TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, March 26, 2016

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA TAARIFA KWA UMMA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA
Kufuatia mabadiliko ya tarehe ya kupokea Mapendekezo ya Mpango na kiwango cha Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017, Ofisi ya Bunge imefanya mabadiliko ya tarehe za shughuli za Kamati za Bunge kuelekea Mkutano wa tatu wa Bunge (Mkutano wa Bajeti) ili kuendana na masharti ya Kanuni za Bunge kuhusu shughuli hizo. Kwa mabadiliko hayo , ratiba ya shughuli za Kamati itakuwa kama ifuatavyo:-
Tarehe 29/3/2016 hadi tarehe 4/4/2016 Kamati za Kudumu za Kisekta zitatembelea na kukagua utekelezaji wa miradi iliyotengewa Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 kwa mujibu wa Kanuni ya 98(1) ya Kanuni za Bunge. Hapo awali kazi hii ilipangwa kufanyika tarehe 31/3/2016 hadi 6/4/2016.
Tarehe 5/4/2016 – Kwa mujibu wa Kanuni ya 96 ya Kanuni za Bunge, Serikali itawasilisha Dondoo na Randama za Vitabu vya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017. Awali kazi hii ilipangwa kufanyika tarehe 29/3/2016;
Tarehe 6/4/2016 – Kwa mujibu wa Kanuni ya 97(1)-(2) ya Kanuni za Bunge kutakuwa na Mkutano wa Wabunge wote ambapo Serikali itawasilisha Mapendekezo ya Mpango na kiwango cha ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017. Awali kazi hii ilipangwa kufanyika tarehe 30/3/2016;
Tarehe 7/4/2016 hadi 15/4/2016 – Kwa mujibu wa Kanuni ya 98 (2) ya Kanuni za Bunge, kwa kipindi cha siku tisa (9) Kamati za Kudumu za Kisekta zitachambua taarifa za utekelezaji wa Bajeti za Wizara zinazosimamiwa na Kamati hizo. Katika kipindi hicho, Kamati ya Bajeti itafanya uchambuzi wa Mapendekezo ya Mpango na kiwango cha ukomo wa Bajeti kwa Mwaka
wa fedha 2016/2017. Awali Kamati ya Bajeti ingefanya kazi hii kuanzia tarehe 31/3/2016 hadi 6/4/2016;

Tarehe 15/4/2016 – Kwa mujibu wa Kanuni ya 98(3) ya Kanuni za Bunge kutakuwa na Kikao cha pamoja kati ya Kamati ya Uongozi na Kamati ya Bajeti ili kujadili mambo muhimu yaliyojitokeza kwenye Kamati za Kisekta wakati wa kujadili utekelezaji wa Bajeti za Wizara mbalimbali;
Tarehe 16 na 17 Aprili, 2016 kama ilivyokuwa imepangwa awali Wabunge wataelekea Dodoma tayari kwa Shughuli za Mkutano wa Tatu wa Bunge ambao utaanza tarehe 19 Aprili, 2016.
Imetolewa na:

Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
25 Machi, 2016.

Papa ashtumu Ulaya kwa kuwapuuza wahamiaji


Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amesema kuwa tabia za watu wa Ulaya za kuwapuuza wahamiaji, ni za kutia wasiwasi.
Katika sala za kuadhimisha siku ya aliyouawa mwanzilishi wa Imani ya Kikristo, Papa alisema kuwa Bahari zimegeuka kuwa mahali pa mazishi ya maelfu ya watu wanaohatarisha maisha yao kila siku kufika Ulaya.
Akihutubia waumini katika Roma, alishutumu tabia za kutumia dini katika kutekeleza visa vya ugaidi.

Wahamiaji
Aliwashutumu pia mabwenyenye wanaotengeneza na kuuza silaha katika juhudi za kuchochea ghasia ili wanufaike.BBC

Thursday, March 24, 2016

Mhasibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani katika jeshi la kuzima moto na uokozi, na Mkandarasi. Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiareni Investment Ltd Bw. Webu Manoth Masawe wamehukumiwa leo tarehe 24/3/2016 kwa kesi ya kuhujumu uchumi katika Mahakama ya wilaya ya Ilala.

Aliyekuwa Mhasibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani katika jeshi la kuzima moto na uokozi na Bw. Naamini Hendry Sangiwa pamoja na Mkandarasi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiareni Investment Ltd Bw. Webu Manoth Masawe wamehukumiwa leo tarehe 24/3/2016 kwa kesi ya kuhujumu uchumi katika Mahakama ya wilaya ya Ilala. Hukumu hiyo ilisomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mhe. Hassan.

Washtakiwa tajwa hapo juu walishtakiwa kwa makosa 7 yakiwemo Matumizi Mabaya ya Madaraka, Kutumia Nyaraka Kumdanganya Mwajiri kinyume na kifungu cha 22 na 31 mtawalia vya Sheria ya kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11/2007, Kughushi Nyaraka kinyume na Kifungu cha 333, 335 (d) (1) na 337 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16, na kuisababishia Serikali hasara kinyume na Aya ya 10(1) ya Jedwali la Kwanza, Kifungu cha 57(1) na 60(1) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200.

