TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, December 28, 2013

DAR ES SALAAM CITY COLLEGE YATANGAZA MUHULA MPYA WA MASOMO KATIKA MWAKA WA 2014.

 Mkuu wa Chuo cha Uhandishi wa Habari na Utawala, Dar es Salaam City College(DACICO TANZANIA), Mr. Idrisa Mziray, ametangaza muhula mpya wa Masomo kwa Wanafunzi waliomaliza masomo ya Kidato cha nne na Sita kwa ajili ya Kujiunga na chuo hicho kilichopo katika Mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya na Sumbawanga.

Akizungumzia Muhula huo mpya wa Masom Mkuu wa Chuo hicho, Bwana Mziray alisema kuwa kwa sasa nafasi bado zinapatikama makao makuu ya Chuo hicho jijini Dar es Salaam Kibamba Ccm, Mbeya Jengo la Huyole na Sumbawanga Mjini ambapo fomu zinapatiokana kwa shilingi Elefu kumi, 10,000/=

ameongeza kuwa, mbali na kozi za Uandishi wa Habari na Utangazaji pia zinapatikana Kozi za Fani mbali mbali ikiwemo ile ya Ugavi, Utawala na ningine nyingi.
 aidha Chuo hicho ambacho kina Makao yake Makuu jijini Dar es Salaam ni Chuo nyenye Manzali ya Kupendeza na pia Huduma ya Kulala(Hostel) zinapatikana maeneo ya Chuo na Usalama ni mkubwa kwa Wanafunzi Wote ikiwa ni pamoja na Huduma nzuri ya Masomo.

======================================================================

USAJILI WA DIRISHA DOGO KUINUSURU MGAMBO KUSHUKA DARAJA!!!!!!!

273f8-63 
Moja ya Kikosi cha Mgambo Shooting mechi za nyuma katika michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara. Picha na Maktaba

VIBONDE wa ligi kuu soka Tanzania bara, Mgambo Shooting ya mkoani Tanga imeanza mazoezi ya kujiandaa na mikikimikiki ya kukwepa mkasi wa kushuka daraja msimu  wa 2013/2014.
Akizungumza leo baada ya mazoezi ya timu hiyo, kocha msaidizi , Moka Shaban Dihimba amesema wameongeza wachezaji wanne katika dirisha dogo la usajili, hivyo watakuwa na nguvu mpya.
“Tulikuwa na mapungufu mengi, wachezaji walikuwa na hofu kubwa,  ndio maana tulifanya vibaya na kushika mkia. Tumewasajili Suleiman Khatib, Bolly Ajali, Amri Sambinga na Issa Ali ambao watatusaidia kupambana kufa na kupona”. Alisema Dihimba.
Dihimba alisema mazoezi yanakwenda vizuri chini ya kocha mkuu, Ramadhan Kampira na kikubwa wanachofanya kwa sasa ni kutafuta kasi na kumiliki mpira ili kuzikabili timu pinzani kwa umahiri.
“Timu za ligi kuu si kwamba zina mpira mkubwa sana, zote zinacheza soka la kawaida na sisi tunaweza kuwamuda kabisa. Nakuhakikishia kuwa kwa mechi 13 zilizobaki, tutabaki ligi kuu”. Aliongeza Dihimba.
Kocha huyo alikiri kufanya vibaya zaidi mzunguko wa kwanza kwasababu walishinda mchezo mmoja tu, wakatoa sare tatu na kufungwa mechi tisa, hivyo kujikusanyia pointi 6 tu katika nafasi ya mwisho.
Alipoulizwa kwanini timu imekuwa na matokeo mabaya hata msimu wa mwaka jana, Dihimba alieleza kuwa wachezaji wao wanakosa uzoefu na wanatawaliwa na hofu hasa wanapokutana timu kubwa.
“Tunakaa na wachezaji kwa muda mwingi na kuwaelekeza nini cha kufanya, lakini wamekuwa wakifanya makosa makubwa yanayoigharimu timu. Wana makosa ya kiufundi na tumeyaona, lakini kwa sasa tumejipanga vizuri kushindana”. Alitamba Dihimba.

WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA WATANGAZWA

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini, akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo (jana), kuhusu wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2014. Kushoto ni Naibu wake, Zuberi Samataba. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo (jana) kuhusu wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2014. Kushoto ni Naibu wake, Zuberi Samataba.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini, jijini Dar es Salaam leo (jana), wakati alipozungumza nao kuhusu wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2014. 
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini, akifafanua jambo wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari, Dar es Salaam 
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini, akielezea jambo wakati alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari, kwenye mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini, akifafanua jambo waandishi wa habari, katika mkutano huo, jijini jana
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini, akisikiliza maswali ya waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo na waandishi jijini, Dar es Salaam 
Na Magendela Hamisi
IDADI ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani umeongezeka kwa asilimia 31.37, huku ufaulu ukiongezeka kwa asilimia 19.
Hayo yalielezwa leo, jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini, wakati akitangaza wanafunzi waliomaliza darasa la saba ambao wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Januari mwakan
Hata hivyo wakati idadi hiyo, ikifanikiwa kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza, wanafunzi 13 matokeo yao yamefutwa kutokana na kubainika kufanya udanganyifu wakati wa mtihani huo kumaliza elimu ya msingi mwaka huu.
Kuhusu ufaulu kuongezeka Sagini alisema kwa asilimia 19 kutokana na watahiniwa 844,938 sawa na asimilia 97.34 waliofanya mtihani huo.
Alisema kati ya hao wasichana walikuwa 446,115 sawa
na asilimia 97.85 wakati wavulana ni 398,823 sawa na
96.78.Wanafunzi  23,045 sawa na asilimia 2.66 hawakufanya mtihani kwa sabanu mbalimbali ikiwemo ugonjwa, vifo na utoro.
“Matokeo hayo ya mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi yanaonesha alama ya juu ufaulu kwa wavulana ni 244 na wasichana ni 241 kati ya 250,” alisema.
Aliongeza kutokana na ongezeko hilo la ufaulu wanafunzi
411,127 kati ya 427,609 waliofaulu wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za Serikali katika awamu ya kwanza ikiwa ni sawa na asilimia 96.15.
Alifafanua wanafunzi hao waliochaguliwa wasichana ni  201,021 na wavulana wakiwa 210, 106 huku akifafanua kuwa wanafunzi 6,482 ambao wamekosa nafasi awamu ya kwanza halmashauri zimetakiwa kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 412 ili kufanikisha wanafunzi hao kujiunga na elimu ya sekondari kuanzia Februar na Machi mwakani.
Alitumia nafasi hiyo, kuitaja mikoa ambayo wanafunzi wake wamekosa nafasi za kujiunga kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza ni  Morogoro wanafunzi 315, Katavi 261, Dar es Salaam 11, 796,  Dodoma 549, Mtwara 120, Mbeya 1484 na Geita 1578.
Aliwataka wazazi washirikiane na halmashauri kutatua tatizo hilo ili kutoa fursa kwa watoto waliochaguliwa kwenda shule.
Hata hivyo, alisema wanafunzi 13 wamefutiwa mitihani yao kutokana na kufanya udanganyifu na kwamba idadi ya udanganyifu kwenye mtihani huo imepunguaikilinganishwa na mwaka jana ambapo waliodanganya walikuwa 219.
CHANZO:  www.bayana.blogspot.com

