Mwimbaji
 wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba katika tamasha la Krismas 
lililofanyika leo kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro likishirikisha
 waimbaji mbalimbali wa muziki huo hapa nchini na mwimbaji wa kimataifa 
kutoka nchini Zambia Ephraim Sekereti wamesuuza mioyo ya mashabiki baada
 ya kushusha burudani ya nguvu katika tamasha hilo, Katika tamasha hilo,
 mashabiki wamejitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Jamhuri, Tamasha hilo
 linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es salaam na 
linatarajiwa kuendelea mkoani Tanga  Desemba 28 mwaka huu.(PICHA NA 
KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MOROGORO)  
 
 
Mwimbaji
 Edson Mwasabwite akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki wake wakati 
akitumbuiza kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro leo jioni. 
 
 
Boniface Mwaiteje naye akawanyanyua kwenye viti mashabiki waliojitokeza kushuhudia tamasha hilo. 
Mwanamama mwenye sauti ya mirindimo Upendo Nkone akakonga nyoyo za mashabiki wake. 
Mwanamama mwingine Upendo Kirahiro akiwaimbisha mashabiki wake. 
 
Hapa akiimba kwa furaha kumtukuza mungu wake mbele ya mashabiki wake kwenye uwanja wa Jamhuri. 
Vijana wa  kazi kutoka kundi la Kitimtim la Rose Muhando wakionyesha umahiri wao katika kucheza. 
Upendo Nkone akicheza na mastaeji shoo wake.
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment