TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, February 1, 2014

WAZIRI MKUU PINDA ATEMBELEWA NA NAIBU WAZIRI MWANDAMIZI WA MAMBO YA NJE WA JAPAN

 Waziri Mkuu  Mizengo Pinda akibadilishana mawazo na Naibu Waziri Mwandamizi wa Mambo ya Nje wa Japan Norio Mitsuya  alipomtembelea ofisini kwake jana.(Picha zote na  Ofisi ya Waziri Mkuu.)
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na Naibu Waziri Mwandamizi wa Mambo ya Nje wa Japan  Norio Mitsuya alipomtembelea ofisini kwake jana 

Manji awawakia wanaomuandama Seif Magari

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji amewaonya wanachama na mashabiki wa timu hiyo wanaotishia maisha Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano ya imataifa wa klabu hiyo, Seif “Magari” Ahmed kuwa sheria kali zitachukuliwa dhidi yao.

Katika taarifa yake aliyoitoa jana, Manji amesema kuwa si suala jema kwa wanachama kumuhusisha Seif na matokeo ya timu hiyo ambayo kwa sasa imeshinda mechi moja na kutoka sare mechi moja katika mzunguko wa pili wa Ligi kuu ya Tanzania Bara.
 
Manji amesema kuwa madai kuwa Seif siyo mwanachama halali  wa Yanga hayana msingi wowote na kuyaita madai hayo kuwa ni ya uzushi na yanaenezwa na maadui zao ambao hawaitakii Yanga mema.
Alisema kuwa hivi karibuni kumekuwa na madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu, taarifa za hujuma ndani ya timu ambazo zimewahusisha uongozi na baadhi ya wanachama jambo ambalo si la kweli.
Alifafanua kuwa ni haki kwa kwa nia njema kwa wanachama kuhoji mwenendo wa timu yao pale wanapoona-hairidhishi na ni wajibu wa wanachama kuchanganua mawazo merna na mabaya na siyo kumuhisha mtu kwa moja kwa moja kutokana na mtazamo hasi walionao.
 
“Ushindi au mwenendo mzuri  wa timu unatokana na viwango vizuri, nidhamu na ushirikiano wa wahusika wote, wachezaji, walimu, viongozi, wanachama na wapenzi kwa ujumla. Uongozi ulikutana na wachezaji, walimu, baadhi ya wanachama na wapenzi na kuyazungumzia na kukubaliana kuhusu mapungufu yaliyojitokeza kwa wahusika wote na kuchukua hatua ya kubadilisha benchi la ufundi,” alisema Manji.
 
Aliongeza kwa kusema kuwa uongozi ulifika mbali zaid kwa kutoa adhabu na onyo kali kwa baadhi ya wachezaji walionyesha utovu wa nidhamu kwa kipindi kilichopita na kusikitishwa kuona kuwa baadhi ya wadau kwa kutumia vyombo vya habari wanachochea na kutengeneza uhasama ambao kwa kweli haupo ama kwa faida zao binafsiau kwa kutumiwa na watu ambao hawana nia njema kwa klabu.
Manji pia aliwaomba wadau wote wanamichezo na hasa wahariri wa michezo kudhibiti matumizi mabaya ya watu au vyombo vya habari yanayochangia sana kuzorotesha michezo nchini.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAPAN NA UJUMBE WAKE IKULU DAR.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Naibu Waziri wa wa Mambo ya Nje wa Japan, Norio Mitsuya (kulia kwake) aliyeongozana na ujumbe wake wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Feb 01, 2014 kwa mazungumzo. Picha na OMR 

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA JUMUIYA YA ISTIQAAMA DAR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akuhutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Jumuiya ya Istiqaama, uliofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Feb 01, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Istiqaama, leo Feb 01, 2014.
Baadhi ya Wanachama wa Jumuiya ya Istiqaama, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akihutubia kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo leo katika Ukumbi wa Karimjee.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, baada ya kufungua rasmi Mkuu wa Jumuiya hiyo leo katika Ukumbi wa Karimjee.
Picha ya pamoja baada ya kufunguliwa mkutano huo.Picha na OMR. 

Polisi 5 wamekufa papo hapo katika Ajali ya Gari Dodoma

Polisi watato wamepoteza maisha papo hapo baada ya kupata ajali mjini dodoma, habari hii inasomeka kwa undani kwenye Mtandao wa Mtaa kwa Mtaa.
 