LORI LA MAFUTA LAKAMATWA LIKISAFIRISHA VIPODOZI HATARI

Baadhi  ya  vipodozi vilivyokamatwa 
Mifuniko ya  tenki la mafuta  ikiwa imefunguliwa baada ya kutolewa vipodozi 
Ndani ya  lori  hilo  baada  ya  kutolewa  vipodozi  hivyo 
Kamanda wa  polisi  mkoa  wa Iringa Ramadhan Mungi  akionyesha shehena ya  vipodozi  ambavyo  vimekamatwa vikisafirishwa  ndani ya  lori la mafuta  leo 
Kamanda  wa  polisi  mkoa  wa Iringa ,Ramadhan Mungi akionyesha lori la mafuta  lililokuwa na shehena ya vipodozi
Jina  la kampuni  linalomiliki  lori  hilo 
Maofisa  wa mamlaka ya chakula  na dawa  Manispaa ya  Iringa  wakikagua  vipodozi  hivyo 
Na Francis Godwin Blog JESHI la  polisi  mkoa  wa  Iringa  limewakamata  watu  wawili  akiwemo  dereva  wa tenki  la  mafuta  lenye namba za usajili  T 247 BHP  wakisafirisha shehena  ya   vipodozi maboksi 779 vikiwa vimewekwa ndani ya tenki  hilo la mafuta  kutoka nchi  za  kusini  mwa Tanzania  kuelekea  jijini  Dar es Salaam .
 
Kamanda  wa  polisi wa mkoa  wa  Iringa Ramadhan  Mungi  alisema  kuwa  lori hilo lenye namba za usajili  T 247 BHP  likiwa na tela  lenye namba T 598 BMK   ni mali ya kampuni ya  World OIL Ltd  ya  Jijini Dar es Salaam lilikuwa  likiendeshwa na  Mohamed  Sadru (23) mkazi  wa  Mbezi Temboni jijini  Dar es Salaam .
 
 Mbali  ya  dereva   huyo  pia  jeshi  hilo  linamshikilia mfanyabiashara  aliyekuwa akisafilisha  mzigo  huo  Bw Kassim Kaifa (23) mkazi  wa jijini Dar es Salaam  kwa tuhuma  za  kuhusika na mzigo  huo.
 
Kamanda Mungi  aliwaeleza  wanahabari  leo    kuwa  mtego wa jeshi  la  polisi  uliweka  baada ya  kupokea  taarifa  kutoka kwa rai  wema kuhusiana na lori  hilo kutumika isivyo  kwa kusafirisha vipodozi  hivyo.
 
Alisema  kuwa  taarifa  kuhusiana na lori  hilo kusafirisha vipodozi  badala ya  mafuta   waliitapata  kutoka  jana  na mtego  wa  kulikamata  lori hilo  umefanikiwa majira ya saa 9 alfajiri  ya leo 
 
Hata   hivyo  alisema  kuwa  sehemu  kubwa ya  vipodozi  hizo   ni  vile  ambavyo vilipigwa marufuku na  serikali kutokana na kuwa na madhara  makubwa kwa afya  ya  watumiaji  wa vipodozi  hivyo.
 
Alisema  kuwa  jeshi la  polisi  limefanikiwa  kumata  vipodozi hivyo kwa  kushirikiana na mamlaka ya  chakula na  dawa ,wakala  wa  barabara  mkoa  wa Iringa  na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) 
 
Kamanda huyo  alisema kuwa  watuhumiwa hao   watafikishwa mahakamani  mara  baada ya  uchunguzi  kukamilika na  kuwa ni mapema  kwa  sasa  kuitaja thamani  ya vipodozi  hivyo na  nchi  ambayo lori  hilo  lilikuwa  likitoka kutokana na sababu  za kiusalama.

UTENDAJI KAZI WA MBUNGE FILIKUNJOMBE WAWAVUTIA WAPIGA KURA WAAMUA KUMBEBA MGONGONI


Wananchi  wa kata  ya Manda  Ludewa wakimfuta  jasho  mbunge  wao  Deo Filikunjombe kama  kumpongeza kwa utekelezaji  mzuri wa ahadi  na uwakilishi  uliotukuka bungeni 
Mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akiwa amebebwa na mpiga kura  wake kama  kumpongeza kwa utendaji wake mzuri 
Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akifurahia  baada ya  kupongezwa kwa  kubebwa mgongoni na mpiga kura wake
Mbunge Filikunjombe kati  akipokea  zawadi ya  mbuzi  kutoka kwa  mkazi wa manda huku mkewe Habiba  akishukuru (picha na Blogu ya Francis Godwin)

