TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Saturday, April 23, 2016
Jumuiya ya Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa Kutoka UGANDA Watembelea Kampuni ya Maxcom Africa - Maxmalipo
Jumuiya ya wakurugenzi wa serikali za Mitaa wapatao 60 Kutoka Uganda wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kampuni ya MAXCOM Africa mapema leo walipokuwa wametembelea Ofisi za Maxmalipo Kujifunza ni jinsi Gani kampuni hii Imeweza kugundua teknolojia inayosaidia kudhibiti makusanyo kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato katika Halmashauri za miji na majiji Nchini Tanzani
WABUNGE WA EALA-TANZANIA WATEMBEELA CLOUDS MEDIA GROUP NA KUPEWA UJUMBE MZITO
Wabunge
wa bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania, na wafanyakazi wa Clouds
Media Group, akiwemo mchekeshaji maarufu Bishanga Bashaija, wakiwa
kwenye moja ya studio za Clouds Media Group, wakati wa kipindi maarufu
cha Leo Tena, Aprili 22, 2016.
WABUNGE
wa bunge la Afrika Mashariki (EALA), kutoka Tanzania, wametembelea Clouds Media
Group,Mikocheni jijini Dar es Salaam
Aprili 22, 2016 ikiwa ni sehemu
ya ziara yao ya takriban siku 20 kutembelea vyombo vya habari kwa nia ya
kuvishirikisha vyombo hivyo kutoa elimu kwa wananchi kuchangamkia fursa
zilizopo kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, inayomiliki kituo cha radio, Clouds FM, Clouds
TV, Bw. Ruge Mutahaba, amewaeleza wabunge hao walioongozwa na mwenyekiti wao
Mh. Chrles Makongoro Nyerere kuwa, Tanzania inakabiliwa na tatizo kubwa la
kutogeuza vipaji kuwa biashara na hivyo kujiingizia kipato.
Ruge
amewahimiza wabunge hao kushawishi serikali ya Tanzania kurekebisha sera zake
za kuwawezesha wananchi na kuwajengea uwezo wa kuvitumia vipaji walivyojaaliwa
na Mwenyezimungu ili kujiingizia kipato.
Akielezea
nia ya ziara hiyo, Mwenyekii Mh. Makongoro Nyerere alisema, wabunge kutoka nchi
wanachama walipewa jukumu la kuwatembelea wananchi wa nchi watokako ili kwahimiza
kuchangamkia fursa zilizopo kwenye Jumuiya hiyo ambayo kwa sasa ina jumla ya
wanachama sita, Tanzania, Kenya Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani Kusini.
“Jumuiya
ya Afrika Mashariki ina soko la kutosha na wananchi wa Jumuiya hii wanyo fursa
ya kwenda kufanya shughuli za kiuchumi bila kizuizi chochote ikiwemo biashara
na kufanya kazi hivyo ni wakati wa watanzania kuacha kulalamika na kuchangamkia
fursa hiyo.” Alisema Mh. Makongoro.
Pamoja
na Mh. Makongoro, wabunge wengine ni pamoja na Mh. Shy-Rose Bhanji, na Mh.
Nderaikindo Kessy.
Mkurugenzi
wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Bw. Ruge Mutahaba,
(kulia), akitoa maelezo ya uendeshaji wa kampuni hiyo, wakati wabunge wa
bunge la Afrika Mashariki (EALA-Tanzania), walipotembelea studio za
Clouds radio/TV Mikocheni jijini Dar es Salaam Aprili 22, 2016. Kutoka
kushoto ni Mwenyekiti wa wabunge hao Mh. Charles Makongoro Nyerere, Mh.
Nderaikindo Kessy, na Mh. Shy-Rose Bhanji.
WAZIRI MKUU: TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA LAPUNGUA
Subscribe to:
Comments (Atom)



Katika
kuhakikisha kuwa Jiji la Dar es Salaam linakuwa safi, Manispaa ya Ilala
imethubutu kwa kuanza kukata miti ambayo imekuwa ikihatarisha usalama
wa wananchi wakiwemo wapita njia na magari, kama picha inavyoonyesha
usafi ukifanyika katika moja ya mitaa wa Samora 23 Aprili, Jijini Dar es
Salaam.









Mkuu wa shule ya Bwawani Sekondari, ACP. Emmanuel Lwinga akitoa
maelezo mafupi ya maendeleo ya shule kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi
kutoa hotuba yake.
Kamishna
wa Utawala na Fedha, Gaston Sanga akiwasalimu wahitimu na wazazi kabla
ya kutoa hotuba fupi kwa wahitimu wa kidato cha sita Bwawani
Sekondari(hawapo pichani).
Mgeni
rasmi Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga akitoa
cheti kwa mwanafunzi mhitimu wa kidato cha sita katika mahafali ya
kwanza ya kidato cha sita Bwawani Sekondari, yaliyofanyika leo Aprili
22, 2016.
Wanafunzi
wahitimu wa Kidato cha sita Bwawani Sekondari wakiimba wimbo wa shule
kwenye mahafali hayo yaliyofanyika leo Aprili 22, 2016, Mkoani Pwani.
Wazazi wa wahitimu wa kidato cha sita shule ya Bwawani Sekondari wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasilisha bungeni Mapitio na Mwelekeo wa
Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi
ya Waziri Mkuu kwa Mwaka 2016/2017.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenhye Ulemavu, Jenista Mhagama (kushoto) na Naibu wake, Dktt. Abdallah
Posi wakiteta bungeni mjini Dodoma Aprili 22, 2016.
Watendaji
wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake wakimsikiliza Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowasilisha bungeni Mapitio na Mwelekeo
wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za
Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka 2016/2017.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya
Mifugo, Mwigulu Nchemba, Bungeni Mjini Dodoma Aprili 20, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Fedha
ambao Aprili 22, 2016 walikwenda Bungeni mjini Dodoma kwa ziara ya
mafunzo.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Afisa Habari wa Chuo Kikuu cha
Dar es salaam, Hamis Dambaya (katikati) na Mhadhiri Msaidizi wa Chuo
Kikuu cha Dar es salaam , Egbert Mkoko kwenye viwanja vya Bunge Mjini
Dodoma Aprili 22, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akisalimiana na Balozi wa Korea Kusini nchini Song Geum aliyemtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Balozi
wa Korea Kusini nchini Song Geum akimuonesha jambo Spika wa Bunge Mhe
Job Ndugai wakati alipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika
wa Bunge Mhe Job Ndugai akisikiliza kwa makini Balozi wa Korea Kusini
nchini Song Geum aliyemtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma. Kulia ni Mke
wa Balozi huyo.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akisalimiana na Balozi wa Kenya nchini Chirau Ali aliyemtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika
wa Bunge Mhe Job Ndugai akimsikiliza kwa makini Balozi wa Kenya nchini
Chirau Ali aliyemtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika
wa Bunge Mhe Job Ndugai (mwenye tai nyekundu katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na Wanafunzi wa shule ya msingi Feza iliyopo Dar es
Salaaam. Wanafunzi hao walikuja kutembelea Bunge.(Picha na Ofisi ya
Bunge)