TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, November 30, 2013

HII NDIYO PIKIPIKI YA MABONDIA MOHAMED MATUMLA NA NASSIBU RAMADHANI

Meneja Masoko wa kampuni ya haojue,Wawa Laida kulia akiwaonesha pikipiki itakayogombaniwa Dar es salaam jana na mabondia Nassibu Ramadhani kushoto na Mohamed Matumla siku ya Desemba 25 katika ukumbi wa friends corner wengine wa pili kushoto ni Rashidi Matumla,Christopher Mzazi na mlatibu wa mpambano uho Kaike Siraju
Mratibu wa mpambano wa ndondi Kaike Siraju akiojiwa akiwa juu ya pikipiki itakayogombaniwa na mabondia Mohamed Matumla na Nassibu Ramadhani siku ya Desemba 25
Bondia Mkongwe Rashidi Matumla akizungumzia mpambano wa mwanae Mohamedi Matumla na Nassibu Ramadhani litakarofanyika Desemba 25
Meneja Masoko wa kampuni ya haojue,Wawa Laida akihojiwa 
Meneja Masoko wa kampuni ya haojue,Wawa Laida kulia akiwaonesha pikipiki itakayogombaniwa Dar es salaam jana  na mabondia Nassibu Ramadhani kushoto na Mohamed Matumla siku ya Desemba 25  wengine wa pili kushoto ni Rashidi Matumla,Christopher Mzazi na mlatibu wa mpambano uho Kaike Siraju 

Meneja Masoko wa kampuni ya haojue,Wawa Laida kulia akiwaonesha pikipiki itakayogombaniwa Dar es salaam jana  na mabondia Nassibu Ramadhani kushoto na Mohamed Matumla siku ya Desemba 25  wengine wa pili kushoto ni Rashidi Matumla,Christopher Mzazi na mlatibu wa mpambano uho Kaike Siraju

WAZIRI WA KILIMO YAMKUTA MAZITO, NI KUHUSU NAPE NAUYE.


3 - Copy
>> Amtaka aandae majibu kwa Kamati Kuu sio kumshambulia magazetini
>> Ahoji busara anayoidai itumike ni ipi?
>> Asisitiza kutetea wakulima ni msimamo wa Chama
>> Amkumbusha CCM ni chama cha wakulima
>> Ahoji busara ya kuachia ushirika kuwadhulumu wakulima.
>> Ahoji busara ya kulazimisha wakulima kutumia mbolea ya Minjingu inayoharibu mazao yao.
>
Katibu wa NEC itikadi na uenezi amemtaka
 Waziri wa kilimo, Chakula na Ushirika kuacha kumshambulia kwenye magazeti badala yake atumie muda huu kuandaa majibu ya kuwasilisha Kamati Kuu kwa hoja zilizoibuliwa na wakulima nchini.
Nape akihutubia mamia ya wananchi wa mji wa Vwawa wilayani Mbozi mkoani Mbeya alionyesha kukerwa na tabia ya hivi karibuni ya Waziri huyo kumshambulia Nape kwenye magazeti kwa maneno ya kejeli badala ya kujibu malalamiko ya wakulima.
 ” Katibu Mkuu tumezunguka wilaya nyingi sana nchini hakuna mahali hakuna malalamiko ya wakulima ambao ni 80% ya watanzania wote. Sasa tumemtaka waziri aje kwenye kamati kuu kueleza anatatuaje changamoto hizi, yeye amekazana kila kukicha kunishambulia kwenye magazeti. Nataka kumpa ushauri wa bure mheshimiwa sana waziri, anachofanya hanishambulii mimi anawashambulia wakulima kwasababu siongei yangu naongea malalamiko
 ya wakulima” alisisitiza Nape
 ”Nimemvumilia sana lakini sasa nimechoka, kila kukicha anatumia maneno ya kejeli na vijembe, kwanini hajifunzi busara ya Naibu wake Adam Malima? aliposikia wito wetu akasema yuko tayari kuja kujieleza kwenye Kamati Kuu kwakuwa chama ndiyo mwajiri wake hivyo atazingatia maamuzi ya chama, yeye waziri kila kukicha Nape Nape Nape, kumshambulia Nape hakuondoi kero za wakulima”! Alisema Nape
 ”Nimesikia leo anasema sina busara!!busara ipi anayohoji? Mie ninayewatetea wakulima wanaolalamika kulazimishwa kutumia mbolea ya Minjingu inayounguza mazao yao na yeye anayeleta mbolea hiyo na kulazimisha wakulima watumie nani anatumia busara hapa? Yeye anayepuuza malalamiko ya wakulima kuumizwa na baadhi ya maafisa ushirika na mimi ninayetaka hatua zichukuliwe dhidi ya maafisa wake nani anatumia busara??”
 ” mimi ninayemkumbusha kutembelea mkoa alioutangaza kuwa ghala la taifa la chakula ambao hajautembelea kwa miaka sasa licha ya kuwa waziri wa chakula na yeye ambaye hajatembelea nani anatumia busara?”
 ” mimi ninayemshauri asikilize kilio cha wakulima wa tumbaku,pamba na korosho badala ya kusikia kilio hicho miaka nenda miaka rudi na
 yeye nani anatumia busara?”
Katika ziara hiyo ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye ameongozana na  Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye imekuwa na mafanikio makubwa  na imeongeza sana imani kwa wananchi wenye mapenzi mema na nchi hii.
Ziara hii imekuwa ya aina yake kwani Katibu Mkuu amepata fursa ya kusikia matatizo ya wananchi kuanzia wakulima ambao ndio asilimia 80%,walimu ambao ni zaidi ya asilimia 60% ya watumishi wa serikali,na kundi kubwa la vijana ambalo pamoja na kuwepo kwa taratibu za kufanya shughuli zao kwa kujiajiri bado wamekutana na vikwazo visivyo vya kawaida.
Uamuzi wa kuwaita Mawaziri kwenye kamati kuu ya chama ili watoe majibu kwa nini matatizo ya wananchi hasa wakulima hayashughulikiwi .
Wakulima wamelalamika sana kuhusu dhuluma  zinazofanywa na vyama vya ushirika na upatikanaji wa pembejeo kuwa wa tabu na cha ajabu Waziri wa Kilimo na watumishi wake wameziba masikio hata kutembelea wakulima kutaka kujua matatizo yao hawataki.