THEM FELIX ATAMBA KUWA MKALI WA KUPASIA NYAVU KATIKA LIGI AMBAPO KAGERA SUGARI ITAKAPOANZA MAZOEZI RASMI JANUARI 2,

1
KLABU ya Kagera Sugar inaingia kambini desemba 31 mwaka huu, lakini mazoezi yataanza rasmi januari pili mwakani kujiwinda na mzunguko wa pili  ligi kuu soka Tanzania bara unaotarajia kuanza kushika kasi januari 25, 2014.
Kocha msaidizi wa klabu hiyo, Murage Kabange ameuambia mtandao huu kuwa nia yao ni kurejesha makali yao kama msimu uliopita.
“Mipango ya kambi imekamilika, mimi na kocha mkuu Jackson Mayanja tunajiandaa kukisuka kikosi chetu upya. Kuna makosa yaliyokuwepo mzunguko wa kwanza, tuliyagundua mapema na sasa kazi ni kurekebisha tu”. Alisema Kabange..
Kabange aliongeza kuwa katika dirisha dogo la usajili wamemuongeza  Andrew Mathew kazembe kutoka Abajalo FC  ili kukamilisha idadi ya wachezaji 25.
“Tulitumia muda mrefu kumchunguza mchezaji huyo, tumezingatia nidhamu na uwezo wake, kwa kiasi kikubwa atatusaidia ngwe ya pili  ya ligi kuu bara”. Aliongeza Kabange.
Aidha kocha huyo alisema tatizo la safu ya ulinzi limepata dawa baada ya beki wao wa kati, Amandus Nestar kurejea uwanjani  kufuatia  kupoma tatizo lake la mguu.
“Karibu mzunguko mzima, Nestar amekuwa akisumbuliwa na mguu, madaktari wamefanya jitihada kubwa kuhakikisha anarejea uwanjani. Hivi ninavyozungumza na wewe, beki huyo yuko tayari kuanza mazoezi na hali hii itaimarisha safu yetu ya ulinzi”. Alisema Kabange.
Kwa upande wake mshambuliaji hatari wa Kagera Sugar, Them Felix alisema kuwa anajiandaa vikali kuhakikisha anaisadia klabu yake kufanya vizuri na hatimaye kuingia tatu bora msimu huu.
Them aliongeza kuwa mchezaji wa mpira wa miguu hana mapumziko, pale timu inapopewa mapumziko, yeye anatakiwa kutafuta njia mbadala ya kufanya mazoezi binafsi ili kulinda uwezo wake na kasi yake.
“Binafsi nimekuwa nikifanya mazoezi na Bukoba Veteran, nimejijanga vizuri na nina uhakika wa kufanya vizuri. Kikubwa Mwenyezi Mungu atupe afya njema”. Alisema Them.
Msimu wa mwaka jana, Kagera Sugar ikiwa chini ya kocha Mkongwe, Alhaji Abdallah Athuman Seif `King Kibadeni Mputa` ilishika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu, huku nafasi ya tatu ikishikwa na Simba, ya pili Azam fc na mabingwa walikuwa Dar Young Africans.
Msimu wa mwaka huu, klabu hii haijawa na matokeo mazuri sana kwani mpaka mzunguko wa kwanza unamalizika, tayari imeshajikusanyia pointi 20 katika nafasi ya sita.