Tuesday, January 28, 2014

Zabuni ya vitalu vya gesi kufungwa mwezi Mei

Na: Teresia Mhagama, Nishati na Madini

 
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ameeleza kuwa zabuni ya vitalu vya utafiti wa mafuta na gesi asilia vilivyo bahari kuu na ziwa Tanganyika kaskazini itafungwa tarehe 15 mwezi wa tano mwaka huu.

Waziri Muhongo alisema hayo wakati alipofanya mazungumzo na Waziri mstaafu wa Nishati na Viwanda kutoka nchini ufaransa Bw.Erick Besson aliyemtembelea wizarani ili kufahamu fursa za uwekezaji zilizo katika sekta za Nishati na Madini akiiwakilisha kampuni ya GDF Suez ya Ufaransa.

“Kampuni unayoiwakilisha ni kubwa, yenye teknolojia ya kisasa na inafanya uwekezaji mkubwa duniani hivyo kama mna nia ya kuwekeza katika uendelezaji wa vitalu vya gesi mnaweza kuingia katika ushindani wa kumiliki vitalu hivyo kwani muda bado unaruhusu”. Alisema Profesa Muhongo.

Waziri Muhongo alimweleza Bw. Besson kwamba Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) linamiliki vitalu viwili vya gesi karibu na mpaka wa Msumbiji lakini linahitaji mbia mwenye nia ya dhati watakayeshirikiana naye katika hatua zote za uendelezaji wa vitalu, kwa sababu TPDC bado inakua, alitoa changamoto kwa kampuni hiyo ya GDF Suez kuingia katika ushindani huo.

Katika suala la usimamizi wa bomba la gesi asilia, Profesa Muhongo alimweleza Bw. Besson kuwa TPDC pia itahitaji kupata uzoefu na pengine mbia aliyebobea katika usimamizi wa bomba hilo atakayeshirikiana na TPDC katika usimamizi wa bomba la gesi nchini.
  
Profesa Muhongo alisema Serikali itasambaza gesi katika makazi ya watu ili kupunguza uharibifu wa mazingira huku akitoa mfano kuwa jiji la Dar es Salaam pekee linatumia si chini ya magunia 50 ya mkaa kwa siku hivyo gesi itapunguza uharibifu wa mazingira.

Alisema huo ni mpango endelevu kwani tayari kuna bomba la urefu wa la 6.3 kilometa kutoka Ubungo hadi Mikocheni linalotoa gesi majumbani na bei yake haizidi shilingi 12,500 kwa mwezi.

Alisema kuwa TPDC itahitaji mbia katika utekelezaji wa mpango huo wa usambazaji gesi majumbani na katika sehemu ambazo bomba la gesi haliwezi kupita kutahitajika mitungi ya gesi ili wananchi wote wafaidi gesi hiyo.

Kuhusu umeme, Waziri Muhongo alimweleza Waziri mstaafu huyo wa Ufaransa kwamba serikali inajikita katika miradi ya usambazaji umeme kwa utaratibu wa ubia au mikopo ya bei nafuu na ina mpango wa kujenga njia ya umeme ya msongo wa 400kv kuelekea ziwa Tanganyika hivyo aliikaribisha kampuni ya GD Suez kuwekeza katika miradi hiyo ya usambazaji umeme.

“Tunatafuta pia wawekezaji katika suala la usambazaji umeme na ujengaji wa vituo vya kupooza umeme na transfoma kubwa kwani tumeamua kufanya uwekezaji mkubwa katika eneo hili mf. jijini Dar es Salaam  tulikuwa na vituo vitano tu vya kupoozea umeme lakini sasa tunajenga vingine vitano vikubwa na vidogo 15 ili kutatua tatizo la umeme jijini Dar es Salaam hivyo unakaribishwa kuwekeza katika eneo hili pia”. Alisema Profesa Muhongo

Aidha Profesa Muhongo alimweleza Bw. Besson kuwa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) linatafuta mbia watakayeshirikiana naye katika kuendesha mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe Kiwira mkoani Mbeya hivyo kama wana nia ya kuwekeza katika eneo hilo pia wanakaribishwa kuingia katika ushindani wa kupata nafasi hiyo.