JE KUPOROMOKA KWA MAJENGO NINI TAFAKARI YA TAIFA?


…………………………………………………………………..
Dar es Salaam. Utafiti uliofanywa hivi karibuni na Taasisi ya Twaweza unaonyesha kuwa licha ya kuwapo sababu nyingine zinazochangia kutokea kwa ajali za kuporomoka kwa majengo, rushwa inaonekana kuwa chanzo kikuu cha kukithiri kwa hali hiyo.
Ripoti ya utafiti huo inaeleza kuwa rushwa imekuwa ikichangia kwa kiasi kikuba majengo mengi kujengwa chini ya kiwango, hali inayochangia kutokea kwa majanga mbalimbali yanayogharimu maisha ya Watanzania.
Utafiti huo umekuja kufuatia tukio la Machi 29 mwaka huu ambapo jengo la ghorofa 36 katika Mtaa wa Indira gandhi liliporomoka na kusababisha vifo na wengine  kadhaa kujeruhiwa.
Akiwasilisha ripoti hiyo, mmoja wa watafiti kutoka katika mradi wa Sikiliza, Dk Thomas Maqway alisema licha ya serikali kusisitiza kuchukua hatua mbalimbali lakini utafiti huo unaonyesha  kuwa wananchi hawana imani na mfumo wa  kisheria katika kuwawajibisha na kuwaadhibu wanaohusika kusababisha ajali zinazotokana na majengo kuporomoka.
Alisema hali hiyo inatokana na mfumo wa rushwa unaonekana kutawala katika ujengaji wa majengo kuanzia ukandarasi, usanifu, vifaa, ujenzi  hadi kwenye ukaguzi wa majengo katika jiji ji la Dar es Salaam.
“Asilimia 78 ya wahojiwa walioshiriki katika utafiti huu wanataja  rushwa ndiyo sababu ya kuendelea kutokea kwa hali hii, hivyo hata uwajibishwaji wa wahusika hawana imani.

WAZIRI GHASIA ACHONGEWA NA CWT JIJINI MBEYA.


