TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, April 16, 2016

Rais Magufuli afungua rasmi mradi wa ujenzi wa barabara ya juu (flai ova) eneo la Tazara

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea maelekezo kuhusu mradi wa barabara za juu eneo la Tazara kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wakala wa barabara (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale katika ufunguzi rasmi wa mradi huo Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbaliwa kitaifa na kimataifa wakati wa ufunguzi rasmi na kuanz akwa ujenzi  wa mradi wa barabara ya juu Tazara Jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia katika hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam.










SERIKALI YA KOREA YAGHARAMIA UJENZI WA HOSPITAL YA CHANIKA UTAKAO GHARIMU BILIONI 8.8 ZA KITANZANIA








Balozi huyo aliipongeza serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na nchi ya Korea katika shughuli mbalimbali jambo linaloimarisha uhusiano baina ya wananchi wa nchi hizo.

DART YAHIMIZWA KUELIMISHA WAKAZI WA DAR










HAKUNA MUDA WA KULALA, WAZIRI MKUU AIAMBIA DART










WANYAMA PORI WAVAMIA MASHAMBA YA WANANCHI NA KUMALIZA MAZAO YAO







“awali tulikuwa tunawafukuza wanyama hawa lakini mamlaka ikaja nakutunyima kufukuza wanyama lakini cha kushangaza mara baada yakutuzuia kufukuza wakatuambia tukiona mnyama tupige simu tatizolililokuja ukipiga simu unaambiwa na viongozi ambao wapo hapa katikakituo cha wanyama pori cha losteti wanasema hawana magari hivyo hawawezikuja kufukuza wanyama na sisi wananchi tunashindwa tufanyajeunakuta tembo kaja au mbogo hivi unamfukuzaje jamani inabidi uache aleakitosheka aondoke “alisema Seuri lazier

MTOTO WA MALKIA WA NORWAY AKUTANA NA VIJANA WALIOINGIA 5 BORA YA SHINDANO LA MASHUJAA WA KESHO LA STATOIL TANZANIA


Mtoto wa Malkia wa Norway (Crown Princess of Norway), Mette Marit akisikiliza kwa makini maeneo ya namna shindano hilo lilivyoendeshwa kutoka kwa Afisa wa Kampuni ya Statoil Tanzania, Eric Mchome.

DONDOO ZA MAGAZETI YA LEO

INAFRIKA BAND YAFANYA KWELI NASHVILLE, TENNESSEE

MKURUGENZI WA HALMASHAURI WA MJI KAHAMA APEWA SIKU TISINI NA WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU AWE AMENUNUA MASHINE YA MIONZI X RAY.

MWANAFUNZI MTANZANIA ASHIRIKI ONYESHO LA UBUNIFU LILILOANDALIWA NA RAIS BARACK OBAMA


WAZIRI NAPE AFANYA ZIARA MKOANI MARA NA SHINYANGA LEO





HADITHI: NDOA YA MTOTO WA TAJIRI BILIONEA NA MTOTO WA MASIKINI_MKULIMA.


Ni simulizi ya kweli ambayo imewatokea  watu mbali mbali.

Mtunzi : Shaaban Mpalule

kufanya maamuzi siku zote ni jambo gumu  linalomuweka mtu kwenye wakati mgumu sana, nampenda sana mke wangu, nipotayari kufa kwa ajili yake kwa kuwa nafahamu thamani yake kwangu, lakini nitaonekanaje kwa wananchi ninapotakiwa kumteka Mhe Rais ili nimuokoe mke wangu asiuwawe, japo ni jambo gumu ila mimi nitaweza tu?

Niliumiza sana kichwa changu kuwaza huyu mwanamke, ninavyompenda, ilikuwa ni mara tu baada ya kukutana naye kwa mara ya kwanza, wakati huo tukiwa bado vijana, macho yangu yalipogongana na macho ya mrembo huyo ghafla mwili na mapigo ya moyo yalinienda mbio sana, sikuwa na njia ingine zaidi ya kutaka kumfahamu, lakini sikuweza kupata fulsa ya kuzungumza naye pamoja na kwamba macho yetu tulipotazamana kila mmoja alihisi kitu Fulani.


