TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, August 23, 2014

Real Madrid Legends yainyuka Tanzania 3-1

 Rais Jakaya kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Tanzania 11
 Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Real Madrid Legends.
 Luis Figo (kushoto), akiruka juu kupiga mpira wa kichwa.
 Hekaheka langoni mwa Tanzania.
 Mohamed Mwameja akiwa ameshika kiuno baada ya kufungwa goli la kwanza.

 Rais Jakaya Kikwete akifurahia jambo na kocha Msaidizi wa Tanzania 11, Jamhuri Kiwhelo 'Julio' mara baada ya mchezo.
 Kiungo wa timu ya Real Madrid Legends, Christian Karembeu akichukua picha ya kumbukumbu na Rais Jakaya Kikwete.
 
Nzuri sana........
Mfunga wa mabao ya timu ya Real Madrid, Reuben akipokea mpira baada ya kupiga 'hat trick' katika mchezo huo.
Beki wa timu ya Tanzania 11, Shadrack Nsajigwa akichuana na mshambuliaji wa Real Madriad Legends, Luis Figo wakati wa mchezo wa Kimatifa wa Kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Mshambuliaji wa timu ya Real Madriad Legends, Luis Figo akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa Tanzania 11 wakati wa mchezo wa Kimatifa wa Kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Mshambuliaji wa timu ya Real Madriad Legends, Luis Figo akimiliki mpira mbele ya beki wa Tanzania 11, Shadrack Nsajigwa wakati wa mchezo wa Kimatifa wa Kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 
Rais Jakaya Kikwete akikabidhi kombe kwa mchezaji wa Real Madriad Legends baada ya kuibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Tanzania 11 katika mchezo maalum wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)


 Benchi la ufundi la Tanzania 11
 Luis Figo akisalimiana na wachezaji wa Tanzania 11.

 Peter Manyika akisalimiana na Luis Figo.

VILIO VYATAWALA MAZISHI YA MAMA MKWE,MKWEWE

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Peter Kakamba
 
Vilio na simanzi viligubikwa katika vijiji vya Ililika na Nyashihima wilayani Geita wakati wa mazishi ya wanawake wawili mama na mkwewe mjamzito waliouawa kwa kukatwa mapanga usiku wa Jumanne katika kijiji cha Ililika.
Miili hiyo ya Nyanjige Mutula (70) na Grace Hayo (18) aliyekuwa mjamzito, ilizikwa katika vijiji tofauti juzi saa 12 jioni kwa hofu ya mwili wa Grace kuharibika baada ya kufanyiwa upasuaji wa kutoa kichanga cha miezi mitano kwenye Kituo cha Afya Kashishi.

Tukio hilo lililoibua hofu kwa  wananchi wa vijiji na kata za Kamena, Nyakamwaga, Lwamgasa na Nyarugusu, walisema mauaji hayo yanahusiana na imani za kishirikina.

Akizungumzia mauaji hayo baada ya maziko, Afisa Mtendaji wa kijiji cha Ililika, Fabian Mugeta, alisema mikakati ya kuwapigia kura za siri watuhumiwa wa tukio hilo, ilikuwa ikiendelea.

Mugeta alisema ililazimika mwili wa Grace kufanyiwa upasuaji kabla ya kusafirishwa kwenda kijijini kwao katika kijiji cha Nyashihima na mwili wa binti huyo kuzikwa tofauti na kichanga chake.

Marehemu Mulita alizikwa katika kijiji cha Ililika kitongoji cha Mwabasabi kulikotokea mauaji hayo, na kuhudhuriwa na baadhi ya wananchi, ndugu na viongozi wa kijiji.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Peter Kakamba, alisema mpaka sasa hakuna mtuhumiwa yeyote aliyekamatwa kufuatia tukio hilo la kinyama lililotokea hivi karibuni.
 
CHANZO: NIPASHE

MWANDISHI WA HABARI ALIFUNGULIA KESI BUNGE MAALUMU LA KATIBA KATIKA MAHAKAMA KUU.

 
Mwenyekiti wa bunge maalumu la katiba Samwel Sitta.

“Ni jambo ambalo ameomba mwenyewe kuhamia huko na ameruhusiwa maana hilo ni jambo la kawaida kama ambavyo wajumbe wengine kama kina Freeman Mbowe waliwahi kuomba, siyo jambo geni.” Hamad Rashid Mohamed

Dar es Salaam/Dodoma. Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma kwa sasa liko katika hatihati ya kuendelea baada ya kufunguliwa kesi ya kuhoji madaraka yake.

