
Mkurugenzi
 Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Cresentius 
Magori (kulia) akifungua semina ya maofisa Ajira na Fedha toka Mkoa wa 
Temeke iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi
 Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Cresentius 
Magori akifungua semina ya maofisa Ajira na Fedha toka Mkoa wa Temeke 
iliyofanyika  jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) toka Temeke wakifuatilia semina hiyo.

Meneja
 Mafao Mkoa wa Temeke, James Oigo akijibu maswali ya washiriki katika 
semina ya maofisa Ajira na Fedha toka Mkoa wa Temeke iliyofanyika  
jijini Dar es Salaam.

Meneja
 wa Idara za Serikali na Balozi wa NSSF, Rehema Chuma akizungumza katika
 semina ya maofisa Ajira na Fedha toka Mkoa wa Temeke iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Meneja
 Kiongozi wa NSSF Mkoa wa Temeke, Yahya Mhamali akizungumza katika 
semina ya maofisa Ajira na Fedha toka Mkoa wa Temeke iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Picha
 ya pamoja kati ya Mkurugenzi Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi 
ya Jamii (NSSF), Cresentius Magori na Maofisa waandamizi walioshiriki 
semina hiyo.

Baadhi
 ya maofisa ajira na Fedha kutoka kampuni na taasisi mbalimbali 
wakifuatilia mada anuai zilizokuwa zikiwasilishwa katika semina ya 
maofisa Ajira na Fedha toka Mkoa wa Temeke iliyofanyika leo jijini Dar 
es Salaam.

Baadhi
 ya maofisa ajira na Fedha kutoka kampuni na taasisi mbalimbali 
wakifuatilia mada anuai zilizokuwa zikiwasilishwa katika semina ya 
maofisa Ajira na Fedha toka Mkoa wa Temeke iliyofanyika leo jijini Dar 
es Salaam.

Baadhi
 ya maofisa ajira na Fedha kutoka kampuni na taasisi mbalimbali 
wakifuatilia mada anuai zilizokuwa zikiwasilishwa katika semina ya 
maofisa Ajira na Fedha toka Mkoa wa Temeke iliyofanyika leo jijini Dar 
es Salaam.

Meza kuu katika semina ya maofisa Ajira na Fedha toka Mkoa wa Temeke iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi
 ya maofisa ajira na Fedha kutoka kampuni na taasisi mbalimbali 
wakijisajili kushiriki katika semina ya maofisa Ajira na Fedha toka Mkoa
 wa Temeke iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Mmoja
 wa maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) toka Temeke 
ambao waliratibu semina ya maofisa Ajira na Fedha toka Mkoa wa Temeke 
iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam akitoa utaratibu, pembeni ni Ofisa
 Mkuu Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Temeke, 
Nour Aziz.

Baadhi
 ya maofisa ajira na Fedha kutoka kampuni na taasisi mbalimbali 
wakijisajili kushiriki katika semina ya maofisa Ajira na Fedha toka Mkoa
 wa Temeke iliyofanyika ijini Dar es Salaam.