1 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Tamisemi), Hawa Ghasia ameingia matatani baada ya Chama cha Walimu Wilaya za Mbozi na Momba mkoani Mbeya kumchongea jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
CWT kilidai Ghasia alikataa kusomewa risala ya walimu wenye kero akidai anazijua, hivyo hana haja ya kusikiliza. Kutokana na kauli hiyo, Kinana aliomba asomewe taarifa hiyo.
Msoma taarifa,Leonard Nyamiye alisema walimu wanaidai Serikali zaidi ya Sh1 bilioni za mishahara ,uhamisho na mengine mengi. Mwalimu huyo alisema kutolipwa madeni hayo kumewafanya waichukie sana CCM na Serikali.
Akizungumza Kinana alisema suala la Ghasia atalifikisha kwa mwajiri wake. Kinana ambaye katika ziara yake amekuwa akikutana na viongozi wa CWT kila wilaya, alikiri kusikia kero za walimu siku nyingi. ”Nakumbuka mwaka 2010 Rais Kikwete alikaa na CWT Taifa kwa saa tisa ili kumaliza tatizo, lakini kila baada ya mwaka linajitokeza”, alisema.
Kinana alisema sasa CCM italivalia njuga na kwamba itajadili chanzo cha tatizo katika kikao cha NEC ijayo. Hata hivyo alidokeza kuwa amegundua kwamba walimu hawana mwajiri mmoja na ndiyo maana wanasumbuliwa.
Alisema walimu kwa sasa wanashughulikiwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Tamisemi, Tume ya Ajira na Hazina jambo ambalo ni kero.

ULIMWENGU,SAMATTA-KATIKA KIBARUA KOMBE LA SHIRIKISHO, MASWALI NI KAMA WATAWEZA KUVAA KIATU CHA DHAHABU.


FAINALI ya pili ya kombe la shirikisho itapigwa leo katika dimba la Mazembe mjini Lubumbashi baina ya wenyeji TP Mazembe dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia.
Katika mchezo wa leo washambuliaji wawili raia wa Tanzania Mbwana Ally Samatta na Thomas Ulimwengu watakuwa wakiiongoza timu yao kutafuta ushindi muhimu na wakihistoria kwao.
Samatta anatarajiwa kuonesha makali yake zaidi huku ikizingatiwa kuwa ni miongoni mwa wachezaji wanaowania tuzo ya CAF ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza klabu za ndani.
Kama mshambuliaji huyo atafunga leo na kuonesha kiwango cha juu, itamsaidia kujiweka mazingira mazuri zaidi ya kubeba tuzo hiyo inayotolewa na shirikisho la soka barani Afrika, CAF.
samataMazembe wanahitaji kushinda mabao 3-0 wakiwa katika dimba lao, kwani fainali ya kwanza walifungwa mabao 2-0 na Watunisia hao dimba la Olympique de Rades mjini Tunis.

Mabao hayo yaliyoipa karaha Mazembe na mashabiki wake, yalifungwa na washambuliaji wawili raia wa Gabon, Ibrahim Didier Ndong aliyefunga bao la kwanza dakika ya 16 na mshambuliaji Taha Yassine Khenissi aliyefunga la pili dakika ya 90.
Siku hiyo Samatta na Ulimwengu wote walianza kikosi cha kwanza pamoja na mkali Tressor Mputu Mabi, lakini bado mambo yalikuwa magumu zaidi kwani Watunisia walionekana kuwa bora zaidi yao na kuweza kutumia nafasi walizopata.
image1 
Thomas Ulimwengu naye mzigoni kama kawaida leo
Bingwa wa Kombe hilo atazawadiwa kitita cha dola za Kimarekani, 625 000, wakati mshindi wa pili atapata dola 432 000.
Mshindi pia atamenyana na mabingwa wa Ligi ya Mabingwa, Al Ahly ya Misri kuwania taji la Super Cup mechi itakayopigwa nchini Misri Februari 2014.
Wachezaji waliokuwa wakiunda kikosi cha Simba SC mwaka 1993 walivalishwa Medali za Fedha na Rais mstafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi baada ya kufungwa mabao 2-0 na Stellah Abidjan ya Ivory Coast mwaka 1993 katika fainali ya pili ya Kombe la CAF Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Awali, Simba ilitoa sare ugenini na kuwapa matumaini Watanzania kwamba taji la kwanza kubwa Afrika lingetua nchini mwaka 1993. 
Baada ya mchezo wa leo wa fainali, kesho, Samatta na Ulimwengu watakwea pipa kuelekea jijini Nairobi Kenya kujiunga na kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania bara, Kilimanjaro Stars kinachojiandaa na mchezo wa pili wa kombe la CECAFA dhidi ya Somalia desemba 2 mwaka huu.
Mchezo wa kwanza, Kili Stars walitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya waliowahi kuwa mabingwa wa soka barani Afrika, timu ya Taifa ya Zambia maarufu kwa jina la Chipolopolo.