Kesi hiyo ilifunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana na Mwandishi wa Habari Saidi Kubenea, kupitia kwa wakili wake Peter Kibatala, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Katika kesi hiyo iliyopewa usajili wa namba 28 ya mwaka 2014, Kubenea anaiomba mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya Mamlaka ya Bunge la Katiba. Kubenea amefungua kesi hiyo akiomba mahakama itoe tafsiri hiyo, chini ya vifungu vya 25 (1) na 25 (2) vya Sheria ya Marekebisho ya Katiba namba Namba 83 ya mwaka 2011.

Sambamba na kesi hiyo ya kuomba tafsiri ya mamlaka ya Bunge hilo, pia Kubenea amewasilisha maombi mahakamani hapo akiiomba mahakama itoe zuio la muda la kusimamisha Bunge hilo ili kusubiri uamuzi wa maombi ya tafsiri hiyo.

Maombi hayo ya kusimamisha Bunge hilo kwa muda yaliyopewa usajili wa namba 29 ya mwaka 2014, pamoja na maombi ya msingi ya tafsiri ya mamlaka ya Bunge yote yalifunguliwa mahakamani hapo jana chini ya Hati ya Dharura.

Katika kesi hiyo ya msingi anaiomba Mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya masharti ya vifungu hivyo vya sheria hiyo na pia itamke kama Bunge hilo lina mamlaka ya kubadilisha maudhui ya Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kwa kiwango gani.

Kwa mujibu wa hati ya madai, Kubenea anadai kuwa msingi wa kesi hiyo unatokana na uamuzi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Desemba Mosi, 2011, lililopitisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Anasema sheria hiyo ilikuwa na lengo la kuratibu mchakato wa kutungwa kwa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Anaendelea kusema kuwa kutokana na sheria hiyo, Rais aliunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba pamoja na mambo mengine vilevile kukusanya maoni ya wananchi kuhusu mapendekezo ya Katiba Mpya na kwamba kwa msingi huo Tume hiyo iliandaa Rasimu ya Katiba.

Anadai kuwa baada ya Tume hiyo kuundwa iliendelea kukusanya maoni ya wananchi yaliyotolewa katika mikutano ya hadhara na katika miundo tofauti ikiwamo mabaraza ya Katiba yaliyoanzishwa kila wilaya kwa lengo hilo.

Hati hiyo inaendelea kueleza kuwa kwa mujibu wa takwimu halisi za tume hiyo, jumla ya watu 333,537 walitoa maoni yao katika nyanja tofauti, tofauti za mapendekezo ya Katiba, ambayo ndiyo Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyatumia kuandaa Rasimu ya Katiba Mpya.

Inaendelea kueleza hati hiyo kuwa baada ya Rais kukabidhiwa rasimu ya mwisho Desemba 8, 2013, kwa mujibu wa vifungu vingine vya sheria hiyo, aliunda Bunge la Katiba kwa lengo la kujadili Rasimu ya Katiba na hatimaye kupata Katiba Mpya.

Hata hivyo, kwa mujibu wa hati hiyo baada ya Bunge la Katiba kuundwa, mjadala uliibuka ndani na nje ya misingi ya kisheria kuhusu mamlaka yake, kama Bunge linaweza kwenda kinyume na Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na tume hiyo.

Inaendelea hati hiyo kubainisha kuwa mjadala huu pia uliibuka ndani ya Bunge la Katiba lenyewe kuhusiana na mamlaka yake katika utekelezaji wa majukumu yake kama lina mipaka au la kwa mujibu wa vifungu hivyo 25 (1) na 25 (2) vya sheria hiyo.

Katika kusisitiza mjadala kuhusu mamlaka ya bunge hilo, hati hiyo inatoa mfano wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) katika mkutano wake wa mwaka, ambacho kilisema kuwa vifungu hivyo havilipi bunge hilo mamlaka ya kubadili rasimu hiyo.

Hati hiyo inaongeza kuwa wakati TLS wakitoa msimamo huo, kuna wataalamu wengine wa sheria wanadai kuwa Bunge hilo linaweza kubadilisha na kuongeza ibara kadri itakavyoona inafaa bila kujali rasimu hiyo.

