Baadhi ya wajumbe wa timu ya ukaguzi wa miradi ya
maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiingia kwenye gati la
Bandari ya Mbaba Bay iliyopo wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.
Mratibu wa shughuli za
ukaguzi wa miradi ya maendeleo, Bw. Senya Tuni (Wapili kulia) akieleza jambo
mara walipoingia kwenye eneo la gati la Bandari ya Mbaba Bay. Wanaomsikiliza ni
Mkuu wa msafara huo, Bibi Florence Mwanri (Kulia), Afisa mazingira wa Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango, Bw. Julius Edward (Watatu kulia). Na kushoto ni Bw.
Jordan Matonya ambae ni Mchumi kutoka Tume ya Mipango.
Afisa
bandari ya Mbaba Bay, Bw. Jarome Urio (Wapili kushoto) akitoa maelezo kwa
wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
walipofanya ziara kwenye bandari hiyo. Timu hiyo iliongozwa na Bibi Florence
Mwanri (Kushoto).
Kiongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya
maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence kushoto
akionesha kitu kwenye sehemu ya gati la Bandari ya Mbaba Bay (halionekani).
Baadhi ya vijana wa Mbaba
Bay wakijivinjari kwenye fukwe za Ziwa Nyasa.
Afisa
bandari ya Mbaba Bay, Bw. Jarome Urio (Watatu kushoto) akionesha sehemu ya gati
iliyoofanyiwa matengenezo.
Baadhi ya utajiri
unaopatikana kwenye Ziwa Nyasa. Dagaa wa Ziwa hili ni maarufu kwa utajiri wake
wa lishe. Kwa mujibu wa wakazi wa Mbaba Bay, dagaa hao uuzwa hadi nje ya nchi.
=============================================
Na:Saidi Mkabakuli, Mbaba Bay
Timu
wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Tume ya Mipango imetembelea
Bandari ya kimkakati ya Mbaba Bay iliyopo wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma
kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Bandari hiyo.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo, kiongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri alisema kwamba Bandari
hiyo ni muhimu kwa uchumi wa nchi kwa kuzingatia eneo la kijiografia la bandari
hiyo.
“Bandari
hii ni muhimu kwani kijiografia inaweza kuzifikia nchini nyingi zilizo kusini
mwa nchi yetu hivyo inaweza kutumika kama lango la kibiashara miongoni mwa
jirani zetu licha ya uhaba wa miundombinu yake,” alisema.
Aliwasihi
wafanyakazi wanaoihudumia Bandari hiyo kufanya kazi kwa bidii bila ya kuchoka
ili kuweza kuvutia wafanyabiashara na watumiaji wengine kuendelea kuitumia
bandari hiyo.
Kwa
upande wake, afisa bandari ya Mbaba Bay, Bw. Jarome Urio aliutaarifu ugeni huo
kuwa Mamlaka ya Bandari ipo katika mkakati wa kuindeleza bandari hiyo ili
kuweza kuihudumia wateja wengi zaidi.
Pia,
Bw. Urio aliwashukuru wajumbe wa timu hiyo ya ukaguzi kwa kwenda kuitembelea na
kujionea maendeleo ya bandari hiyo.
“Tunafarijika
sana kuona viongozi wa serikali wanapokuja kututembelea kwani hali hii uongeza
hamasa ya utendaji kazi wetu,” alisema.
Kwa
mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/2012 – 2015/2016) bandari
ni mojawapo ya vipaumbele vitano vya kimkakati vyenye lengo la kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa nchi ili
kuweka misingi wa uchumi kwa watu walio wengi.
Vipaumbele vingine ni Kilimo ambapo lengo kuu likiwa ni kuongeza tija
katika uzalishaji wa mazao ya kilimo ili kujitosheleza kwa chakula na kuwa na
ziada ya kuuza nje ya nchi; Maendeleo ya viwanda:
Msisitizo umewekwa katika kuvutia, kuanzishwa na kuendeleza viwanda
vinavyotumia malighafi zinazopatikana nchini (kama vile viwanda vya nguo,
mbolea, saruji, makaa ya mawe, chuma na bidhaa za chuma) na pia sekta ya madini
kwa lengo la kuongeza mapato ya Serikali.
Pamoja na kipaumbele cha Maendeleo ya
rasilimali watu na ujuzi:
Mpango unahimiza kuwekeza katika elimu (hasa katika elimu ya juu na vyuo vya
ufundi) na huduma za afya (kuongeza ubora na upatikanaji wa huduma) katika
kujenga nguvu kazi itakayotuletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii; na Utalii, Biashara,
na huduma za Fedha ambapo jitihada zimewekwa kwenye uendelezaji uwezo wa
kuuza katika masoko ya ndani na nje, kuongeza
idadi ya watalii na matumizi yao wawapo nchini, na kuongeza upatikanaji
wa huduma za kifedha.





Mkurugenzi
wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Aldegunda
Kombo akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi hiyo kuhusu
matumizi ya takwimu sahihi katika kupanga shughuli za maendeleo nchini
wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo jijini
Dar es salaam.
Mwakilishi
kutoka nchi washirika wa maendeleo Bw. Jacques Morisset (kushoto)
akizungumza na wadau mbalimbali kuhusu mchango wa matumizi ya takwimu
sahihi katika maendeleo ya taifa lolote wakati wa maadhimisho ya Siku ya
Takwimu Afrika leo jijini Dar es salaam.
Mtakwimu
Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Mohammed Hafidh akisisitiza
jambo kuhusu athari, madhara na ya matumizi ya takwimu zisizo sahihi.































Mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Mratibu Mwandamizi
wa Mradi Bw. Nehemia Murusuri (wa kwanza kulia) pamoja na Mwakilishi wa
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Mratibu wa Mradi wa Kuondoa Umaskini,
Kukuza Uchumi na Utunzaji Endelevu wa Mazingira, Bw. Telesphory
Kamugisha (wa pili kulia). Wengine ni baadhi ya wageni waliohudhuria
sherehe hizo. 




























Wasoma Utenzi Nezi Khamis na Amina Haji kutoka Jambiani wakihani
utenzi wao wakati wa Mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika
ukumbi wa Visitors Inn Hotel Jambiani Wilaya ya Kusini akiwa katika
ziara zake za kuimarisha Chama cha Mapinduzi CCM katika Mkoa wa Kusini
Unguja, {Picha na Ikulu.]
Mabalozi
na Wenyeviti wa Maskani Wilaya ya Kusini Unguja wakimsikiliza Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa
CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipookuwa akizungumza na Viongozi hao
wa Mashina wa Jimbo la Muyuni katika ukumbi wa Visitors Inn Hotel
Jambiani Wilaya Kusini akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama Mkoa
wa Kusini Unguja leo, {Picha na Ikulu.]










Mwandikishaji
wa kituo cha cha kujiandikisha cha kura kwa ajili ya uchaguzi wa
Serikali za Mitaa, Beatrice Likundo (kulia) kilichopo kwenye Shule ya
Msingi Mivinjeni jijini Dares Salaam akimwandikisha jina leo Mkazi wa
Mtaa wa Mivinjeni ,Evod Millinga kwa ajili ya uchaguzi huo.

Mwenyekiti
wa Bunge, Mussa Azan Zungu akiongozwa na Mpambe wa Bunge kutoka kwenye
ukumbi wa Bunge wakati alipositisha kikao cha Bunge cha asubuhi
Novemba 26, 2014, (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
