TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, June 22, 2012

Katiba mpya iwe na dira ya maendeleo

Posted: 20 Jun 2012 11:02 PM PDT
Na Halfan Diyu

KATIBA muongozo ambao taifa lolote limejiwekea jinsi ya kuendesha shughuli za kila siku za taifa lao.
Taifa linakuwa imara linapokuwa na katiba imara na viongozi bora, wenye maono ya kuwaletea maendeleo wananchi wao.
Taifa lazima lisimamie misingi ya haki na ianishwe katika katiba kwani ni haki pekee huleta watu pamoja na kiondoa misingi yote ya unyonyaji.
Pia, ndio sheria mama nchini na katiba zote zinazotengenezwa na taasisi au vyama vya siasa zinapaswa kuakisi yale yote
yaliyopo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na si kupingana, kinyume na hapo itakuwa batili.
Maendeleo ya nchi nyingi zilizoendelea yamechangiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuwa na katiba imara na inayokidhi mahitaji ya sekta mbalimbali kama za elimu, afya, utamaduni, uchumi, siasa, uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa wananchi kuzungumza au kutoa maoni yake.
Hakuna ubishi kuwa nchi ya Marekani ni moja ya mataifa ambayo yamekuwa na katiba imara inayogusa sekta zote nilizotaja hapo juu na ambayo imedumu kwa muda mrefu bila
kufanyiwa marekebisho ya mara kwa mara.
Matokeo yake tunashuhudia Taifa hilo likisimama kwa muda mrefu kwa kuwa na uchumi imara duniani.
Nchini baada ya kuundwa kwa katiba mwaka 1977, tayari yameshafanyika marekebisho kumi na nne hadi mwaka 2005, ambapo ya kwanza yalifanyika mwaka 1979.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba nchini, Bw.Deus Kibamba anasema marekebisho ya kwanza ya mwaka 1979 yaliingiza moja ya mambo muhimu katika taifa letu, ambapo ni
kuanzishwa kwa Mahakama ya Rufaa.
Mwaka 1980 yalifanyika tena marekebisho katika Katiba na moja ya marekebisho hayo ni kuingizwa kwa katiba ya Zanzibar katika Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Mwaka 1982 yalifanyika marekebisho ya mfumo mpya wa kuchagua wakuu wa mikoa, mwaka 1984 marekebisho bora ambayo yalizingatia maoni ya wananchi ambapo suala la haki za binadamu liliingizwa katika katiba.
Hayo ni baadhi ya marekebisho machache tu ambayo yalifanyika katika hiyo miaka niliyoitaja hapo juu na kufikia hadi mwaka 2005 jumla ya mabadiliko kumi na nne yalifanyika na mengi yaligusa masuala ya siasa na muungano, achilia machache kama ya haki za binadamu ambayo yanagusa jamii yote bila kubagua.
Vilevile ubora na uimara wa katiba mpya ijayo uende sambamba na kudumu kwa miongo mingi na si kufanya marekebisho ya mara kwa mara ambayo yanagharimu fedha nyingi za walipa kodi.
Katika kipindi hiki Taifa lipo katika vuguvugu la kuanza mchakato wa kukusanya maoni ya katiba mpya, ambapo ifikapo tarehe 26 mwezi Aprili mwaka 2014 Katiba hiyo inatakiwa
iwe imekamilika.
Wananchi waelimishwe umuhimu wa kuchangia maoni ya masuala mbalimbali yanayogusa maisha yao ya kila siku na si kuwa na mawazo mgando ya kuchangia katika masuala ya
muungano na siasa tu, ingawa pia yana umuhimu katika mustakabali wa Taifa.
Nionavyo jamii inatakiwa kupata uelewa na nafasi ya kuchangia maoni yao ili kupatikana kwa katiba bora, imara itakayogusa sekta zote kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Posted: 20 Jun 2012 11:00 PM PDT

Posted: 20 Jun 2012 10:59 PM PDT

Na Mwandishi Wetu

BENDI ya muziki wa dansi ya Mashujaa 'Wana Kibega', inatarajia kufanya ziara maalumu kwa mashabiki wake wa Kanda Ziwa mwishoni mwa wiki.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja wa bendi hiyo, Martin Sospeter alisema onesho la kwanza litafanyika Ijumaa mjini Kahama, mkoani Shinyanga.
Alisema Jumamosi watatoa burudani mjini Geita na Jumapili watakuwa jijini Mwanza.
Meneja huyo alisema wameandaa shoo ya nguvu kwa wapenzi wa mikoa hiyo ikiongozwa na Lilian Internert, akiwa na wengine ambao wataonesha shoo zao mpya zilizoundwa hivi karibuni.
Sospeter alisema katika maonesho hayo nyimbo zao zote zitapigwa, ikiwa pamoja na zilizokuwa hazijawahi kusikika kwenye vyombo vya habari.
"Kuna nyimbo mpya ambazo zitaanza kusikika huko huko, tunafanya kama kuwatambulisha wapenzi wa Kanda ya Ziwa waone mambo mapya ya Mashujaa," alisema Sospeter.
Alisema bendi hiyo itarejea Dar es Salaam Jumatatu na kuendelea na ratiba yake ya kila wiki, huku ikiandaa ziara yake ya mikoa ya Kusini ambayo itafanyika mwezi ujao.
Posted: 20 Jun 2012 10:56 PM PDT

Na Heri Shaaban, Pwani

WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenela Mukangara amesema Mashindano ya Shule za Sekondari (UMISSETA) ya mwaka huu yatatumika kuunda timu ya pili ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars).
Akizungumza katika ufunguzi wa mashindano hayo yaliyofanyika juzi mjini Kibaha, Waziri Fenela alisema haina budi kuunda timu B ya wanawake kwa kutumia wachezaji watakaopatikana katika michuano hiyo.
"Ombi langu la mapendekezo haya, najua litatekelezwa mara moja ili tuwe na timu mbili za wanawake za soka ili zije kuwa tishio siku za baadaye.
"Nimeshudia mechi ya mpira miguu ya wanawake kwa timu za Kanda Nyanda za Juu Kusini, iliyofungwa mabao 10-1 dhidi ya Kanda Mashariki ambazo zimeonesha mpira mzuri," alisema.
Alisema mashindano hayo ni chachu ya kuibua vipaji vya wanamichezo mbalimbali, ndiyo maana mwaka huu michezo hiyo imewashirikisha wadau mbalimbali katika sekta hiyo, ili waweze kuangalia vijana wenye vipaji.
Waziri huyo alisema michezo ni ajira inatakiwa kutambua mchango wake, hivyo Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISSEMI kwa ushirikiano na Wizara ya Mafunzo ya Ufundi zinatakiwa kufanikisha mashindano hayo ambayo ndiyo chachu ya kupata wachezaji wa timu ya Taifa wa baadaye.
Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Jumanne Sagin amezuia walimu wakuu kuuza maeneo ya viwanja vya shule badala yake vibaki kwa ajili ya michezo.
Posted: 20 Jun 2012 10:37 PM PDT

Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Ufaransa (AF), Sullivan Benetier (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es Salaam juzi, kuhusu kituo hicho kuandaa Maadhimisho ya Siku ya Muziki Duniani inayofanyika leo, kwa kushirikisha bendi na vikundi mbalimbali vya muziki. Kulia ni Kiongozi wa Bendi ya FM Academia Nyoshi Saadat. (Picha na Charles Lucas) 
Posted: 20 Jun 2012 10:36 PM PDT

Na Mhaiki Andrew, Songea

WACHEZAJI 20 na viongozi watatu wa timu ya soka ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya mkoa wa Ruvuma, imeondoka jana mjini hapa kwenda jijini Dar es Salaam kushiriki mashindano ya Taifa ya Copa Coca-Cola 2012.
Akizungumza mjini hapa juzi usiku katika halfa ya kuwaaga vijana hao, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa (FARU) Joseph Mapunda,  alisema kazi iliyokuwa mbele yao ni kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa kombe hilo mwaka huu.
Wachezaji waliondoka pamoja na viongozi wao kuwa ni Joseph Hilly, Adeligoti Kipipa, Amosi Bandawe, Ramadhan Ramadhan, Peter Malekoni, Maneno Zuberi na Severin Mkandawile (Mbinga), Panjo Mshindo, Anthon Heneko, Omari Ally na Shaban Chitete (Tunduru).
Wengine ni Edward Songo, Mapunda Sandali, Ebroni Haule, Sunday Kalonga, William John, Juma Said, Ally Abdallah.
Aliwataja wachezaji wengine kuwa ni Shanely Michael na Hamis Yasin kutoka Manispaa ya Songea na Kocha Mkuu wa timu hiyo Francis Samatta, msaidizi wake Francis Kasembe na mkuu wa msafara, Emmanuel Kamba.
Mapunda alisema wilaya zingine tatu za Namtumbo, Nyasa na Songea Vijijini katika  wachezaji wake hawakuweza kuteuliwa baada ya  kushindwa kushiriki mashindano hayo.
Posted: 20 Jun 2012 10:35 PM PDT

