Cristiano
 Ronaldo ameifungia bao Real Madrid jana usiku na kuvunja rekodi ya 
mmoja wa washambuliaji waliopo katika orodha ya kufunga mabao mengi 
zaidi enzi zao wakisakata soka.
Mshambuliaji
 huyo raia wa Ureno amefunga mabao 164 katika michezo 151 na kuvunja 
rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa Mexico, Hugo Sanchez aliyefunga 
mabao 164 katika mechi 207.
Ronaldo
 ameingia katika orodha ya wafungaji wanne wa juu waliowahi kufunga 
mabao mengi katika historia ya Real, lakini amebakiwa na rekodi tatu 
kuzivunja, yaani ya Santillana mwenye magoli 186,  Alfredo Di Stefano 
magoli  216 na Raul aliyetia kambani magoli 228. 
Real 
Madrid waliwafunga Valencia mabao 3-2 jana, shukurani zimwendee Ronaldo 
kwa kichwa chake mahiri dakika ya 40  kufuatia mpira mzuri wa adhabu 
uliochongwa na Agel Di Maria alimbadili Gareth Bale katika mchezo huo.
Madrid walipata bao la tatu na la ushindi kupitia kwa kinda wao mwenye miaka 20 Jese Rodriguez katika dakika ya 84.
Bao la kwanza lilifungwa na Angel Di Maria katika dakika ya 28 kufuatia kuwazidi ujanja mabeki wa Valencia.
 Mabao ya Valencia yalifungwa na Pablo Piatti dakika ya 34 na Jérémy Mathieu dakika ya 62.
Kikosi
 cha Valencia jana: Guita, Pereira, Ruiz, Mathieu, Romeu, Feghouli, 
Bernat, Parejo (Banega, 84), Cartabia, Piatti (Guardado, 80), Jonas.
Kikosi
 cha Real Madrid: Lopez, Arbeloa (Carvajal, 80), Ramos, Nacho, Marcelo, 
Alonso, Modric, Di Maria (Illarramendi, 87), Isco (Jese, 73), Ronaldo, 
Benzema.
 
Rekodi:
 Bao la Cristiano Ronaldo jana usiku dhidi ya  Valencia limemfanya 
aungane na wafungaji wanne waliowahi kufunga mabao mengi katika historia
 ya Real Madrid
 
Akiruka kwa furaha: Ronaldo aliifungia bao la pili Real Madrid katika ushindi wa mabao 3-2 jana usiku
 
Jitihada
 ya timu: Ronaldo akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga bao 
la pili lililowafanya waende mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-1
 
Kifua mbele: Angel di Maria  na beki wa kushoto Marcelo  wakishangilia bao la Margentina huyo
Amesawazisha: Mchezaji wa Valencia,  Pablo Piatti (katikati) akishangilia na wachezaji wenzake baada ya kusawazisha bao
 
Kipute kinaendelea: Beki wa Valencia, Mfaransa , Jeremy Mathieu akishangilia baada ya kusawazisha bao la pili dakika ya 62
 
Mshindi: Mshambuliaji  Jese (kushoto) akishangilia  na mchezaji mwenzake Luka Modric baada ya kuifungia Madrid bao la ushindi
 
Aaaah! nimekosaje?: Beki wa Real Madrid,  Sergio Ramos akishika kichwa chake baada ya kupoteza nafasi ya wazi  kufunga  bao
Changamoto: Kiungo wa Real Madrid ,  Xabi Alonso akimtoka winga wa Valencia  Pablo Piatti katika mchezo wa jana usiku
No comments:
Post a Comment