Mnamo mwaka 2009 Serikali ilitoa zabuni ya Ujenzi wa uzio wa Chuo cha Zimamoto na Uokozi kilichopo Mbopo Bunju katika Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Kampuni ya Kiareni Investment Ltd (Mzabuni), ilipatiwa zabuni hiyo na kulipwa Kiasi cha Shilingi 81, 963, 360/=.
Hata hivyo taratibu za utoaji zabuni hazikufuatwa, na Mzabuni ambaye ni Kampuni ya Kiareni Investment Ltd, alifanya kazi yenye thamani ya kiasi cha Shilingi 13, 784, 652/= tu kati ya fedha yote aliyolipwa. 

Ili kuwezesha malipo ya Shilingi 81, 963, 360/= kulipwa pasipo kazi kukamilika, Washtakiwa walitoa zabuni kwa Mkandarasi pasipo Mkataba (LPO), na Kughushi Hati ya kuonesha kazi imekamilika (Certificate of Works Completion).
Washitakiwa wote watatu walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala mwanzoni mwa mwaka 2014 na kusomewa mashtaka yao Mbele ya Hakimu Mkazi Hassan, ambapo washitakiwa walifunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi No. 06/2014. 

Upande wa Jamhuri katika Kesi hii uliwakilishwa na Wakili STANLEY HILMAR LUOGA akisaidiana na Wakili EMMANUEL JACOB, wote waendesha Mashitaka wa TAKUKURU Makao Makuu.
Upande wa washtakiwa wote waliwakilishwa na Wakili wa Kujitegemea MDUMA.
Upande wa Jamhuri uliita Mashahidi 7 na kupeleka vielelezo 21 ili kuthibitisha kesi dhidi ya washtakiwa. Upande wa washtakiwa hawakuita shahidi hata mmoja walijitetea wenyewe.
Mshitakiwa wa kwanza Dotto Salehe Mgogo, ambaye alikuwa Kaimu Mkuu wa Mafunzo wa Wizara ya Mambo ya Ndani katika idara ya Jeshi la Zimamoto na Uokozi alifariki dunia mwaka 2014 baada ya kusomewa mashitaka na hivyo Mashitaka dhidi yake yalifutwa kwa mujibu wa sheria. 

MKUU WA MKOA WA KIGOMA AWATAKA WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI KUTAJA KIIASI CHA FEDHA KILICHOTUMIKA KUWALIPA WATUMISHI HEWA 169











Wafanyabiashara wa soko kuu Mkoa wa Lindi watoa malalamiko kuhusu changamoto wanazokutana nazo katika biashara zao.


sokoni
Mmoja wa wafanyabiashara hao aliyejitambulisha kwa jina la Maria Mahenge ameeleza moja ya changamoto katika soko hilo ni udogo wa Soko hilo kwani wafanyabiashara wamekuwa ni wengi na kupelekea bidhaa zao kuweka msongamano unaopelekea mzunguko wa hewa ndani ya soko hilo kuwa mdogo hivyo kupelekea bidhaa zingine kuharibika hasa ukizingatia badiliko la Tabia nchi, kwani hivi sasa kunajoto kali sana.
Kwa upande wa Ndg Shaibu Ramad Langa ambaye naye ni mfanyabiashara wa soko hilo aliweza kuelezea changamoto ambazo amekumbana nazo ameeleza kuwa mzunguko wa pesa ni mdogo hivyo kupelekea mauzo kuwa hafifu.
Aidha Makamu mwenyekiti wa soko hilo naye ameeleza kuwa soko kuu kwa sasa ni dogo kwa kuwa watu ni wengi na hawana kazi zingine za kufanya tofauti na biashara hivyo inapelekea kujazana katika soko hilo, hali hiyo inatokana na mkoa kukosa viwanda vidogo vidogo na vikubwa, hivyo inawalazimu wananchi kufurika sokoni kuja kutafuta riziki.
Pia aliweza kutoa rai kwa mamlaka husika iweze kupanua soko hilo kwani kwa sasa soko hilo ni dogo na halitoshi kwa sasa.

SERIKALI YATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA WANAHABARI KUFUATIA CHA MTANGAZAJI MWANDAMIZI WA ZAMANI WA RAEDIO TANZANIA (RTD) SARA DUMBA



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO










TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye ametuma salamu za rambirambi kwa  wanahabari wote kufuatia kifo cha ghafla cha aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe na  Mtangazaji Mwandamizi wa zamani wa Redio Tanzania(RTD), Dar es salaam  Marehemu Sara Dumba.

