO Machungu rungu la Magufuli yaanza.
TANZIA- TAARIFA YA MSIBA DMV
Posted: 18 Jan 2016 12:54 PM PST
Mzee George Sebo enzi ya uhai wake.
Familia ya Sebo inasikitika kutangaza kifo cha mpendwa wao mzee George Sebo kilichotokea leo January 18, 2016 katika hospitali ya Prince George Maryland, Nchini Marekani.
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI ATEMBELEA IDARA YA UHAMIAJI ZANZIBAR. TAXES, ACCOUNTING AND LIFE INSURANCE SERVICES HATUA AMBAZO ZIMECHUKULIWA DHIDI YA STANBIC BANK TANZANIA LIMITED KUHUSU USHIRIKI WAKE KUWEZESHA MKOPO WA SERIKALI WA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 600 RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI AWAASA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU KUSIMAMIA NA KUDUMISHA MILA NA TAMADUNI ZA DINI YAO Peter wa P-Square mgonjwa, anahitaji maombi KIPINDI CHA JUKWAA LANGU KINACHORUSHWA LIVE KILA SIKU YA JUMATATU USIKOSE I WAS LOST, VIDEO MPYA YA ROSE KACHUCHURU Kichupa cha leo Sheikha - Bahati (Official HD Music Video) TCRA kufungia vituo sita vya televisheni, redio 20 Hupandi ndege bila barua, kibali cha Ikulu Wataka Mwinyi, Mkapa, JK wapunguziwe mishahara UCHAMBUZI WA MAGAZETI WAJAPANI KUWEKEZA KWENYE UZALISHAJI UMEME NCHINI DAWASCO YABAINI WIZI WA MAJI KIWANDA CHA BAHARI CHEMICALS LTD SERIKALI YALIFUTA GAZETI LA MAWIO YALIYOJIRI KWENYE MECHI YA SIMBA NA MTIBWA SUGAR KATIKA PICHA Wakazi New Video: Kanuni Za Hela CUF kuandamana Pemba kisa Hamad.
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI ATEMBELEA IDARA YA UHAMIAJI ZANZIBAR.
Posted: 17 Jan 2016 10:16 AM PST
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Hamad Masauni, akisalimiana na Maofisa wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar wakati wa ziara yake kutembelea Idara hiyo ya Uhamiaji Zanzibar.kushoto Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar.
TIGO YAFUNGUA DUKA LA KISASA SAME 'Mgonjwa wa Magufuli' afungwa Muhimbili KIKWETE NA MWAKILISHI MAALUM WA MAREKANI Barakah Da Prince - SIWEZI [Official Music Video] Tuhuma mpya Bandari DONDOO ZA MAGAZET SHEREHE MURWA YA JAMBO LEO YA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA 2016 IYK - Columbus, Ohio | Karibuni Ibada ya Kiswahili | Jumapili hii 17 Januari 2016 | Kuanzia saa Kumi kamili jioni Kichupa cha leo Single sally Ft mesen selekta - Cossovo BREAKING NEWS: CHADEMA YANYAKUWA KITI CHA MEYA WA KINONDONI, NI BONIFACE JACOB MGODI WA BUZWAGI WAPONGEZWA KWA KUZINGATIA SHERIA ZA MAZINGIRA JE WEWE NI MSANII NA UNAKAZI YAKO UNAHITAJI KUUZA??? SERIKALI YAWATAKA WANANCHI WALIOVAMIA ENEO LA KAMBI WA WAZEE NUNGE KUSITISHA UJENZI RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AMPIGA CHINI KATIBU TAWALA MWANZA DK. SHEIN AWAAPISHA MAKATIBU, MANAIBU NA MSHAURI WA RAIS IKULU LEO UZINDUZI WA ‘STIKA’ MAALUM YENYE UJUMBE WA KUTOKOMEZA MAUAJI YA WATU WENYE ALBINISM SERIKALI YAWATAKA WATOA HUDUMA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA WASAJILIWE NA BARAZA LA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA HALI HALISI YA BARABARA YA "MARKET STREET" JIJINI MWANZA. WHAT'S GOING ON WITH DICOTA? ISUZU JOURNEY BUSES FOR SALE MAKAMU MWENYEKITI WA CCM (BARA) AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA CHINA LUMUMBA LEO