Naye Waziri mstaafu wa Viwanda na Nishati kutoka nchini Ufaransa, Bw. Besson alimshukuru Profesa Muhongo kwa  taarifa nzuri kuhusu fursa za uwekezaji nchini na ameahidi kupata taarifa zaidi za uwekezaji katika mashirika ya TPDC, STAMICO na TANESCO ili kuona jinsi kampuni ya Suez itakavyoshirikiana na mashirika hayo katika kuendeleza sekta za Nishati na Madini.
PICHANI JUU: 

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiwa pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Marcel Escure (kulia kwa Waziri) pamoja na Waziri Mstaafu wa Viwanda na Nishati wa Ufaransa Bw. Eric Besson (kulia kwa Balozi),  pamoja na watendaji kutoka Ubalozi wa Ufaransa na Wizara ya Nishati na Madini, wakati walipomtembelea wizarani ili kufahamu fursa za uwekezaji katika sekta za Nishati na Madini..

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA WAZIRI WA FEDHA NA MANAIBU WAKE IKULU DAR.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 28, 2014 kwa mazungumzo, akiwa ameongozana na manaibu wake, Mwiguku Nchemba na Adam Malima
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkurugenzi wa Kampuni ya Statoil Tanzania Oystein Michelsen, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 28, 2014 kwa mazungumzo. Kushoto ni Meneja wa Biashara wa Kampuni ya Statoil Tanzania, Oivind Holm.
 -Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya na manaibu wake, Mwigulu Nchemba na Adam Malima, wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 28, 2014 kwa mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Statoil Tanzania Oystein Michelsen (wa pili kushoto) Meneja wa Biashara wa Kampuni ya Statoil Tanzania, Oivind Holm (wa pili kulia) Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa kampuni hiyo, Genevieve Kisanga (kulia) na Msaidizi wa Mkurugenzi, Grace Usara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

KIJANA ATUMBUKIZWA KWENYE MAFUTA YA MOTO

KIJANA ATUMBUKIZWA KWENYE KALAI LA MAFUTA YA CHIPSI, HABARI HII BADO INAFANYIWA UCHUNGUZI ZAIDI

NAPE KATIKATI YA WANANCHI SOKO LA MWANJELWA MBEYA

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa  Nape Nnauye akicheza draft na vijana wafanyabiashara wa soko la Sido Mwanjelwa jijini Mbeya. Nape yupo mjini Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za miaka 37 ya CCM ambazo kitaifa zitasheherekewa mkoani hapo.Katibu wa NEC alikutana na vijana mbali mbali ambao walifurahi sana kumuona kiongozi wao akiwa pamoja nao kiasi soko zima lilipuka kwa nyimbo za hamasa za CCM zilizoimbwa na Kapteni John Komba,Nape pia alipata fursa ya kusalimiana na baadhi ya madereva wa Taxi wa kituo maarufu cha Mafiati.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akila chakula cha mchana kwenye kibanda cha Mama Lishe anayefahamika kama Bi. Tandiwa Tewete kwenye soko la Sido Mwanjelwa mjini Mbeya.
 
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikatiza katikati ya soko la Sido Mwanjelwa kwenda kwenye viwanja vya mpira vya soko hilo kushuhudia mechi ya mpira ya wafanyabiashara wa sokoni hapo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiangalia mechi ya mpira kati ya timu ya soka ya sokoni Sido wauza Mitumba na wafungua Mabelo kwenye uwanja wa mpira wa sokoni Sido.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa timu za mpira sokoni Sido Mwanjelwa mjini Mbeya mara baada ya mpira kumalizika.

Askari amfurahisha malikia wa Uingereza

 Hapa akikaa chini kabisa na kuvua kofia kama ishara ya heshima
       Hapa akiinamisha kichwa chini baada ya kuamka

Pichani ni Sajenti Rusiate Bolavucu, 32, ambaye ameweza ku make head lines kwa kitendo chake cha kuketi kitako huku akiinama chini na baadae kuinamisha kichwa chini akiwa miongoni mwa askari maalum walioandalia kwa ajili ya kumpokea malikia wa Uingereza alikuwa ziarani huko Fiji Siku ya Juzi.
Wengi wamempongeza Askari huyo kwa kitendo chake hicho cha kishujaa na kuonesha Heshima ya Hali ya Juu, ingawa baadhi ya watu wamemponda kwa kumwambia amejidhalilisha, wewe unaonaje?