Pokeeni salamu za rambirambi zangu za dhati kwa kuondokewa na  Mwanahabari  mahiri Bi. Sara Dumba aliyekuwa mfano wa kuigwa” amesema Mhe. Nape.
Mbali na utangazaji wake mahiri, Bi. Sara Dumba alikuwa mzalendo wa kweli aliyetumikia tasnia hii ya Habari naSerikali kwa uadilifu na upendo wa kweli, tutamkumbuka na tutaukosa mchango wake. Ni wajibu wetu kumuombea mapumziko mema kwa mwenyezi Mungu na kumshukuru kwa mchango wake alioutoa kwa moyo wa dhati.
Hakika Sara tutamkumbuka, nawapa pole wananchi wote wa wilaya ya Njombe kwa kuondokewa na kiongozi wao mpendwa  mwenzao,ameongeza Waziri Nape.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante  Ole Gabriel  naye ametuma salamu hizo Salaam ziwafikie familia, ndugu jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu ambao unawagusa sana, naelewa machungu waliyonayo na huzuni, hata hivyo kwa pamoja ni wakati wa kuzidi kumuombea Marehemu katika safari yake ya mwisho,amesema Profesa Elisante na kuwatakia moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Baadhi ya wafanyakazi wenzake waliowahi kufanya kazi  pamoja naye ambao ni Aloisia Maneno amesema Bi. Sara alikuwa mwalimu wake katika masuala ya utangazaji kwa kuwa ndiye aliyemfundisha jinsi ya kuandaa kipindi cha watoto  cha Cheichei  Shangazi.
 Abdul Ngarawa  amesema kuwa Bi. Sara alikuwa mchapakazi hodari, mtu mwenye kipaji cha utangazaji, mcheshi, mtu mwenye ushirikiano na wafanyakazi wenzake na jasiri asiyeogopa kusema ukweli hata kwa wakuu wake wa kazi pale ambapo kazi hazikufanyika vizuri.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Hajjat Halima Kihemba akizungumzia uhusiano wake na marehemuamesema kwamba yeye alianza kazi RTD  mwaka  1971 ambapo Bi. Sara alimkuta tayari akiwa kazini kati ya mwaka 1974, hivyo walifanya naye kazi pamoja kwenye Idhaa ya Kiingereza ya (External Services) marehemu akiwa  msaidizi wake.
   Alikuwa ni mtu  mwenye mchango mkubwa na yuko tayari kufanya kazi wakati wote  unapomwihitaji usiku na mchana, mshauri hususan kwa watoto wa kike kuacha kujidharau na kuona kwamba hawezi kufanya kazi ya taaluma ya habari na mtu aliyependa maendeleo.

Kwa  upande wake, Bakari Msulwa ambaye ni Mkuu wa Kanda ya Kati Dodoma - TBC akimzungumzia  Bi.Sara Dumba amesema kuwa alihamishiwa mkoani Morogoro  mwaka 1990 akiwa mwakilishi wa RTD  na baade Mkuu wa Kanda ya Kati Dodoma  hadi alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi mwaka 2006 .Ameongeza kwamba ni mama aliyekuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za wanawake, aliandaa vipindi mbalimbali vya biashara na alikuwa yuko tayari kuambiwa ukweli.
Kwa kweli Bi. Sara alijenga historia nzuri katika tasnia  ya masuala ya habari na utumishi wa umma akiwa katika ngazi ya ukuu wa wilaya, hivi karibuni nilionana naye mkoani Tabora miezi miwili iliyopita alikuwa na mtazamo wa kuwaunganisha  wafanyakazi wa RTD  ili waweze kuwa na umoja utakaoweza kutupatia nafasi ya kusaidiana kwenye masuala mbalimbali,” Amesema Msulwa.
 Msulwa amebainisha kuwa Bi. Sara alisema hayo baada ya  kubaini kwamba  hakuna historia ya wafanyakzi wa RTD. Hivyo ameacha changamoto  kwa hao  kuacha historia zao  ili  ziweze kuwa na manufaa kwa watu wengine.
Bi. Sara amefariki   dunia tarehe 21 Machi,  mwaka 2016 Wilayani Njombe,  baada  kuugua ghafla. Alizaliwa Oktoba 19, 1956. Bi. Sara alianza kazi katika Radio ya Taifa, Radio Tanzania Dar-es-Salaam (RTD) na baadaye Shirika la Utangazaji Taifa (TUT) sasa TBC.
        Marehemu  Sara Dumba kabla ya kuteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya mwaka 2006alivuma katika kipindi cha Majira(yaani habari za hapo kwa hapo) na vipindi vingine vingi.
 Kwa mujibu wa taarifa za Katibu Tawala wa  Mkoa wa Njombe Jackson  Saikadau  amesema mwili wa marehemu  unatarajiwa kuagwa kesho Machi 24, mwaka huu  jijini Dares Salaam na kuzikwa nyumbani kwake eneo la  Mbutu  Mwembe Mdogo, Kigamboni.

   Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi, Amina.

IMETOLEWA NA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO
23, MACHI, 2016.