Usiku wa siku hiyo nilikuwa nimezoea chakula mapema sana lakini siku hiyo sikuwa na furaha hata chembe, nilihisi nimeshiba pamoja na kwamba sikuwa nimepata kula kwa masaa hayo ya usiku,na muda mwingi nilibaki kuwaza kwa nini imenitokea hali hiyo na aijawahi kutokea wakati wote pamoja   kwamba nimewahi kukutana na wasichana wengi warembo, na wakati mwingine nilipewa jina mitaani kwamba mtu wa warembokutokana na sifa niliyokuwa nayo ya kuwa karibu sana na wasichana wengi warembo ambao ni wazuri sana.

“Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.”
Sasa kama mungu alisema si vema huyo mtu kuwa peke yake, nikajiuliza, je huyu ni nani basi ambaye mungu amemweka ili afanane naye?
Tena Bwana Mungu akasisitiza katika kumwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.

Kumbe wakati najaribu kutafakari tayari usingizi mzito ukanipitia nikalala; nilipostuka ilikuwa ni usiku mkubwa sana , sikupata tena usingizi maana nakumbuka nilikurupuka kutoka usingizi ule mzito nikiwa nimelowa jasho mwili wote kutokana na joto la chumba kuwa kali, hivyo nilichukua kitabu change Agano jipya –kitabu cha neno la mungu na kuanza kusoma hadi ilipofika asubuhi.

Hakuna kitu kibaya kama moyo kupenda, moyo ukipenda unaweza kuwa kichaa tena unaweza kuitwa chizi wa mapenzi, au utasikia kachizika huyu, ndiyo ile mtu anaonekana kuwa na mapenzi ya fujo, wakati mapenzi ni matamu na yanatakiwa kuwa mapenzi ya kweli (Mapenzi ni maisha).

Niliendelea na shuguli zangu mapema asubihi ya siku hiyo, nakumbuka niliamka 11:30 alfajili, nikavaa vifaa vyangu vya michezo hadi uwanjani ambako ilinibidi nifanye mazoezi mengi ili kupoteza hisia za mawazo iliyokuwa inatawala ndani ya nafsi yangu, na bahati nzuri hali ya hewa ya siku hiyo ilikuwa ya mvua mvua ivyo nilifanya mazoezi  kwa muda mrefu tofauti na siku nilizofanya mazoezi najua.

“Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,
 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua” nilijaribu kuitafakari sana hiyo mistari ilikuwa ni baada ya kusoma neno la mungu usiku wa jana kwa hiyo ilikuwa imekaa kichwani, nikaanza kujiuliza Wana wa MUNGU ni kina nani na waliwaona Binti za Wanadamu ya kuwa ni wazuri wakajitwalia  wowote, je kumbe kuna wana wa mungu na binti za wanadamu, ndipo nilipogundua kwamba kumbe inawezekana wewe ukawa ni bint wa wanadamu, ama wewe ni mwana wa mungu? Lakini mbona mungu mwenyewe ameweka utaratibu huo kuwa  “wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana; hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye sifa.
Je ni sahihi kuwaza mambo  ya kale na ambayo ni mabaya katika kutengeneza jambo jema? “Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu siku zote. 

 Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo.
Bwana akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya. 

Wakati wa nuhu kila mnyama wa mwitu kwa jinsi yake, na kila mnyama wa kufugwa kwa jinsi yake, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi, kwa jinsi yake, na kirukacho kwa jinsi yake, kila ndege wa namna yo yote.
Waliingia katika safina alimo Nuhu, wawili wawili, wa kila chenye mwili kilicho na pumzi ya uhai ndani yake. Na walioingia, waliingia mume na mke, wa kila kitu chenye mwili, kama vile alivyomwamuru Mungu;
 
Usikose kufuatilia Adithi hii kila siku 0713869133/0767869133