MSANII WA BONGO MUVI AJINYONGA LEO

CAPTAIN SAM CHEKINGO AFARIKI DUNIA.

Marehemu Captain Sam Chekingo
Habari zimetufikia punde kwamba rubani wa ndege maarufu nchini Captain Sam Chekingo amefariki dunia Jumanne asubuhi nyumbani kwake Kinondoni jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa marehemu Balozi Cisco Mtiro, misa ya kumuombea marehemu itaanza saa nne asubuhi kesho Jumatano 29 Jan 2014 nyumbani kwake, kabla ya mwili wake kupelekwa katika makaburi ya Kinondoni saa tisa alasiri.

Marehemu Kepteni Chekingo atakumbukwa kama mmoja wa marubani mahiri na wa muda mrefu wa ndege za serikali alikotumikia toka enzi za Rais wa awamu ya kwanza hayati Mwalimu Nyerere. Alistaafu kazi serikalini na kujiunga na Umoja wa Mataifa akifanyia kazi zake Congo Brazaville, kabla ya kurejea nyumbani na kujiunga na ATC alikofanyia kazi hadi mauti yalipomkuta.

Mola aiweke Roho ya marehemu mahali pema peponi

AMINA

MAADUI WA ZITTO WAMTIA KASIKASHI MAGIGE

Na Mwandishi Wetu

KUNDI la watu ambao inadaiwa kwamba wamekula yamini ya kumchafua Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe kwa namna yoyote ile, wamemuonjesha machungu Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige.
Zitto, baada ya msululu wa tuhuma ambazo nyingi zilibainika kupikwa makusudi ili kuichafua taswira yake mbele ya jamii, sasa hivi anahusishwa kutoka kimapenzi na Magige, ikidaiwa kuwa walisafiri pamoja kwenda Dubai kwa ajili ya kufanya mambo yasiyofaa.
Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa tuhuma hiyo ya Zitto na Magige ni nyingine kati ya zile zilizopikwa, kwani ukweli wake ni wa kufikirika.
Imebainika kuwa safari ya Dubai ambayo inasemwa kuwa Zitto na Magige walisafiri, inapotoshwa kwa sababu ukweli ni kwamba wabunge hao walisafiri pamoja na timu nzima ya Kamati ya Hesabu za Serikali Bungeni (PAC) kwa shughuli za kikazi na hakukuwa na suala la mapenzi kati yao.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.
Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe, aliye makamu mwenyekiti wa PAC, akiizungumzia skendo hiyo ya Zitto na Magige alisema: “Nimeona ujumbe ambao unasambazwa kuhusu Zitto na Catherine (Magige), ni uongo mkubwa, hakuna kitu kama hicho.
“Nimeona wanazungumzia zaidi tiketi, ni kweli tulisafiri kamati nzima kwenda Dubai. Wajumbe wote wa PAC tulikwenda Dubai baadaye Uingereza. Zitto ndiye hakwenda Uingereza, yeye aliishia Dubai na kurudi nchini.
“Katika hili namsikitikia zaidi Magige kwa sababu anaingizwa kwenye vita ambayo haijui, siyo mzoefu wa kashfa hizi za kuzushiwa, Zitto angalau naweza kusema amezoea. Nitasimama kokote kumtetea Catherine na hata Zitto. Hili limeandaliwa makusudi kumchafua Zitto na hii ni vita ndani ya Chadema wao kwa wao.”
Mjumbe wa PAC, Esther Matiko, ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Mkoa wa Mara, alisema: “Hilo suala ni la uongo kabisa, walioanzisha hiyo tuhuma  pengine wanataka kumchafua Catherine. Tulifikia hoteli moja na chumba changu na kile cha Catherine, vilikuwa karibukaribu, hakuna kitu kama hicho kinachosemwa.
“ Catherine alisafiri na mwanaye wa kike anayesoma kidato cha kwanza, na alikuwa akilala naye chumba kimoja, sasa hayo mambo yangewezekanaje? Hizi ni siasa tu. Kwanza Catherine hii siyo safari yake ya kwanza, kila tunaposafiri kwenda nje, huwa analala chumba kimoja na dada Lucy (Owenya, Mbunge wa Viti Maalum Chadema).
“Kitendo cha kupendelea kulala chumba kimoja na dada Lucy maana yake hapendi hayo mambo, tena ni kuonesha anaogopa manenomaneno kama haya. Safari zote huwa analala na dada Lucy, kasoro hiyo tu ndiyo alilala na mwanaye wa kike. Zaidi ya hayo, namsemea Zitto, yeye ni mwenyekiti wetu, amekuwa akitaka tuwe na maadili ndiyo maana hajawahi kuwa na uhusiano na mjumbe yeyote.”
Zitto hakupatikana kuzungumzia tuhuma hiyo lakini Catherine alipopatikana alisema kuwa hana maneno kwa sababu anajua kinachosemwa ni uongo, akaongeza: “Wanatishia wana video, waiweke wazi kama ni kweli. Hizi siasa za kuchafuana kwa vitu vya uongo hazifai hata kidogo, haziisaidii nchi.”

MOHAMMED ENTERPRISES TANZANIA'S EXPANSION PLAN IN AFRICA

BeqsooUCAAIEJjg
The World Economic Forum brought together political, business and civil society leaders to discuss economic development issues. It also attracted a host of entrepreneurs, among them Forbes' youngest member of the rich list, Mohammed Dewji, Group Chief Executive Officer of Mohammed Enterprises Tanzania. CNBC Africa's Bronwyn Neilson spoke with him about the company's expansion on the continent.

Cech ampeleka Diego Costa Chelsea

Ni kama golikipa Petr Cech wa Chelsea amempeleka mshambuliaji wa Atletico Madrid Chelsea baada ya golikipa wa Chelsea anayecheza kwa mkopo Atletico Madrid Thibaut Courtois kuhofia bench akiorudi kwenye timu hiyo na sasa anatumika kama chambo.

Chelsea na Atletico Madrid zinaelezwa kuwa zimefikia makubaliano ya kubadilishana wachezaji hao deal itakayomfanya Diego Costa kutua Stamford Bridge msimu ujao na Courtois kubakia Atletico,hii ni kwa mujibu wa media za Hispania.

Costa ametumbukia wavuni mara 19 msimu huu katika La Liga na hesabu kubwa za kocha wa Chelsea Jose Mourinho ni kunasa mshambuliaji.
Chelsea walimtaka Courtois kusaini mkataba mpya licha ya kwamba hajawahi kucheza kwenye timu hiyo lakini kipa huyo ameomba asajiliwe moja kwa moja Atletico

Awali Courtois alisema atarudi Chelsea endapo atakwenda kuwa golikipa chaguo la kwanza mbele ya Petr Cech kwasababu hawezi kwenda kwenye timu ambayo atasugua benchi,kwake kubwa ni kucheza iwe Chelsea au klabu nyingine.