Na Mwandishi Wetu

SIGARA ya Embassy kupitia chapa yake ya Club E, inakuja na pati ya Hollywood Glam Night. Pati hiyo itafanyika kesho jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Blue Pearl ulioko Ubungo Plaza kuanzia saa 2 usiku.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam juzi na Tumaini Toroka ambaye ni Meneja wa Embassy ilieleza kwamba pati hiyo ambayo itakuwa na maudhui ya Hollywood, ambapo wanachama na wapenzi wa burudani watapata watashuhudia burudani mbalimbali na vivutio vya Hollywood.
Alisema wanachama wa Club E, wataingia bure kwenye pati hiyo kwa kupitia mwaliko maalumu na kwa watu wengine ambao si wanachama na wangependa kuhudhuria, watalipa sh. 30,000. Kiingilio hicho kitajumuisha vinywaji pamoja na chakula.
Alisema kwa miaka mitano iliyopita, Club E imejijengea jina kwa kufanya pati zenye ubora na hadhi ya hali ya juu kwa wanachama wake.
"Ukiacha suala la kuburudisha wanachama wake, kwa kipindi cha miaka mitano, Club E pia imeweza kutoa mchango wake kwa kuinua wanamuziki wetu wa ndani ambao wamepata muda wa kuimba kwenye jukwaa moja na wasanii mbalimbali wa bara la Afrika na Marekani.
Alisema Club E ilianzishwa mwaka 2007 kwa lengo la kuwaleta pamoja na kuwaburudisha wanachama wake, ambao ni wavutaji wa sigara ya Embassy.
"Tangu kuanzishwa kwake Club E imefanya pati nyingi na kuwaleta wasanii wengi wa ndani na nje ya nchi kutumbuiza. Wasanii walioletwa na Club E ni pamoja na Werrason, Miriam Makeba, Amani, Blue 3, Lady Jay Dee, Mbilia Bell, Tshalla Muana, JB Mpiana, FM Academia, Chaka Khan na Falii Ipupa," alisema.
Posted: 20 Jun 2012 10:34 PM PDT
Baadhi ya mashabiki wa soka wa klabu za Ligi Kuu ya England, waliojitokeza kwenye kushiriki mashindano ya kumsaka 'Shabiki Bomba' kwenye Castle Lager Superfans yaliyofanyika Kimara jijini Dar es Salaa jana (kulia) ni Msumi Maneno akifanyiwa usaili kwa ajili ya kinyang'anyiro hicho. Mshindi wa mashindano hayo atakwenda Afrika ya kusini kushuhudia Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani. (Na Mpigapicha Wetu)
Posted: 20 Jun 2012 10:31 PM PDT

Na Mhaiki Andrew, Songea

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa filamu ya Adelahida, ambayo imechezwa na waigizaji wazawa wa mkoa huo. Uzinduzi huo utafanyika katika Ukumbi wa Songea Klabu, Julai Mosi mwaka huu.

Akizungumza mjini hapa jana Mratibu wa filamu hiyo, Shukrani Faraja alisema filamu hiyo ni muhimu kwa vizazi vya sasa katika kuelewa historia ya zamani ya mababu.

Alisema filamu hiyo itakapoingiwa sokoni itasaidia kuelewa mila, desturi na tamaduni za mababu wa mkoa huo ambazo walikuwa wakiziendekeza ikiwemo kuuwa watoto watakaobainika wamezaliwa mapacha zaidi ya wawili kwa imani za kutokea mikosi katika ukoo wao.

Faraja alisema pamoja na filamu hiyo waigizaji wake wameelezea mambo mengi, huku wakiowanisha na kipindi chote ambacho Tanzania inajitawala.

Mratibu huyo alisema uzinduzi huo utakwenda sambamba na maigizo mbalimbali ikiwemo na wasanii wa kizazi kipya, ngoma za asili za makabila ya Mkoa wa Ruvuma na wazee wa kimila ikiwa ni tambiko lao kabla ya filamu hiyo kuingia sokoni.
Posted: 20 Jun 2012 10:29 PM PDT
Na Zahoro Mlanzi

WACHEZAJI wapya wa Yanga, Said Banahuzi na Juma Abdul 'Baba Ubaya', wameanza mazoezi na timu hiyo yanayoendelea katika Uwanja wa Kaunda, Dar es Salaam na kufanya timu hiyo kuzidi kuimarika.
Wachezaji hao wamesajiliwa msimu huu wakitokea Mtibwa Sugar ambapo wameungana na nyota mwingine, Nizar Khalfan katika kuhakikisha wanaimarisha timu hiyo inayojiandaa na michuano ya Kombe la Kagame na Ligi Kuu Bara.
Gazeti hili lilishuhudia wachezaji hao wakifanya mazoezi ya pamoja na wenzao ambao walianza tangu Jumatatu wakiwa chini ya Kocha Msaidizi, Fredy Felix 'Minziro' huku mashabiki wakionekana kuvutiwa nao.
Pamoja na kufanya mazoezi hayo, lakini kivutio kikubwa kilikuwa kwa Baba Ubaya ambaye hucheza beki wa kushoto, alikuwa akionesha umahiri wake katika kuuchezea mpira na kupiga pasi zenye uhakika.
Beki huyo ambaye ni tunda na Kituo cha Michezo cha Tanzania (TSA), baada ya kuonesha uwezo mkubwa akiwa kituoni hapo ndipo aliposajiliwa na Mtibwa akiichezea timu ya vijana (U-20) lakini msimu uliopita alipandishwa na kuchezea timu ya wakubwa.
Baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo, Minziro alisema anapata matumaini mapya baada ya kuona kila kukicha wachezaji waliosajiliwa na timu yake wanakuja, hivyo ataanza programu ya mazoezi siku si nyingi.
Alisema wachezaji waliokuwa katika timu ya Taifa (Taifa Stars) bado hawajaanza mazoezi, lakini ana imani baada ya siku chache za kupumzika watajiunga na wenzao kufanya mazoezi.
Timu hiyo ndiyo mabingwa watetezi wa Kombe la Kagame, ambalo walilitwaa mwaka jana chini ya aliyekuwa Kocha Mkuu, Sam Timbe lakini baadaye alifukuzwa na mikoba yake kuchukuliwa na Kostadin Papic.

