TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, January 2, 2012

Youssou N'dour atangaza kuwania urais

Mwanamuziki mashuhuri wa Senegal Youssou N'dour atangaza kugombea urais dhidi ya rais wa sasa Abdoulaye Wade. 

Msimamo wa Ligi Kuu ya England

MTGPNT
1Man City193745
2Man Utd193245
3Tottenham181539
4Chelsea201437

5Arsenal20836

6Liverpool19934
7Newcastle19130
8Stoke20-929
9Norwich20-525
10Everton18-124
11Swansea20-323
12Aston Villa20-423
13Fulham20-423
14West Brom19-822
15Sunderland19121
16Wolves20-1417
17QPR20-1617

18Wigan19-2015
19Blackburn20-1414
20Bolton19-1913

SHEREHE ZA MWAKA MPYA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI ZIMBABWE

 
Usiku wa kuamkia tarehe 1 Januari 2012, Jumuiya ya Watanzania, maafisa wa Ubalozi pamoja na waalikwa kutoka Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na Balozi wa Malawi na Balozi wa Ethiopia nchini Zimbabwe walihudhuria hafla ya kukaribisha mwaka mpya.
katika picha ya juu Mhe. Balozi Adadi akishereheka na watanzania.Mhe. Balozi Adadi akiteta jambo na wageni wake ambao ni Balozi wa Malawi na Balozi wa Ethiopia.
Watanzania na waalikwa wengine wakipata chakula sambamba na kuukaribisha mwaka mpya. katika Ubalozi wa Tanzania Harare

Waziri Dk Mwinyihaji Makame akutana na wabunge wa Afrika Mashariki

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais na menyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Mwinyihaji Makame,alipokuwa kaizungumza na Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki,walipofika ofisini kwake Ikulu Mjini Zanzibar jana,Wabunge hao walisisitiza juu ya wananchi kupewa elimu ya kutosha kuhusu Jumuiya hiyo na shuhuli zake kwa wajumbe,(kutoka Kulia) Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Wazanzibari wanaoishi Uhaibuni,Khamis Ali,Mbunge Dk Said Kharib Bilal na Mbunge Bi Septuu Mohamed. (02/1/2012)
(Picha na Ramadhan Othman Ikulu).

MATUMLA AMGALAGAZA CHEKA KWA POINTI

Mohamed Matumla Kushoto na Cosmas Cheka wakioneshana uwezo wa kutupa Masumbwi jana huko mkoani Morogoro
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akikingiana ngumi na Rais Wa PST Emanuel Mlundwa kabla ya kuanza kwa mpambano jana
kutoka kushoto ni Rashid Matumla,Mohamedi Matumla,Mbwana Matumla na Mkwanda Matumla (picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

FAMILIA TANO ZAWAKAMBIA MORANI, ZAOGOPA KUTEMBEZWA MITAANI UCHI

Familia tano zenye watoto zaidi ya ishirini zimelazimika kukimbia makazi yao ya kudumu kwa kipindi cha wiki tano sasa kwa kuhofia kutembezwa uchi na kupigwa na vijana wa kabila la kimasai”Morani”mara baaada ya kufanya ibada sanjari na kufanya tohara kwa njia za kisasa zaidi
Familia hizo zimelazamika kufanya hivyo kwa kuhofia maisha yao pamoja na maisha ya watoto wao ambapo kundi kubwa la vijana wa kimasai wanawatafuta kwa makosa ya kuharibu na kuvunja mila zao kwa njia ya Sala pamoja na Kufanya tohara Mahospitalini.
Hayo yametokea katika eneo la Oljoro Mkoani hapa ambapo kwa muda wa wiki tano familia hizo zimelazimika kukimbia makazi yao kwa kuhofia kutembezwa mitaani Uchi, pamoja na kupigwa kipigo kikali.
Akiongea na WAANDISHI WA HABARI mmoja wa wanafamilia waliolazimika kukimbia nyumba zao kwa hofu ya kutembezwa mitaani Uchi Bw Korduni Wilson, alisema kuwa Morani hao wamekuwa wakifanya vibaya sana kwa kuwa mila wanazozitaka zina madhara sana.
Bw Korduni alieleza kuwa wameamua kufikia uamuzi huo wa kukimbia nyumba zao kwa kuwa wao tayari wameshajua na kufahamu madhara ya kufanya tohara kwa njia ya kienyeji sanjari na kuabudu mila ambazo Morani hao wanazitaka.
“kati ya hizi familia tano nyinginezo hazijakimbia kwa kuwa wamefanya tohara kwa watoto wao bali Morani hao wamekuwa wakidai kuwa wanaharibiwa mambo ya Kimila hasa pale wanaposali kwa maana hiyo wanakataa hata makanisa kwa kuhofia Matambiko, na Mila”aliongeza Bw Korduni.
  
