TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, January 18, 2013

MH WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AZINDUA TOVUTI YA CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA SEREKALI ZA MITAA (TALGWU)

  January 18, 2013 
IMG_1262 
Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiimba wimbo wa mshikamano kabla ya kuanza mkutano mkuu wa Baraza la wafanyakazi wa Serekali za mitaa Talgwu jana amabao una fanyika mjini Dodoma kushoto kwa waziri mkuu ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa( Tamisemi) Mh Hawa Ghasia na kulia kwa waziri mkuu ni mwenyekiti wa (Talgwu) Edna Mwaigomole pamoja naviongozi wengine  Picha na Chris Mfinanga
IMG_1277 
Mh. Waziri mkuu Mizengo Pinda akizindua Tovuti ya chama cha wafanyakazi wa wa serekali za mitaa kulia kwa waziri mkuu anaye shuhudia uzinduzi huo ni Mwenyekiti wa chama hicho Bibi Edna Mwaigomole na aliye vaa tai ni mtalamu wa kompyuta uzinduzi ume fanyika leo mjini Dodoma Picha na Chris Mfinanga
IMG_1294 - Copy 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo mjini Dodoma baada ya kuuzindua.
IMG_1302 
Mh. Waziri mkuu Mizengo Pinda akiwasili kufungua mkutano mkuu wa Baraza la wafanyakazi wa serekali za mitaa Talgwu kushoto kwa waziri mkuu ni Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Tawala za mikoa (Tamisemi) Mh Hawa Ghasia na kulia ni Mwenyekiti wa Talgwu Edna Mwaigomole mkutano huo unafanyika mkoani Dodoma Picha na Chris Mfinanga

WASANII WA FILAMU BONGO KUCHEZA FILAMU NIGERIA NA DRC CONGO
Pix-1
Mkurugenzi wa Mad Mad Entertainment, Yasmin Razak (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu kampuni yake kuingia mikataba na wasanii wa filamu wa Tanzania watakaokwenda Nigeria na Jmahuri  ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa ajili ya kutengeza filamu. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Superior, Issack Kasanga na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba. DSC_8498
Msanii wa filamu, Steve Nyerere (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano hupo.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Superior, Issack Kasanga na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba.  
……………………………………………………………….
KAMPUNI ya Mad Mad Entertainment iliyopo jijini London nchini Uingereza, imeanzisha program maalum ya kupeleka wasanii wa filamu za bongo nje ya nchi kwa lengo la kukuza sanaa hiyo hapa nchini.
 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Yasmin Razak alisema ameamua kufanya kazi na wasanii  hao ili kuleta mabadiliko na kuwakwamua kiuchumi wasanii wa filamu hapa nchini.
 “Kwa muda mrefu niliokaa London sioni kama sanaa hii ina maendeleo, nikafikiria kitu gani nifanye ili  kukuza tasnia hii, katika mkataba na kampuni msanii atakayetengeneza filamu na wasanii wa nje atalipwa kiasi cha Sh. 50 milioni pamoja na malipo mengine yatakayokuwepo kwenye mkataba, ikiwa ni pamoja na asilimia fulani kwa kila kazi itakayouzwa hapa nchini.
“Nimekuwa nikifanya kazi hiyo na wasanii wengi kutoka Nigeria wakiwemo kina Omotola, Two Face na wengineo na pia Ghana, Congo na hata Uingereza, hivyo nimeonelea kuwa itakuwa vema Tanzania nao kuingia katika mchakato huo,”alisema Razak.
Razak ambaye amewahi kufanya kazi ya filamu na Fally Ipupa,  alitaja vigezo vya msanii atakayechaguliwa ikiwa ni pamoja na umaarufu,  kuijua lugha ya kiingereza, uwezo wa kuigiza na kuuvaa uhusika wowote pamoja na mavazi.
Naye rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba aliwataka wasanii hao kujipanga katika kuhakikisha wanaingia kwenye ushindani huo na kuwataka wale watakaochaguliwa kujituma na kuonyesha nidhamu ya uhakika.
“Hapa kuna kuinua vipaji, soko la kimataifa na mengineyo, hivyo ni vema kufanya kazi kikamilifu kwa wale watakaochaguliwa na si kujisahau, wanatakiwa wasanii watatu na tupo katika hatua za awali za mchujo,” alisema
Mwakifamba.
Naye muigizaji Issa Musa maarufu kama Cloud, alisema kuwa lugha itakuwa ni tatizo kubwa kwa wasanii walio wengi, hivyo kuitaka kampuni hiyo iangalie namna ya kuweza kuwasaidia wasanii hao.

Rais Kikwete apokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi wa Msumbiji na Indonesia

8E9U4363 
Balozi mpya wa Msumbiji nchini Tanzania Dkt.Vicente Mebunia Veloso na Balozi Mpya wa Indonesia nchini(4395) Mhe.Zakaria Anshar wakiwasilisha hati zao za utambulisho kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo(picha na Freddy Maro).
8E9U4395 
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi wa  Indonesia ikulu jijini Dar es Salaam.

DK SHEIN KUONGOZA MKUTANO WA BARAZA LA BIASHARA 

January 17, 2013 

Shein Pix

            Na Ali Issa-Maelezo Zanzibar 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuongoza Mkutano wa saba wa Baraza la Biashara Zanzibar utakaofanyika Jumamosi Januari 19 katika ukumbi wa Salama Hoteli Bwawani mjini Zanzibar.
 Akitoa taarifa kwa Vyombo vya habari huko Gulioni katika Jengo la ZSTC Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Ali Haji Vuai alisema mkutano huo wa saba utazikutanisha Sekta za Umma na Sekta Binafsi, ambao utajadili mada mbili muhimu ambazo ni Maendeleo ya uwekezaji katika viwanda na Ubiya unaohitajika katika viwanda vya Zanzibar.
 Amesema wameamua kuzungumzia masuala hayo kutokana na Sekta ya Viwanda Zanzibar kuwa nyuma sana jambo ambalo pia huchangia ukosefu wa Ajira kwa vijana na mapato kwa maendeleo ya Zanzibar.
 Ameongeza kuwa Zanzibar ina fursa nzuri ya kuanzisha viwanda vipya na kuvifufua vile vilivyokuwepo awali jambo ambalo litachochea kasi ya maendeleo na ukuaji wa uchumi kwa Zanzibar.
 Vuai amefahamisha kuwa Viwanda vilivyokufa Zanzibar vilitokana na sababu mbalimbali na kwamba Mkutano huo utakuwa ni sehemu muafaka ya kuelezea chanzo cha kufa viwanda hivyo na kubuni mipango mipya ya kufufua sekta hiyo.

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake (WAMA) Mama Salma Kikwete afunga kongamano la Ulimwengu la afya ya uzazi mjini Arusha

3-mama Salma Kikwete akifunga kongamano leo 
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisisi ya WAMA , Mama Salma Kikwete akifunga kongamano la Ulimwengu la Afya ya Uzazi la  siku 3 Katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa AICC mjini Arusha leo, Kongamano hilo lilewashirikisha wataalamu wa masuala ya afya ya  uzazi wapatao 800 kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni, (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
4- washiriki wa kongamano wakifuatilia hotuba ya ufungaji 
Baadhi ya wataalamu wa  kongamano la ulimwengu la afya ya uzazi wakimsikiliza Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA , Mama Salma Kikwete (hayupo pichani wakati wa kufunga kongamano Jan,17,2013 mjini Arusha, ambapo wataalamu wa masuala ya afya ya uzazi zaidi ya 800 kutoka ndani na nje ya nchi wamehudhuria, (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO)
5-- Baadhi ya wataalamu wakongamano la ulimwengu la afya ya Uzazi wakibadilishana mawzo 
Baadhi ya wataalamu wa  kongamano la ulimwengu la afya ya uzazi wakimsikiliza Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA , Mama Salma Kikwete (hayupo pichani wakati wa kufunga kongamano Jan,17,2013 mjini Arusha, ambapo wataalamu wa masuala ya afya ya uzazi zaidi ya 800 kutoka ndani na nje ya nchi wamehudhuria, (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO)
6-- mandhar ya ukumbi wa kokgamano la ulimwengu la Afya ya Uzazi mjini Arusha 
Wajumbe mbalimbali wa mkutano huo wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa kmataifa wa AICC Arusha leo.
11-mama na watendaji wakuu wakielekea katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa AICC- 
Mke wa Rais na Mwenyikiti wa Taasisisi ya WAMA ,Mama salma Kikwete (alievaa kitnge) akiogozana na watendaji wakuu wakielekea katika eneo la kupigia picha ya pamoja
13-Picha ya pamoja na watendaji wakuu wa kongamano la Ulimwengu la Afya ya Uzazi 
Picha ya pamoja na watendaji wakuu wa kongamano la Ulimwengu la Afya ya Uzazi.
16-Mama Salma Kikwete akifurahia ngoma ya msanja ya kikundi cha akina mama huko Arusha 
Mama Salma Kikwete akifurahia ngoma ya msanja ya kikundi cha akina mama huko Arusha

WANANCHI WATAKIWA KUACHA KUJICHULIA SHERIA MIKONONI

KAMANDA-11868905953 
Mahmoud Ahmad Arusha
…………………………………………..
Wananchi wenye hasira kali hapa nchini wametakiwa kuacha kujichukulia sheria mikononi na kuwapiga ama kuwachoma moto watu wanaodaiwa kuwa ni wezi bila ya kujua kama madai wanaotuhumiwa nayo ni ya kweli au la na wengine kujikuta wakipoteza maisha bila ya kuwa na hatia na kutakiwa kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria na usalama.
Kauli hiyo imetolewa na wananchi mbali mbali wakati wakiongea na waandishi wa habari kwenye matukio mawili tofauti yaliyotoke kwenye sehemu mbili tofauti kwenye kituo kikuu cha mabasi na kituo kidogo cha vifodi jijini hapa jana.
Katika tukio la kwanza kijana anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 37 mkazi wa jijini hapa mwenye ugonjwa wa akili alipata mkong’oto wa kufa mtu baada ya kupiga gari la mtu lililokuwa kwenye stand hiyo na kumwaga vyakula na karanga za wafanyabiashara ndogo ndogo na vijana stand hapo kumpa mkong’oto huo.
Vijana hao huku wakimpa mkong’oto kijana huyo walikuwa wakimwambia kuwa wanampa dawa ya sigareti kubwa kwani dawa yake wanayo wao kijana huyo aliendelea kupatiwa mkong’oto nhadi askari wa jeshi la polisi aliyekuwa doria stand hapo kumuokoa na kumfikisha kwenye vyombo vya usalama kumuokoa na kipigo hicho kutoka kwa vijana wasio na chembe hata ya huruma kwa mgonjwa huyo.
Katika tukio la pili kijana anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 17 mkazi wa jiji hili alipata mkong’oto wa paka mwizi hadi kushindwa kujua uelekeo wake wa kwenda baada ya kudai kuiba vitu kwenye duka moja stand ndogo ya vifodi
Waandishi walipohoji kwa mwenye duka hilo ni vitu gani vimeibiwa kwenye duka hilo alishindwa kuthibitisha kuwa alIIbiwa nini dukani humo huku mgambo wa jiji wakiangali bila ya kuchukuwa hatua yeyote.
Taarifa zinadai kuwa wananchi mbali mbali wamekuwa wakipatiwa mkong’oto bila ya kuwa na hatia ya makosa wanayotuhumiwa na kuwataka wananchi mbali mbali kutokujichukulia sheria mikononi
Alipohojiwa kamanda wa polisi mkoani hapa Liberatus Sabas kuhusiana na wananchi kujichukulia sheria mkononi alisema matukio mengi ya kujichukulia sheria mkononi ni tatizo hapa nchini huku akiwataka watanzania kujenga mazoea ya kujichunguza kabla  ya kujichukulia sheria mkononi.

WAZIRI MWANRI AWACHACHAMALIA WANAOPIGA MIMBA WANAFUNZI

IMG_6469
Na Kibada Kibada wa Fullshangwe-Katavi
Naibu  Waziri wa nchi  Ofisi ya waziri mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)  Agrey Mwanri amewaagiza viongozi na Watendaji wa serikali kuhakikisha wanakomesha suala la mimba mashuleni.
Waziri Mwanri alitoa agizo hilo (leo) wakati akizungumza na wananchi  kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha  Kilida Kata ya Mamba wilayani Mlele Mkoani Katavi katika ziara yake ya kukagua na kuhimiza shughuli za maendeleo na kuona jinsi gani Halmashauri zinasimamia fedha za serikali zinazoletwa kwenye halmashauri kwa ajili ya shughuli za maendeleo katika kutekeleza miradi na kupeana mikakati jinsi ya kusimamia fedha hizo ili zifznye kazi iliyokusudiwa.
 Amesema  ni wajibu wa viongozi kuhakikisha suala la mimba linakomeshwa kabisa mashuleni na haitoshi kila mara viongozi kuripoti tu, suala la mimba mashuleni bila hatua kuchukuliwa kwa wale wahusika wanaofanya vitendo hivyo vya kuwapa mimba watoto wa kike.
“Haitakiwi kuripoti tu,pia inatakiwa kueleza ni hatua gani zimechukuliwa  kuhakikisha hao wanofanya vitendo hivyo wamechukuliwa hatua zipi za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo”alisema kwa kufoka Mwaniri.
Aliagiza kufuatia kusomewa  taarifa ya Mkoa kuhusu maendeleo ya Mkoa  iliyosomwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Lauten Kanoni   ikieleza hali ya elimu na jinsi suala la mimba kwa watoto wa kike linavyo shughulikiwa
 Aidha katika taarifa hiyo ilieleza  hali ilivyo kwa sasa ilieleza kuwa mimba kwa mkoa wa katavi zimepungua kutoka wasichana waliopata ujauzito mwaka 2011  (63)  na  mwaka 2012  mimba zilipungua kufikia  (61)   sawa na asilimia tano .taarifa ambayo haikueleza namna wanavyolishughulikia tatizo la mimba na kueleza wangapi walichukuliwa hatua za kisheria kulingana na makosa hayo.
Na ni mikakati gani inafanywa kuhakikisha wanakomesha kabisa suala la mimba mashuleni kwa wanafunzi wengi wanapatiwa mimba na wazazi na jamii inaangali badala yake wanamalizana kwa kupeana zawadi huko huko majumbani hali hiyo inayofanya kuendelea kila mwaka.
 “Juhudi kubwa inatakiwa kufanyika ili kuhakikisha  wale wote wanaohusika wanachukuliwa hatua kali za kisheria kukomesha suala hili kwa kushirikiana wote viongozi wananchi, serikali, jamii, wazazi, walimu na wanafunzi kwa nafsi yao kukomesha suala la mimba kwa watoto wa kike mashuleni”alimaliza Mwanri.

Push Mobile, Channel Ten kutoa zawadi ya gari Valentine Day

IMG_6184 
Meneja Mauzo na Masoko wa Push Media Mobile, Rodney Rugambo akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa shindano la kampeni maalum ya kuadhimisha sikukuu ya wapendanao ‘ Valentine Day’ iliyoandaliwa kwa kushirikiana na Kampuni ya African Media group (AMG) kupitia kituo cha televisheni cha Channel Ten na Redio Magic FM. Kushoto ni AFISA Masoko na Mauzo wa AMG,  Prosper Vedasto
………………………………………………………………….
KAMPUNI ya Push Media Mobile itatoa zawadi ya gari aina ya Vitz lenye thamani ya shs milioni 8 kwa mshindi wa kampeni maalum ya kuadhimisha sikukuu ya wapendanoa “Valentine Day” ikayoa adhimishwa Februari 14.
Hayo yalisemwa na Meneja Mauzo na Masoko wa Push Media Mobile, Rodney Rugambo katika uzinduzi wa kampeni hiyi pamoja na Kampuni ya African Media group (AMG) kupitia kituo cha televisheni cha Channel Ten na Redio Magic FM.
Rugambo alisema kuwa wameamua kutoa zawadi kubwa hiyo ili kuwafanya wapendanao wegi kushiriki na kupata nafasi ya kushinda. Alisema kuwa ili kuingia katika droo ya shindano hilo, unatakiwa kutuma neno “Penzi” kwenda namba 15678 na kujibu maswali mbali mbali yahusiyo masuala ya mapenzi na siku ya Valentine.
“Hii ni promosheni ya kwanza kubwa hapa nchini na mshindi kujishindia gari, lengo kubwa ni kutoa ufahamu kuhusiana na sikukuu ya wapendanao na vile vile kuwazawadia wadau waokwa kushiriki katika shughuli zao za ujenzi wa taifa,” alisema Rugambo.
Alisema kuwa mbali ya zawadi hizo, washiriki wa promosheni hiyo pia watapata nafasi ya kujisha kompyuta (Laptop) aina ya HP yenye thamani ya shs milioni 1.5, simu aina ya Blackberry Curve yenye thamani ya shs 500,000 na Home theatre ya thamani ya shs 400,000 na Ipad.
Kwa mujibu wa Rugambo, lengo lao kubwa ni kuifanya sikukuu ya wapendanao kuwa kubwa kama nyingine kwani mapenzi ni kitu muhimu sana katika maisha ya kila siku.
Alisema kuwa mipango yao ni kuwekeza katika sikukuu hiyo ambayo jamii imeanza kuitilia mkazo japo si siku ya mapumziko kama sikukuu nyingine. Alisema kuwa kwa mwaka huu, wameweka bajeti ya shs milioni 30 ili kufanikisha zaoezi hilo.

MAKAMO MWENYEIKI CCM ZANZIBAR DK. SHEIN, AZUNGUMZA NA VIONGOZI OFISI KUU YA CCM KISIWANDUI

IMG  335 
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akisisitiza jambo alipokua akizungumza na  Viongozi wa Tawi la
CCM Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui,wakiwemo Viongozi wa  Jumuiya mbali
mbali za Chama  hicho katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui
Mjini Zanzibar jana,Makamo  Mwenyekiti alifanya ziara maalum ya
kusalimiana na Viongozi hao ikiwa  ni pamoja na  kuimarisha Chama cha
Mapinduzi,(CCM) (kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali
Vuai.  [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
IMG  5323 
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,(wapili kulia) akizungumza na  Viongozi wa Tawi la CCM Afissi
Kuu ya CCM Kisiwandui,wakiwemo Viongozi wa  Jumuiya mbali mbali za
Chama  hicho katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui  Mjini
Zanzibar jana,Makamo  Mwenyekiti alifanya ziara maalum ya kusalimana
na Viongozi hao ikiwa  ni pamoja na  kuimarisha Chama cha
Mapinduzi,(CCM) (kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali
Vuai, [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
IMG 321 
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,na Rais waZanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali MohamedShein,akizungumza na  Viongozi wa Tawi la CCM Afissi Kuu ya CCMKisiwandui,wakiwemo Viongozi wa  Jumuiya mbali mbali za Chama  hichokatika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui  Mjini Zanzibarjana,Makamo  Mwenyekiti alifanya ziara maalum ya kusalimana naViongozi hao ikiwa  ni pamoja na  kuimarisha Chama cha Mapinduzi,(CCM)(kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai,na (kushoto)Mwenyekiti wa Tawi  Nadra Juma  Mohamed.[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]

36 WACHUKUA FOMU TFF, 18 WAREJESHA

IMG_6931
Wakati kesho ndiyo mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu za kuwania uongozi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPL Board) waombaji 36 wameshachukua na 18 tayari wamesharejesha.
 Idadi hiyo ni kufikia leo mchana (Januari 17 mwaka huu). Pia Kamati ya Uchaguzi ya TFF inasisitiza kuwa wanaorejesha fomu hizo kwa email wanatakiwa kuzituma kwa Katibu Mkuu wa TFF kwa email ya tfftz@yahoo.com na si kwa email binafsi za wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi au maofisa wa TFF.
 Waombaji wanne walioongezeka katika orodha ni Blassy Kiondo kwa Kanda ya Katavi na Rukwa, Eliud Mvella (Mbeya na Iringa), Geofrey Nyange (Morogoro na Pwani), na Omari Abdulkadir kwa Kanda ya Dar es Salaam.
 Orodha kamili ya waombaji ni Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi na Omari Mussa Nkwarulo (urais) wakati waombaji wa umakamu wa rais mpaka sasa ni Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia.
 Kwa upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama (Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).
 Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo na Elly Mbise (Arusha na Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama (Njombe na Ruvuma).
 Athuman Kambi na Zafarani Damoder (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Geofrey Nyange na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), Elias Mwanjala na Eliud Mvella (Iringa na Mbeya), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir na Shaffih Dauda (Dar es Salaam).
 Kwa upande wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) waliochukua fomu mpaka sasa ni wawili tu. Yusuf Manji amechukua fomu ya uenyekiti wakati Said Mohamed amechukua fomu ya kuwania umakamu mwenyekiti.