2013 NA MAJONZI YA WASANII WETU.

mangweaAliyekuwa mwanamuziki mahiri wa muziki wa Hip Hop Albert Mangwair.
==============================================
Mwaka 2013 ukiwa unaelekea ukingoni, umekuwa wa huzuni kwenye tasnia ya filamu kutokana na wasanii wengi kupoteza maisha.
Pia katika mwaka huu wa 2013 kumetokea vifo vya wasanii na kuacha mapengo kwenye tasnia hiyo kama ifuatavyo, Januari 2, mwigizaji Juma Kilowoko almaarufu Sajuki alifariki dunia, baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kifo chake siyo tu kiliacha pengo bali kilistua watu kutokana na juhudi mbalimbali zilizofanyika kuokoa maisha yake, ikiwemo kwenda nchini India kupata matibabu.
Lakini cha kufurahisha aliyekuwa mkewe Wastara Sajuki anaendelea kufanya kile alichokuwa akifanya na mpendwa mumewe yaani kuendeleza kuigiza, ni matumaini atayafanyia kazi yale yote yaliyokuwa yakifanywa na marehemu mumewe.
Januari 8, msanii maarufu wa miondoko ya muziki wa mnanda au mchiriku, Omari Omari alifariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu na kuthibitika kuwa alikuwa anaumwa kifua kikuu.
Omari Omari ni miongoni mwa vijana waliojipatia umaarufu kupitia muziki huo unaopendwa zaidi maeneo ya uswahilini.
Aprili 17, mwanamuziki mkongwe katika miondoko ya taarabu na muziki wa mwambao Fatuma Binti Baraka maarufu Bi Kidude alifariki dunia na kuzikwa visiwani Zanzibar, ambako ndiyo nyumbani kwao.
Msiba wa Bi Kidude ulihudhuriwa na waombelezaji wengi ikilinganishwa na msiba wa mwigizaji Steven Kanumba, ambao ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo wanasiasa.
Mei 28, mwanamuziki mahiri wa muziki wa Hip Hop Albert Mangwair maarufu Mangwea, alifariki dunia nchini Afrika Kusini katika Hospitali ya St Heleni Joseph jijini Johannesburg na kuzikwa nyumbani kwao Morogoro.
Mwanamuziki huyu, alipata maziko ya kutukuka huko nyumbani kwao Morogoro baada ya kuwa na maandano ambayo hayakuwahi kutokea , hata mapokezi ya mwili wake ulipofika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere yalikuwa ya kihistoria, kutokana na watu kufurika na kusukuma gari lililobeba mwili wake hadi maeneo ya Tazara jijini Dar es Salaam.
Julai 13, mwanamuziki wa Hip Hop Langa Kileo alifariki dunia, Julai 10, mwigizaji Kash maarufu Jaji Khadija alifariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa, aliwahi kutamba na igizo la ‘tamu chungu’.
Septemba 8, mwigizaji Zuhura Maftaha, maarufu Melisa alifariki dunia, ingawa wakati anafikwa na umauti alikuwa anafanya shughuli nyngine baada ya kujitoa kwenye masuala ya uigizaji.
Novemba 11, mtangazaji wa kipindi cha taarabu cha Passion FM, na mwanamuziki wa miondoko hiyo Nyawana ‘Matashtiti’ Fundikira, alifariki dunia, nyimbo aliyowahi kutamba nayo ni ‘nipo kamili nimejipanga’.
Nyawana alizikwa nyumbani kwao Tabora ikiwa ni kutekeleza kauli yake aliyoitoa akiwa hai kuwa akifa akazikwe kwao.
Imeandaliwa na Kalunde Jamal
Kalunde Jamal
CHANZO: MWANANCHI

Jackie Cliff adaiwa kunaswa na dawa za kulevya nchini China

Jackie akiwa  katika chumba maalum alipopekuliwa ambapo  rafiki yake Chief Rocker amethibitisha kukamatwa kwa mwanadada huyo nchini china huku ubalozi wa Tanzania nchini humo umethibitisha kukamatwa kwa mrembo huyo. kwa hisani ya www.chinadaily.com 1508030_623954184329431_195299988_n 
Pipi za dawa za kulevua zikipangwa 1524777_623954147662768_2846804_n 
Wapiga picha wakiwajibika kazini ili kuripoti tukio la kukamatwa kwa Jackie

KARUME: MAJUMBA YA MPAPA YANAHITAJI KULINDWA

index

 

 

Na Ali Issa MAELEZO














Rais mstaafu wa awamu ya sita wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Amani Adeid Karume amesema majumba ya Mpapa yaliyokabidhiwa wananchi 24 kutoka shehia 6 ya jimbo la bambi yanahitaji kulindwa na kutuzwa ili yaweze kudumuzaidi uhai wake. Hayo ameyasema leo huko bambi wakati alipokua akiyakabidhi njumba hizo kwa familia hizo katika sherehe za kuzifungua nyumba hizo kwa wakadhi waliopewa katika kuazimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanbar. Amesma azma ya awali ya mapinduzi ya Zanzibar ni kumpatia makazi bora mwana nchi wa ya Zanzibar ndio Rais wa awamu ya kwaza Abeid Aman Karume ni kuwajengea wananchi wake makazi hayo,hivyo azma hiyo ipopalepale na serikali haitorudi nyuma. Alisema nyumba hizo ni sehemu Ya nyumba zilizo jengwa sehemu mbali mbli za Zanzibar ijapo kluwazilisita kutokana na matukio yalio tokea miaka iliopita. Amesema majumba hayo yamemaliza na kuazia leo nihuru wananchi kuyatumia kwa kuweka familiazao