QML yaingia ubia na BEML Ltd ya India

Posted: 19 Jun 2012 11:16 PM PDT

Na Godfrey Ismaely

KAMPUNI ya Quality Motors Limited (QML) ambayo ni miongoni mwa kampuni zinazomilikiwa na Kampuni ya Quality Group nchini imeingia makubaliano ya usambazaji wa bidhaa mbalimbali na Kampuni ya BEML Limited kutoka nchini India.
Makubaliano hayo ambayo yalienda sambamba na kutiliana sahihi za mikataba jana nchini, yanahusisha usambazaji wa bidhaa za kampuni hiyo Afrika Mashariki, Sudani Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Malawi na Msumbiji.
Akisaini mkataba huo Meneja Mkuu wa Biashara za Kimataifa wa BEML Bw. Narayana Bhat alisema anayofuraha kubwa kushirikiana na kampuni kubwa kama Quality Group na kuahidi ushirikiano mzuri katika maendeleo ya nchi za Afrika kwa kusambaza bidhaa zenye viwango bora katika ujenzi na uchimbaji wa madini.
Alisema, Afrika Mashariki ina rasilimali kubwa ya madini hivyo ushirikiano huo wa kampuni hizo mbili utafaidisha kwa kiwango kikubwa Afrika.
"BEML imefungua hivi karibuni tawi lingine mjini Johannesburg, nchini Afrika  Kusini ili kuhudumia kwa ukaribu zaidi soko la Afrika Mashariki kwa ukaribu zaidi na kwa wakati mwafaka," alisema Bw. Bhat. 
                                 Kwa upande wake Mkurugenzi wa Quality Group Bw. Sridhar Thiruvengadam alisema kampuni yake imechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Tanzania katika maeneo mbalimbali kwa kuungana na kampuni kubwa duniani inayoshughulika na usambazaji wa bidhaa za uchimbaji madini, ujenzi, reli na ulinzi.
Hata hivyo Kampuni ya BEML ni miongoni mwa kampuni kubwa zaidi duniani inayomilikiwa na Serikali ya India ambayo ina uzoefu wa muda mrefu hususan utengenezaji na usambazaji wa vifaa vya ujenzi zikiwemo reli, uchimbaji wa migodi pamoja na ulinzi.
Pia kwa mujibu wa BEML kwa sasa baada ya kufungua tawi lake nchini AfrikaKusini, tayari shehena ya kwanza ya bidhaa mbalimbali ipo njiani na inategemewa kuwasili Dar es Salaam hivi karibuni
Posted: 19 Jun 2012 11:15 PM PDT

Na Mwandishi wetu

KAMPUNI  ya Mawasilino ya  Vodacom Tanzania, imezindua vifurushi vipya vya intaneti ambavyo vitawawezesha wateja wake kupata huduma ya intaneti kwa shilingi 250 kwa siku.
Huduma hiyo ya 'Wajanja Intanet' imeboreshwa zaidi ili kuwawezesha wateja kuelewa huduma za intaneti na kuchagua kikamilifu huduma zitakazowafaa hivyo kuweza kuperuzi na kupata taarifa kwa kasi na kwa bei nafuu kupitia mtandao wa Vodacom.
Hata hivyo, Vodacom ilisisitiza kuwa huduma ya kuperuzi facebook na twitter zitaendelea kuwa bure kwa wateja wote.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza alisema kuwa  kampuni hiyo imerahisisha huduma hiyo kwa wateja wake ili kuwawezesha kuelewa kiasi ambacho wanatumia katika huduma za intaneti, suala ambalo limekuwa kikwazo kikubwa kwa watumiaji wa intaneti kote nchini.
Alibainisha kuwa Kampuni hiyo imeona umuhimu wa watoa huduma za mawasiliano kama Vodacom kuondoa utata ambao unawazuia wateja kutumia mfumo mpya  wa teknolojia ya intaneti katika mawasiliano.
“Tumeiweka huduma yetu katika njia ambayo ni rahisi kwa wateja wetu kuelewa kwani tunaamini kuwa hii ni njia rahisi ya kuongeza matumizi ya intaneti katika kueboresha maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Wateja wote wa malipo ya baada au ya kabla watapata huduma ya interneti kwa kasi kupitia simu zao za mkononi na modem.
Aliendelea kusema kuwa kutokana na huduma hiyo mpya, sasa Wateja wa Vodacom watapata huduma isiyo na kikomo na yenye kasi kwa siku saba mfululizo kwa Sh. 10,000 au Sh. 30,000 kwa siku thelathini
Posted: 19 Jun 2012 11:14 PM PDT

Posted: 19 Jun 2012 11:11 PM PDT

Heri Shaaban na Radhia Adam

SHIRIKISHO la Michezo la Mashirika ya Umma na Kampuni Binafsi Tanzanuia (SHIMMUTA), limeandaa Mkutano wa Halmashauri kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa ya maendeleo ya Shirikisho hilo kwa kipindi cha mwaka 2012 na 2013.
Kwa mujibu wa taarifa iliyomwa kwa vyombo vya habari juzi na Katibu Mkuu wa SHIMMUTA, Award Safari ilieleza kuwa mkutano huo utahusisha wajumbe kutoka kila taasisi mwanachama.
Safari alisema mkutano huo unatarajia kutafanyika Julai 12 mwaka huu.
"Agenda ya mkutano huo zitakuwa kupokea na kujadili taarifa za maendeleo za shirikisho kwa kipindi cha mwaka 2011/2012 ikihusisha taarifa za michezo iliyopita ya mwaka jana iliyofanyika jijini Tanga, pamoja na kujadili taarifa ya fedha ya mapato na matumizi.
Alisema katika mkutano huo wajumbe watapitia na kujadili bajeti ya mapato na matumizi ya mwaka 2012/2013, ikiwa pamoja na kupitisha mkoa ambao Kamati ya Utendaji ya SHIMMUTA imeuchagua kwa ajili ya kufanyia michezo ya mwaka huu.
Pia alisema shirikisho hilo linakaribisha wajumbe wawili kutoka katika taasisi, mashirika na kampuni ambayo hayakupelekewa barua za mwaliko, lakini yanataka kujiunga na kuhudhuria mkutano huo.
Aliwaomba wajumbe watakaoudhuria mkutano huo ambao utafanyika kwenye jengo la Benjamini Mkapa kuwa kila mjumbe atakayeshiriki gharama zote zitakuwa juu yake.
Posted: 19 Jun 2012 11:11 PM PDT


Na Mwandishi Wetu

MWNJILISTI Kabula George, anatarajia kugawa DVD za albamu ya Nitang’ara Tu kwa kila mtu atakayeingia kwenye Ukumbi wa kanisa la TAG Magomeni Mikumi Julai 8, mwaka huu wakati wa uzinduzi wake.
Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Mwinjilisti Kabula alisema ameamu kuweka utaratibu huo, ili kila mtu atakayeingia ukumbini humo aondoke na DVD kwa kuchangia kiasi cha sh. 5,000.
Mwinjilisti Kabula alisema tayari DVD hizo tayari zinapatikana katika maduka mbalimbali yaliyoteuliwa jijini Dar es Salaam.
DVD hizo pia zinapatikana katika mikoa mbalimbali ukiwemo Mwanza, Arusha, Dodoma na Kahama mji
Amewataka mashabiki wake kununua DVD halisi ili wanufaike na ubora wa nyimbo hizo, ambazo zinamafundisho kwa kila anayeziangalia.
Posted: 19 Jun 2012 11:09 PM PDT

Meneja wa bia ya Castle Lager, Kabula Nshimbo (kulia) akicheza mfano wa mpira wa miguu kwenye uzinduzi wa kampeni ya kumtafuta Shabiki Bora wa Castle kwenye kampeni ya Castle Super Fan, ambapo mshindi atapata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika timu ya Afrika ya Ushangiliaji (Africa United Super Fan) Afrika ya Kusini. Na Mpigapicha Wetu
Posted: 19 Jun 2012 11:07 PM PDT


Na Heri Shaaban

MAMLAKA ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imesema kuwa suala la dawa bandia ni tatizo la Dunia nzima hivyo amewataka wananchi kushirikiana na serikali kiziba mianya ya uingizaji dawa bandia ili kulinda maisha ya Watanzania kwa ujumla.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam hivi karibuni na Mkurugenzi wa TFDA Bw.Hiti Silo
Bw.Silo alisema kuwa kutokana na tatizo hilo kuwa la kidunia hivyo akuna budi kwa wadau,taasisi wananchi kushirikiana na mamlaka hiyo pamoja na serikali kudhibiti njia za uingizaji wa bidhaa bandia.
"Kutokana na changamoto hizi TFDA imeweza kuunda vikosi kazi kwa ajili ya kusimamia udhibiti wa dawa bandia kila pembe ya nchi kwa kushirikiana na jeshi la polisi kulinda mifumo ya njia hizo," alisema Bw.Silo.
Aliwaomba wananchi wanapopata taarifa za uingizaji wa dawa bandia, kutoa taarifa ngazi zinazohusika ili wahusika waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Alisema kuwa mamlaka hiyo pia imeweza kuimarisha mipaka yote katika vituo vya forodha zinapoingia bidhaa kwa ajili ya ukaguzi kabla mzigo kurusiwa kuingia nchini.
Kwa upande wake Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt.Hussein Mwinyi alikabidhi cheti kwa  Mamlaka ya chakula na Dawa  Tanzania TFDA na taasisi zingine zilizoshiriki madhimisho hayo ya siku ya famasia na kuwataka kutoa elimu ya kutosha  kwa wananchi ili wajuwe matumizi ya dawa bandia.
Posted: 19 Jun 2012 11:05 PM PDT

