TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, July 23, 2016

JK AKABIDHI RASMI KIJITI CHA UENYEKITI KWA DKT JOHN POMBE MAGUFULI JIONI YA LEO MJINI DODOMA


Ntahakikisha Serikali inahamia Dodoma :Rais Magufuli

Na. Immaculate Makilika- Dodoma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema katika kipindi cha uongozi wake atahakikisha Serikali inahamishia makazi yake mjini Dodoma. Amesema hayo leo, wakati alipokuwa akihutubia wajumbe wa Chama cha Mapinduzi(CCM) katika Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama hicho uliofanyika mjini Dodoma mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti.“Nitahakikisha katika awamu ya uongozi wangu, Serikali inahamia Dodoma, najua viongozi wengine wote nao watanifata, kwa kuwa sasa miundombinu ya Dodoma inaweza kukidhi mahitaji yote” alisema Rais Magufuli.Rais Magufuli aliendelea kusema kuwa katika kipindi cha miezi nane ya uongozi wake chini ya Serikali ya Awamu ya Tano ameweza kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuanza kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.Akiongelea maeneo ya utekelezaji katika kipindi chake Dkt. Magufuli alisema kuwa mpaka sasa Serikali imefanikiwa kusimamia suala la utoaji wa elimu bure kwa shule za Msingi na Sekondari nchini na kuwezesha udahili kuongezeka zaidi tofauti na miaka iliyopita.Aidha Dkt. Magufuli alisema kuwa Serikali yake pia imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika ukusanyaji wa mapato ya serikali hali itakayosaidia kuimarisha utoaji wa huduma muhimu za jamii.Aidha, Serikali ya Awamu ya Tano imeagiza ndege mbili mpya zinazotarajiwa kuwasili nchini Septemba mwaka huu,Rais Dkt. Magufuli aliongeza kuwa Serikali yake kwa kushirikiana na Serikali ya Uganda wamefanikiwa kujenga bomba la kusafirisha mafuta kutoka Hoima katika ziwa Alberti nchini Uganda kwenda bandari ya Tanga ambapo mafuta hayo yatasafirishwa sehemu mbalimbali duniani na bombahilo litazalisha zaidi ya ajira 20,000.Vile vile, Rais Magufuli alisema kuwa Serikali yake imeweza kurudisha nidhamu ya kazi kwa watumishi wa umma na kuweza kuondoa watumishi hewa waliokuwa na waliokuwa wamefikia 12,500,na kuongeza kuwa kwa mwaka huu Serikali imetenga fedha za matumizi jumla ya shilingi trilioni 29.5, ambapo asilimia 40 ya fedha hizo zitapelekwa katika kutekeleza shughuli za maendeleo.Mkutano Mkuu Maalum wa CCM ulihudhuriwa na wajumbe zaidi 2,000 ulimpitisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa mshindi na Mwenyekiti wa Chama hicho kwa kura 2398 kati ya kura 2398 zilizopigwa ikiwa ni sawa na asilimia 100.Rais Magufuli anakuwa Mwenyekiti wa awamu ya Tano baada ya kupokea uongozi huo kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama hicho anayemaliza muda wake Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka 10.

BENKI YA CRDB YAKABIDHI TIKETI ZA NDEGE KWA WASHINDI WA KAMPENI YA 'SHINDA NA TEMBOCARD

MGANA MSINDAI ALIYEKUWA CHADEMA AMWAGA YAKE YA MOYONI MKUTANO MKUU WA CCM LEO MJINI DODOMA


NAIBU WAZIRI MALIASILI NA UTALII, ENG. RAMO MAKANI ATEKELEZA AHADI YA SERIKALI ALIYOITOA BUNGENI YA KUTEMBELEA ENEO LA MGOGORO WA HIFADHI YA MSITU WA SAYAKA MKOANI MWANZA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kushoto) akiongoza kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama cha Wilaya ya Magu alipotembelea Wilayani humo hivi karibuni kuona eneo la mgogoro katika Hifadhi ya Msitu wa Sayaka ambapo aliahidi kwa niaba ya Serikali kupitiwa upya maeneo yoye ya Hifadhi yenye migogoro nchini na kutafutiwa suluhu ya kudumu.












makabidhiano ya halmashauri kwa wakurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa

Angalia Kipindi Chote Cha ' Nyumbani Na Diaspora' TBC1

JK AKABIDHI KIJIKI KWA DKT JOHN POMBE MAGUFULI

Serikali yasisitiza matumizi ya bidhaa za ndani.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Uledi Mussa akiongea na wadau mbalimbali wa uchumi nchini hawapo pichani wakati wa kufunga mkutano wa mwaka wa mashauriano ya ushiriki wa watanzania Katika uwekezaji uliofayika jijini Dar es salaam.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) Bi. Beng’i Issa akiongea na wadau mbalimbali wa uchumi nchini hawapo pichani wakati wa kufunga mkutano wa mwaka wa mashauriano ya ushiriki wa watanzania Katika uwekezaji uliofayika jijini Dar es salaam.
 