Rais Kikwete atembelea na kuwafariji wagonjwa Muhimbili


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali mtoto Andrew Simba(15) aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati Rais alipowatembelea na kuwafariji  baadhi ya wagonjwa katika wodi ya Mwaisela leo.(picha na Freddy Maro). D92A7350

JOTO LA MAPINDUZI CUP 2014 LAZIDI KUPANDA, KOCHA ITALIA MGENI RASMI SIMBA SC, AFC LEOPARD ZIKICHUANA!!

MAANDALIZI ya kombe la Mapinduzi linalotarajia kuanza kutimua vumbi januari mosi mwakani yanakwenda vizuri na timu zote zilizothibitisha kushiriki zinatarajia kuwasili desemba 31 mwaka huu.
Msemaji wa kamati ya mashindano , Farouk Karim amesema kuwa timu za Tusker fc, AFC Leopard za Kenya, KCC, URA za Uganda , Simba sc, Yanga, Azam fc na Mbeya City za Tanzania bara tayari zimeshathibitisha kushiriki na kamati ya maandalizi imeshakamilisha  taratibu za kuzipokea.
SIMBA imepangwa kufungua pazia la michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kucheza na AFC Leopards ya Kenya Januari Mosi wakati Yanga wakishuka dimbani siku inayofuata kuikabili Tusker FC.
290024_heroa (1)
kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Italia, Cesare Prandelli.
Karim amesema mgeni rasmi katika mechi ya ufunguzi itakayopigwa januari mosi majira ya saa mbili usiku katika uwanja wa Aman kisiwani Unguja baina ya Simba sc dhidi ya AFC Leopard ya Kenya atakuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Italia,  Cesare Prandelli.
Pambano la Simba na Leopards litatanguliwa na mechi kati ya wenyeji KMKM na KCC ya Uganda litakalopigwa saa 10 jioni kwenye uwanja huohuo.
“Ninavyozungumza na wewe muda huu, Prandelli yupo hapa Zanzibar mapumzikoni na tayari amekubali kufungua michuano hii yenye maana kubwa katika miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar”. Alisema Karim.
simba mpya 
Kikosi cha Simba sc
Karim alisema katika michuano ya mwaka huu viwanja viwili vitatumika ambavyo ni Gombani kisiwani Pemba na Aman Kisiwani Unguja.
“Uwanja wa Gombani upo katika hali nzuri na unavyojua una nyasi za bandia. Uwanja wa Aman umefanyiwa ukarabati mkubwa na hivi sasa wataalamu kutoka China wapo hatua za mwisho kabisa kukamilisha shughuli yao”. Alisema Karim.
Mratibu huyo alitoa wito kwa wadau, wapenzi wa soka visiwani Zanzibar kujitokeza kwa wingi kwani kamati ya mashindano inategemea mapato ya milangoni kufanikisha mipango.
“Michuano hii inagharimu zaidi ya shilingi milioni 600, hatuna fedha hizo, tunategemea mapato ya milangoni, hivyo mashabiki kufika kwao  kwa wingi ndio mafanikio yetu”. Aliomba Karim.
afcleopards (1) 
AFC Leopard
Aidha ameziomba taasisi na makampuni ya bara na visiwani kujitokeza kufanya matangazo katika michuano hiyo ili angalau wapate pesa za kuendeshea michuano hiyo.
Michuano iliyopita, Azam fc walitwaa ubingwa, lakini mwaka huu kuna changamoto mpya hasa kutokana na uwepo wa timu za Dar Young Africans na Mbeya City ambazo hazikushiriki.
Mechi zote za hatua ya makundi na robo fainali zitafanyika kwenye viwanja wa Gombani Pemba na Aman Unguja, wakati nusu fainali na fainali zitapigwa kwenye Uwanja wa Aman.
Katika michuano iliyopita Simba waliishia nusu fainali baada ya kuondolewa na Azam FC kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya mechi kumalizika kwa sare ya 2-2 hata baada ya kuongezwa dakika 30.