ZAIDI YA MILLION 31.9 ZAGHARAMIA VIFAA LIGI YA MOHAMMED DEWJI, SINGIDA

Mwenyekiti wa CCM jimbo la Singida mjini, Hamisi Nguli (kushoto) akikabidhi vifaa vya michezo kwa kiongozi wa tawi la Mitunduruni.
 
Foleni ya viongozi wa matawi katika jimbo la Singida mjini wakikabidhiwa vifaa vya michezo kwa ajili ya timu zao kushiriki kombe la MO inayotarajiwa kuanza Januari 20 mwaka huu.
 
Baadhi ya msaada wa vifaa vya michezo vilivyotolewa na mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji kwa ajili ya kuendeleza mchezo wa soka jimboni kwake. (Picha zote na Nathaniel Limu).
……………………………………………………….
Mbunge wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Gullam Dewji,ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 31.9 vitakavyotumika kwenye ligi ya kombe lake, inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi januari 20 mwaka huu.
Vifaa hivyo ni pamoja na jezi pea 854,mipira 122,soksi pea 854 na cloves za magolikipa 61.Vifaa hivyo ni kwa ajili ya timu zitakazoshiriki ligi ngazi ya kitongoji katika jimbo la Singida mjini.Baada ya ligi hiyo,itafuatwa na ligi ngazi ya kata ambayo atakuwa na vifaa vyake pia.
Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vifaa hivyo,mwenyekiti wa CCM jimbo la Singida mjini, Hamisi Nguli amepongeza mbunge Dewji kwa kuendelea kutoa misaada mikubwa mbalimbali katika jimbo lake kwa lengo la kuendeleza wapiga kura wake na wananchi kwa ujumla.
“Dewji toka awe mbunge wa jimbo la Singida mjini,siku zote yupo karibu zaidi na vijana. Amewasaidia mambo mengi makubwa ikiwemo kuwaendeleza kimichezo na pia ametoa pikipiki kwa ajili ya vijana wa bodaboda watakaojiunga katika vikundi”,alisema.
Awali msaidizi wa mbunge Dewji, Duda Mughenyi,amesema msaada huyo wa vifaa,ni mwendelezo wa Dewji kuhakikisha vijana wanatumia michezo kujiendeleza kimaisha.

MKE WA RAIS NA MWENYEKITI WA TAASISI YA WAMA AFUNGA MKUTANO WA MAMA NA MTOTO LEO JAN 17,2013-ARUSHA

1- Mama Jk (kushoto) akielekea ARS ((kushoto) NW wa Afya Dr. Seif Rashid 
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete(kushoto) pamoja na Naibu wa Wizara ya Afya Dkt.Seif Rashid (mwenye miwani) wakielekea kupanda ndege katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa- JK- Nyerere jijini Dar es Salaam 16-jan 2013 kuelekea  Arusha kwaajili ya kufunga mkutano wa masuala ya Afya na Mtoto jan. 17,2013. Mkutano huo unawashirikisha wajumbe wapatao 700 wa ndani na nje ya nchi. (picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
2- MMama Salma akisalimiana na wafanyakazi wa ndege- (kulia) NW wa Afya Dr. Seif Rashid 
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) Mama Salma Kikwete (mwenye kilemba) akisalimiana na wafanyakazi wa ndani ya ndege katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es Salaam Jan 16,2013 wakati akielekea kufunga mkutano wa Masuala ya Afya na Mtoto hapo Jan 17,2013 mkoani Arusha. Mkutano huo anawashirikisha wajumbe wapatao 700 wa ndani na nje ya nchi, (kulia) ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Seif Rashid. (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
3-- Mama Jk akiangalia ngoma ya utamaduni wakati wa mapakeezi, (mwenye miwani) ni Mk wa uwt -kILIMANJARO MAMA  FLORA ZELOTE 
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete(kulia) akiangalia vikundi vya sanaa ya  ngoma mbalimbali za utamaduni  alipowasili  katika  kiwanja  cha ndege cha Kimataifa cha Kilimnjaro (KIA) jan 16.2013 kwaajili ya kufunga mkutano wa masuala ya Afya ya Mama na Mtoto hapo Jan 17,2013 mkoani  Arusha. Aliengozana nae  wapili ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake mkoa wa Arusha (UWT) Flora Zelote (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
4-KIKUNDI CHA NGOMA YA MSANJA KIKITUMBUIZA 
Kikundi cha kinamama  cha ngoma ya Msanja  kikitumbuiza katika mapokezi ya Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama salma Kikwete (hayupo pichani)   kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa Kilimanjaro  (KIA ) Jan 16,2013.(Picha na Mwanakombo  Jumaa  wa MAELEZO).
7-MAMA JK (KULIA) AKISALIMIANA NA MKUU WA MKOA WA ARSMwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo  Wanawake(WAMA) kulia, Mama Salma Kikwete akizungumza na Mkuu wa Mkoa Arusha Magesa Mulongo (kushoto)  wakati  alipowasil katika Uwanja wa ndege wa kimataifa Kilimanjaro (KIA) Jan 16,2013.- Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.
8- Mama jk (kulia) akisalimiana na mkuu wa wilaya ya ars John Mongela- KIa 
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Jan 16,2013. –Picha na Mwnakombo Jumaa- MAELEZO.
………………………………….
Mahmoud Ahmad Arusha
Kauli mbiu ya kongamano la ulimwengu la Afya ya uzazi linaloendelea jijini Arusha imepewa msisitizo na kuwa hakuna mama atakayekufa wakati akileta kiumbe duniani na pia Afya ya mama na mtoto ipewe kipaumbele.
 Kauli hiyo imeendelea kutolewa na Mke wa Rais mama Salma Kikwete wakati akiwasilisha na kuzungumza na washiriki wa kongamano hilo jijini hapa na kuwataka watafiti na wataalamu hao kuja na majibu yatakayosaidia kupunguza vifo vya wakinamama wakati wa kujifungua.
 Mama kikwete alisema kuwa takwimu zinaonyesha kupungua kwa kiasi kidogo tatizo la kujifungua na kupoteza maisha hapa nchini na kuwataka wataalamu humu nchini kuchukuwa uzoefu walioupata kuchangia kupunguza vifo vya wamama wakati wa kujifungua sanjari na watoto huku wajawazito zaidi ya 459 hufa kila mwaka wakati wakijifungua.
 “Asilimia 90% ya nchi zilizoendelea wanaweza kupunguza ama kuokoa maisha ya kinamama na watoto huku hapa nchini wakiandaa mpango endelevu wa kuokoa maisha ya wamamawajawazito wakati wa kijifungua na kutoa rai kuwa wamama wasife kwa magonjwa ambayo yanaweza kupatiwa tiba”alisema mama Salma.
 Mama Salma alisema kuwa suala la afya ya uzazi liwe mpango endelevu kwa serekali na asasi mbali mbali na kuitaka serekali kulipa kipaumbele suala la afya ya mama na mtoto licha ya majukumu mbali mbali iliyonayo.
 Nae naibu waziri wa Afya na maendeleo ya jamii hapa nchini Seif  Raishid alisema kuwa serekali kupitia wizara hiyo wameweka kipaumbele suala la mama afya ya uzazi na kuwa hakuna mama atakaeyekufa wakati akiwa analeta kiumbe duniani sanjari na watoto na wamejipanga kuongeza wigo wa kuwafikia wakinamama kwa kuongeza zahanati kuwa karibu na usafiri sanjari na huduma muhimu.
 Rashid akwataka watanzania walioshiriki kongamano hilo kutoa uzoefu walioupata kutatua tatizo la afya ya mama na watoto ilikupunguza vifo ambvyo vinawezekana kuepukika kutokana na kukosa eidha huduma muhimu wakati wakujifungua.
 Kwa upande wake mkurugenzi wa afya dkt dumilia chalamila alisema kuwa mkutano huo umewashirikisha zaidi ya wataalam na watoa maamuzi zaidi ya 800 kutoka mataifa mbali mbali ulimwenguni wakichangia uzoefu katika kulipatia ufumbuzi suala la afya ya uzazi.