TIGO YAFUNGUA DUKA LA KISASA SAME
Posted: 16 Jan 2016 12:20 PM PST
Katibu wa wilaya ya Same Mhe. Evagry Keiya (katikati)akikata utepe kufungua duka la Tigo Same, wanaoshuhudia ni Meneja wa huduma kwa wateja Tigo, Mwangaza Matotola(kushoto) na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia) mapema mwishoni wa wiki iliyopita
KITUO CHA UTAFITI CHA RCRSDS KUZINDUA MFUMO WA KIELEKTRONIKI WA KUKUSANYA, KUHIFADHI TAARIFA ZA KITAFITI ZA UWAJIBIKAJI WA TAASISI ZA BINAFSI NA UMMA KESI YA KUPINGA MATOKEO INAYOMKABILI MBUNGE WA JIMBO LA BUNDA MJINI MKOANI MARA YAAHILISHWA. TAXES, ACCOUNTING AND LIFE INSURANCE SERVICES KHUTBA YA IJUMAA SUBRA -SH MSELLEM BIN ALLY KIGAMBONI BRIDGE MSIBA Kichupa cha leo Pam D Ft Mesen Selekta - Popo lipopo (Official Video) PROF. MUHONGO ASIMAMISHA SHUGHULI ZA KAMPUNI YA OFF - ROUTE TECHNOLOGY ILIYOPO KYELA DKT. KIJAJI ATOA SIKU 3 KUPATA MIKAKATI YA NAMNA YA KUTATUA SUALA LA UBADILISHANAJI WA FEDHA UNAOFANYWA KIHOLELA (BLACK MARKET) TUNDUMA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI YATOKA YATIZAME HAPA Tanzania on Top in terms of mobile money usage in Africa KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI MJI KAHAMA YAIMBUA MAMBO MAKUBWA Lowassa: Najiandaa kwa uchaguzi 2020 Elimu bure kaa la moto D’ salaam Mishumaa ya kale LIIIIVE Ijumaa 5:00pm EST USIKOSE Walioozesha watoto miaka 13 kukamatwa Skylight Band wafunika Usiku wa Mameneja Maisha Basement DONDOO ZA MAGAZETI MATUKIO MBALIMBALI YA MAHAFALI YA 18 YA CHUO CHA KIMATAIFA CHA DIPLOMASIA DAR ES SALAAM JUZI MUME WA MWANAMUZIKI CELINE DION AFARIKI DUNIA Wahamiaji haramu 48 wafukuzwa
KITUO CHA UTAFITI CHA RCRSDS KUZINDUA MFUMO WA KIELEKTRONIKI WA KUKUSANYA, KUHIFADHI TAARIFA ZA KITAFITI ZA UWAJIBIKAJI WA TAASISI ZA BINAFSI NA UMMA
Posted: 15 Jan 2016 12:34 PM PST
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Utafiti wa Shughuli za Maendeleo ya Jamii Tanzania (RCSDS),Abraham Shempemba (kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo , kuhusu mafanikio ya tafiti zao walizozifanya zinazoonesha takwimu za misaada iliyotolewa kisekta, gharama zilizotumika, uwajibikaji wa jamii na jinsi ilivyonufaika. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa kituo hicho, Chrizostom Thadeo.
(PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
KITUO cha Utafiti wa shughuli za maendeleo ya jamii Tanzania(RCSDS), kinatarajia kuzindua mfumo wa kielektroniki wa kukusanya, kuhifadhi na kuweka angani taarifa za kitafiti za uwajibikaji wa taasisi za binafsi, za umma na watu binafsi serikali kuu na za mitaa na hata mtu mmoja mmoja.
‹
›
Home
View web version