HELP FOR UNDERSERVED COMMUNITIES INC YAFADHILI WANAFUNZI 11 MASOMO YA UFUNDI VETA NCHINI

photo 1 (1)  
Baadhi ya vijana waliopata ufadhili wa kozi mbalimbali za ufundi toka Help for Underserved Communities Inc. (HUC), wakisubiri taratibu za ujazaji fomu za kujiunga katika Chuo cha Mafunzo ya Ufundi(VETA) jijini Dar es salaam, hivi karibuni. photo 2  
Monica Mhelela na Fadhili Munda wakijaza fomu za kujiunga na kozi za ufundi VETA jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Vijana hao ni miongoni mwa vijana wanaofadhiliwa na Help for Underserved Communities Inc. (HUC) | Monica and Fadhili Munda fill application forms to attend training at Vocational Education and Training Act (VETA) recently. These are among 11 youth who got scholarships from Help for Underserved Communities Inc. (HUC).photo 4  
Baadhi ya vijana walipata ufadhili wa masomo ya ufundi toka Help for Underserved Communities Inc. (HUC), wakijaza fomu za kozi mbalimbali walizoomba VETA, jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kutoka kulia ni Monica Mhelela, Joseph Mboya na Hassan Bakari.photo 5  
Jamila Mwenda na Joseph Mboya wa Dar es Salaam, wakionesha nyuso za furaha baada ya ndoto zao za kusomea usekretari kwa Jamila na ufundi magari kwa Joseph kutimia. Jamila na Joseph ni miongoni mwa vijana 11 wanaofadhiliwa na Help for Underserved Communities Inc. (HUC)photo 6 
Vijana 11 waliopata ufadhili wa kozi mbali mbali VETA kupitia ufadhili wa Help for Underserved Communities Inc. (HUC), yenye makao yake Marekani. Picha zote na Nathan Mpangala. Zaidi: : https://www.facebook.com/pages/Help-for-Underserved-Communities-HUC-USA/412893725452394 
Na Nathan Mpangala
Help for Underserved Communities Inc. (HUC), imefadhili wanafunzi 11 kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya na Morogoro kozi mbalimbali za ufundi zinazotolewa VETA, ambapo baadhi yao wameshaanza mafunzo na wengine wanatarajiwa kuanza Januari mwakani.
Akizungumzia ufadhili huo, Rais wa asasi hiyo, Bi. Zawadi Sakapalla – Ukondwa, alisema, “ufadhili umelenga vijana wenye nia ya kujiendeleza lakini wamekuwa wakishindwa kufanya hivyo kutokana na uyatima na wazazi au walezi kutokuwa na uwezo wa kuwasomesha”.
Majina, kozi na mikoa wanayotoka vijana hao ni;  Joseph Mboya, Saidi Makope,  Yasini Musa (ufundi magari, Dar es Salaam), Neema Bungara (umeme wa magari, Dar es salaam), Francis Mustafa (ufundi magari, Morogoro), Hassan Bakari, Fadhili Munda (udereva, Dar es Salaam), David Mwasyeba (udereva wa pikipiki, Mbeya), Jamila Mwenda (usekretari/kompyuta, Dar es Salaam), Monica Mhelela (saluni na utengenezaji nywele, Dar es Salaam) na Rose Mawawa (ufundi cherehani, Dar es Salaam).
HUC ni asasi isiyo ya kiserikali yenye makao yake Marekani, inayosaidia upatikanaji wa maji safi na salama ya kunywa, maktaba za kijamii na vifaa vya elimu kwa maeneo yenye upungufu wa huduma za kujamii. Habari zaidi: https://www.facebook.com/pages/Help-for-Underserved-Communities-HUC-USA/412893725452394