Taarifa Za Msanii TID Kukamatwa Na Polisi Jana Usiku.

Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Khaleed Mohamed 'TID' yupo mahabusu katika Kituo cha Polisi Oysterbay tangu jana usiku baada ya kukamatwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi msichana anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake, Mariam Nnauye.

Huyu Ndio Mariam Nnauye. Taarifa zinasema kuwa ugomvi ulianza maisha club jana usiku baada ya TID kumkuta Mpenzi wake akiongea na mwanaume mwingine bila ruhusa ya Top In Dar na ndio Top akamvuta mpenzi wake na kumpiga makofi.Bila kijali mapenzi yao binti huyo alikwenda moja kwa moja kituo cha polici Osterbay na kutoa taarifa ya kupigwa naTid.

Tid ametoka mida ya saa tano asubuhi kwa Dhamana na ataripoti tena polici jumatatu.

 

"Kindness Covers All of My Political Beliefs"

Welcome to this Thanksgiving Edition of West Wing Week, your guide to everything that's happening at 1600 Pennsylvania Avenue, and beyond. This week, the President traveled to the west coast for a three day, three city swing, sat down for an interview with Barbara Walters, met with student entrepreneurs, held a video conference with Peace Corps volunteers, and announced a breakthrough in diplomatic talks with Iran. That's November 22rd to November 28th or "Kindness Covers All of My Political Beliefs."
Watch this week's edition of West Wing Week

 
 
  Top Stories
In his weekly address, President Obama gave thanks to all the men and women defending our freedom and acknowledged their sacrifice might mean they can’t spend the holidays with their families. The President also recognized that as Americans, we gather together this Thanksgiving to lift up those who need a helping hand, letting us move forward as a country and lead us to a brighter tomorrow.
This Saturday, November 30th, Senior Advisor Valerie Jarrett will join a number of White House and Cabinet Officials, along with millions of Americans around the country, in paying tribute to small businesses that drive our economy, and help to define the spirit of our communities.
President Obama pardoned two 20-week-old, 38-pound turkeys named Popcorn and Caramel -- and announced Popcorn as the official "National Thanksgiving Turkey," after the American public weighed in on their favorites via Twitter, Facebook, and Instagram.

Hii ndiyo Ndege inayotembeza kombe la Dunia nchi mbalimbali Duniani. Hapa ilipotua kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Hii ndiyo Ndege inayotembeza kombe la Dunia nchi mbalimbali Duniani. Hapa ilipotua kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Thursday, November 28, 2013

KILI STARS , CHIPOLOPOLO HAKUNA MBABE


 Na Mwandishi Wetu, Nairobi
  Timu ya taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro jana imeshuka uwanjani kumenyana na Zambia, katika mechi ya ufunguzi ya michuano ya Kombe la Chalenji.

Kilimanjaro Stars na Zambia zimechuana kuwania pointi tatu katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Machakos ulioko nje kidogo ya jiji la Nairobi. 
 
Timu hiyo ya Tanzania Bara iliyopangwa Kundi B, ilihitaji ushindi ili kupata pointi tatu ambazo zingeiweka katika nafasi nzuri kwenye michuano hiyo. 
 
Akizungumzia mchezo huo wa jana, Kocha Mkuu wa Kili Stars, Kim Poulsen alisema timu yake imeshindwa kupata ushindi kutokana na wachezaji wengi kuwa wachovu wa safari, 
 
Alisema kikosi chake kimefanya mazoezi  magumu, amb a y o bado wachezaji wanauguza viungo vyao,  hata hivyo kulikuwa na upinzani mkubwa dhidi ya Zambia inayosifika kwa kutandaza soka ya kiwango bora Afrika. 
 
Kilimanjaro Stars iliwategemea zaidi wachezaji kama Mrisho Ngasa, Amri Kiemba, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Said Morad, Athuman Idd na Salum Abubakar. 
 
Pia, wamo Frank Domayo, Himid Mao, Haruna Chanongo, Ramadhan Singano ‘Messi’, Farid Mussa na Elias Maguli.
Katika mechi ya ufunguzi iliyochezwa juzi mchana timu ya taifa ya Zanzibar iliifunga Sudan Kusini mabao 2-1 katika mchezo mkali uliokuwa na ushindani.

MTOTO MWINGINE WA MANGULA AFARIKI,JK AMLILIA

 Na Mwandishi Wetu 
 
  Rais Jakaya Kikwete, amemtumia salamu za rambirambi Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Philip Mangula, kufuatia kifo cha mtoto wake, Peter Philip Mangula, kilichotokea juzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa amepelekwa kwa matibabu akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu.

"Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa za kifo cha mwanao (Peter Philip Mangula)," alisema kwa masikitiko Rais Kikwete katika salamu zake.
 
Rais Kikwete aliongeza kusema kuwa; nasikitishwa zaidi na taarifa za kifo hiki kwa kuzingatia kwamba ni katika kipindi kifupi kilichopita, Mangula alimpoteza binti yake, Neema Nemela Mangula aliyefariki dunia kutokana na ajali ya gari, hivyo ni dhahiri kwamba kifo cha kijana wake huyu kimeongeza machungu na simanzi kwa familia ya Mangula na kimesababisha pengo kubwa kwa wanafamilia kwa ujumla. 
 
"Kutokana na taarifa hizo za kusikitisha, ninakutumia wewe salamu zangu za rambirambi na pole nyingi kwako wewe binafsi na kwa familia yako yote kwa ujumla kwa kupotelewa na mtoto wako."
Alisema anamuomba Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mjalie yeye na familia yake moyo wa uvumilivu na ujasiri ili kuhimili machungu ya kuondokewa na kijana wao. 

JELA MAISHA KWA KULAWITI MTOTO


 Na Prosper Mgimwa, Katavi 
 
  Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemuhukumu, Leonald Wiliamu (19), mkazi wa Kijiji cha Mwese Namba Moja Wilaya ya Mpanda kifungo cha maisha jela kwa tuhuma ya kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka saba (jina tunalo).

  Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda, Chiganga Ntengwa, baada ya mahakama kutokuwa na mashaka na ushahidi uliotolewa mahakamani wa mashtaka.
 
Katika kesi hiyo ambayo ilikuwa na washtakiwa wawili mshtakiwa mwingine alikuwa na umri wa 17 ambaye alihukumiwa adhabu kuchapwa viboko vinne kutokana na kuwa na umri chini ya miaka 18.
  Washtakiwa hao walidaiwa kutenda kosa hilo la kumlawiti mtoto huyo Julai 31, mwaka huu saa mbili usiku nyumbani kwao. Watuhumiwa hao walikuwa wameajiriwa kufanya kazi ya kuchunga mifugo kwa baba mzazi wa mtoto huyo. 
 
  Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Chiganga alisema baada ya kusikiliza mwenendo mzima wa kesi, mahakama iliwaona washtakiwa wanakabiliwa na kosa hilo la kulawiti. 
 
  Washtakiwa kabla ya kusomewa hukumu walipewa nafasi ya kujitetea, ambapo waliiomba mahakama iwaachie huru kutokana kwa kile walichodai kuwa walisingiziwa kutenda kosa hilo na baba wa mtoto huyo kwa kuwa walikuwa wakimdai mshahara kwa muda mrefu. 
 
  Akisoma hukumu hiyo, Ntengwa alisema Wiliamu anahukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto huyo na mwenzake, Yohane anachapwa viboko vinne

MHARIRI GAZETI LA UHURU AFARIKI

Na Rose Itono
  Mhariri na Msanifu Mkuu Msaidizi wa gazeti la Uhuru, Dunia Mzobora, amefariki dunia usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kutokana na ugonjwa wa shinikizo la damu.