Kwa mujibu wa hati hiyo, mvutano huo ndani ya Bunge hilo ulisababisha baadhi ya wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutoka nje na kususia vikao, wakidai kuwa rasimu hiyo haiwezi kubadilishwa. Msimamo huo wa wajumbe wa Ukawa, kwa mujibu wa hati hiyo ni tofauti na wajumbe wengine waliobaki wanaodai kuwa Bunge hilo lina mamlaka ya kubadili vifungu vya rasimu.

Kwa mujibu wa hati hiyo, utungaji wa Katiba ni jambo la kitaifa ambalo si tu kwamba linabeba matumaini ya Watanzania bali pia linabeba mustakabali na ustawi wa nchi.

Hivyo, hati hiyo inaeleza kuwa tafsiri sahihi ya mamlaka ya Bunge la Katiba dhidi ya Rasimu ya Katiba ni jambo muhimu sana katika kuongoza mchakato huo ili kuhakikisha kuwa unakwenda kwa mujibu wa sheria zinazohusika.

Katika hati ya maombi, Kubenea anaomba mahakama itoe amri ya kusimamisha kwa muda vikao vya Bunge la Katiba vinavyoendelea Dodoma, kusubiri uamuzi wa Mahakama kuhusu mamlaka yake.

Katika hati ya kiapo chake aliyoiambatanisha na kesi na maombi hayo, Kubenea anadai kuwa hata baada ya Wajumbe wa Ukawa kutoka nje, wajumbe waliobaki wanaendelea kujadili rasimu hiyo.

Hati hiyo ya kiapo inaeleza kuwa kufunguliwa kwa kesi hiyo sambamba na maombi hayo ya kusimamisha kwa muda Bunge la Katiba si tu kunalenga kupata tafsiri ya Kimahakama kuhusu mamlaka ya Bunge la Katiba.

Rafu Kamati za Bunge Maalumu
Wakati kesi hiyo ikifunguliwa, kumekuwa na taarifa ndani ya kamati za Bunge zinazoendelea kuchambua rasimu hiyo zinazoeleza kuchezwa rafu ili kuwezesha upatikanaji wa akidi kwa ajili ya hatua ya kupiga kura kupitisha ibara za rasimu hiyo katika baadhi ya kamati.

Hivi sasa kamati nyingi ziko katika hatua ya kupiga kura ili kupitisha ibara za Rasimu ya Katiba, kazi ambayo inahitaji theluthi mbili ya wajumbe kutoka pande za muungano kwa mujibu wa kanuni za Bunge Maalumu.Ili kutimiza matakwa hayo, gazeti hili limebaini kuwa rafu zimeanza kuchezwa hasa katika kamati ambazo zimeshindwa kutimiza sharti hilo. Moja ya rafu hizo ni ile ya mjumbe wa Kamati namba tano, Maida Hamad Abdallah kuhamishiwa kinyemela katika Kamati namba 8, kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kuwezesha upatikanaji wa akidi katika kamati aliyohamia.

Habari zinasema mjumbe huyo kutoka Zanzibar alishiriki kupiga kura juzi mchana na wajumbe wa kamati hiyo walielezwa kuwa amepelekwa ili kuziba nafasi ya Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum ambaye hawezi kushiriki vikao hivyo kutokana na kwamba ni mgonjwa.

Hata hivyo, suala hilo lilizua mvutano kiasi baada ya baadhi ya wajumbe kuhoji uhalali wa uhamisho huo ambao ni kinyume cha kanuni za Bunge Maalumu, hasa ikizingatiwa kwamba alipigia kura mambo ambayo hakushiriki kuyajadili na kuyafanyia uamuzi.

Mwenyekiti wa Kamati namba tano, Hamad Rashid Mohamed alithibitisha Abdallah kuhamia kamati namba nane inayoongozwa na Naibu Spika wa Bunge la Muungano, Job Ndugai kwa maelezo kwamba aliomba mwenyewe.

“Ni jambo ambalo ameomba mwenyewe kuhamia huko na ameruhusiwa maana hilo ni jambo la kawaida kama ambavyo wajumbe wengine kama kina Mbowe (Freeman) waliwahi kuomba, siyo jambo geni,” alisema Rashid.