Na Zahoro Mlanzi

WAKATI mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Yanga ukiendelea, wanachama walioweka pingamizi kwa baadhi ya wagombea wanaowania uongozi wa klabu hiyo akiwemo aliyekuwa Mfadhili wa klabu hiyo, Yusuph Manji wametakiwa kuwasilisha vielelezo vya pingamizi walizoweka kwa Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo.
Shughuli hiyo ya kupokea vielelezo itaanza saa nne asubuhi makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Twiga na Jangwani na watatakiwa kutetea hoja zao.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa kamati hiyo Jaji Mstaafu, John Mkwawa alisema juzi saa 10 jioni ilikuwa ni siku ya mwisho ya kupokea pingamizi mbalimbali za wagombea uongozi wa klabu hiyo.
"Tunashukuru zoezi limekwenda vizuri na wapo wagombea waliowekewa pingamizi mgombea Yusuph Manji, ambaye anawania nafasi ya uenyekiti amewekewa pingamizi na wanachama watatu wenye kadi namba 007933, 008272 na 006225," alisema Mkwawa na kuongeza;
"Sara Ramadhani ambaye pia anawania uenyekiti naye amewekewa pingamizi na mwanachama mwenye kadi namba 003353 na 001702, lakini kwa pingamizi lililoletwa dhidi yake inaonesha walioweka wanataka ufafanuzi kama kiongozi aliyejiuzulu anaweza kugombea, hivyo hilo linahitaji ufafanuzi tu''.
Alisema mgombea Yono Kavela, ambaye anawania Makamu Mwenyekiti naye amewekewa pingamizi na mwanachama mwenye kadi namba 003974 na Ali Mayai ambaye anawania Ujumbe wa Kamati ya Utendaji.
Alisema baada ya kupokea pingamizi hizo, kamati imepanga siku ya leo kupokea ushahidi ambao unaweza kuwa wa binafsi au kwa maandishi (document) na si lazima aliyeweka pingamizi kuwepo siku hiyo.
Mkwawa alisema usaili utafanyika Juni 22, mwaka huu tofauti na ilivyopangwa awali kutokana na kutoa nafasi kwa kupitia vielelezo vya ushahidi vitakavyotolewa.
Alitoa hadhari kwa watu wanaoanza kufanya kampeni kabla ya siku hazijafika pamoja na wale wanaoingilia kamati hiyo katika shughuli zake.
Mbali na hilo, Mkwawa alizungumzia pingamizi la mwanachama Abeid Abeid 'Falcon', kwamba wamelitupia mbali kutokana na kujichanganya katika maelezo aliyoyawasilisha kwa kamati hiyo.
Posted: 19 Jun 2012 11:04 PM PDT
Msanii wa kundi la Wanaume Halisi, Juma nature akifanya vitu vyake wakati wa tamasha maalumu la kuitambulisha airtel supa5 mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Arusha.
Posted: 19 Jun 2012 11:00 PM PDT

Na Zahoro Mlanzi

WAKATI mshambuliaji kutoka Zambia, Davies Mwape akioneshwa mlango wa kutokea timu ya Yanga, imempa nafasi ya mwisho Mghana Kenneth Asamoah kuonesha makali yake katika michuano ya Kombe la Kagame la sivyo naye watamuacha.
Mbali na hilo, kiungo mpya wa timu hiyo, Nizar Khalfan jana alianza rasmi kibarua cha kuitumikia timu hiyo kwa kufanya mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzake zaidi ya 17 waliokuwepo katika mazoezi hayo.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo kwenye Uwanja wa Kaunda, Dar es Salaam jana Kocha Msaidizi wa timu hiyo Fredy Felix 'Minziro', alisema Asamoah imeamuliwa abaki kwa ajili ya michuano ya Kombe la Kagame lakini Mwape tayari ameshamalizana kila kitu na uongozi.
"Ni kweli Mwape licha ya kwamba unamuona mazoezi lakini hatutakuwa naye kwa msimu ujao, tayari uongozi umeshamalizana naye na hata Asamoah, naye anaangaliwa katika Kombe la Kagame na kama akiendelea kuonesha kiwango kile kile naye tutafikiria cha kufanya," alisema Minziro.
Alisema wachezaji hao wanalipwa fedha nyingi, hivyo walipaswa kuonesha kiwango tofauti na wachezaji wazawa ambapo kwa Mwape alishindwa kufanya hivyo, ndiyo maana wakaamua kusitisha mkataba wake ila Asamoah watamuangalia katika michuano hiyo.
"Unajua ukiwa mshambuliaji ni lazima ufunge tu huna jinsi na usipofunga mashabiki hawatakuelewa, Mwape katika mechi na Zamaleki ndiyo iliyomuweka pabaya kwa kupoteza nafasi nyingi za wazi," alisema Minziro.
Akizungumzia maandalizi kwa ujumla, Minziro alisema kwa sasa anawajenga wachezaji wake kuwa na stemina, ambapo baada ya wiki moja ataendelea na programu nyingine.
Wakati huohuo, Nizar ameanza rasmi mazoezi na timu hiyo ambapo mashabiki waliojitokeza katika mazoezi hayo walionesha kufurahishwa na uamuzi wake wa kujiunga na timu yao, ambapo kila alipogusa mpira walimshangilia.
Wachezaji ambao jana walikuwepo mazoezini ni kipa Yaw Berko, Godfrey Taita, Oscar Joshua, Nadir Haroub 'Canavaro', Ibrahim Job, Athuman Idd 'Chuji', Hamis Kiiza, Stephano Mwasika, Jeryson Tegete, Idrisa Rajab, Juma Seif 'Kijiko', Pius Kisambale, Asamoah, Omega Seme, Salum Telela na wengine watatu wa timu yao ya vijana.
Posted: 19 Jun 2012 10:59 PM PDT


Na Mwandishi Wetu

MATAMASHA ya kuitambulisha huduma Airtel Supa5 utaendelea tena mwishoni mwa wiki ambapo safari hii itakuwa ni zamu ya jiji la Mwanza ambalo wakazi wake watapata burudani katika viwanja vya wazi vya Furahisha.
Akizungumzia tamasha hilo jana  la kuitambulisha Supa5 jijini Mwanza Ofisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde alisema lengo la kuunganisha utambulisho huu kwa burudani ni kuwavutia vijana na wateja wengi kuhudhuria na kujifunza faida za Supa5 ili waitumie zaidi.
Alisema tamasha hilo litafanyika kwa siku mbili mfululizo ambapo Jumamosi watatoa fursa kwa wasanii chipukizi kujitokeza kwa wingi kuonesha vipaji vyao sambamba na kupata huduma ya Airtel Supa5.
Ofisa huyo alisema Jumapili itakuwa uzinduzi kamili ambapo wasanii wakongwe watatoa burudani, akiwemo Juma Nature na kundi zima la Wanaume Halisi, Mwasiti 'Soja' na Roma Mkatoliki watatoa burudani kwa wateja watakaohuduria tamasha hilo ambalo ni la bure.
Matinde alisema lengo la huduma hiyo ni kuhakikisha Airtel inatimiza dhamira yake iliyojiwekea ya kufikisha na kupunguza gharama za mawasiliano nchini kote bila kuwasahau vijana na wanafunzi kunufaika kwa kupata internet bure wakati wa usiku, kutuma sms bure na faida nyingine nyingi.
Huduma ya Airtel Supa5 ilizinduliwa hivi karibuni jijini Dar es salaam na baadaye kuendelea na matamasha katika mikoa ya Dodoma, Morogoro, Iringa na Arusha.