Akizungumza kwa njia ya simu jana, Mhariri Mtendaji wa gazeti la Uhuru, Josia Mufungo, alisema marehemu kabla ya mauti yake alikuwa kazini kama kawaida ambapo saa mbili usiku alimaliza kazi zake na kurejea nyumbani.
Alisema usiku wa saa sita walipata taarifa kutoka kwa familia yake kuwa Dunia amezidiwa na kukimbizwa haraka hospitali kwa ajili ya matibabu.
"Marehemu alikimbizwa Hospitali ya Agha Khan lakini walishindwa na kuamua kumpeleka Muhimbili kwa matibabu zaidi na saa 12 za asubuhi alifariki", alisema.
Mufungo alisema marehemu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu kwa muda mrefu na kuongeza kuwa msiba wake utafanyika nyumbani kwake Tabata Kimanga, ambapo anatarajiwa kuzikwa leo saa 7.00 za mchana na shughuli zote za mazishi zitakuwa hapo hapo nyumbani kwake.
Alisema marehemu ameacha mjane na watoto watano. Alijiunga na gazeti la Uhuru mwaka 1989 kama mwandishi mwanafunzi ambapo baadaye alipanda hadi kufikia nafasi aliyokuwepo

LHRC YATAKA KATIBA MPYA IOKOE MUUNGANO


Na Mariam Mziwanda 
 
  Muungano wa Tanzania na Zanzibar umefananishwa na mgonjwa aliyelazwa kwenye Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU), hivyo Watanzania wametakiwa kuunusuru kupitia Katiba Mpya inayotarajiwa kupatikana kabla ya uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia, wakati akifungua mkutano wa siku tatu wa asasi za kiraia. 
 
Alisema ni muhimu kwa wananchi kupewa fursa ya kujadili Muungano na kuufahamu kwa kina kuwa unahitajika ili kuepukana na chuki zinazopandikizwa kutoka kwa wanasiasa wenye uchu wa madaraka.
“Kuna wanasiasa wachache wanaotumia nafasi zao ndani ya jamii kupotosha wananchi kuhusu muungano, wanapandikiza chuki kwa ahadi za kisiasa ili wapate madaraka,” alisema. 
 
Aliongeza kuwa elimu ya faida za Muungano ikiwafikia vizuri wananchi na kupewa fursa ya kujadili ipasavyo kwa muda uliopo kabla ya Bunge la katiba inatosha kuufanya hudumu na kuwa matunda kwa vizazi vijavyo.
Alisema Muungano uliopo unategemea kufa au kupona kutokana na maamuzi ya nchi kupitia katiba mpya kwani umegubikwa na kero nyingi ambazo kwa muda mrefu hazijapatiwa tiba.
 
“Muundo wa Muungano ni tatizo hususani katika uundaji wa Serikali yenyewe hali inayosababisha wananchi wa pande zote mbili kulalamika, lakini wakati uliopo unatosha kupitia Bunge la katiba kunusuru muungano ulipo,” alisema.
Akileleza changamoto kubwa ambazo wananchi wanatakiwa kuzipatia majibu kupitia katiba mpya ili kuwa nyenzo ya uhai wa Muungano huo alisema ni pamoja na utatuzi wa suala la mapato katika mgawo wa asilimia nne kwa Zanzibar na uwepo wa uhuru wa kuchagua viongozi. 
 
Kwa upande wa mjumbe wa AZAKI takriban 36, Baraka Mohamed Shamte, alisema Watanzania bado wanahitaji Muungano na kwamba jambo la muhimu ni kujadili matatizo yaliyopo na kuyafanyia kazi ili uendelee kudumu.
“Kuanzishwa kwa Muungano hakukuwa kwa bahati mbaya historia ya Muungano wananchi wake ni wamoja, vijana wa leo wakishasoma na kupata shahada wanafikiri wanafahamu kila kitu, kulikuwa na sababu tosha za kuungana kwa nini Muungano huo haukuwa na Kenya nchi nyingine ni vyema kuwa wa kweli katika kuzungumzia Muungano,” alisema.
 
Kwa upande wake Ramadhan Suleiman Nzori aliwataka vijana wasomi kutambua kuwa wanategemewa sana katika kulinda na kuthamini Muungano na wasichukue vitu vidogo vidogo na kuona ni rahisi kuvunja Muungano uliopo.

UTEKAJI WATOTO, UCHUNGUZI MKALI WAENDELEA


  Siku moja baada ya gazeti hili kuripoti habari za watoto wanadaiwa kutekwa na kufichwa katika handaki lililopo kwenye msitu wa Mabwepande, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, ambalo ndani yake kuna jengo kubwa lenye vyumba, Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi mkali, anaripoti Masau Bwire.

Chanzo chetu cha habari kimedokeza kuwa, uchunguzi huo unafanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani Pwani. 
 
