TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, September 26, 2014

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KIVUKO CHA MV TEGEMEO-MWANZA


Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kivuko kipya cha MV Tegemeo kitakachotoa huduma kati ya Kahunda hadi kisiwa cha Maisome katika Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza. Wengine walioshikilia utepe ni pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli , Mbunge wa Buchosa Dkt Charles Tizeba na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo.

Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa kivuko hicho kipya cha MV Tegemeo.

Kivuko kipya na chakisasa cha MV Tegemeo kama kinavyoonekana, kimetengenezwa kama mfano wa Meli kutokana na huduma zake.

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akimuonesha Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal jinsi kivuko kipya cha MV Tegemeo kinavyofanya kazi.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mhandisi Marceline Magesa akimuonesha Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal baadhi ya sehemu ndani ya Kivuko hicho kipya.

Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal kulia akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kutoka kukagua sehemu ya kuendeshea kivuko hicho

Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli wakifurahia ngoma iliyokuwa ikichezwa ndani ya kivuko hicho kipya.

Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal kushoto akifurahia jambo na  Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Dkt Charles Tizeba  kabla ya uzinduzi wa Kivuko cha MV Tegemeo.