Pages

Sunday, September 21, 2014

YANGA SC, STEND UNITED, POLISI MORO ZAHENYESHWA UFUNGUZI LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA 2014/2015 KWA KUDONDOKEA PUA.

KLABU za Yanga, Polisi Moro, Stend United na Kagrera Sugar zimeambulia vipigo tofauti katika michezo ya ufunguzi wa ligi kuu Tanzania msimu wa 2014/2015.

Yanga ilipoteza mchezo wake dhidi ya Mtibwa Sugar uwanja wa Jamhuri kwa kufungwa bao 2-0 huku Ndanda FC ikiisambaratisha Stend United uwanja wake wa nyumbani Shinyanga kwa kuhenyesha kwa kupata ushindi wa bao 4-1 wakati Polisi Moro SC nayo ilikiona cha mtema kuni mbele ya Azam FC kwa bao 3-1 jijini Dar es Salaam.

Mbeya City ilishindwa kuitumia vema uwanja wa Sokoine mbele ya JKT Ruvu kwa kumalizika mchezo kwa sare tasa ya 0-0 wakati Mgambo ilifanikiwa kuifumua Kagera Sugar kwa bao 1-0 mkoani Tanga na Prinson ikaizabua JKT Shooting kwa kuilaza bao 2-1 katika uwanaj wa Mabatini mkoani Pwani.

No comments:

Post a Comment