TSA yahimiza vyama kutoa mafunzo

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul 'Diamond' akiwa amebebwa juu na wacheza shoo wake wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 'Wajanja' lililofanyika katika ufukwe wa bahari ya Coco, Dar es Salaam juzi. Tamasha hilo lilidhaminiwa na Vodacom Tanzania. Na Mpigapicha Wetu

Na Zahoro Mlanzi

KLABU ya Simba, imetangaza rasmi kusitisha mkataba wa kiungo wake, Salum Machaku kwa ajili ya maslahi ya klabu na ya mchezaji mwenyewe.
Mbali na hilo, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Milovan Cirkovic anatarajia kutua nchini Ijumaa akitokea mapumzikoni nyumbani kwao Serbia, huku wachezaji wa kigeni 'Maproo' nao wanatarajia kuanza kuwasili siku hiyo.
Akizungumza na gazeti hili Makamo Makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam jana Ofisa Habari wa klabu hiyo Ezekiel Kamwaga, alithibitisha kuachwa kwa Machaku kwa kusema kiungo huyo sasa ni mchezaji huru.
"Ni kweli Simba imeamua kusitisha mkataba na Machaku kwa maslahi ya klabu na yake binafsi, hivyo kuanzia hivi sasa huyo ni mchezaji huru na timu yoyote inaweza kumsajili," alisema Kamwaga.
Alipotakiwa kuanisha zaidi sababu za kusitisha mkataba wa kiungo huyo, Kamwaga alisema ni uamuzi wa kawaida ambao wamefanya kama walivyofanya kwa wachezaji wengine na ndiyo maana wameangalia maslahi yake na ya klabu pia.
Mbali na hilo, Kamwaga alisema Cirkovic pamoja na wachezaji Felix Sunzu na Emmanuel Okwi wanatarajia kutua nchini kati ya Alhamisi na Ijumaa ambapo moja kwa moja watajiunga na wenzao walioko kambini.
Akizungumzia suala la kambi, Kamwaga alisema wana wiki ya pili tangu timu hiyo iingie kambini ambapo walianza kwa kuingia 'gmy' na jana jioni walitarajia kuanza mazoezi ya uwanjani kwenye viwanja vya Sigara, Dar es Salaam.

Alisema katika mazoezi hayo ndipo watakapoonekana wachezaji wao wapya waliowasajili msimu huu kwa ajili ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Kagame ambalo linatarajiwa kuanza rasmi Julai 14, mwaka huu.
Posted: 19 Jun 2012 12:18 AM PDT

Na Elizabeth Mayemba

WAZEE wa Kamati ya Muafaka ya Yanga wamewajia juu baadhi ya wanachama wa klabu hiyo ambao walikwenda kumtolea lugha chafu Seif Ahmed 'Magari', ambaye amekuwa msaada mkubwa kwa timu yao baada ya kufanikisha zoezi zima la usajili yeye pamoja na mfanyabiashara Abdallah Binkleb, ambaye amejitosa katika kinyang'anyiro cha Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo.
Akizungumza Dar es Salaam jana Katibu wa Wazee hao, Ibrahim Akilimali alisema tayari wafanyabiashara hao walisusia kufanya usajili huo, lakini walitumia busara zao na kuwabembeleza ili waendelee na kazi hiyo.
"Kuna wanachama watatu pamoja na kiongozi mmoja wa Kamati ya Utendaji ambao bila aibu walikwenda kwa Seif na kumtolea lugha chafu, hali ambayo ilisababisha asusie kazi hiyo yeye pamoja na wenzake lakini ikabidi tuwaangukie ili waendelee na tunashukuru Mungu walituelewa wazee wao," alisema Akilimali.
Alisema baada ya kukamilika kwa utaratibu mzima wa uchaguzi watachukua hatua kali kwa wanachama hao wakorofi, kwani wanalenga kuipeleka pabaya timu yao hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na michuno ya Kombe la Kagame na Ligi Kuu Tanzania Bara.
Katika hatua nyingine, Wazee hao wameazimia kulifuta tawi la Uhuru na kuwataka wanachama wake wakajisajili kwenye matawi mengine kwani tawi hilo lipo kwa ajili ya kueneza migogoro.
"Uanachama hatuwezi kuwafuta isipokuwa wakajisajili kwenye matawi mengine, tutalisimamia na kuhakikisha linafutwa kabisa," alisema.
Katika hatua nyingine uongozi wa klabu hiyo umemfungashia virago mshambuliaji wake, Mzambia Davies Mwape hivyo si mchezaji wao tena.
"Mwape tumemalizana naye hivyo si mchezaji wa Yanga tena, tunaliweka wazi hilo," alisema Katibu Mkuu wa Yanga Selestine Mwesigwa.
Posted: 19 Jun 2012 12:17 AM PDT

Posted: 19 Jun 2012 12:14 AM PDT

Na Zahoro Mlanzi

TIMU ya Yanga, imeanza rasmi mazoezi jana kwenye Uwanja wa Kaunda, Dar es Salaam ikiwa na wachezaji tisa wakiwemo kipa Yaw Berko na Keneth Asamoah huku kiungo wao mpya, Nizar Khalfan akiwa jukwaani akiangalia.

Gazeti hili lilifika Makao Makuu ya klabu hiyo, Mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam jana saa tatu asubuhi na kuikuta timu hiyo ikiendelea na mazoezi huku mashabiki wachache wa timu hiyo walijitokeza kuiangalia.

Wachezaji waliokuwepo katika mazoezi hayo yaliyokuwa chini ya Kocha Msaidizi, Fredy Felix 'Minziro' ni Berko, Oscar Joshua, Asamoah, Jeryson Tegete, Athuman Idd 'Chuji', Omega Seme, Ibrahim Job, Idrisa Rajab na Godfrey Taita.

Mazoezi hayo yaliendelea mpaka saa nne na nusu ambapo baada ya kumaliza wachezaji walisoma dua ya pamoja na kwenda kwenye vyumba vyao, huku mashabiki wakionekana kufurahishwa na kitendo hicho.

Gumzo lilikuwa kwa wachezaji Asamoah na Berko ambao waliripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari kwamba wangeachwa na kufanya kuwepo makundi ya mashabiki kutumia muda mwingi kuwazungumzia, huku kila mmoja akishindwa kuelewa juu ya uwepo wa wachezaji hao.

Pia Nizar naye alikuwa kivutio licha ya kwamba hakufanya mazoezi kutokana na kuwa na udhuru, alikuwa akizongwa na mashabiki hao na kuamua kukaa mbali na wachezaji wenzake walipokuwa uwanjani.

Baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo, Minziro alizungumza na gazeti hili na kusema kwamba timu yake imeanza mazoezi kwa ajili ya Ligi Kuu na Kombe la Kagame na kwamba wachezaji wengine wataendelea kuwasili.

Alisema ana imani kwa usajili walioufanya watatetea ubingwa wao wa Kagame pamoja na Ligi Kuu, hivyo amewataka mashabiki wa timu hiyo kuendelea kuwapa ushirikiano wachezaji wapya waliosajiliwa.

Akizungumzia kuhusu suala lake la kulipwa mshahara, Minziro alisema ameshamalizana na uongozi wa Yanga na kwamba kila kitu kinakwenda vizuri.
Posted: 19 Jun 2012 12:10 AM PDT

Na Mwandishi Maalumu, Maputo

KOCHA wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Kim Poulsen amesema baada ya kupoteza mechi dhidi ya Msumbiji 'The Mambas', sasa atajipanga upya kwa ajili ya mashindano yajayo kwani timu yake imeonesha uwezo mkubwa katika mechi hiyo ya juzi.
Kim aliishuhudia Taifa Stars, ambayo kwa sasa inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, ikiondolewa na Msumbiji kwa penalti 6-7 baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare bao 1-1 kwenye mchezo huo wa kusaka kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika mwakani.

Akizungumza na vyombo vya habari, Kim alisema  Stars walicheza vizuri lakini wapinzani wao walitumia nafasi nzuri ya kuwa nyumbani na kushinda.

"Nawapongeza kwa kushinda, lakini najivunia vijana wangu kwa jinsi walivyoweza kucheza kwa umakini muda wote wa mchezo.

"Nilijua Msumbiji wangeshambulia kwa nguvu, lakini na sisi tuliweza kucheza soka yetu ya kawaida na kutegeneza nafasi nyingi, nashukuru tumeweza kusawazisha lakini katika penalti lolote linaweza kutokea.

Naye kocha wa Msumbiji, Gert Engels aliwasifu Stars kwa kucheza vizuri huku akiwapongeza wachezaji wake kwa kushinda mchezo huo.

"Tanzania ni timu nzuri inacheza kwa uwelewano mkubwa, lakini wakati wa mapumziko niliwaambia wachezaji wangu watulie na wacheze kama nilivyoowaagiza.