ripoti ya mafuriko Dumila yamchefua JK

Rais Jakaya Kikwete ameikataa taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera kuhusu waathirika wa mafuriko na waliokosa makazi na kumpa siku moja kukaa na timu yake kuandaa nyingine inayoendana na hali halisi ya janga hilo. Eneo la Dumila, Morogoro lilikumbwa na mafuriko makubwa na kusababisha wakazi wake kupoteza makazi na mali huku mamia ya magari yakiwamo mabasi yanayosafirisha abiria kukwama baada ya kubomoka kwa Daraja la Magole linalounganisha Barabara ya Dar es Salaam na Dodoma.
Mvua hizo zilizonyesha kwenye Wilaya ya Kilosa, ndizo zilisababisha kufurika kwa Mto Mkundi unaopita kwenye eneo hilo.
Taarifa ya Bendera - Bendera alitoa taarifa ya mafuriko kwa Rais Kikwete kwa niaba ya viongozi wa mkoa, wakiwamo wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wakuu wa taasisi mbalimbali akisema wananchi 12,472 wamepoteza makazi. Alisema pia kuwa nyumba 1,141 zilibomoka na 2,551 ziliingiliwa na maji huku kaya 2,759 zikiathiriwa na mafuriko. Bendera alisema misaada ya mahema na vyakula imeanza kutolewa pamoja na dawa za kukabiliana milipuko ya magonjwa endapo itatokea.
Alisema pia kuwa tayari baadhi ya miundombinu imeanza kurejea kama kawaida huku huduma za majisafi zikitolewa na magari ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kikosi cha Zimamoto Morogoro na Kampuni ya China ya High Quality Consulting and Development Solutions. Bendera alisema pia kuwa jumla ya Sh53.7milioni zinahitajika kwa ajili ya ujenzi wa makazi ya muda ya waathirika hao.
JK aikataa taarifa - Rais Kikwete aliyekuwa akikatizakatiza taarifa hiyo ya Bendera kwa maswali na ufafanuzi, alizikataa takwimu hizo akisema hazionyeshi uhalisia. Akizungumza na wananchi wa eneo hilo wakiwamo waliokuwa kwenye kambi iliyoko Sekondari ya Magole, Rais Kikwete aliwahakikishia upatikanaji wa vyakula, dawa na majisafi na salama.
Pia aliviagiza viwanda vya magodoro kuzisaidia haraka iwezekanavyo, familia zilizoathirika na kuahidi kuwa Serikali italipa baadaye ili kuwaepusha wakazi hao na hasa watoto na athari za kiafya.
Alisema kazi ya ujenzi wa makazi ya muda itafanywa JWTZ na si makandarasi kuepusha baadhi ya viongozi kujinufaisha kwa mafuriko hayo. Rais Kikwete aliwataka Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), kuangalia uwezekano wa kutoa magogo yaliyoziba katika makaravati na kuzibua mifereji ili kuruhusu maji kupita kwa urahisi.
Akizungumzia ripoti hiyo Rais Kikwete alisema: “Mmeshindwa kufafanua watu walioathiriwa na mafuriko hayo ni wangapi na wanasaidiwa vipi hasa katika mahitaji mbalimbali na muhimu ya kimsingi kama chakula.
“Taarifa yenu inanitia shaka. Sasa ninawataka viongozi wa mkoa pamoja na Mkuu wa Mkoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wote wa halmashauri kurudia upya kumbukumbu zenu na kupata idadi kamili ya waathirika ili kujua namna ya kuwasaidia. “Ninyi kama viongozi na mnashughulikia maisha ya watu, mnatakiwa kuwa na kumbukumbu zenye usahihi wa majina na kama hamna uhakika wa majina mnaomba vyakula kwa ajili ya nani? Misaada mingine kwa wahisani ya nini?
“Tunataka tujue wanasaidiwaje, kina mama ni wangapi na kina baba, watoto, tutoe misaada kadri inavyostahiki. Sasa kwa takwimu hizi mnafahamu hawa watu wako wapi? Tutawasaidiaje? Wameathirika kwa kiasi gani?.” Rais Kikwete alisema kiongozi mzuri hupimwa wakati wa kipindi cha matukio na matatizo au majanga yanapotokea. Aliwataka viongozi hao kujipanga kwa kuwatambua watu walioathiriwa na mafuriko kwa kuwa na majina sahihi na idadi yao.
Miundombinu - Meneja wa Tanroads Mkoa wa Morogoro, Injinia Doroth Mtenga alisema ofisi yake itatumia kiasi cha Sh400 milioni kukamilisha matengenezo ya eneo la tuta la Daraja la Magole katika Mto Mkundi lililozolewa na maji na kusababisha mafuriko makubwa.
Fedha hizo zitatumika kurekebishia makaravati na madaraja mengine madogo katika eneo hilo kutoka Wami Dakawa hadi Daraja la Mkundi, Magole ambayo huathiriwa mara kwa mara pindi mto huo unapojaa. Mtenga alisema kuwa ujenzi huo unakusudiwa kukamilika ndani ya wiki ya kwanza ya Februari na kama hali ya hewa itaendelea kuwa nzuri, ukarabati huo unatarajiwa kuendelea na kukamilika taratibu na magari yataweza kupishana kama ilivyokuwa awali.
Wakati hayo yakifanyika, mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), wameanza kazi ya kurudishia nguzo na nyaya za umeme zilizoharibiwa na mafuriko hayo huku wataalamu wa Kampuni ya Matrac Telecom, wakirekebisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwenda Mkoa wa Dodoma ambao pia uliharibiwa.
Kaimu Mkurugenzi wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani amekabidhi kwa uongozi wa Mkoa wa Morogoro vifaa tiba, magodoro 100 na dawa mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya Sh80 milioni.
Chanzo - Mwananchi