Pia aliongeza kuwa mara baada ya Morani hao kuona kuwa Kanisa linakubali na kusisitiza waumini wake kufanya Tohara kwa njia ya kisasa sanjari na kukataa Mila ambazo zina madhara kwa Mtanzania Morani hao waliktaa amri hiyo na kuvunja Kanisa la T.A.G oljoro hali ambayo ilisababisha hasara kubwa sana.
Katika hatua nyingine Msimamizi na Muangalizi wa makanisa ya T.A.G mkoani hapa Bw Simion Vomo alisema kuwa wao kama kanisa hawataweza kuwasikiliza Morani hao kwa kuwa madai yao hayana Msingi Kisheria
Aliongeza kuwa Kanisa litalazimika kuchukua hatua kali na za kisheria,kwa kuwa Morani hao wanasababisha amani ndani ya miji na Maboma ya wananchi kukosekana hali ambayo kama haitaweza kuchukuliwa tahadhari basi itazaa matatizo makubwa sana katika jamii.
Awali Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Bw. Akili Mpwapwa alisema kuwa bado polisi wanaendelea na Upelelezi,hivyo familia hizo tano ambazo zimelazimika kukimbia makazi yao kwa kuwahofia Morani hao, wanatakiwa kutoa Taarifa ili Sheria ichukue mkondo wake kwa kuwa wanachokifanya Morani hao ni Makosa.(Na:Shaaban Mpalule)

Shule ya kufundishia mpira yapata msaada wa vifaa vya michezo.

Na Gladness mushi , Arusha. SHULE ya kufundisha mpira wa miguu ijulikanayo kama Future Stars Academy iliyopo jijini hapa imenufaika na msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya shs, 4.5 milion. Msaada huo umetolewa na wafadhili kutoka chama cha mpira cha vijana jimbo la Florida Marekani ikiwa ni njia mojawapo ya kuchangia swala zima la michezo kwa shule hiyo. Akizungumzia kuhusiana na shule hiyo , Mkurugenzi wake, Alfred Itaeli alisema kuwa, lengo la shule hiyo ni kufundisha michezo kwa wanafunzi waliopo mashuleni ambapo wanafunzi zaidi ya 152 kutoka shule mbali mbali za mkoa wa Arusha wanafundishwa michezo katika shule hiyo. Alisema kuwa, shule hiyo iliazishwa kwa lengo la kuinua vipaji vya michezo kwa wanafunzi ambapo hadi sasa wana jumla ya timu sita kuanzia umri wa miaka 11 hadi 17 . Itaeli alisema kuwa, shule hiyo ilianzishwa mwaka 2009 likiwa na lengo la kuwaweka wanafunzi pamoja ambapo wanajifunza mpira wa miguu . Ambapo mwaka jana wanafunzi hao wamefanikiwa kushiriki mchezo wa kikombe cha ligi ya Afrika Mashariki ambapo mchezo huo ulifanyikia Nairobi na ilizishirikisha jumla ya timu 94 ambapo timu hiyo ya Future stars Academy ilifanikiwa kushinda nusu fainali ambapo lengo lao ni kuchukua kombe . ‘pamoja na kuwa sisi tunajitahidi sana kuleta maendeleo ya michezo katika jamii yetu kwa ujumla bado changamoto ni nyingi sana zinazotukabili ,hivyo tunaomba watu binafsi na mashirika wajitokeze kwa wingi kuchangia vifaa mbalimbali vya michezo kwani hivi bado havitoshelezi ikilinganishwa na kuwa uhitaji ni mkubwa sana’alisema Itaeli. Alitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni apmoja na ukosefu wa viwanja vya michezo na vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuendeleza vijana hao kwani michezo imeweza kwa kiasi kikubwa sana kuwaondoa katika changamoto mbalimbali zikiwemo za kuondokana na makundi yasiyofaa(Na :Mwandishi Wetu)