Wanapaswa kuitunza hii timu ya Taifa Stars kwa sababu ina wachezaji wengi chipukizi wenye vipaji vya hali ya juu ni bahati mbaya tu tumewafunga kwenye penalti.

Naye beki Erasto Nyoni, alisema wamepokea kwa masikitiko matokeo hayo lakini aliahidi kuisaidia timu hiyo kwenye michezo mingine.

"Tunatakiwa kujipanga upya kwa ajili ya mechi za kusaka tiketi ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia 2014, lazima tukubali matokeo," alisema Nyoni.

Naye nahodha msaidizi wa Stars, Aggrey Morris alisema hawana kingine zaidi ya kujiuliza wapi walipokosea, ili kurekebisha makosa hayo.

Watanzania wengi waliojitokeza kushuhudia mchezo huo walioneshwa kufurahhishwa na kiwango cha Stars na kusema hata kama wameondolewa, walicheza kwa kujituma.

Anuary Aziz, ambaye anafanya kazi Maputo alisema hajawahi kuona Watanzania wanaoishi nchini hapa wakijitokeza hivyo kushangilia timu yao na kuongeza kuwa walishapata taarifa kuwa Taifa Stars imeboreshwa.

“Kwa kweli timu imebadilika na kocha huyu asisumbuliwe aachwe afanye kazi yake, tumeshindwa lakini vijana wamecheza hadi dakika ya mwisho kwa kweli tumefurahi na tumeshangilia sana.
“Tanzania tutafika mbali sana tuwe na subira tu kwani wachezaji wetu wanatupa matumaini sana…mchezo huu ulikuwa wa kwetu lakini tumeshindwa kwa penalti tumekubali matokeo na tunajua tutafika mbali,” alisema Mohamed Ali ambaye ni Mtanzania mwingine anayeishi Maputo.
Stars inategemewa kuwasili leo usiku ikitokea Maputo kupitia Nairobi.
Posted: 19 Jun 2012 12:06 AM PDT
Mashabiki wa Taifa Stars wanaoishi nchi Msumbiji wakiishangilia timu yao wakati wa mechi ya kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika iliyochezwa juzi jijini Maputo. Stars ilifungwa kwa mikwaju ya penalti 7-6. Na Mpigapicha Wetu
Posted: 19 Jun 2012 12:03 AM PDT

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nassib Adbdul ‘Diamond’ anatarajia kupamba mashindano ya kumsaka Redd's Miss Dar Intercollege 2012, yaliyopangwa kufanyika Juni 22 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa , uliopo mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Akizungumza Dar es Salaam jana Mratibu wa mashindano hayo Dina Ismail alisema mbali na Diamond, onesho hilo pia litapambwa na burudani kutoka bendi ya Skylight ambayo ipo chini ya mshiriki wa Tusker Project Fame mwaka juzi, Anneth Kushaba.
Alisema maandalizi yanakwenda vyema ambapo warembo 14, watakaosghiriki wanaendelea na mazoezi katika hoteli ya The Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
“Mwaka huu tumejipanga vyema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar Intercollege anafanya vizuri katika fainali za Miss Tanzania,” alisema Dina.
Warembo watakaoshiriki mashindano hayo  wanatoka vyuo vya  Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time, Ustawi wa Jamii,  Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo Kikuu Huria (OUT ambapo taji hilo linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM.
Dina aliwataja wanyange watakaopanda jukwaani kuwa ni Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda  Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
Posted: 19 Jun 2012 12:01 AM PDT
Mchezaji wa timu ya soka ya NBC, Hussein Shabani (kulia), akiwania mpira na Henry Justin wa Barclays wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika Dar es Salaam juzi. NBC ilishinda kwa penalti 4-3. (Na Mpigapicha Wetu)

Posted: 19 Jun 2012 12:00 AM PDT

Na Amina Athumani

CHAMA cha Kuogelea Tanzania (TSA), kimewataka wanachama wake 13 kuandaa mafunzo ya kuogelea na uokoaji kama yaliyofanywa na Klabu ya Tanzania Marine Swiming Clab (TMSC), ili kuwasaidia Watanzania wengi kupata mbinu ya kujiokoa.
Akizungumza Dar es Salaam juzi wakati wa kuhitimisha mafunzo ya kuogelea na uokoaji yaliyofanywa na TMSC Katibu Mkuu wa TSA, Noel Kiunsi alisema hii ni mara ya kwanza klwa mwanachama wa TSA kuandaa mafunzo hayo ambayo kwa kiasi kikubwa pia yanasaidia kuutangaza mchezo huo.
Alisema TSA imeanzisha programu ya kuendeleza mafunzo ya uokoaji chini ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT), ambapo kwa sasa wapo katika mchakato wa kupata fedha kwa ajili ya kuanza programu hiyo ambayo itakuwa ikiendeshwa na TSA pamoja na wanachama wake, ambao ni klabu kwa nchi nzima.
Kiunsi alisema msukumo wa kuanzisha programu hiyo umetokana na matukio endelevu yanayotokea majini, hasa katika vyombo vya usafiri huku akizitaja ajali za majini ambazo ziliwahi kupoteza maisha ya watu wengi kama ajali ya Meli ya MV Bukoba na ile ya MV Spice Islander.
Alisema endapo Watanzania wengi watapatiwa mafunzo hayo kutaepusha wimbi la watu kuzama majini, hasa yanapotokea majanga katika vyombo vya usafiri na hata vile vya angani ambavyo hukimbilia baharini kwa kunusuru maisha yao.
Kiunsi aliwataja wanachama TSA ambao watashirikiana kuendesha programu hiyo kuwa ni Talis, Hopac, UDSM, TMSC, Dar swim, Stringleis, Isamilo, Agakhan, JKT na klabu za Zanzibar.
Posted: 18 Jun 2012 11:58 PM PDT

Na Zourha Malisa

SIKU chache baada ya serikali kuwasilisha bajeti ya mwaka wa fedha 2012/2013, bungeni mjini Dodoma, baadhi ya wasanii wameipongeza kwa kuweza kutambua mchango wa kazi zao kwa kuwaingiza katika mfumo rasmi utakaolinda kazi zao.
Wasanii hao wameipongeza serikali kwa jitihada za kuinua uchumi wa nchi na kipato cha msanii kwa kulinda kazi za wasanii kupitia mapato yatakayopatikana.
Akizungumza Dar es Salaam jana Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba alisema mfumo wa sekta rasmi utapunguza wizi wa kazi za wasanii pamoja na kulinda haki ya msanii.
“Kutakuwa na takwimu sahihi za mauzo ya kazi za wasanii na mapato ya wasanii, pia yataeleweka na mwisho wa mwaka unaweza kujua nani ameuza kwa kiwango gani,” alisema.
Alisema watakuwa na kila sababu ya kudai serikalini kwani kila kitu kitakuwa kipo wazi hivyo serikali itoe elimu kwa jamii, ili kujua kazi ipi ni sahihi kununua kwa ajili ya kuongezea pato la taifa.
Aliongezea kwamba wanyonyaji wanauchukia mfumo huo, kwani walishazoea kuwakandamiza wasanii hivyo mfumo huu ni tiba kwa wale wote waliozoea kujinufaisha kwa kupitia nguvu za wasanii.
Posted: 18 Jun 2012 11:53 PM PDT

Na Amina Athumani

MWANAMUZIKI wa kizazi kipya nchini Mh. Temba kesho anatarajia kutoka na wimbo wake wa kwanza wa taarab utakayojulikana kama 'Usisemwe kwani wewe nani'.
Akizungumza Dar es Salaam jana, mtayarishaji wa wimbo huo Haji Ndanda kutoka studio ya HVP iliyopo Kigamboni, alisema wimbo huo wa taarabu ni wa kwanza kuutoa na kwamba ana imani italiteka soko la muziki huo.
Alisema Temba amezoeleka kuimba muziki wa kizazi kipya na kwamba kwa mara ya kwanza ameamua kuja na staili mpya ya taarabu.
Mtayarishaji huyo alisema wimbo huo utaanza kuonekana na kusikika katika vyombo mbalimbali vya habari kesho na kwamba ipo katika video na audio.
Alisema wimbo huo ameamua kumshirikisha msanii mwenzake wa muziki wa kizazi kipya, Z-Anto ili kuongeza vionjo na kwamba ana imani mashabiki wengi wa taarabu wataupokea vizuri hasa kutokana na uhodari wa Temba aliouonesha katika video ya wimbo huo.
Posted: 18 Jun 2012 11:51 PM PDT