"Polisi wapo katika uchunguzi mkali tangu leo (jana), asubuhi, si vyema kuzitoa taarifa mapema kabla uchunguzi haujakamilika, tunaweza kuharibu upelelezi na wahusika kukimbia. 
 
" Watoto wal i o j i o k o a w a m e p e l e k w a h o s p i t a l i kuchunguzwa afya zao baada ya kuhojiwa na kutoa picha kamili ya eneo lenye handaki, hivyo uchunguzi ukikamilika mtaambiwa," kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa jina lake. 
 
Utekaji watoto wanaodaiwa kuwa zaidi ya 60 katika handaki hilo, unadaiwa kufanywa na raia wa kigeni (Wazungu), wakishirikiana na Watanzania ambapo watoto hao hufungiwa katika vyumba hivyo, kuteswa, kulawitiwa na kubakwa. 
 
Watoto waliodai kutoroka kwenye handaki hilo ni Emmanuel Robert (11) anayesoma darasa la tano Shule ya Msingi Maendeleo iliyopo Tabata, Segerea, Dar es Salaam na mdogo wake Godianus Robert (8), anayesoma darasa la tatu shuleni hapo. 
 
Watoto hao walidai kutekwa na Wazungu wawili asubuhi ya Septemba 2 mwaka huu, wakati wakienda shuleni na kufanikiwa kutoroka katika jengo hilo Septemba 23 mwaka huu.  
 
Wakiwa wamechoka na afya zao kuzorota katika Kituo kidogo cha Polisi, Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani, watoto hao walisema ndani ya jengo hilo kuna watoto wengi wa kike na kiume. 
 
Wa l i s e m a w a t o t o h a o wanafanyishwa kazi na kuteswa kwa kutandikwa fimbo, kuchomwa moto na kupigwa shoti ya umeme hasa wanapowaulizia wazazi wao ambapo baadhi yao hubakwa na kulawitiwa. 
 
Akizungumza na Majira, Emmanuel alisema baada ya kutekwa yeye na mdogo wake, walifungwa na vitambaa vyeusi usoni hadi walipofikishwa ndani ya jumba hilo la mateso.
Aliiomba Serikali kufanya jitihada za hali na mali ili kuwaokoa watoto wengine waliopo katika jengo hilo. 
 
Mama mzazi wa watoto hao, Martha Godianus (29), ambaye anafanya shughuli za mama lishe, njia panda ya Barakuda, Tabata Manispaa ya Ilala, alisema amehangaika zaidi ya miezi mitatu kuwatafuta watoto hao bila mafanikio. Juzi Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei alikiri kupata taarifa za tukio hilo na kuanza kuzifanyia kazi

PINDA AWASHUKIA MAOFISA MIPANGO


Na Mwandishi Maalum

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amewataka maofisa mipango miji nchini kurekebisha utendaji wao wa kazi ili waweze kubadili taswira mbaya iliyojengeka miongoni mwa jamii dhidi yao.

Alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua Mkutano wa Kwanza wa Wataalam wa Mipango miji waliosajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango miji ulioanza jana jijini Dar es Salaam.
“Taswira ya utendaji kazi katika taaluma ya mipango miji na katika sekta ya ardhi kwa ujumla miongoni mwa wananchi na Serikali sio nzuri sana. 
 
 Watafiti wanatueleza kuwa kati ya asilimia 60 na 80 ya makazi kwenye miji yetu hapa nchini yamejengwa kiholela.
Na kwa kiwango hicho hicho wakazi wa mijini wako kwenye makazi hayo na wanaishi kiholela,î alisema. 
 
“Wako wanaosema ninyi ndiyo chanzo cha hiyo migogoro, wako wanaosema ninyi kwa rushwa ndiyo wenyewe, mimi sishangai madai haya ila ninawasihi muwe na roho ngumu katika kushinda vishawishi hivi,” alisisitiza. 
 
Aliwataka wajadili masuala yanayohusu migogoro ya ardhi baina ya wafugaji na wakulima, baina ya mipaka ya vijiji, baina ya wilaya, baina ya wanavijiji na hifadhi za Taifa au maeneo ya uchimbaji madini na kujadili njia za kutatua migogoro hiyo ili kuwa na mipamgo endelevu. 
 
Aliwataka waangalie suala la ukuaji wa miji iliyokaribu na Jiji la Dar es Salaam kwa kuangalia dhana ya miji mikubwa kubeba vijiji vinavyoizunguka na hasa kuangalia uwezekano wa kupunguza mrundikano wa watu katika jiji hilo. 
 