KWENYE 255 YA XXL YA CLOUDS FM OMMY DIMPOZ AFUNGUKA SABABU YA VIDEO YA TUPOGO KUTO FANYIKA MPAKA LEO


BONGO FLAVA ARTIST OMMY DIMPOZ AMEFUNGUKA SABABU YA NGOMA YAKE YA TUPOGO KUTOFANYIWA VIDEO MPAKA LEO LICHA YA KUWA NI MOJA KATI YA COLLABO KUBWA KUWAHI KUFANYWA KATI YA MSANII WA BONGO NA MSANII MKUBWA HOT IN AFRIKA, COZ ALIIFANYA NA J MARTINS,KAMA ZILIVYO NGOMA ZOTE ZA OMMY DIMPOZ KUWA ZINAFANYAGA VIZURY HATA TUPOGO HAIKUPATA SHIDA KUTOP UP HADI NAFASI YA KWANZA KWENYE CHAT MBALIMBALI IKIWEMO CLOUDS FM TOP 20, WENGI TULITEGEMEA VIDEO YAKE INGEFANYIKA FASTA, NA PENGINE INGEMUWEKA KTK RAMANI YA MUZIKI WA AFRIKA, ANGEONEKANA KAMA SASA DIAMOND ANAVYOFANYA VIZURY ZAIDI BAADA YA COLLABO YAKE NA DAVIDO,
SASA DIMPOZ AMEELEZEA SABABU ZA TUPOGO KU DELAY

NA PIA OMMY DIMPOZ AKAFUNGUKA KUHUSU TOUR NDEFU ANAYOTARAJIA KUANZA SIKU NYINGI NDANI NA NJE YA NCHI

DC Kiteto, Emboley Murtangos aaswa kutowabughudhi wakulima 50

Na:BERNAD DANIEL

Mwenye miwani ni Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Martha Umbula na Jane Mutagurwa Mkurugenzi wa Halamshauri ya Wilaya ya Kiteto
 
NA.MOHAMED HAMAD
 
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara Martha Umbulla ameaswa kuacha kuwaondoa wakulima 50 waliofungua kesi dhidi ya Halamshauri katika eneo linalogombaniwa la Emboley Murtangos kuwa waachwe kwa kuwa kesi iko mahakamani
Kesi iko mahakama ya Rufaa yenye namba 140/2012, imepangwa kusikilizwa Feb 13 mwaka huu kwamba hivi karibuni Mkuu wa Wilaya alitoa amri kuwataka watu wote wanaoishi na kufanya shughuli za kibinadamu kilimo,ufugaji,na uchomaji mkaa watoke kuwa waachwe mpaka kesi imalizike
Jumla ya wakulima 50 wakiongozwa na Tito Shumu walifungua kesi ya msingi kupinga amri ya Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kuvunja makazi yao kwa madai kuwa wamevamia na kuanzisha vitongoji haramu kwa kufanya shughuli za kilimo
Kwa mujibu wa barua ya Wakili G. S. OKWONG’A anaye watetea wakulima ya Jan 23 mwaka huu kwa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto kupitia amri yake ya Jan 21 .2014 kuwataka wakulima hao kuondoka ameombwa kusitisha kutokana na kuwepo kesi inayoendelea mahakama ya Rufaa Dar
“Mheshimiwa kwa kuwa kuna kesi ya msingi Mahakama ya Rifaa na imepangwa kusikilizwa tarehe 13/2/2014 tunakuomba utumie busara zako kusitisha amri ya kuwaondoa wateja wetu katika eneo lenye mgogoro mpaka hapo kesi itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi”ilisema sehemu ya barua hiyo
Hata hivyo pamoja na taarifa hiyo ya kimaandishi kwa Mkuu huyo wa Wilaya pia alipatiwa viambatanisho vya vivuli vya wito wa Mahakama na pia hoja ya maandishi aliyoitoa ya kuwataka watu wote waliopo katika eneo la Emboley Murtangos waondoke mara moja
“Watu wote wanaoishi na kufanya shughuli za kibinadamu, hususani kilimo,ufugaji,uchomaji wa mkaa katika eneo lote la Hifadhi ya Emboley Murtangos muondoke mara moja kulingana na amri iliyotolewa na Mahakama ya Rufaa Tanzania mwaka 2012”
“Kwa mujibu wa mamlaka niliyopewa mnatakiwa muondoke wote ndani ya siku mbili kuanzia  Jan 21-23 mwaka huu,yeyote atakayekaidi amri hii atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kutokutii amri halali ya mahakama”ilieleza amri hiyo ya Mkuu wa Wilaya
Amri hiyo imekuwa ikitolewa na baadhi ya viongozi mbalimbali wa Wilaya, Mkoa,na hata Taifa kuwa pamoja na kufahamu suala hili liko mahakamani, wamekuwa wakiwahadaa wananchi na kuwapa usumbufu uliodaiwa kuleta madhara makubwa kwao
Jan 16 mwaka huu Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyewasili Wilayani Kiteto kutoa pole kutokana na maafa ya watu 10 yaliyofanywa na kikundi cha watu wachache kwa maslahi yao binafsi ambapo aliagiza wakamatwe mara moja na kufikishwa mahakamani
Jumla ya watu 35 walikamatwa na Polisi, 12 walifikishwa mahakamani na kufunguliwa kesi ya mauaji, 10 wako chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi,7 waliachiwa huru  baada ya Polisi kujiridhisha na wengine 6 wanaendelea kuhojiwa juu ya mauaji ya watu 10 Jan 12 mwaka huu katika vitongoji vya Kwa Mtanzania na Laitime Wilayani humo.
Mwisho