Hata hivyo, Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad alisema hakuwa na taarifa za uhamisho huo. Alipoulizwa kuhusu iwapo Kanuni zinaruhusu alisema suala la kupanga ujumbe wa kamati liko chini ya mamlaka ya mwenyekiti wa Bunge hilo.

“Kwa kweli sifahamu na wala sina taarifa hiyo, hilo suala la kanuni pengine hebu zisome ili ufahamu zinasemaje kuhusu mjumbe kuhama kutoka kwenye kamati moja kwenda kamati nyingine,” alisema Hamad.

Wajumbe wa Bunge Maalumu waliokwisharipoti wanakaribia 450, idadi ambayo ni zaidi ya theluthi mbili ya akidi inayotakiwa, lakini hali ni tofauti kwenye kamati kutokana na sababu mbalimbali, utoro ikiwa mojawapo.

Kutokana na mwenendo huo na wajumbe wengi kutoingia kwenye vikao licha ya kuripoti, kuna wasiwasi iwapo akidi itapatikana wakati wa kupitisha rasimu hiyo wakati Bunge Maalumu litakapoanza kukutana kwa umoja Septemba 2 mwaka huu.

Matakwa ya kanuni
Kanuni ya 55 (1) ya Kanuni za Bunge Maalumu Toleo la 2014 inasema: “Kamati zinaundwa na mwenyekiti kwa namna ambayo itawezesha kila mjumbe kuteuliwa kuwa mjumbe wa kamati mojawapo.”

Fasili ya pili ya kanuni inasema wakati wa kufanya uteuzi wa wajumbe hao, mwenyekiti atazingatia kwa kadri inavyowezekana idadi ya wajumbe inalingana kwa kila kamati na uwiano kutoka pande zote za muungano.

Kadhalika kanuni hiyo inasema katika uteuzi wake mwenyekiti atazingatia idadi ya kila aina ya wajumbe ilivyo katika Bunge Maalumu, jinsia, wajumbe wenye mahitaji maalumu na uwepo wa wajumbe wenye utaalamu wa sheria.

Kanuni hiyo iko kimya kuhusu uhamishaji wa wajumbe na fasili yake ya nne inasema: “Ujumbe katika kamati utadumu kwa kipindi chote cha maisha ya Bunge Maalum.”

Waraka wa uchambuzi wa mgawanyo wa wajumbe katika kamati unaonyesha kuwa Kamati namba tano alikotoka Maida ina wajumbe 52 na kati yao 34 wanatoka Tanzania Bara na 18 Zanzibar wakati kamati alikohamia pia ina wajumbe 52; 35 kutoka Tanzania Bara na 17 kutoka Zanzibar.
Kwa maana hiyo hata kama uhamisho wa Maida ungekuwa na lengo la kuimarisha uwiano kwa maana ya pande za muungano, ni dhahiri kwamba unaathiri kwa maana ya idadi wajumbe kutoka Zanzibar katika kamati namba tano.
Gazeti hili lilimtafuta Ndugai kwa lengo la kupata maelezo jinsi alivyompokea mjumbe huyo, lakini kutwa nzima ya jana simu yake ilikuwa ikiita bila majibu. Kadhalika Maida naye alitafutwa lakini simu yake ilikuwa imezimwa wakati wote. Maida hakuwamo kwenye kamati yake ya awali namba nne ilipokutana jana mchana baada ya kuwa wamepumzika asubuhi kupitia sura za nyongeza.
Kupitisha uamuzi
Kanuni hizo pia zinaelekeza kwamba wakati wa kupitisha uamuzi lazima wajumbe wawe wamefikia theluthi mbili kwa pande zote za muungano, jambo ambalo limekuwa gumu kutokana na mahudhurio hafifu kwenye kamati

Friday, August 22, 2014

Naibu Waziri Fedha aifagilia UTT Microfinance

Naibu Waziri wa Fedha Mwiguru Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wakuu wa Taasisi ya kifedha ya UTT Microfinance, baada ya kukata utepe kuzindua taasisi hiyo, Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kifedha ya UTT Balozi Fadhil Mbaga (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Bw. James Washima wakimwangangalia Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Mwiguru Nchemba.

Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mwiguru Nchemba (wa pili kushoto), akikata utepe kuzindua rasmi Taasisi ya huduma za Kifedha ya UTT Microfinance, Dar es Salaam jana. Wa pili Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi Balozi Fadhili Mbaga na Mtendaji Mkuu wa UTT, Bw. James Washima (kushoto).
 Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mwiguru Nchemba (wa pili kushoto), akikata utepe kuzindua rasmi Taasisi ya huduma za Kifedha ya UTT Microfinance, Dar es Salaam jana. Wa pili Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi Balozi Fadhili Mbaga na Mtendaji Mkuu wa UTT, Bw. James Washima (kushoto).


Naibu Waziri wa Fedha Bw. Mwiguru Nchemba (katikati), akimsikiliza kwa makini Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kifedha ya UTT Microfinance, Bw. James Washima wakati akimuonyesha vipeperushi, Dar es Salaam jana.  Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi, Balozi Fadhil Mbaga.
=====================================

     Naibu Waziri Fedha aifagilia UTT Microfinance

                     Na: Nyakasagan Masenza
 
NAIBU Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mwiguru Nchemba, amesema Serikali imevutiwa na utendaji kazi mzuri wa Taaisisi ya kifedha ya UTT Microfinance kuwa na matawi 10 katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa muda mfupi.

Akizungumza wakati wa kukata utepe kuzindua rasmi Taasisi hiyo Sukari House Dar es Salaam jana, Naibu Waziri amesema, Serikali imefurahishwa na dhamira ya kweli ya kufikisha huduma za kifedha karibu na wananchi kila pembe ya nchi kunakofanywa na UTT.

“Hii inaonyesha, mmeshaanza kutoa aina nane ya huduma kama mikopo, uwakala wa Bima, Uwakala wa Benki, uwakala  mkuu wa mitandao ya simu (mobile money super agent) kwa mwaka mmoja tangu kuanzishwa”.

Bw. Nchemba amesema, kazi kubwa iliyoifanya ndani ya muda mfupi na kuwa na matawi 10 katika maeneo mbalimbali ya nchi yameifurahisha na kuahidi kuwa Serikali itatoa ushirikiano wa karibu kwa taasisi hiyo ili iweze kufikia malengo iliyokusudia.

Naibu Waziri amebainisha kuwa uwa serikali iliamua kwa makusudi kuanzisha taasisi hiyo ili kuwezesha wananchi kiuchumii hususan wenye miradi, kama biashara ndogondogo na za kati ambao wamekuwa wakipata changamoto nyingi katika kupata mikopo na huduma nyingine za kifedha toka taasisi kubwa za kifedha na  mabenki ya biashara ambayo mara nyingi muundo na mfumo wa taasisi hizo huambatana na masharti magumu.

“Wengi walishindwa kupata mikopo stahiki kutokana na masharti, hususani wenye vipato vya chini, sharti la dhamana ya mali isiyo hamishika kama nyumba, kiwanja na mali, ambavyo hawana”, anasema Bw. Nchemba na kusisitiza kuwa Serikali imeanzisha UTT Microfinance kuchochea ukuaji wa uchumi na kuwainua watanzania walio wengi.

Awali kabla ya uzinduzi huo, UTT Microfinance imezindua rasmi mtandao wa matawi sehemu mbalimbali nchini kwa lengo la kufikisha huduma za kifedha karibu na wananchi hususan mikopo nafuu kwa wajasiriamaliri ambapo matawi 10 yaliyopo katika miji ya Dar es Salaam, Arusha, Dodoma, Mbeya, Mwanza na Zanzibar ulizinduliwa rasmi katika hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali, wakurugenzi wa mashirika, Makampuni na Taasisi mbalimbali pamoja na wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.

Kwa upande wake, Mweneykiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya UTT MFI Balozi Fadhili Mbaga, alisema watahakikisha kuwa UTT MFI inatekeleza azma yake kwa ufanisi na pia itashirikiana kwa karibu na wadau mbalimbali.

“Tunapenda kusisitiza dhamira yetu ya kuendelea kushirikaiana na wadau mbalimbali hususan Tanzania Microfinance Association katika jitihada za jumla za kuwa na mfumo mzuri wa huduma za kifedha na mitaji midogo na kuhakikisha kuwa huduma hizi zinawafikia watanzania wengi zaidi na kuwa chachu muhimu ya maendeleo ya jamii yetu”, anasema Balozi Mbaga.