Kutoka
 kushoto ni Meneja Kiongozi wa NSSF Mkoa wa Temeke, Yahya Mhamali, Ofisa
 Mkuu Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Temeke, 
Nour Aziz na mmoja wa maofisa wa NSSF wakijadili jambo kabla ya kuanza 
kwa semina ya maofisa Ajira na Fedha toka Mkoa wa Temeke iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya 
Jamii (NSSF) Mkoa wa Temeke limefanya semina kwa maofisa ajira na Fedha 
zaidi ya 150 kutoka katika makampuni na taasisi anuai za eneo hilo ikiwa
 ni jitihada za kutoa elimu juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na 
taasisi hiyo.
Semina hiyo iliyofunguliwa na 
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Cresentius Magori imefanyika leo 
jijini Dar es Salaam, ambapo washiriki mbali na kupewa elimu juu ya 
mafao saba yanayotolewa na shirika hilo pia wameelezwa namna ya mfumo 
mpya wa ukokotoaji mafao kwa mujibu wa sheria ya Mamlaka ya Usimamizi wa
 Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).
Akifungua semina hiyo Mkurugenzi 
Uendeshaji wa NSSF, Cresentius Magori aliwataka washiriki kuitumia 
vizuri elimu watakayoipata juu ya shughuli za shirika hilo ikiwemo 
kuwaelimisha wafanyakazi umuhimu wa mafao mbalimbali yanayotolewa na 
NSSF ili waweze kuzitumia vema fursa zilizopo katika mafao hayo.
Alisema wapo baadhi ya wafanyakazi
 ambao hukimbilia kujitoa mara baada ya kuacha kazi jambo ambalo 
alieleza lina athari kubwa kwao hapo baadaye kwani kitendo cha kujitoa 
mara kwa mara huenda kikamkosesha sifa za kupata mafao hapo baadaye.
“Fao la kujitoa lipo…lakini hii 
kitu ya kujitoa sio nzuri maana inaweza kumkosesha mwanachama kupata 
penseni hapo baadae. Maana ili mwanachama apate pensheni kuna idadi ya 
michango ambayo inatakiwa awe ametimiza…sasa kama ataendelea kujiunga na
 kujitoa anaweza asifikishe,” alisema Magori.
Aidha alisema wapo baadhi ya 
wafanyakazi wamefikia hatua ya kugushi barua kuwa wameacha kazi ili 
wachukue michango yao jambo ambalo ni hatari na kinyume cha sheria, 
hivyo kuwataka maofisa ajira hao kuwa makini na mchezo huo mbaya kwani 
unaweza kuwaingiza matatizoni endapo watabainika kushiriki ulaghai huo.
Akizungumzia uhai wa NSSF 
aliwahakikishia wanasemina hao kuwa shirika hilo lipo salama kutokana na
 mafanikio na mikakati iliyonayo hivyo wasidanganyike na taarifa zozote 
zisizo rasmi ambazo wakati mwingine zimekuwa zikiwaongopea wananchini.
“…Mfuko wetu upo salama na imara 
hatujafilisika na hatuwezi kufilisika, maana kwa ukaguzi ambao ulifanywa
 hivi karibuni unaonesha shirika liposalama kwa miaka 50 ijayo sasa 
tutafilisika kwa vipi? Bado tumekuwa wa kwanza kimataifa kufanya vizuri 
kiutendaji kadri ya tulivyojipangia katika utoaji huduma na huduma 
zimeboreshwa,” alisema Magori.
Kwa upande wake Meneja Kiongozi wa
 NSSF Mkoa wa Temeke, Yahya Mhamali alisema licha ya uboreshaji wa 
huduma ndani ya shirika hilo kwa sasa mtu atakayemshawishi mteja/wateja 
wapya kujiunga na mfuko huo atapata asilimia 10 ya mchango wao wa kwanza
 mara baada ya kuanza kuchangia ikiwa ni kama asante kwake.
“…Hii sio rushwa maana sisi kila 
siku tunazunguka kushawishi wananchi kujiunga na mfuko wetu sasa kama 
wewe umetusaidia na mwanachama akaja kwetu kwanini tusikupe asante? 
Maana hapa umelisaidia taifa kwa mwanachama huyu kuingia katika eneo 
salama kwa maisha yake ya baadae,” alisema Mhamali.
Akitoa ufafanuzi katika mada yake 
kwa wanasemina, Meneja Mafao Mkoa wa Temeke, James Oigo alisema NSSF kwa
 sasa inaendelea kutoa mikopo kwa wanachama wake kupitia Saccos 
mbalimbali ikiwa ni hatua ya kuwajali wanachama wake hivyo kuwashauri 
wanachama kutumia fursa hiyo kujiletea maendeleo kwa kupata mikopo iliyo
 na riba nafuu.
 *Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment