TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, May 9, 2012

TCIB yakoshwa na NEC, yaikabidhi cheti

TCIB yakoshwa na NEC, yaikabidhi cheti
Posted: 08 May 2012 12:48 AM PDT

Na Agnes Mwaijega

KITUO cha Taarifa kwa Wananchi (TCIB), kwa mara ya kwanza  kimeikabidhi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) cheti cha usimamizi bora wa uchaguzi katika Jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Ofisa Utawala TCIB, Bi.Deborah Mushi, alisema pamoja na mapungufu yaliyojitokeza wakati wa  uchaguzi huo, bado NEC ilijitahidi kusimamia uchaguzi huo vizuri.
Bi. Mushi alisema kwa mujibu wa ripoti yao ya utafiti uliofanyika wakati wa mchakato mzima wa uchaguzi, NEC iliendesha uchaguzi ambao ulikuwa huru na haki.
"Kwa asilimia 70 NEC ilijitahidi kufanya kazi yake vizuri na ndiyo maana tumeamua kuipa cheti maalumu cha usimamizi mzuri katika uchaguzi wa Arumeru Mashariki," alisema.
Hata hivyo alitoa mwito kwa tume hiyo kuhakikisha inachukua hatua kali dhidi ya wale wote waliotumia lugha ya matusi katika kampeni za uchaguzi huo.
"Mimi nadhani kwa upande mwingine ni wajibu wa NEC kuhakikisha inaajiri watendaji wengi watakaosimamia suala la maadili katika chaguzi kwa ngazi zote za serikali kuanzia kata hadi taifa," alisema.
Alisema kuna umuhimu wa Serikali kuwa na utaratibu wa kutoa elimu endelevu kwa wasimamizi wa masuala ya uchaguzi kwa kuanzisha vipindi maalumu kwa ajili ya mafunzo na si kusubiri hadi wakati wa uchaguzi.
Bi. Mushi alitoa mwito kwa Serikali na NEC kuhakikisha zinatoa ruzuku inayostahili kwa vyama vyote vya siasa ili viweze kushiriki kikamilifu katika chaguzi.
Kwa kipindi kirefu NEC imekuwa ikilaumiwa kwa kushindwa kusimamia uchaguzi. Hatua ya NEC kupata cheti hicho inatafsiriwa kuwa inachangiwa na uongozi mpya wa tume.
Posted: 08 May 2012 12:43 AM PDT
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Bw. Benjamin  Mkapa, akiwasili eneo la   Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana, ili  kutoa ushahidi ya kesi inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania, nchini Italia, Profesa Victor Mahalu na aliyekuwa Ofisa Utawala wa Ubalozi huo, Bi. Grace Martin, wanaokabiliwa na mashitaka ya kuhujumu uchumi na kuisababishia Serikali, hasara ya zaidi ya Euro Mil 2. (Picha na Prona Mumwi)
Posted: 08 May 2012 12:40 AM PDT
Posted: 08 May 2012 12:39 AM PDT
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akimwapisha, Fenera Mkandara, kuwa Waziri mpya wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Ikulu Dar es Salaam jana. (Picha na Nyakasagani Masenza)
Posted: 08 May 2012 12:31 AM PDT
Wakazi wa jiji ambao majina na kazi wanazofanya (havikufahamika), walikutwa na kamera yetu kando ya makutano ya Barabara za Msimbazi na Uhuru, Dar es Salaam jana, wakiwa wameshikana mashati baada ya kutokuelewana katika shughuli zao. (Picha na Rajabu Mhamila)
Posted: 08 May 2012 12:27 AM PDT
Ili kukabiliana na tatizo la ulanguzi wa tiketi za usafiri wa boti ziendazo visiwani Unguja na Pemba, baadhi ya mawakala wenye ofisi zilizopo Feri, Posta jijini, wamechora bei halisi ya nauri katika kuta za ofisi zao, kama zinavyoonesha katika picha iliyopigwa, Dar es Salaam jana. (Picha na Charles Lucas)
Posted: 08 May 2012 12:24 AM PDT
Na Mwandishi wetu