“Miji ya Kibaha, Mkuranga na Bagamoyo inatumikaje kusaidia kupunguza msongamano katika jiji la Dar es Salaam,” Waziri Mkuu alihoji.
Alisema wataalamu wa mipango miji wanapaswa kuwa na maono makubwa ya baadaye kama kweli wanataka kupunguza majanga katika siku za usoni. 
 
“Angalieni utafiti wa gesi unaoendelea pale Mtwara na mjipange, angalieni mpango wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na kuunganisha na reli ya kati, angalieni Lindi na upatikanaji wa Liquified Naturala Gas (LNG), pangeni miji kwa siku za baadaye siyo sasa,” alisisitiza. 
 
Aliwataka wanataaluma hao wasimamie vyema taaluma yao kwani katika miaka 37 ijayo, (mwaka 2050) inakadiriwa kwamba nusu ya watu wote watakuwa wakiishi mijini. “ Kuweni wakweli, tumieni weledi wenu la sivyo katika miaka 37 ijayo kama wanavyosema watafiti, itakuwa balaa tupu,î alisema.
 
Mapema akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wataalamu hao kutoka mikoa yote hapa nchini, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka, alisema maofisa mipango miji wanakabiliwa na changamoto ya kufikiri na kubuni aina ya miji ambayo itakidhi mahitaji ya jamii ya baadaye. 
 
Alisema hata hivyo maofisa hao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kushindwa kutoa maamuzi au ushauri wa kitaalamu kwa kuhofia kuadhibiwa na madiwani.
Wizara ya Fedha. " Kwa nafasi yake ndiye alikuwa akishiriki kuandaa bajeti ya upinzani bungeni, kuwasilisha bajeti ya wizara ya fedha akiwa waziri kivuli, lakini kwa kuvuliwa wadhifa wake maana yake haaminiki tena," alisema mmoja wa watoa habari ndani ya chama hicho kwa sharti la jina lake kutochapishwa gazetini.
 
Hata hivyo, juhudi za kumpata Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika, ili kuweza kuzungumzia suala hilo ziligonga mwamba kutokana na simu yake ya kiganjani kutopokelewa.
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi Makao Makuu jijini Dar es Salaam leo linatarajia kufanya mahojiano na Katibu wa CHADEMA mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kileo, baada ya mahojiano hayo kukwama kufanyika jana kutokana na malalamiko yanayodaiwa kuwasilishwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe. 
 
Mahojiano hayo yalikuwa yafanyike Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam jana mchana, lakini yaliahirishwa muda mfupi baada ya Kileo kuwasili akiwa na mwanasheria wake na makada wengine wa CHADEMA.
Baada ya kufika maofisa wa Polisi walifanya mazungumzo na mwanasheria wake, lakini baada ya muda walikubaliana yafanyike leo saa tano.
 
Akizungumza na gazeti hili jana, Kileo, alisema awali mahojiano yalitakiwa yafanyike jana saa nane mchana, lakini walichelewa kufika makao makuu ya polisi kutokana na wakili wake kuchelewa kwani alikuwa na kesi makao makuu ya Polisi. 
 
Kileo, alipoulizwa anatakiwa polisi kwa ajili ya makosa gani, alisema hana taarifa kwa undani, kwani alipigiwa simu na ofisa aliyejitambulisha kwa jina la Mbutta na kumwambia kuwa anatakiwa kufika makao makuu ya Polisi kwa mahojiano kutokana na malalamiko ambayo Zitto, ameyafikisha. 
 
"Niliambiwa nahitajika kujibu tuhuma ambazo Zitto amezifikisha Polisi, lakini sikuelezwa ni tuhuma gani hizo," alisema Kileo. Alipoulizwa ni kwa nini Zitto apeleke shtaka hilo Makao Makuu ya Polisi, badala ya vituo vingine kama ilivyo kawaida, Kilewo alijibu; "Mimi sijui labda wapigie polisi ili muwaulize swali hilo."
Gazeti moja (sio Majira) jana lilichapisha habari inayoeleza kuwa Zitto, amemfungulia mashtaka Kileo akimtuhumu kusambaza waraka katika mitandao ya kijamii unaomhusisha na mipango ya kufanya mapinduzi ya chama hicho.