TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, April 22, 2016

HADITHI: NDOA YA MTOTO WA TAJIRI BILIONEA NA MTOTO WA MASIKINI_MKULIMA. SEHEMU YA NNE



Mkononi alishika funguo za gari aina ya Land Rover(free Rander) ya kisasa kabisa, alikuwa ni Christopher aliyekuja kunikabidhi siku hiyo wakati tukiwa kwenye Msiba wa Mwenzetu patric Nyembela aliyekuwa amefiwa na kaka yake maeneo ya Mwananyara, “shika hizi funguo amenipa dada Regina” alisema Chriss wakati huo nikiendelea kumtazama Chriss ambaye alikuwa akinikabidhi funguo za gari,

 “asante chriss    nilisema huku nikijaribu kupepesa macho yangu na moja kwa yaliweza kugongana na macho ya Regina ambaye kwa wakati huo alikuwa akishuhudia tukio kwa mbali huku akiwa ameketi kati kati ya wanawake wenziwe kwenye mkeka wakati huo” wakati huo macho ya Regina yalikuwa makali sana kutokana na sikuwa tayari kupokea hizo funguo kwa chriss.

“chukua ilikuwa ni sauti ya Regina, wakati huo pia nilikuwa na wenzangu vijana, wengi na miongoni mwao alikuwa ni Aluta Warioba ambaye alinisisitiza kuchukua zile funguo, nilizipokea kisha akasema niliondoe lilipokuwa limeegeshwa gari hilo, lakini kutokana na kwamba sikuwa na ujuzi wa kuendesha gari, sikuweza ilibidi nimuombe tena Aluta aweze kunisaidia kuliondoa mahala hapo na kuliweka pembeni kasha aliponirejeshea funguo nilimuomba na mimi tena kwa upendo Chriss amrudishie Regina funguo zile kwa kuwa sikuwa tayari kuendesha gari kutokana na kwamba sikuwa mjuzi wa kuendesha.
“nakupatia funguo za gari utaki kwa nini”?

 ‘’hapana, siku ingine Regina nilimwambia, umenikwaza sana Shaaban alisema “ najua ila kuna sababu ndiyo maana nimefanya hivyo, pole ila jisikie tu huru, waala hakuna tatizo nilimwambia, alionekana kutabasamu maana mwanzo alionekana kama kachukizwa sana na kitendo kile, na baada ya hapo alitoa wito wa kuwapa chakula watu wote waliokuwa kwenye msiba wakati huo, ambapo aliwaomba tuongozane kwenda kupata chipsi kuku ama niseme kila mtu apendacho maeneo maarufu sana kwa hapa jijini Americani chipsi na wote tukaelekea maeneo hayo.

Baada ya kufika kila mmoja alielekezwa utaratibu wa chakula kwamba anaweza kuagiza kile apendacho, sikuwa tayari kuagiza kutokana na mimi sipendi kula kula sana, na tabia hiyo hata nyumbani uwashangaza sana ndugu na familia yangu, hivyo baada ya watu wote kuagiza nilibaki mimi ambaye nilikuwa sijaagiza chakula, lakini alipogundua aliniuliza kwa nini sikuagiza chakula nilimjibu kwamba nimeshiba,

 “hapana shaaban inabidi ule pia, hivyo ilibidi awaite wahudumu kuja kunisikiliza na mimi ilibidi niagize tu pamoja na kwamba nilikuwa nimeshiba, nilimuomba mhudumu anitengenezee chipsi mayai pekee, maana sikuwa na sehemu ya kukiifadhi kile chakula tumboni mwangu, kilipoletwa nilikula kidogo wakati huo akinishuhudia na kwa kuwa alikuwa yupo na wanawake wenzio na tulikuwa kwenye msiba baada ya kuona nimeanza kula aliondoka kuungana na wenziwe na mimi nikibaki kwenye kundi la wenzangu vijana tukiendelea kubadilishana mawazo na kuzungumza masuala mbali mbali ususani vichekesho na masuala ya michezo.

Baada ya tukio hilo wote tulirejea tena kwenye msiba pale ambapo wengi walikuwa wameacha magari yao akiwepo yeye maana kutoka eneo la msiba hadi americani chipsi aikuwa mbali, hivyo tulikwenda kwa miguu, “baada ya kufika eneo la msiba tulikaa kwa muda wa nusu saa na ilipotimia majira ya saa 5 tano za usiku kila mmoja sasa alikuwa tayari kuondoka maana tulikaa zaidi ya masaa 6 pale kwenye msiba huo.

 “baba naondoka alinifuata Regina na kuiaga na mimi nikamtakia siku na safari njema usiku ule, na wakati yeye yeye akiondoka name pia niliweza kuondoka na rafiki zangu kina Eric Mwingizi, Dotto Peter na wengine wengi kuelekea maeneo ya Tanesco drive in kwa usafiri wa Eric mwingizi na kuwaacha wengine kama kina Aluta Warioba, Wasira Nyerere,Abdul Kanali Misuli tulizoea kumuita Abdul kutokana na jinsi misuli yake ilivyojengeka kwa mazoezi, na  Kalemaa wakiendelea kumfariji Patric Nyembela usiku ule na watu wengine waliendelea kuwepo hadi kesho yake. 

Tukio hilo la msiba lilitufanya tena kutoonana kwa kipindi cha wiki nzima ambapo wengi walishinda katika msiba kutokana na Patric alikuwa ni miongoni mwa wachezaji wa kutumainiwa wa pazi hivyo ilikuwa ni heshima ya pekee kusubiri kwa muda bila kukutana ama bila wachezaji kufika uwanjani, hivyo hata mimi sikuwa tayari kwenda uwanjani pamoja na kwamba niliishi maeneo hayo ya uwanja zaidi tulikuwa tukipishana kwenye msiba, nikifika naambiwa Regina kaondoka lakini baada ya Wiki kumalizika maisha yaliendelea tena kama kawaida kwa kushiriki michezo yetu kama ilivyokuwa kwa siku zote.


Usikose kufuatilia Adithi hii kila siku 0713869133/0767869133

No comments:

Post a Comment