TANZANIA YAANZA RASMI KUTUMIA MFUMO WA KIMATAIFA WA UKAGUZI

Mohamed-Mtonga 
NA GLADNESS MUSHI -ARUSHA
 Tanzania imeanza kutumia rasmi mfumo wa kimataifa katika masuala ya ukaguzi wa ndani ambapomfumo huo utaweza kupunguza Viashiria mbalimbali vya ubadilifu wa fedha za umma
 Hayo yamebinishwa  leo na mkaguzi mkuu wa ndani hapa Nchini Bw Mohamed Mtonga wakati akifungua mafunzo kwa wakaguzi wa ndani kutoka katika kanda ya kaskazini
 Mohamed alisema kuwa mpango huo wa ukaguzi kwa mfumo wa Kimataifa umeanza kutumika rasmi hapa nchini July  Mosi ambapo utaweza kutoa na kuonesha viashiria mbalimbali ambavyo vinakwamisha shuguli za ukaguzi ndani ya Serikali kuu pamoja na  Serikali za Mitaa.
 Alisema kuwa kupitia mfumo huo mpya wa kimataifa wa ukaguzi wa ndani utaweza kuboresha  na kuwafanya wakaguzi wa ndani kufanya kazi zao kwa uhuru zaidi tofauti na mfumo uliokuwa hapo awali ambao ulikua hautoi fursa kwa wakaguzi wa ndani
 Alifafanua kuwa hapo awali wakaguzi wa ndani walikuwa wanashindwa kutekeleza  majukumu yao kutokana na viashiria vya vitu mbalimbali kama vile rushwa na uhusiano baina ya mkaguzi na mkaguliwa hali ambayo ilikuwa chanzo cha kukwamisha malengo mbalimbali ya ukaguzi hapa nchini ingawaje  ndani ya mfumo wa ukaguzi kimataifa suala hilo halipo kabisa.

SHIRIKA LABUNI MBINU MPYA YA KUWAFUATILIA MAMA WAJAWAZITO KWA SIMU ILI KUPUNGUZA VIFO NYAKATI ZA KUJIFUNGUA

6029AFC0-AFF0-4C91-B402-D2E48ADB0A9A_w640_r1_s 
Na Gladness Mushi -Arusha
 SHIRIKA  la Jhpiego  la jijini Dar es saalam limefanikiwa kubuni aina mpya ya mradi ujulikao kama Maisha ambapo mradi huo utaweza kutumia simu za mkononi kwa ajili ya kufuatilia afya za mama wajawazito  kwa malengo ya kupunguza vifo vya wajawazito
 Akiongea na “Fullshangweblog”mjini hapa mapemajana Meneja mradi wa shirika hilo Dkt Dunstan Bishanga alisema kuwa mradi huo wa maisha umeanza kutekelezwa kwa mkoa wa Morogoro
 Dkt Bishanga aliongeza kuwa mradi huo una malengo ya kuhakikisha kuwa inapunguza vifo vya mama wajawazito hapa nnchini lakini njia pekee ya kuwakutanisha wahudumu wa afya pamoja na wajawazito ni simu za mkononi hasa  kwa kuwapa wajawazito taarifa mbalimbali
 Pia alisema kuwa Mradi huo ambao kwa sasa umeanza kutumika katika Mkoa wa Morogoro lakini wanaendelea kufanya tathimini mbalimbali za kuhakikisha kuwa unasambaa nchi nzima kwani una uwezo mkubwa sana wa kuokoa maisha ya mama wajawazito
 Hataivyo aliongeza kuwa mara baada ya mkoa wa Morogoro kunufaika na mradi huo wataweza kwenda mikoani ikiwa ni pamoja na kuongeza zaidi ubunifu zaidi ili kuimarisha zaidi afya ya mama kwa manufaa ya Nchi nzima kwani vifo hivyo vinasababisha sana Umaskini katika jamii.
 Awali alisema kuwa suala la mama wajawazito ni suala ambalo linatakiwa kuchukuliwa tahadhari kubwa sana ikiwa ni pamoja na kufuata taratibu sahihi za afya kutoka kwa wataalamu hivyo nao wazazi wa kiume wana nafasi kubwa sana ya kufanya hivyo

Miss Demokrasia Tanzania- INAKUPA POLE SANA BW. ERASTO MAPUNDA KWA KUMPOTEZA MKE WAKO MPENDWA