Na Amina Athumani

MWAKILISHI wa Tanzania katika michezo ya Olimpiki bondia wa ngumi za ridhaa Selemani Kidunda, amesema ingawa amekosa mapambano ya kimataifa bado ana nafasi ya kufanya vyema katika michezo hiyo.
Michuano ya Olimpiki inatarajia kufanyika London, Uingereza Julai 27 mwaka huu ambapo Tanzania itawakilishwa na wanamichezo sita akiwemo Kidunda na wanariadha Zakia Mrisho, Samson Ramadhan, Dickson Marwa na Faustin Musa pamoja na muogeleaji Magdalena Mushi.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kindunda alisema mechi za kirafiki alizocheza makocha wake wamepata nafasi ya kurekebisha makosa yaliyojitokeza na kwamba bado anayo nafasi nzuri ya kufanya vyema kwenye michezo ya Olimpiki.
Alisema hakupata mapambano mengi ya kimataifa kama kama ilivyoshindikana kwenda Botswana na yale yanayoendelea nchini Kenya kutokana na Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) kukumbwa na ukosefu wa fedha.
Kidunda ambaye kwa sasa yupo Kibaha, Pwani katika kambi iliyopo Shule ya Sekondari ya Filbert Bayi, ananolewa na kocha Zakaria Gwandu pamoja na bondia mmoja kwa ajili ya kumpa sapoti.
Wawakilishi hao wa Tanzania katika michezo Olimpiki wanatarajia kuondoka nchini Julai 8, mwaka huu kwenda kwenye michuano hiyo.
Posted: 18 Jun 2012 11:45 PM PDT

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

PAZIA la mashindano ya Epiq Bongo Star Search (EBSS) kwa Mkoa wa Dodoma, limefungwa rasmi jana huku vipaji vingi vikiwa vimejitokeza na kuwavutia majaji.
Kilichovutia zaidi ni washiriki wa miaka 16, ambao walionekana kuimba vyema na kuwafurahisha hata kwa washiriki wenzao waliofurika katika Ukumbi wa Royal Village.
Akizungumzia mshindano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Benchmark Production inayoandaa EBSS, Ritha Paulsen alisema amevutiwa na wingi wa washiriki mkoani hapa, hasa idadi ya washiriki ya wasichana.
Alisema ikiwa ni mara ya kwanza kuruhusu washiriki wa miaka 16 kuingia katika usaili wa EBSS 2012, ameshuhudia hazina kubwa ya vipaji  vya washiriki wa umri huo.
Katika usaili huo kulikuwa na washiriki wa aina mbalimbali wakiwemo wanafunzi, wafanyabiashara ndogondogo, vijana wa mitaani na wadau wengine wa muziki.
Kwa kuthamini umuhimu wa akina mama na watoto mshiriki aliyefika kuonesha kipaji chake katika ukumbi huo alipewa nafasi ya kuimba, ili aweze kuwahi kuondoka.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel ambao ni wadhamini wakuu wa EBSS 2012 Awaichi Mawalla, mbali na kuvutiwa na ushiriki wa vijana waliojitokeza, pia alihamasisha upimaji wa damu kwa kuchangia damu kwa kituo cha damu mkoani Dodoma.
“Kwa kupitia EBSS 2012, tunataka kuwafikia vijana si tu katika muziki bali hata katika kuhamasisha masuala mbalimbali yahusuyo jamii kama vile hili la kuchangia damu na mengineo,” alisema Awaichi.
Washindi watakaopatikana watatangazwa baadaye katika vyombo vya habari. Baada ya Dodoma kwa sasa inafuata Zanzibar Ijumaa ijayo katika eneo la Ngome Kongwe.
Posted: 18 Jun 2012 11:44 PM PDT
Madam Ritha akipokea mtoto kutoka mshiriki huyu aliyekuja nae katika shindano hilo kabla ya kuanza ya kuanza kuimba.
Posted: 18 Jun 2012 11:37 PM PDT

Na Victor Mkumbo

BONANZA la michezo mbalimbali la Vyuo vya Elimu ya Juu vya Dar es Salaam lililofanyika juzi lilikuwa kivutio kwa wadau waliojitokeza.
Bonanza hilo lililoshirikisha vyuo saba ambalo lake lilikuwa kuibua vipaji lilifanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam.
Vyuo vilivyoshiriki bonanza hilo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM), Chuo Cha Ustawi wa Jamii, Chuo Kikuu cha Biashara (CBE), Chuo cha Ualimu (DUCE) na Chuo Kikuu cha Kampala (KIU).
Katika bonanza hilo ambalo lilifanyika kwa mwezi mmoja lildhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Tanzania Breweries (TBL) kupitia kinywaji chake cha Grand Malt, ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni Bernad Marcelline, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya kumalizika bonanza hilo, Marcelline alisema michezo hiyo imefanikiwa kuimeibua vipaji vya wanafunzi wa vyuo hivyo katika michezo mbalimbali.
Alisema vijana hao hawana budi kujikita katika fani mbalimbali za michezo, kutokana na kuwa michezo ni ajira.
Marcelline alisema washindi walioshinda kwenye michezo mbalimbali wanatakiwa wawe changamoto kwa kuwashawishi wenzao kuingia katika fani ya michezo.
Naye Meneja wa Grand Malt Consolata Adam, alisema wanatarajia kuendelea kudhamini bonanza hilo katika mikoa yote yenye vyuo vikuu.
Posted: 18 Jun 2012 11:37 PM PDT

Na Victor Mkumbo

MNYANGE Lisa Jensen, ndiye atakayewakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo ya Miss World 2012, yatakayofanyika Inner Mongolia nchini China mwaka huu.
Lisa aliibuka kidedea katika mashindano madogo ya Redd's Miss Tanzania, yaliyofanyika juzi katika Ukumbi wa 327 Dar es Salaam.
Mrembo huyo aliibuka mshindi baada ya kuwashinda wenzake tisa, ambapo mashindano yalishirikisha warembo 10 ambao waliwahi kushiriki fainali za Miss Tanzania zilizopita.

Katika mashindano hayo ya Redd's Miss Tanzania, yalikuwa tofauti na ilivyozoeleka ambapo warembo hawakuulizwa maswali ila walikuwa wanatoa mada tofauti tofauti kuhusu upeo wao na jinsi ya kuisaidia jamii.
Baada ya kuibuka mshindi Lisa alizawadiwa sh. milioni 2, kugharamiwa gharama zote za safari pamoja na kambi ya mwezi mmoja ambayo itakuwa Dar es Salaam, kabla ya kwenda China katika mashindano ya Miss World 2012 na gharama zote zitalipwa na Kampuni ya Lino Agency ambayo ndiyo inayoandaa Miss Tanzania.
Warembo walioshiriki katika mashindano hayo ni Gloryblaca Mayowa, Hamisa Hassan, Queen Saleh, Christine Willium, Pendo Laizer, Lisa Jensen, Mwajabu Juma, Neema Saleh, Jenifer Kakolaki na Stella Mbuge.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na Hamisa Hassan huku Pendo Laiser akishika nafasi ya tatu.
Katika mashindano hayo kulikuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa kikundi cha ngoma za asili cha Wanne Stars pamoja na Saluti Dancers.
Posted: 18 Jun 2012 11:36 PM PDT
Miss tz
Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Miss World, Lisa Jensen (wa pili kulia), akivishwa taji na Miss Tanzania Salha Israel,baada ya kutangazwa mshindi katika shindano la Redd's Miss Tanzania lililofanyika juzi, kushoto ni mshindi wa pili Hamisa Hassan na kulia ni mshindi wa tatu Pendo Laiser(Picha na Victor Mkumbo)
Posted: 18 Jun 2012 11:32 PM PDT
Na Amina Athumani

