Waziri
 Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa 
akiwahutubia Vijana waliojiajiri kwa kazi ya kuendesha pikipiki za 
kupakia abiria maarufu kama Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam (hawapo 
pichani) wakati wa Tamasha Maalum la Bodaboda lililofanyika leo kwenye 
Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam.Mh. Lowassa alikuwa ni 
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo iliyofana sana.
 Naibu
 Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Dkt. Makongoro Mahanga akizungumza machache
 kwenye Tamasha hilo kabla ya Kumkaribisha Mgeni Rasmi kwenye Tamasha 
hilo,Mh. Edward Lowassa (kulia).Katikati ni Kamanda wa Polisi Kitengo 
cha Usalama Barabarani Tanzania,DCP. Mohammed R. Mpinga.
Kamanda
 wa Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani Tanzania,DCP. Mohammed R. 
Mpinga akizungumza akitoa hotuba yake mbele ya Vijana waliojiajiri kwa 
kazi ya kuendesha pikipiki za kupakia abiria maarufu kama Bodaboda 
wa Mkoa wa Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa Tamasha Maalum la 
Bodaboda lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es
 Salaam.
Mwenyekiti
 wa Chama cha Waendesha Pikipiki Wilaya ya Ilala,Michael Roewe akisoma 
Risala yao mbele ya Mgeni Rasmi,Mh. Edward Lowassa (hayupo pichani) 
wakati wa Tamasha Maalum la Bodaboda lililofanyika leo kwenye Viwanja 
vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam.
Waziri
 Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea 
Risala ya Chama cha Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam,Kutoka kwa 
Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Pikipiki Wilaya ya Ilala,Michael 
Roewe.
Waziri
 Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa 
akikabidhi Zawadi kwa Afisa wa Benki ya FNB kwa kutoa Mchambo mkubwa kwa
 Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam.
Waziri
 Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa 
akikabidhi Zawadi kwa Afisa wa Mfuko wa PSPF kwa kutoa Mchambo mkubwa 
kwa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam.
Waziri
 Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea 
Zawadi Kutoka kwa Mwenyekiti wa Muda wa Shirikisho la Waendesha Bodaboda
 Mkoa wa Dar es Salaam,Said Magamba.
Salamu kwa waendesha Bodaboda.
Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya wanaounda kundi la KIBEGA,wakitoa Burudani mbele ya Waendesha Bodaboda hao.

Sehemu ya Waendesha Bodaboda hao wakifatilia kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi.
Msanii Linex akifanya yake Viwanjani hapo mapema leo.
Mgeni
 Rasmi katika Tamasha la Waendesha Bodaboda Mkowa wa Dar es 
Salaam,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward 
Lowassa akiondoka viwanjani hapo huku Vijana Bodaboda wa Mkoa wa Dar es 
Salaam wakimsindikiza kwa shangwe.
Waziri
 Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwaaga 
Vijana wa Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati alipokuwa akiondoka 
viwanjani hapo huku shangwe zikitawala viwanjani hapo.
Vijana wa Bodaboda wakilisukuma gari la Mh. Lowassa ikiwa ni sehemu ya Furaha waliokuwa nayo.




















No comments:
Post a Comment