Marehemu Judith Chikaka Mapunda enzi za uhai wake.
Mwili wa Judith Chikaka ukiwa umelazwa ndani ya Jeneza Pamoja na mwili wa marehemu Mtoto wake mchanga.
Marehemu Judith Chikaka alifariki siku ya Jumapili  ya tarehe 13/01/2012 katika Hospitali ya Mwananyamala wakati alipofikishwa hapo kwa ajili ya kujifungua, kwa bahati mbaya na mapenzi yake muumba alifariki kabla ya kujifungua.
Mume wa Marehemu Judith, Bwana Erasto Mapunda akiwa amembeba mtoto wake wa kwanza aliyezaa na mkewe.
Baba mzazi wa marehemu Judith, Mzee Chikaka
Mama mzazi wa marehemu Mama Chikaka sakiwana majonzi makubwa baada ya kumpoteza mtoto wake kipenzi
Padre kutoka Parokia ya Kigamboni akiendesha Ibada ya misa takatifu ya kumwombea Judith alale kwa amani. Ibada hiyo ilifanyika nyumbani kwa Marehemu Judith maeneo ya Kigamboni Kibada.
Baadhi ya viongozi wa CCM Temeke wakitoa rambi rambi zao.
Spika wa Bunge la wanafunzi wa chuo cha Ardhi akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya wanafunzi wenzake.
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania Bwana S. Nyambui akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya wanachama na chama chao kwa ujumla.
Mume wa marehemu Judith akiweka Shada la maua katika nyumba ya milele ya mkewe
Kushoto ni mwakilishi wa Familia ya marehemu akipokea rambi rambi kutoka kwa wafanyakazi wenzake wa marehemu kutoka wizara ya Ardhi
Mwakilishi kutoka Wizara ya Ardhi upande wa michezo akitoa salamu zake kwa niaba ya wanamichezo wenzake.
 Hii ndio nyuma ya milele ya marehemu Judith Chikaka Mapunda.
Marehemu Judith  alizikwa jana katika makaburi ya Kibada maeneo ya Kigamboni, ameacha Mume na Mtoto mmoja.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEME MAHALI PEMA PEPONI.
AMIN.

SOKO LA BUGURUNI WAMUOMBA RAIS JAKAYA KIKWETE KUTEKELEZA AHADI YA KUJENGO SOKO

Sokola Buguruni 
 WAFANYABIASHARA wa soko la Buguruni lililoko wilayani Ilala jijini Dar es Salaam wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kutekeleza ahadi yake kwa vitendo kwa kuwajengea soko jipya wafanyabiashara hao kinyume chake watasitisha kulipa ushuru.
 Akizunguza na Mwandishi wa habari hizi kwa niaba ya wenzake jijini, mmoja wa wafanyabiashara hao, Maulu Mali alisema hawaamini kama serikali haina fedha za kujenga soko hilo. 
Alisema wamefikia hatua hiyo baada ya viongozi mbambali akiwemo Rais kushindwa kutekeleza ahadi zao za kujenga soko hilo ambapo kwa uchakavu wa soko hilo inawafanya washindwe kufanyabiasha zao kwa mafanikio.
Mali alisema hadi sasa wamechoka kudanganywa hivyo ni vema wakasitisha kulipa ushuru hadi hapo watakapohakikishiwa vingine tena kwa vitendo wala si kwa maneno.
Alisema hali ni mbaya katika soko hilo haswa katika kipindi hiki cha mvua, bidhaa za wafanyabiashara hao zinaharibika kutokana na kuvujiwa. 
Alisema ndani ya soko hilo hivi sasa kumejaa maji yaliyochanganyika na uchafu, baada ya mifereji  kuziba hali inayohatarisha afya zao na maradhi ya mlipuko. 
Alipoulizwa Ofisa Masoko wa wilaya hiyo, Athuman Mbelwa, kuhusu tatizo linalowakabili wafanyabiashara hao, Mbelwa alikiri kuwa soko hilo liko katika hali mbaya likifanana na kiota cha ndege.

BONDIA IDDY MNYEKE AJIFUA KUMKABILI SADIKI MOMBA FEBRUARI 14

Bondia Iddy Mnyeke kulia akioneshana umbwamba wa kutupiana masumbwi na Mussa Sunga wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala  Dar es salaam jana Mnyeke anajiandaa na Mpambano wake zidi ya Sadiki Momba February 14 katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Iddy Mnyeke kulia akioneshana umbwamba wa kutupiana masumbwi na Mussa Sunga wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala  Dar es salaam jana Mnyeke anajiandaa na Mpambano wake zidi ya Sadiki Momba February 14 katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es salaam
Bondia Iddy Mnyeke kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Mussa Sunga katika Mazoezi yanayoendelea Kambi ya Ilala Dar es salaam jana Mnyeke anajiandaa na Mpambano wake zidi ya Sadiki Momba February 14 katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MWENYEKITI WA AU NA RAIS WA BENIN MHE BONI YAYI

b1 
Rais Jakaya Mrisho akiongea na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa Benin Mhe Boni Yayi Ikulu jijini Dar es salaam jana Januari 16, 2013
b8 
Rais Jakaya Mrisho akimuaga Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa Benin Mhe Boni Yayi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa  Julius Nyerere  jana Januari 16, 2013
b7 
Rais Jakaya Mrisho akimuaga Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa Benin Mhe Boni Yayi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa  Julius Nyerere  jana Januari 16, 2013
b2 
Rais Jakaya Mrisho na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa Benin Mhe Boni Yayi wakiongea katika mkutano na wanahabari Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2013
b4 
Rais Jakaya Mrisho akiandika jambo akiangaliwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa Benin Mhe Boni Yayi Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2013

MZEE MKAPA NA MZEE MSUYA WATOA MAONI

CRC-Mzee Mkapa Nje1 
Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa akifurahia jambo na Wajumbe wa Tume na Sekretarieti ya Tume Mabadiliko ya Katiba jijini Dar es Salaam jana(Jumatano, Jan 16, 2013). Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu leo jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya. Kushoto ni Mwenyekiti Jaji Joseph Warioba na kulia ni Mjumbe wa Tume Dkt. Salim Ahmed Salim, Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na Katibu wa Tume Bw. Assaa Rashid.
PICHA NAKATIBA TUME YA KATIBA
CRC-Mzee Msuya1 
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Cleopa Msuya akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu mchakato wa Katiba Mpya jana (Jumatano, Januari 16, 2013) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba.
CRC-Mzee Mkapa na Jaji WariobaMwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akibadilishana mawazo na Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Jan 16, 2013). Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu jana jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.
CRC-Mzee Mkapa akiongea4 
Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa (kulia) akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani (katikati) na Dkt. Salim Ahmed Salim. Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu jana (Jumatano, Jan 16, 2013) jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.
CRC-Mzee Mkapa akiongea 
Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa (kulia) akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani (katikati) na Dkt. Salim Ahmed Salim. Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu jana (Jumatano, Jan 16, 2013) jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.