KLABU a kuogelea ya Tanzania Marine Swimming Club (TMSC), jana ilimaliza mafunzo ya kuogelea na kujiokoa kwa watu zaidi ya 50 yaliyofanyika katika fukwe za chuo cha Mwalimu Nyerere, Kigamboni.
Mafunzo hayo ya siku mbili yaliandaliwa na TMSC na kudhaminiwa na Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yakilenga kutoa mbinu za uokoaji, kuogelea na jinsi ya kujiweka katika hali ya kusubiri kuokolewa pindi maafa yanapotokea.
Akizungumza wakati wa kufunga semina hiyo ambayo iliendeshwa kwa nadharia na vitendo Mratibu wa mafunzo hayo, Geofrey Kimimba alisema programu hiyo itakuwa endelevu kwa kuwa ni moja ya malengo ya klabu yake.
Alisema wameamua kuandaa semina hiyo kutokana na ukweli kwamba majanga ya majini yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara, lakini Watanzania wanashindwa jinsi ya kujisaidia pindi majanga hayo yanapotokea.
Kimimba alisema kwa kufanya hivyo itasaidia idadi ya watu wengi kujiokoa ama kuokoa wenzao, pale watakapopatwa na janga la kuzama kwa chombo cha majini ama mafuriko kama yaliyowahi kutokea jijini Dar es Salaam Desemba mwaka jana.
Alisema mikakati ya klabu yake ni kuhakikisha wanatoa mafunzo hayo mara kwa mara, ingawa muitikio wa Watanzania unahitaji zaidi kusukumwa kutokana na watu wengi kushindwa kujitoa hata pale wanapoamua kuendesha mafunzo hayo bila kiingilio.
Mratibu huyo alisema semina hayo ililenga zaidi kuwafundisha Watanzania ambao hawajawahi kuogelea na hawajui jinsi ya kujiokoa na kwamba mafunzo hayo yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa, kutokana na washiriki wote kuelewa kwa vitendo walichofunzwa.
TMSC kwa sasa ina waogeleaji 55 tangu kuanzishwa mwaka 2009 ambapo mpaka sasa klabu hiyo imeshiriki michezo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.
"Tumefanya hivi ili kusaidia kizazi chetu cha Tanzania, ambacho kisingekuwa na uwezo wa kulipia gharama kubwa katika klabu nyingine ambazo zinaonekana asilimia kubwa ya washiriki wake ni wazungu," alisema Kimimba.
Alisema klabu hiyo inatumia bahari katika kutoa mafunzo kwa waogeleaji wake, tofauti na klabu nyingine ambazo zinatumia mabwawa na kwamba waogeleaji wake, ingawa wanatumia bahari wamekuwa wakitoa upinzani mkubwa katika michezo ya ndani na nje ya nchi.
Posted: 18 Jun 2012 11:31 PM PDT
Na Amina Athumani

WAANDAAJI wa tamasha la filamu la Zanzibar International Film Festrival (ZIFF), wameandaa warsha na kongamano kwa waandaaji na watayarishaji wa filamu.
Warsha hiyo itaanza Julai 9, mwaka huu na kushirikisha watayarishaji na waandaaji kutoka nchi mbalimbali, zitakazoshiriki tamasha hilo linalofanyika kila mwaka Ngome Kongwe, Zanzibar.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa tamasha hilo, Martine Mhando alisema
warsha hizo zitasaidia kuongeza ujuzi katika kupiga picha na kuhariri filamu.
Alisema pia kutakuwa na warsha maalumu ya uongozaji itakayotolewa na Mario Van Pleebles, ambaye ni muongozaji wa filamu wa kimataifa ambapo itawasaidia zaidi waongozaji wa filamu wa hapa nchini.
Mhando alisema tamasha hilo kwa mwaka huu litawavutia zaidi washiriki kutokana na ZIFF kujipanga na kufanya mabadiliko makubwa mwaka hadi mwaka.
Mbali na warsha hizo, tamasha hilo pia linatoa nafasi kwa wasanii wa filamu kutoka nchi mbalimbali kwa kazi zao kuingia kwenye tuzo za ZIFF, ambazo zinatolewa kwa msanii aliyefanya vizuri katika ikiwemo tuzo ya filamu bora, msanii bora na tuzo nyingine.
Posted: 18 Jun 2012 11:30 PM PDT
Mshambuliaji wa Taifa Stars, Thomas Ulimwengu akiwatoka mabeki wa timu ya Msumbiji katika mechi ya kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika mwakani iliyochezwa jana jijini Maputo. Stars ilifungwa kwa penalti 7-6. (Na Mpigapicha Wetu)
Posted: 18 Jun 2012 11:28 PM PDT

Na Mwandishi Wetu, Maputo

TIMU ya Taifa (Kili Taifa Stars), jana imetolewa kiume na Msumbiji 'Mambas' katika mechi ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON), zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
Katika mechi hiyo Taifa Stars ilitolewa kwa mikwaju ya penalti 7-6, baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika muda wa kawaida. Katika hatua hiyo ililazimika kupigiana penalti zaidi ya tano baada ya kila timu kufunga mikwaju yote.
Mechi hiyo ilipigwa katika Uwanja wa Taifa wa Zampeto jijini Maputo.
Katika mechi hiyo timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 dakika 90 za kawaida na kulazimika kutumika sheria za kupigia penalti ambapo washindi waliibuka na mabao 7-6.
Awali timu hizo ambazo zilikutana jijini Dar es Salaam, mwanzoni mwa mwaka huu zilitoka sare sare ya bao 1-1.
Katika mechi hiyo Stars ndiyo iliyoanza kufungwa kipindi cha kwanza kwa bao lililofungwa na Jeremies Saito aliyeunganisha krosi ya Helder Pelembe.
Kipindi cha pili Stars iliingia kwa nguvu na kutandaza soka la uhakika kwa lengo la kutafuta mabao, lakini ukuta wa wapinzani wao ulikuwa mgumu kupitika kutokana na mabeki wake kuwa imara.
Juhudi za vijana hao wa Poulsen zilizaa matunda dakika ya 90, baada ya kupata bao lililofungwa na Agrey Morris baada ya kuunganisha kona iliyochongwa na Amir Maftah.
Baada ya dakika 90 kumalizika ndipo sheria za mikwaju ya penalti ikatumika ambapo wachezaji wa Stars Mbwana Samatta, Morris na Kelvin Yondani walikosa na kuifanya Msumbiji kusonga mbele.
Posted: 18 Jun 2012 11:27 PM PDT
Na Mwandishi Wetu

UCHAGUZI wa Yanga, uliopangwa kufanyika Julai 15 mwaka huu umeingia 'gundu' baada ya aliyewahi kuwa Mhazini wa klabu hiyo Ahmed Falcon kuwawekea pingamizi wagombea wote.
Akizungumza Dar es Salaam jana Falcon alisema ameamua kuweka pingamizi kutokana na kwamba uchaguzi unafanyika na katiba ambayo haijasajiliwa na Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo.
"Nimeamua kuwawekea pingamizi wanaowania uongozi Yanga kwa kuwa wanafanya uchaguzi usio halali kuwa katiba wanayotumia bado haijasajiliwa na msajili," alisema.
Alisema yeye kama mwanachama halali wa Yanga, hawezi kuona taratibu zinakiukwa baadhi ya watu kutokana na maslahi yao binafsi.
Falcon ambaye alijiuzulu Yanga, wakati wa uongozi wa Imani Madega alisema huu si wakati wa kufumbia macho madudu yanayotaka kufanywa na wasioitakia klabu hiyo mema.
Alisema atahakikisha anafuatilia maslahi ya Yanga hadi kieleweke kwa kuwa kukaa kimya ni kuitakia mabaya klabu hiyo kongwe.
"Ni lazima tuwe na uchungu na klabu yetu, hatuwezi kuona kanuni na taratibu zinavunjwa makusudi kwa kuwa ilitakiwa kuisajili katiba kama ilivyo kwa vyama vingine," alisema.
Baadhi ya wanachama waliojitokeza kuwania uongozi wa klabu hiyo ni pamoja na aliyewahi kuwa mdhamini Yusuf Manji, John Jambele na Sarah Ramadhan wanaowania nafasi ya Mwenyekiti.
Wagombea wengine waliojitokeza ni Yono Kevela, Ayoub Nyenzi, Ally Mayay na Clement Sanga wanaowania nafasi ya Makamu Mwenyekiti.