Ameishukuru serikali kwa ushirikiano inayotoa kwa taasisi hiyo na kuahidi kuzifanyia kazi changamoto zilizo mbele yao kuhakikisha wanavuka malengo waliyojiwekea. ameiomba serekali isisite kuwaunganisha na wabia na washirika mbalimbali ili kuwa na mtandao mpana zaidi wenye nguvu ya kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa UTT MFI James Washima, alisema wanaamini Serikali haikufanya makosa hata kidogo katika kuanzisha UTT MFI, akiahidi kututumia uzoefu wao wa mwaka mmoja, ambao umebaini kuwa huduma za kifedha na mikopo hususan kwa wajasiriamali na watanzania wa kada za kati na chini zilisubiriwa kwa hamu kubwa sana.

Bw. Washima amesema kiu ya Watanzania kwa huduma za UTT hivyo taasisi yao imejipanga kutoa huduma nzuri. Ameahidi kuwa ndani ya miezi sita wataongeza idadi ya wafanyakazi kwani waliopo ni wachache ambapo mfanyakazi mmoja anahudumia wateja zaini ya 1,000.

 “Huu ni muitikio mzuri kutoka kwa jamii na sisi tunajitahidi kukabiliana nao kwa ufanisi” anabainisha Bw. Washima na kuongeza kuwa hivi sasa wana matawi 10,  manne yakiwa Dare s Salaam - Sukari House, Azikiwe, Kijitonyama na Chang’ombe.

Bw. Washima anayataja matawi mengine kuwa ni Arusha lililopo Ngarenaro, Meru lililopo Jengo la Posta Meru,  Dodoma lililopo Posta Dodoma, Mbeya barabara ya KKKT, Mwanza katika jengo la Posta na Zanzibar, Jengo la Posta Kijangwani.

Akizungumzia m,afanikio ndani ya mwaka mmoja wa uwepo wao, Bw. Washima anasema wameweza kukuza mtaji wa Taasisi toka  Shilingi billion 5.4 mnamo Julai mwaka 2013 na kufikia bilioni 12  Juni, 2014. Pia taasisi imefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya Tsh 5.316 bilioni, kwa wakopaji 6,102 – huku 84% ya wakopaji wote wakiwa ni wanawake.

Anabainisha kuwa pia wameanzisha huduma za moja kwa moja kwa muhusika (Tailor-made) kama vile mikopo kwa ajili ya Bima ya matibabu, Hati Malipo (Contract Financing loans), mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali wadogo wadogo (Group loans), Mikopo kwa ajili ya SACCOS, Mikopo maalumu kwa miradi inayolenga kuongeza thamani ya bidhaa na ajira ikiwemo viwanda vidogo vidogo, mikopo kwa wafanyakazi wa Serikali. Hata hivyo, pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana, Washima alieleza baadhi ya changamoto zinazowakabili ikiwa kuibuka kwa taasisi na kampuni zisizo rasmi ambazo hutoa huduma za kifedha hususan mikopo kwa watu wa kada za chini.

Mtendaji huyo amesema mengi ya makampuni haya mara huwa ya kilaghai na yenye kuchukua riba kubwa bila utaratibu maalum suala ambalo badala ya kuwasaidia watu, huwaumiza na kuwaua kabisa kiuchumi.

“Tunaiomba serikali iharakishe utungwaji wa sera ya kurasimisha huduma hizi ili zifanywe kwa utaratibu maalum na pia ziratibiwe na kudhibitiwa vizuri ili wananchi wasiendelee kutaabika na kufilisiwa na watu wasio na nia njema ambao hutumia fursa ya udhaifu wa kisera kujinufaisha” alisema Washima.

UTT MFI ni Taasisi ya huduma za fedha na mikopo iliyoanzishwa mnamo Juni 2013 kwa lengo la kutekeleza sera za serikali katika uwezeshaji kiuchumi hususan kwa wajarisiamali, watumishi wa umma, wakulima, wenye viwanda vidogo, watu wasio na ajira rasmi na wananchi wote kwa ujumla.

UTT MFI pia inalenga kuwapa fursa wamiliki wa Vipande vya UTT AMIS kutumia vipande vyao kama dhamana wakati wa kuchukua mikopo, kupanua wigo na kurahisisha uwekezaji wa vipande vya UTT na hivyo kukuza utamaduni wa kuwekeza kwa wananchi.