Mdau wa Uchumi nchini na Mkurugenzi wa taasisi binafsi inayojihusisha na biashara Namaingo Business Agency Bi. Biubwa Ibrahim akichangia hoja wakati wa kufunga mkutano wa mwaka wa mashauriano ya ushiriki wa watanzania Katika uwekezaji uliofayika jijini Dar es salaam.
Mdau wa Uchumi nchini na Mkurugenzi wa Mfuko wa Bima (NIC) Bw. Sam Kamanga akichangia hoja wakati wa kufunga mkutano wa mwaka wa mashauriano ya ushiriki wa watanzania Katika uwekezaji uliofayika jijini Dar es salaam.
wadau mbalimbali wa uchumi nchini wakifuatilia kwa makini majadiliano ya wachngiaji mada wakati wa kufunga mkutano wa mwaka wa mashauriano ya ushiriki wa watanzania Katika uwekezaji uliofayika jijini Dar es salaam.


Na Ally Daud-Maelezo

Serikali imesisitiza matumizi ya bidhaa za ndani ya nchi zinazotengenezwa na watanzania ili kukuza uchumi wa nchi na kupanua ukubwa wa masoko ili kuleta maendeleo.

Akizungumza hayo wakati wa kufunga mkutano wa mwaka wa mashauriano ya ushiriki wa watanzania Katika uwekezaji Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Uledi Mussa amesema kuwa watanzania wajifunze kupenda na kutumia bidhaa za ndani ili kuweza kuinua nchi kiuchumi kwa maendeleo ya Taifa letu.

“Ni lazima watanzania tujifunze kubadilika kifikra na kimtazamo katika kutumia bidhaa zilizopo nchini kuchangia Katika kukuza uchumi wa nchi yetu ili kupiga hatua Katika maendeleo ya Tanzania”alisisitiza Bw.Uledi.

Aidha Bw. Uledi amesema kuwa mwekezaji yeyote awe wa ndani au wa kigeni anapaswa kutumia wafanyakazi wa nchini kama kama anataka kuwekeza Katika Taifa letu ili kutoa fursa kwa watanzania kushiriki Katika kuinua uchumi.

“Mwekezaji wa kigeni au wa ndani inampasa atumie wataalamu na wafanyakazi wa Tanzania kama anataka kuwekeza nchini mwetu ili vijana wetu wa kitanzania wapate fursa ya kuchangia Katika kuinua uchumi wa nchi”.aliongza Bw. Uledi.

Mbali na hayo Bw. Uledi Mussa amesema kuwa kiwanda chochote kinachowekeza nchini wanapaswa kutumia malighafi kutoka Tanzania ili kuweza kupiga hatua kimaendeleo Katika Taifa letu kwa ujumla.

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) Bi. Beng’i Issa amesema kuwa Katika mkutano huo wenye kauli mbiu ya “Ongeza Ushiriki Inua Uchumi” umetoka na mkakati wa kuhakikisha makampuni yote ya uwekezaji kutoka nje yajiandikishe Katika soko la Hisa (DSE) ili kuongeza ushirikina umiliki wa watanzania Katika makampuni husika.

Aidha bi. Issa ameongeza kuwa mkutano huo umelenga kuwa wakandarasi wote ambao wa ndani wanapewa malipo yao kwa wakati kama walivyokubaliana ili kumsaidia mtanzania kushiriki Katika kukuza uchumi wa nchi.

Friday, July 22, 2016

EALA EULOGISES HON HAFSA MOSSI AT SPECIAL SITTING.
















UTIAJI SAINI MAKUBALIANO YA AWALI YA UJENZI WA RELI YA KATI (STANDARD GAUGE)







TBL YAZINDUA BIA MPYA YA NDOVU RED MALT JIJINI DAR ES SALAAM

 Maua yaliyohudumia tukio hilo.