MAOFISA WA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI WATEMBELEA KIWANDA CHA TBL ARUSHA

Baadhi ya maofisa kutoka Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kutoka Dar es Salaam wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Uzalishaji Bia wa Kiwanda cha Bia cha TBL Arusha, Ben Mwanri (wa pili kushoto), walipotembelea Kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) cha Arusha, wakati wa  ziara ya siku moja kujionea shughuli mbalimbali za kiwanda hicho mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya maofisa kutoka Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kutoka Dar es Salaam, wakiangalia eneo ambapo maji yaliyotumika kiwandani yanachujwa tayari kwa matumizi mengine, walipotembelea Kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) cha Arusha, wakati wa  ziara ya siku moja kujionea shughuli mbalimbali za kiwanda hicho mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya maofisa kutoka Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC), Usalama, wakitembelea mwishoni mwa wiki Kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), cha Arusha, walipofanya ziara ya siku moja kujionea shughuli mbalimbali za kiwanda hicho.
Baadhi ya maofisa kutoka Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC), Usalama, wakitembelea mwishoni mwa wiki Kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), cha Arusha, walipofanya ziara ya siku moja kujionea shughuli mbalimbali za kiwanda hicho.
Baadhi ya maofisa kutoka Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kutoka Dar es Salaam wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Uzalishaji Bia wa Kiwanda cha Bia cha TBL Arusha, Ben Mwanri (wa pili kushoto), walipotembelea Kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) cha Arusha, wakati wa  ziara ya siku moja kujionea shughuli mbalimbali za kiwanda hicho mwishoni mwa wiki.
Kiongozi wa ujumbe wa maofisa wa Jeshi kutoka Chuo ChaTaifa cha  Ulinzi (NDC) Mafunzo ya Kijeshi na Usalama, S.M Minja  (kushoto) akimkabidhi zawadi  Meneja wa Uzalishaji Bia wa Kiwanda cha Bia cha TBL Arusha, Ben Mwanri, walipotembelea kiwanda hicho mwishoni mwa wiki.

RAIS DK. JAKAYA KIKWETE AZINDUA AWAMU YA KWANZA YA JENGO JIPYA LA HOSPITALI YA SHREE HINDU MANDAL JIJINI DAR ES SALAAM

 
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasha mshumaa kama ishara ya uzinduzi wa Awamu ya Kwanza ya jengo jipya na Awamu ya pili ya Hospitali ya Shree Hindu Mandal ya jijini Dar es salaam leo katika Mtaa wa Nyanza, ambapo huduma hiyo itapunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali jijini na kuongeza wigo wa utoaji huduma n kuongeza vitanda vya kulaza wagonjwa, Hospitali ya Shree Hindu Mandalilianzishwa mwaka 1931 ikianza na Zahanati anayeshuhudiatukio hilowa pili katikati ni Mwenyekiti wa hospitali hiyo Bw Ramesh Patel.
 
Rais Dk. Jakaya Kikwete akikata utepe wakati wa uzinduzi wa hoapitali hiyo uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
 
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wafanyakazi pamoja na wananchi waliohudhuria katika uzinduzi huo leo.
 
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi akimkaribisha Rais Jakaya Kikwete ili kuzungumza na wafanyakazi wa hospitali hiyo.

Mwenyekiti wa Hospitali ya Shree Hindu Mandal Bw. Ramesh Patel akielezea historia ya hospitali hiyo.
 
Rais Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili hospitalini hapo kwa ajili ya kuizindua, kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi na Kulia ni Bw. Ramesh Patel Mwenyekiti wa Hospitali hiyo.
 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Raymond Mushi akizungumza na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi na Kulia ni Bw. Ramesh Patel Mwenyekiti wa Hospitali hiyo.
 
Baadhi ya madaktari na wauguzi wakisubiri kuwasili kwa Rais Jakaya Kikwete
 
Baadhi ya madaktari na wauguzi wakisubiri kuwasili kwa Rais Jakaya Kikwete

 
Baadhi ya wauguzi na wafanyakazi wa hospitali hiyo wakiwa katika hafla ya uzinduzi huo.
 
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi , Madaktari , Wauguzi pamoja na wafanyakazi wa hospitali ya Shree Hindu Mandal mara baada ya kuzindua rasmi leo

Waziri Simba akabidhi vyerehani kwa wajane

 
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba akimsikiliza Gavana wa Lions Ukanda wa Uganda na Tanzania, Joseph Kiwanuka, wakati alipomtembelea leo ofisini kwake akiwa na ujumbe wa watu watano.
 
Waziri Simba akiangalia baadhi ya vyerehani viwili viliyotolewa na Lions kwa ajili ya kuwasaidia wanawake wajane. Vyerehani hivyo ni kati ya 100 vitakavyotolewa na Lions kuwawezesha wanawake kujikimu kimaisha.
 
Waziri Simba akimkabidhi mmoja wa wafaidi wa vyerehani vilivyotolewa na Lions Bi. Jane Fuiko wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi zilizofanyika leo ofisini kwa Waziri.
 
Gavana Kiwanuka akimkabidhi cherehani Waziri Simba kabla ya kumkabidhi mfaidika wa pili wa vyerehani hiyo Bi. Mariam Mohamed.
………………………………………………………………
Usu-Emma Sindila na Sakina Mfinanga

Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto Mhe.Sophia Simba  amekabidhi msaada wa vyerehani  viwili kati ya 100 vilivyotolewa kwa wanawake  wajane wa Mkoa wa  Dar es Salaam  ofisini kwake leo kutoka Taasisi ya Lions Club,
Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi  vyerehani hivyo, Gavana wa Lions Ukanda wa Tanzania na Uganda, Ndg. Joseph Kiwanuka, amesema taasisi yao imekuwa mstari wa mbele kuisaidia jamii hasa wanawake na watoto, kuboresha huduma za maji kwa kuchimba visima ambavyo huwasaidia wananchi hasa wanaokaa sehemu zenye shida ya maji.
Amesema Lions imekuwa ikisaidia watoto wenye matatizo ya moyo kuwapeleka nchini India kwa ajili ya matibabu,kuwasaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kwa kuwapeleka shule hasa zile za awali na wameanzisha mkakati wa kuwaelimisha wanafunzi mashuleni kuhusu utumiaji wa madawa ya kulevya ili watoto wasijihusishe na vitendo hivyo.
Kwa upande wake Waziri Simba ameishukuru taasisi ya Lions kwa misaada mbalimbali ambayo wamekuwa wakiisaidia jamii na zaidi kwa msaada huo wa vyerehani kwa wajane kwa kuwa utawawezesha kujikwamua kimaisha wao wenyewe,  watoto na familia zao.
Aidha, Waziri Simba amewapongeza Lions kwa kazi kubwa wanayofanya kupitia mradi wao wa kuelimisha wanafunzi juu ya madhara ya utumiaji wa dawa za kulevya na kuongeza kuwa Serikali inafanya jitihada kuhakikisha kila kata inakuwa na shule ili kusaidia kupunguza wimbi la watoto wasiojua kusoma na kuandika.

UJUMBE KUTOKA JIJI LA MWANZA WATEMBELEA MANISPAA YA ILALA KUJIFUNZA MBINU ZA UKUSANYAJI MAPATO

 
Mstaiki meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula na ujumbe wa kamati yake ya fedha wametembelea halmashauri ya manispaa ya Ilala kwa maagizo ya Mhe.Waziri Mkuu kuja kujionea mbinu za kisasa za kukusanya mapato.
 Mstaiki Meya wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala Mhe Jerry Silaa amewakaribisha na kuwaeleza jinsi walivyoweza na wanavyoendelea kukusanya mapato.
 
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala Mhe Jerry Silaa akiueleza ugeni huo kutoka jiji la Mwanza mambo mbalimbali  jinsi walivyoweza na wanavyoendelea kukusanya mapato.
 
Mtahiki Meya wa Ilala  Mhe Jerry Silaa akiwa na ugeni huo kutoka jiji la Mwanza katika kikao kilichozungumzia mbinu za ukusanyaji wa  mapato.

MFANYAKAZI WA NDANI AJINYONGA TABATA MARAKUDA

 
Mwili wa mwanadada ambaehatukulipata jina lake mara moja unkichukuliwa na Polisibaada ya kujinyonga katika eneo la Tabata Barakuda jijini Dar es salaam bado haijafahamika ni chanzo cha kujinyongwa kwake,taarifa zaidi zinasema msichana huyo alikuwa akifanya kazi za ndani (House Girl) Picha kwa hisani ya www.tzdadaz.blogspot.com. 
 
Hapa mwili ukitolewa  na Polisi katika chumba alichojinyongea katika eneo la Tabata Barakuda jijini Dar es salaam bado haijafahamika ni chanzo cha kujinyongwa kwake

SERIKALI KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU KUTEKELEZA MPANGO WA MIRADI WA AFYA YA MAMA

 
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi
……………………………………………………………………….
Na Gladness Mushi -Arusha
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
SERIKALI kwa kushirikiana na wadau inaendelea kutekeleza mpango wa miradi ya miaka mitano wa kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga wakati wa kujifungua na walio chini ya miaka mitano ikiwa ni hatua ya kuboresha huduma ya mama na mtoto na kuokoa maisha yao.
 Hayo yameelezwa na Daktari bingwa wa akina mama na watoto wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ,Dk Koheleth Winani, kwenye kikao cha pamoja na baadhi ya wakuu wa  mashirika mbalimbali wanaohudhuria mkutano mkuu wa kimataifa wa afya ya mama na mtoto, wanaoshirikiana na serikali kutekeleza mpango huo wa kupunguza vifo vya mama na watoto nchini walipokuwa wakitoa ufafanuzi wa maswala mbalimbali kwa wanahabari.
 Dakta Winani, amesema 75% ya watanzania wanaishi vijini ambako hawapati huduma zilizo bora wakati wa kujifungua kutokana na umbali na maeneo mengine kutopitika hasa wakati wa maska kutokana na miundo mbinu duni na kusababisha wajawazito kujifungulia majumbani au wengine kupoteza maisha wakati wakipelekwa kwenye Hospital , Vituo vya afya na Zahanati..
 Amesema kuwa mpango huo unalenga kupunguza idadi ya vifo vya wajawazito na watoto 500 mwaka 2000 hadi kufikia 19 ifikapo mwaka 2015 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya Milenium, na kusisitiza kuwa ushirikiano kati ya serikali na wadau hao ni muhimu kwa kuwa serikali peke yake haiwezi kutekeleza mpango huo kwa ufanisi.
 Kwa upande wake daktari Dustan Bishanga, ambae ni mkurugenzi wa mradi wa Maisha unaofadhiliwa na ,shirika la misaada la Kimarekani, USAID , kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2008 kwa thamani ya Dola milioni 40 umeboresha huduma ya afya ya mama na mtoto mchanga.
 Dakta Bishanga, amesema  mradi umetengeneza mwongozo unaotumika na wadau wengine kutekeleza mradi hiyo ,pia mradi huo unatengeneza mitaala ya kufundishia  watoa huduma kwa kushirikiana na wizara ya afya ili kutoa mafunzo  na uratibu wake katika vituo tofauti tofauti vipatavyo 250 nchini kote Tanzania bara na Zanzibar lengo ni kuboresha huduma ya mama na mtoto mchanga na kuokoa maisha

HABARI ZA UA MIGUU TFFCHAGUZI KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA W


 
WATATU WACHUKUA FOMU ZA URAIS TFF
Wadau watatu wa mpira wa miguu wamechukua fomu za kuwania urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kufanya idadi ya waliojitosa katika uchaguzi huo utakaofanyika Februari 24 mwaka huu kufikia 30.
 Hata hivyo, idadi hiyo ni kwa wale wanaochukua fomu hizo katika ofisi za TFF, kwani vilevile zinapatikana kupitia tovuti ya TFF ya www.tff.or.tz ambapo mwisho wa kuchukua na kurejesha ni saa 10 kamili alasiri Januari 18 mwaka huu.
 Waliochukua leo (Januari 16 mwaka huu) kuwania urais ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Jumanne Nyamlani, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA), Jamal Emil Malinzi na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kigoma, Omari Mussa Nkwarulo.
 Mwengine aliyechukua leo ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA), Elias Mwanjala anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kuwakilisha Kanda ya Iringa na Mbeya.
 Orodha kamili ya wadau waliochukua fomu kwenye ofisi za TFF ni Athuman Jumanne Nyamlani, Jamal Emil Malinzi na Omari Mussa Nkwarulo (urais), Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia (umakamu wa rais).
 Kwa upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama (Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza). 

SERIKALI KUFUATILIA MAENDELEO YA MIRADI INAYOZINDULIWA WAKATI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana nchini kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akisisitiza kwa wajumbe wa mkutano wa tathmini ya mbio za Mwenge mwaka 2012 kuhusu serikali kufuatiliaji  maendeleo ya miradi inayozinduliwa wakati wa mbio za Mwenge mjini Zanzbar.
 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Ali Nassoro Lufunga akizungumza na viongozi na waratibu wa mbio za Mwenge kutoka maeneo mbalimbali nchini kuhusu maandalizi ya mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2013.Mkoa wa shinyanga ulikuwa mwenyeji wa kilele cha mbio za Mwenge kwa mwaka 2012.
…………………………………………….
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
 Zanzibar.
Serikali inaandaa utaratibu wa kufuatilia maendeleo ya miradi yote inayozinduliwa wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru ili kuhakikisha kuwa miradi hiyo inakua endelevu na kuwanufaisha wananchi.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Zanzibar na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana nchini kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel wakati akitoa tathmini ya mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2012 na maendeleo ya miradi iliyozinduliwa wakati wa mbio hizo kwenye mkutano wa viongozi na waratibu wa mbio za Mwenge kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Amesema serikali ina wajibu wa kufuatilia kwa karibu miradi yote iliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru 2012 katika Halmashauri za wilaya, manispaa na Miji ili kuhakikisha kuwa gharama kubwa iliyotumika wakati wa uanzishaji na ujenzi wa miradi hiyo inawanufaisha wananchi kutoka kizazi kimoja hadi kingine ili kutunza hadhi na heshima ya Mwenge wa Uhuru.
Amesema mbio za Mwenge wa uhuru zimezindua miradi mingi nchini yenye thamani ya mabilioni ya fedha na kuongeza  kuwa si dhamira ya serikali kuona kuwa mwenge wa uhuru unatumika tu kuzindua miradi ya maendeleo bali kuhakikisha uendelevu wa miradi hiyo.