MDAU WA WWW.ELIMUBORA.COM AMALIZA KOZI YA WEB DESIGN

Evance ambae anaratibu website ya www.elimubora.com akiwa anapokea cheti baada ya kuhitimu kozi fupi nchini India. Amewataka watanzania hususan wadau wa masuala ya IT kufuatilia udhamini mbalimbali wa kozi fupi utolewao na chuo hicho kwa taarifa zaidi ingia katika libeneke lake la www.elimubora.com

RAIS JAKAYA AWAAPISHA MAKATIBU WAKUU WAWILI NA NAIBU KATIBU MKUU MMOJA IKULU DAR LEO

Rais Jakaya Kikwete aklimwapisha Mh Eliakim C. Maswi kuwa Katibu Mkuu wizara ya Nishati na Madini katika hafla iliyofanyika Iukulu leo jijini Dar es salaam. (PICHA ZOTE NA IKULU) Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, akimpongeza na kumkabidhi zawadi ya ua Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Eliackim Chacha, baada ya kuapishwa leo Ikulu Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Ikulu, Susan Paul, Katibu Mkuu Ikulu, Peter Alanambula Ilomo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliackim Chacha, kabla ya kuapishwa wakati Makamu akiingia katika Ukumbi huo kwa ajili ya kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa makatibu hao walipokuwa wakisubiri kuapishwa rasmi kushika nafasi hizo Ikulu Dar es Salaam leo Januari 2, 2012.
Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Naibu wake, Adam Malima, Katibu Mkuu wa wizara hiyo aliyeapishwa leo Januari 2, 2012, Ikulu Dar es Salaam pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara hiyo baada ya kuapishwa Katibu huyo.
Rais Jakaya kikwete akimwapisha Mh Peter Ilomo kuwa Katibu Mkuu Ikulu PICHA NA IKULU
Rais Jakaya Kikwete akimwapisha Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mh Suzana Mlawi PICHA NA IKULU
Rais Dk. Jakaya Kikwete wa pili wa tatu kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa rais Dk. Gharib Bilal wa pili kutoka kushoto na makatibu walioapishwa leo kutoka kulia ni Mh Peter Ilomo Katibu Mkuu Ikulu, Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mh Suzana Mlawi,Balozi Ombeni Sefue katibu mkuu kiongozi na mwisho kushoto ni Mh Eliakim C. Maswi Katibu Mkuu wizara ya Nishati na Madini (Mwandishi Wetu).

UWF yatoa msada kwa familia iliothirika na mafuriko huko kigogo mji mpya

Mwenyekiti wa UWF - Unity Of Women Friends,Mwate Madinda akikabidhi kiasi cha fedha taslim kwa familia ya Mzee Shaaban Mkana,ambao walithirika na mafuriko huko Kigogo mji mpya,jijini Dar,pamoja na kukabidhi kiasi cha fedha pia UWF walitoa msaada wa vifaa, chakula na vitu mbalimbali,mwishoni mwa wiki,Kushoto kwa Mwenyekiti ni Mwenyekiti wa mradi wa SOMKI (somesha mtoto wa kike),Maryam Shamo pamoja na mwanachama wa UWF,Bi.Galina Ajmy.
UWF - Unity Of Women Friends wakijumuika na marafiki wa karibu na kukabidhi misaada ya vifaa, chakula na fedha taslim kwa familia ya mzee Shaaban Mkana ambao waliathirika na mafuriko huko Kigogo mji mpya,mwishoni mwa wiki.
Kikundi cha UWF kimejikita katika kuwakomboa watoto wa kike wasio na uwezo katika kupata elimu kupitia mradi wao wa SOMESHA MTOTO WA KIKE (SOMKI), pia wamejiwekea utamadumuni wa kutembelea vituo mbali mbali kama hospitali, vituo vya kulelea watoto n.k. kuwafariji wakati wa sikukuu mbali mbali.Ukitaka kuona kazi mbalimbali zilizowahi kufanywa na UWF,(Mwandishi Wetu)