WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali imepanga kuajiri walimu
zaidi ya 35,000 kwa ajili ya shule za sekondari ili kukabiliana na
tatizo la uhaba wa walimu nchini.
tatizo la uhaba wa walimu nchini.
Ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Februari 19, 2015) wakati
akizungumza na mamia ya wakazi wa kata ya Kiwere, mara baada ya
kukagua ujenzi wa maabara na kuzindua nyumba nne za walimu kwenye
shule ya sekondari ya Kiwere, tarafa ya Kalenga, wilayani Iringa.
Waziri Mkuu alisema walimu hao watagawanywa kwenye shule kulingana na mahitaji yaliyokwishawasilishwa na kwamba watakapopata mgao wao hawana budi kuziangalia kwanza shule zenye miundombinu iliyokamilika kama ilivyo kwa shule hiyo.
Viongozi
mbali mbali wakijumuika na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakitoa
heshma za mwisho kwa marehemu Salmin Awadh Salmin katika ukumbi wa
Baraza la Wawakilishi Chukwani.

Mkurugenzi wa Mradi wa “AIDS free”, Bw. Samson Kironde(wa pili kushoto)
akitoa maelezo mafupi namna mradi huo utakaotekelezwa ndani ya Jeshi la
Magereza na Polisi katika mazungumzo rasmi yaliyofanyika Ofsini kwa
Kamishna Jenerali wa Magereza leo februari 20, 2015(wa pili kulia) ni
Mkurugenzi wa Operesheni na Fedha, Bw. Mike Hames(wa kwanza kushoto) ni
Afisa Mwandamizi anayeshughulikia masuala ya UKIMWI kutoka USAID, Bw.
Erick Mlang’ha.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akisisitiza jambo
katika mazungumzo rasmi yaliyofanyika Ofsini kwake leo februari 20, 2015
kati ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza, Polisi na Wasimamizi
Wakuu wa Mradi wa “AIDS – free” utakaotekelezwa ndani ya Jeshi la
Magereza.








Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wauguzi wa Kituo cha Afya cha
Mlowa katika jimbo la Ismani kabla ya kuzindua kituo hicho akiwa katika
ziara ya mkoa wa Iringa Februari 19, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akipima mapigo ya moyo ikiwa ni ishara ya kuzindua
kituo cha afya cha Mlowa katika jimbo la Isimani akiwa katika ziara ya
mkoa wa Iringa Februari 19, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akimsikiliza kwa makini Rais
Barack Obama (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba yake
katika Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani
uliofanyika katika Ukumbi wa Loy Henderson wa Wizara ya Mambo ya Nje,
jijini Washington DC nchini humo leo. Mkutano huo uliowashirikisha
Mawaziri wanaoshughulika na masuala ya usalama kutoka mataifa mbalimbali
duniani, Maafisa Waandamizi wa Umoja wa Mataifa (UN), Vyama vya Kiraia
na Sekta Binafsi ulijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupambana na
vurugu na ugaidi dunaini. Katika hotuba yake, Obama alisema mapambano
dhidi ya watu wenye msimamo mkali hayawezi kulinganishwa na mapambano
dhidi ya waislamu, hivyo hakuna dini yoyote inayowajibika kwa ugaidi,
isipokuwa watu ndio wanaowajibika kwa vurugu na ugaidi. Picha zote na
Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.