IMEELEZWA kwamba Taasisi ndogo ndogo zinazotoa mkopo nchini zipo katika hatari ya kufilisika kutokana na  mazingira hali yalisi ya maisha.
"Hali hii ni hatari kwa taasisi hizi kwani ipo hatari ya kuongezeka kwa mikopo na kusababisha taasisi hizo kufilisika,"alisema  Bw.
Joel Mwakitalu, Mwenyekiti Makamu wa Tanzania Chama Taasisi za
Fedha nchini (TAMFI).
Alisema  duniani kote, mfumo wa kukopesha kwa kikundi  ni mbinu bora kwa ajili ya kuendeleza  mikopo kwa maskini ambao hawana dhamana kwani wanatakiwa kupata mikopo kutoka tawala na mabenki.
Bw. Mwakitalu alisema  hivi karibuni alisikia katika vyombo vya habari kuwa vikundi vinavyochukua mkopo vipo katika hali ngumu kutokana na mabadiliko ya maisha,ukuaji wa miji ,changamoto na kuongezeka kwa watoa mikopo.
kundi mikopo mbinu ilikuwa kuwa gumu kutokana na mabadiliko
maisha, ukuaji wa miji changamoto na kuongezeka kwa watoa mikopo.
"Mabadiliko ya maisha, ukuaji wa miji changamoto na kuongezeka kwa mikopo
 ni baadhi ya mambo kuchochea hatari ya kufilisika kwa taasisi hizo
Alisema baadhi ya sababu zinazochangia taasisi hizo kufilisika mfumo mbaya wa ukopeshaji ambapo kuna mapungufu katika sheria na sera za serikali gharama za maisha majanga matumizi mabaya ya fedha , matatizo ya kifamilia na shinikizo.
Wadau katika mjadala  huo waliaafiki kuwa watu wanaokopa kuanzia sh.milioni marejesho yake si mazuri ukilinganisha na wanaochukua chini ya hapo . wakakubaliana naye kuhusu hatari ya mikopo,hasa kwa kiasi sh. milioni 1.lakini wanaochukua chini ya hapo marejesho ni mazuri 
Alisema kama mwanachama akishindwa kurudisha mkopo wa sh.1000,000 inakuwa vigumu kwa wanachama kumsaidia mwanachama mwenzao kutokana na mazingira ya hali halisi
Mkurugenzi Mtendaji wa Tujijenge Microfinance   Bw. Jimmy Makugira, alisema
tatizo la ni kubwa . "Lakini baadhi ya taasisi ndogo za fedha zina lawama
na lawama,wengine hawana wakaguzi wa ndani na pia wao huajiri maofisa ambao hawana uzoefu na kuaribu kila kitu.
Washiriki alilaumu kuwa ukosefu wa kumbukumbu kwa taasisi za mikopo ni  miongoni mwa sababu zinazochangia mteja moja kupata mkopo mara tatu au zaidi  kutoka taasisi nyingine kwa wakati mmoja na wengine hutumia vitambulisho tofauti.
Kazi ya TAMFI ni kuimarisha sekta ndogo za fedha za Tanzania kwa kukuza
ushirikiano na ushirikiano kati ya mashirika ya wanachama wake,
kutoa mafunzo, kufanya utafiti, na kushawishi serikali
ya Tanzania.
Posted: 08 May 2012 12:18 AM PDT
Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal (kulia), akiwapongeza Manaibu Waziri wapya, baada ya kuapishwa Ikulu, Dar es Salaam jana. (Picha na Michael Machella)
Posted: 08 May 2012 12:16 AM PDT

Na Charles Mwakipesile, Mbeya

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya (CCM), Dkt.Mary Mwanjelwa, amesema hajutii kukosa kuteuliwa katika Baraza jipya la Mawaziri lililoapishwa jana kwa kuwa halikuwa lengo lake la kuwania ubunge na hana mpango wa kuhamia CHADEMA, kama inavyoelezwa.
Alisema uvumi huo unaenezwa na watu aliodai ni wapinzani wake kisiasa mkoani hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari akiwa ameongozana na Katibu wa CCM mkoani Mbeya, Bi.Cerena Shumbuso, Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi, Bw.Bashiru Madodi na viongozi wengine, Dkt.Mwanjelwa alisisitiza kuwa yeye ni kada aliyeivishwa na kuandaliwa na CCM kwa miaka mingi, hivyo hawezi kukurupuka kwenye kutoa maamuzi.
Alisema kamwe hawezi kuhama CCM kwa madai ya kukosa kuteuliwa katika nafasi za uwaziri kwa kuwa makubaliano yake ya kuwania nafasi ya ubunge ni kuwatumikia wananchi wa Mbeya na si kuteuliwa kuwa waziri.
Alisema anafahamu kuwa CCM ina wabunge wengi wasomi na wachapa kazi kama yeye, hivyo ni amri ya mamlaka ya uteuzi kuangalia mbunge yeyote anayeonekana kufaa kuteuliwa bila kuhojiwa wala mtu kuchukia na kuamua kukimbia chama.
"Siwezi kuhama CCM kamwe eti kwa sababu sijateuliwa kuwa waziri, hapana mimi nimefurahi sana wenzangu ndani ya chama kuteuliwa na kuonekana wanafaa tena anayeteua ni rais ambaye  ninaamini hakurupuki na uwezo wake ni mkubwa  wa kupembua mambo, hivyo siwezi kukosa akili kwa kuhama chama kwa madai ya kuchukia kutoteuliwa,"alisema.
Alisema anaamini kuwa bado anakubalika ndani ya chama hicho hususani Jumuiya ya Umoja wa Wanawake iliyomteua kutokana na imani waliyonayo kwake atagombea tena kupitia kundi la viti maalumu (CCM) mwaka 2015 kwa kuwa anaamini kuwa amefanya mambo makubwa ndani ya jumuia hiyo hadi sasa.
Dkt.Mwanjelwa alisema kuwa atagombea nafasi hiyo baada ya kumaliza kipindi cha miaka mitano ili kuonesha kuwa lengo lake ni kuwatumikia wananchi wa Mbeya.
Posted: 08 May 2012 12:13 AM PDT
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akimuapisha Balozi Hamis Kagasheki, kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha mawaziri iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam jana. (Michael Machella)
Posted: 08 May 2012 12:11 AM PDT
Na Gladness Mboma

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini Bw. Zitto Kabwe, amesema watamshangaa Rais Jakaya kikwete, kama hatamchukulia hatua za haraka kwa kumfikisha mahakamani aliyekuwa Waziri wa Fedha, Bw. Mustapha Mkulo na wenzake, waliotuhumiwa moja kwa moja na wabunge kwa ubadhirifu.

Bw.Zitto alitoa kauli hiyo jana kwenye viwanja vya Ikulu, ambapo alishiriki tukio la kuapishwa kwa mawaziri na manaibu waziri.
"Kuna wale waliotuhumiwa moja kwa moja kama vile Mkulo, tunataka ndani ya muda mfupi Rais atawafikisha mahakamani,"alisema Bw. Zitto ambaye juzi aliwatahadharisha Mawaziri kutofanya sherehe na kuvishwa maua wakati watakapoapishwa, alisema kuwa wapo mawaziri waliokwenda na maua hayo, lakini yalikataliwa getini.
Katika tukio la jana hakuna waziri aliyevalishwa taji la maua baada ya kuapishwa na ndugu wa karibu, lakini hakuna ushahidi kuwa yalizuiliwa mlango wa kuingilia Ikulu kama alivyodai Bw. Zitto.
Alisema kwamba sasa wana kazi ya kusimamia Serikali ili iendelee kuwawajibisha wale wote wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu wa mali ya umma.
Bw. Zitto alisema kuna watu ambao hawana makosa, ila kosa lao limesababishwa na watendaji wa chini, hivyo inabidi Rais Jakaya Kikwete ashikilie msimamo wake wa kuwawajibisha wale watendaji wote waliosababisha hasara kwa umma. 
Alisema kuwa wamedhihirisha kwamba bunge lina uwezo wa kung'ata na halina meno ya plastiki na kwamba uteuzi wa mawaziri hao umetokana na shinikizo lao.
Posted: 08 May 2012 12:08 AM PDT

Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akimuapisha Dkt. Hussein Mwinyi, kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam jana. (Picha na Nyakasagani Masenza)
Posted: 08 May 2012 12:05 AM PDT

Makamu wa Rais, Dkt. Mohamed Gharib Bilal (kulia), akimpongeza Bi. Janeth Mbene, baada ya kuapishwa Ikulu, Dar es Salaam jana kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi. (Picha na Nyakasagani Masenza)
Posted: 08 May 2012 12:03 AM PDT

Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akimuapisha Mhandisi Paul Chiza kuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, wakati wa hafla Ikulu Dar es Salaam jana. (Michael Machella)
Posted: 07 May 2012 11:58 PM PDT

Na Mwali Ibrahim

BINGWA wa mchezo wa Kickboxing nchini, Japhet Kaseba ametamba KO ya Francis Cheka dhidi ya Mada Maugo, haimtii hofu katika pambano lao litakalofanyika Sikukuu ya Sabasaba katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kaseba amejitapa hivyo licha ya pambano lao la mwaka 2009 dhidi ya Cheka kukung'utwa kwa KO ambapo pambano la sasa litakuwa katika uzito wa kilogram 75, raundi 12 huku Cheka akiutetea ubingwa wake wa IBF aliounyakua baada ya kumtwanga Maugo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kaseba alisema yeye hatishwi na matokeo hayo zaidi anaendelea na mazoezi ili kuhakikisha katika pambano hilo hafanyi makosa.

"Yale ni matokeo yake na Maugo lakini mimi hayanitishi zaidi ya kunipa changamoto ya kuweza kujiweka sawa na kuweza kumkabili katika mashindano hayo," alisema.

Alisema tayari ameishaanza mazoezi kwa ajili ya pambano katika gym yake iliyopo komakoma, Mwanyamala na ana imani atafanya vyema kwani ana muda mrefu wa kujiandaa.

Alisema katika kipindi chote kabla hajapata pambano alikuwa akifanya mazoezi, hivyo ana imani hadi kufikia siku hiyo atakuwa amepata mazoezi ya kutosha.
Posted: 07 May 2012 11:56 PM PDT

Na Amina Athumani

TIMU ya Taifa ya netiboli (Taifa Queens), leo itafungua pazia la michuano ya Kombe la Afrika kwa kuumana na Lesotho katika mchezo utakaopigwa saa nane mchana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kabla ya mchezo huo utatanguliwa na mchezo kati ya Botswana itakayomenyana na Malawi ambapo mchezo huo nao utachezwa kwenye uwanja huo huo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Netoboli Tanzania (CHANETA), Rose MKisi alisema maandalizi kwa ajili ya michuano hiyo imekamilika.

Alisema timu zote nane zimeshawasili kwa ajili ya michuano hiyo itakayofunguliwa na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete.

Alisema tayari viongozi mbalimbali kutoka Shirikisho la Netiboli Duniani (IFNA) pamoja na waamuzi mbalimbali watakaochezesha michuano hiyo wamewasili.

Alisema ratiba nyingine ya michuano hiyo itatolewa leo mara baada ya ufunguzi zitakazopambwa na nyimbo za mataifa mbalimbali yanayoshiriki michuano hiyo kwa kupigwa kwa blast band.
Alisema kwa upande wa Taifa Queens ipo kwenye ari ya ushindani na kwamba makocha wote kutoka Bara na Zanzibar wamejipanga kuhakikisha timu hiyo inaaza vema michuano hiyo.
Taifa Queens inaundwa na Pili Peter, Irene Elias, Beth Kazinja, Jacqueline Skozi, Restuta Boniface, Doritha Mbuta na Lilian Sylidion.
Wengine ni Matalena Muhagama, Paskalia Kibayasa, Siwa Juma, Subira Juma, Subira Songwe, Penina Mayunga, Evodia Kazinja, Niza Nyange, Mwanaid Hassan, Lydia Samwel na Joyce Edward.

Michuano hiyo itafikia kilele chake Mei 12, mwaka huu ambapo hii ni mara ya pili kufanyika kwa michuano hiyo ambapo mara ya kwanza ilifanyika 2009.
Michuano hiyo itaiwezesha Tanzania kupanda viwango vya Dunia vya IFNA ambapo kwa sasa Tanzania ipo nafasi ya 20.
Posted: 07 May 2012 11:55 PM PDT

Na Rehema Mohamed

MAWAKILI upande wa utetezi katika kesi inayomkabili msanii maarufu nchini, Elizabert Michael 'Lulu', wamewasilisha mahakamani ombi la kutaka mahakama hiyo imuone mshtakiwa huyo ana miaka chini ya 18 hivyo kesi hiyo ihamishiwe katika mahakama ya watoto.

Ombi hilo liliwasilishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana na mmoja wa mawakili wanaomtetea Lulu, Kened Fungamtama mbele ya Hakimu, Agustina Mmbando wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Wakati Fungamtama akiwakilisha ombi hilo, aliiambia mahakama hiyo kuwa mshtakiwa huyo ana miaka 17, hivyo shauri lake linatakiwa kuhamishiwa katika mahakama ya watoto.
Aliongeza kuwa upande wa mashtaka haujawasilisha mahakamani hapo pingamizi lolote kuhusu umri wa miaka hiyo hata pale mshtakiwa mwenyewe alipoieleza mahakama kuwa ana miaka 17 badala ya 18.
Katika kuunga mkono ombi hilo Fungamtama aliwasilisha cheti cha kuzaliwa  alichodai kuwa cha mshtakiwa ili mahakama hiyo iweze kujiridhisha kuhusu umri wa mshtakiwa huyo kinachoonesha mwaka na mahali alipozaliwa.
Hata hivyo wakili wa serikali katika kesi hiyo, Elizabert Kaganda alipinga ombi hilo na kudai kuwa ameshtushwa na ombi hilo kwakuwa kesi imekuja kutajwa na kwamba mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza ombi lolote kwakuwa kesi hiyo haitasikilizwa mahakamani hapo.
Kaganda alidai kuwa kesi hiyo bado ipo katika hatua ya upelelezi ambao bado haujakamilika na kwamba miongozi mwa vitu wanavyovichunguza ni pamoja na umri wa mshtakiwa huyo.
Aliongeza kuwa katika cheti cha kuzaliwa kilichooneshwa mahakamani hapo na Fungamtama, alidai kuwa hawawezi kukiamini kwani kina jina la Dayana Elizabert wakati mshtakiwa anaitwa Elizabert Michael.
"Mheshimiwa hakimu tunaomba tupewe hicho cheti tukichunguze pia tupewe muda tuchunguze zaidi kuhusu umri wake,kama itabainika ana miaka chini ya 18 mshtakiwa ana haki zote za kushtakiwa katika mahakama ya watoto"alisema Kaganda.
Akitoa uwamuzi wa maombi hayo hakimu Mmbando aliutaka upande wa utetezi kusubiri kesi hiyo itakapowasilishwa katika Mahakama Kuu ndipo wawasilishe maombi hayo kwakuwa mahakama hiyo hivi sasa haina mamlaka.
"Mahakama hii inajua kuwa shauri lililo mbele yake ni la mauaji,hatuna mamlaka ya kutoa uamuzi wowote kwa sasa ,maombi yoyote yafanyike Mahakama Kuu"alisema Mmbando.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 21, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.Katika kesi hiyo Lulu anashtakiwa kwa kudaiwa kusababisha kifo cha msanii mwenzake wa filamu, Steven Kanumba.
Posted: 07 May 2012 11:53 PM PDT
Mtuhumiwa wa kesi ya mauaji ya aliyekuwa msanii maarufu wa filamu nchini, Steven Kanumba, Bi. Elizabeth Michael 'Lulu', akiwa chini ya ulinzi mkali wa askari magereza, wakati akitolewa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana, mara baada ya kesi kuahirishwa kwa mara ya tatu. (Picha na Prona Mumwi)
Posted: 07 May 2012 11:48 PM PDT
Posted: 07 May 2012 11:45 PM PDT

Na Grace Ndossa

NAIBU  Waziri wa Habari, Michezo, Vijana na Utamaduni, Amos Makalla amesema  changamoto zilizopo kwenye sekta ya michezo atahakikisha anazitafutia ufumbuzi.

Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana baada ya  kuipishwa kuwa Naibu Waziri katika wizara hiyo na Rais Jakaya Kikwete na kueleza kuwa anatambua changamoto zilizopo katika sekta hiyo
"Natambua changamoto zilizopo katika sekta hiyo, hivyo wadau wa michezo wamepata mtu anayefaa katika nafasi hiyo na kuahidi kuchapa kazi kwa kushirikina na  wanamichezo,"alisema Makalla.
Aliongeza:"Kwa kuwa mimi ni mwanamichezo nitahakikisha nafasi hiyo naitumia vyema kuimarisha changamoto zinazoikabili sekta hiyo".
Alisema changamoto zilizopo katika sekta hiyo anazitambua na hivyo atazifanyia kazi ili waweze kusonga mbele bila kurudi nyuma.
Hata hivyo, alitamba kuwa anaimudu nafasi aliyochaguliwa kwani kwa kushirikiana na waziri wataangalia changamoto zilizopo katika sekta hiyo na kuzifanyia kazi.
Alisema kuwa wadau wa michezo wakae mkao wa kula kwani  hata yeye ni mwana michezo na ni Kapteni wa time ya Wabunge.
Posted: 07 May 2012 11:43 PM PDT

Na Victor Mkumbo

WACHEZAJI na viongozi wa klabu ya soka ya Azam FC, wamepewa tuzo na uongozi wa klabu hiyo baada ya kufanya vizuri katika Ligi Kuu Bara na kushika nafasi ya pili.
Wachezaji hao walipewa tuzo za vyeti baada ya kuonekana kujituma vilivyo katika Ligi Kuu na kuonesha ushindani mkubwa.
Katika hafla hiyo, iliyofanyika Dar es Salaam juzi usiku, mshambuliaji John Bocco alizawadiwa tuzo ya kuwa mfungaji bora wa msimu uliopita baada kufunga mabao 19 ambapo hakuna mchezaji wa timu yoyote aliyofikia idadi hiyo.
Naye Mwenyekiti wa klabu hiyo, Abubakar Bakhresa, alisema wachezaji hao hawana budi kuwa waangalifu katika kipindi hiki cha likizo.
Alisema kwakuwa wametoa mchango mkubwa katika kufanikisha timu hiyo kushika nafasi ya pili, wasibweteke bali waendelee na nidhamu waliyokuwa nayo katika kipindi chote cha msimu uliopita.
Alisema kutokana na mafanikio hayo wanatarajia mwakani kujipanga vizuri na hatimaye kutwaa ubingwa wa ligi hiyo.
Posted: 07 May 2012 11:41 PM PDT
Watoto Yasini Juma (kushoto) na Haruna Magara wakiwania mpira wakati wa mchezo wao uliofanyika nyumbani kwao Buguruni Kisiwani Dar es salaam juzi.Ukosefu wa viwanja vya kuchezea kunasababisha watoto mbalimbali kucheza sehemu zozote zenye nafasi.Picha na Rajabu Mhamila
Posted: 07 May 2012 11:35 PM PDT

Na Zahoro Mlanzi

MECHI ya Ligi Kuu Bara iliyowakutanisha watani wa jadi, timu za Simba na Yanga iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 260,910,000 huku kila timu ikipata sh. 62,646,395.
Mchezo huo ulikuwa ni moja kati ya michezo ya kufunga pazia la ligi hiyo uliochezwa juzi ambapo Simba iliweka historia nyingine kwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0.
Kwa ushindi huo, Simba ambayo ilishatwaa ubingwa huku ikiwa na mechi moja mkononi, imefanya ubingwa huo kuwa na raha ya aina yake baada ya kuifunga Yanga.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari Dar es Salaam na Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura ilieleza kwamba mechi hiyo ilihudhuriwa na watazamaji 41,733.
"Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh. 10,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 VIP C, sh. 30,000 VIP B na sh. 40,000 VIP A ambapo watazamaji 36,980 walinunua tiketi za sh. 5,000 wakati 203 walikata za sh. 40,000," alisema Wambura.
Alisema kutokana na mapato hayo kila timu ilipata sh. 62,646,395, asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 39,799,830 wakati TFF ilipata sh. 19,908,361.
Alisema gharama za mechi kabla ya mgawo ni nauli ya ndani ya waamuzi na kamishna sh. 20,000, posho ya kujikimu kwa kamishna sh. 40,000, mwamuzi wa akiba sh. 30,000, gharama za tiketi sh. 8,539,950.
Pia alisema maandalizi ya uwanja ni sh. 400,000, umeme sh. 300,000, ulinzi na usafi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina ni sh. 2,000,000.
Posted: 07 May 2012 11:33 PM PDT

Na Elizabeth Mayemba

KUFUATIA kipigo cha mabao 5-0 dhidi ya Simba, mmoja wa aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya klabu ya Yanga Habert Marwa,baada ya kuonyesha kusikitishwa sana na kipigo hicho, alisema ili timu hiyo iwe na mafanikio makubwa haina budi iongozwe na vijana.

Akizungumza Dar es Salaam jana na mwandishi wa habari hizi baada ya kuhojiwa  Marwa alisema, ili timu iwe na hadhi yake ni lazima iongozwe na isimamiwe na  vijana ambao ndiyo nguvu kazi.

"Kama jina lenyewe la timu Young Africans, hivyo  nguzo ya ushindi ni vijana kama ilivyo pia kwa wachezaji, kama uongozi utasajili wachezaji wazee lazima timu ifanye vibaya, lakini wakisajili wachezaji wenye umri mdogo watafanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kwa kuwa watakuwa ni damu changa," alisema Marwa.

Alisema timu inapofungwa wanaoumia na kusononeka wengi wao ni vijana ambao pia hujitolea kwa hali na mali kuichangia timu kimapato kwa kulipia viingilio na kuishangilia timu yao inapocheza.

Kwa hali hiyo Marwa alishauri vijana wenye moyo na jitihada za namna hiyo ndiyo wanaostahili kupewa jukumu la kuiongoza Yanga.

Marwa alisema Mwenyekiti wa klabu hiyo, Llloyd Nchunga alifanya kosa kubwa sana kuwakabidhi wazee timu bila kushauriana na vijana baada ya uongozi wake kushindwa.

"Tunaamini kabisa wazee wanamawazo mazuri sana ya kuushauri uongozi unapokuwa na dhamira sahihi ya ushindani, kwani uzoefu walioupata enzi hizo wakiwa viongozi tena vijana ungewasaidia viongozi kwa wakati huu kufanya vizuri," alisema.

Alisema aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Davis Mosha ambaye alijiuzulu wadhifa huo, alijitahidi kwa kiasi kikubwa kuwashawishi na kuwashirikisha yeye na vijana wengine kuchangia kwa fikra na uwezo wa kiuchumi pamoja na nguvu kazi ili timu hiyo iweze kupata mafanikio na hadhi yake pindi tu baada ya yeye kuchaguliwa.
"Baada ya Mosha kujiuzulu wengi wao na mimi nikiwemo tulijiuzulu siku moja baada ya yeye kujiuzulu," alisema
Pia aliwaasa vijana kujitokeza kwa wingi kwenda kuchukua kadi za uanachama wa klabu hiyo, badala ya kuwa mashabiki tu ili wapate fursa ya kuchagua viongozi bora na imara.
Hata hivyo alipoulizwa uwepo wake ndani ya klabu hiyo alisema "Baada ya kujiuzulu niliendelea kuwa mwanachama na shabiki kama ilivyokuwa awali, ikiwa na kutoa mawazo kama nilivyotoa mchango wangu huu wa mawazo kwa sasa,"alisema.