WAZIRI MUHONGO AWEKA SAINI LESENI ZA UCHIMBAJI MADINI

1Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo akisaini moja ya Leseni alizozitoa za uchimbaji Madini. Wanaoshuhudia, aliyesimama ni Kaimu Kamshina wa Madini anayeshughulikia Leseni Bw.  John Mayopa na anayeangalia ni Kamshina wa Madini Paul Masanja.2Mmoja wa Wamiliki Kampuni ya J.S Contractors Bw. Sisti Siyvester Mganga akieleza jambo kuhusu Kampuni ya J.S na namna itakavyofanya kazi. Kampuni hii inatarajia kuzalisha madini  aina ya ‘dimension stone’ na kokoto za ujenzi katika eneo la  Kihangaiko Bagamoyo.3Mwakilishi wa Kampuni Ya Osiris Gold T) Ltd. Bw.Shehzada Walli akimweleza Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof esa.Sospeter Muhongo kuhusu Kampuni hiyo. Leseni  iliyosainiwa ya kampuni hiyo itaiwezesha kuchimba madini ya Dhahabu katika eneo la Rwamgaza Geita.
4Mwakilishi wa Kampuni ya Kamal Steel akieleza jambo wakati wa kikao cha kusaini Leseni za Uchimbaji Madini. Kampuni hiyo imepewa Leseni ya kuchimba madini aina ya ‘Marble’ katika eneo la Kidayi Kilosa.


Na Asteria Muhozya
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo   ameweka saini Leseni tatu za Uchimbaji wa Madini kwa Kampuni zinazotarajia kuzalisha madini aina mbalimbali kulingana na maeneo waliyoomba kufanya shughuli hizo.
Kampuni zilizosainiwa Leseni ni Kampuni ya J.S Construction, inayomilikiwa na Bw. Sisti Slyvester Mganga ambaye ameingia ubia Bw. Nakui Chen Kampuni hiyo yenye Leseni ML 501/2014 ina eneo la ukubwa wa km 0.29. Aidha, shughuli za uchimbaji zitafanyika katika eneo la Kihangaiko Bagamoyo na   Madini yatakayozalishwa ni ‘dimension stone’ na kokoto za ujenzi za granite.
Vilevile, kampuni nyingine iliyowekewa saini ya Leseni ni Osiris Gold (T) Ltd. inayomilikiwa na Watanzania Ezekieli Kihali na Shehdaza Walli leseni namba ML 513/2014. Madini yatakayozalishwa na Kampuni hii ni dhahabu katika eneo la ukubwa wa km 9.94, Rwamgaza Geita
Aidha, Mhe. Muhongo ameweka saini leseni ya uchimbaji wa madini aina ya Marble kwa Gagan S.Gupta, Sameer S.Gupta na Shailesh B.Bhandari ambao wanamiliki Kampuni ya Kamal Steel katika eneo la Kidayi Kilosa. Kampuni hii yenye Leseni ML 514/2014 ina eneo la Km 9.52.
Wakati akitoa Leseni hizo za uchimbaji, amewakumbusha wamiliki wa leseni kuhusu kodi na wajibu wa mwenye leseni katika jamii inayohusika ili wananchi na Taifa waweze kufaidika na rasilimali hizo. Uwekaji saini huo umefanyika katika ofisi za Wizara ya Nishati na Madini, Dare s Salaam.