TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, June 3, 2016

HEINEKEN HOSTS THE BIGGEST FOOTBALL PARTIES IN DAR TO #CHAMPIONTHEMATCH

NAIBU WAZIRI WA HABARI MGENI RASMI AZANIA BANK KIDS RUN 2016 YATAKAYOFANYIKA KESHO KUTWA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR E SALAAM

 
Dotto Mwaibale

NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mbio za Watoto za Azania Kids Run 2016, zitakazofanyika Jumapili Juni 5 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa Azania Kids Run 2016, zinazodhaminiwa na Benki ya Azania, Wilhelm Gidabuday, amesema kuwa Naibu Waziri Wambura atakuwa mgeni rasmi katika kinyang'anyiro hicho kitakachokuwa na mbio za kategori tano.

Gidabuday amebainisha kuwa, maandailizi yote ya Azania Kids Run 2016 yanaenda vema, ikiwamo idadi kubwa ya wazazi na walezi kujitokeza kusajili watoto wao, huku akiwataka wengi kutumia siku mbili zilizobaki kuhakikisha wanawapa vijana wao nafasi ya kushiriki.

"Mbio hizi zinazotarajia kushirikisha zaidi ya watoto 2,000, zinatarajia kufanyika Jumapili Juni 5, 2016 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, zikihusisha watoto chini ya miaka 16, ambako Naibu Waziri Wambura atakuwa mgeni rasmi," alisema Gidabuday.

Amewasisitiza wazazi, walezi na wadau kujitokeza kusajili watoto wao na kwamba fomu bado zinapatikana katika matawi yote ya Benki ya Azania, Ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) zilizoko Samora Avenue na Ofisi za Shirikisho la Riadha Tanzania (RT).

Gidabuday ametumia nafasi hiyo kuwahakikishia wazazi na walezi wa watoto watakaoshiriki Azania Kids Run 2016 kuwa, usalama wa watoto wao wakati wa shindano utakuwa kipaumbele chao na kuwatoa hofu ya usalama wakati wa kukimbia.

"Barabara zote zitakazotumiwa na watoto kukimbilia zitakuwa na uangalizi maalum ikiwa ni pamoja na gari za huduma ya kwanza na matibabu kwa watakaohitaji kupatiwa huduma hizo," amesema Gidabuday katika mkutano na wanahabari Dar es Salaam.

Ofisa Masoko Mwandamizi wa Azania Bank, Othman Jibrea, amezitaja zawadi za washindi mbalimbali wa mbio hizo, huku akiweka msisitizo kwa kutawaka wazazi kuendelea kusajili watoto wao kuwa sehemu ya tukio hilo la kihistoria.

"Mshindi wa kwanza mbio za Kilomita 5 ni Sh. 200,000, mshindi wa pili Sh. 150,000 na mshindi wa tatu sh. 100,000, pamoja na medali, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo, wakati mshindi wa nne hadi wa 10 watapata kifuta jasho cha sh. 15,000," amesema.

Katika mbio za kilomita 2, Jibrea alitaja zawadi kuwa ni sh. 100,000 kwa mshindi, huku atakayeshika nafasi ya pili akitarajiwa kulamba sh. 75,000 na wa tatu kujitwalia sh. 50,000, kategori ambayo pia washindi wa nne hadi wa 10 watapata kifuta jasho cha sh. 15,000.

Aidha, amebanisha kuwa, kategori ya mbio za kilomita moja mshindi atatwaa sh. 75,000, huku wa pili akibeba sh. 50,000 na wa tatu akijishindia sh. 40,000, ambako pia washindi wa nne hadi wa 10 watapata kifuta jasho kama kilivyotajwa hapo juu.

Pia kutakuwa na mbio za mita 50 na 100, ambazo zitakimbiwa na watoto chini ya miaka mitatu, ambako washindi washindi wote watafunguliwa akaunti katika Benki ya Azania, itakayokuwa na kianzio cha sh.15,000, sanjari na begi la shule lenye vifaa vyote muhimu.
Waratibu wa mbio hizo wakionesha fulana zitakazotumiwa na watoto watakao kimbia mbio hizo. Kutoka kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Peter Mwita, Mratibu wa Mbio hizo, Wilhelm Gidabuday, Ofisa Masoko Mwandamizi wa Bank ya Azania, Othman Jibrea na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Tullo Chambo.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Tullo Chambo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana wakati akimkaribisha Ofisa Masoko Mwandamizi wa Bank ya Azania, Othman Jibrea (katikati), kuzungumza na wanahabari kuhusu mbio hizo zitakazofanyika kesho kutwa. Kulia ni Mratibu wa Mbio hizo, Wilhelm Gidabuday.
Mwanafunzi Rachel Stephen wa Shule ya Sekondari ya Mburahati (kulia) na Mwenzake Ali Muhidin kutoka Shule ya Msingi Muungano wakizungumzia ushiriki wa mbio hizo.
Ofisa Masoko Mwandamizi wa Bank ya Azania, Othman Jibrea (katikati), akizungumzia kuhusu mbio hizo.
Mratibu wa Mbio hizo, Wilhelm Gidabuday (kulia), akizungumzia kukamilika kwa maandalizi ya mbio hizo.
Wanahabbari wakichukua taarifa hiyoMPALULEBLOGS:

KAMPUNI YA SAFARI INDOOR DIGITAL (SID) KUTOA ELIMU KUPITIA MABASI.






JK AKUTANA NA BALOZI WA ZAMANI WA MAREKANI CHARLES STITH LEO

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimkaribisha Ofisini kwake,  Balozi wa zamani wa Marekani hapa nchini Tanzania, Balozi Charles Stith, alipomtembelea kwa ajili ya mazungumzo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mjini Dar es Salaam, leo Juni 3, 2016.

UWEKAJI JIWE LA MSINGI UJENZI WA MAKTABA YA KISASA, CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM 02 JUNE, 2016.

LEO KATIKA BUNGE JUNI 3,2016.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson akiendesha kikao cha 36 cha mkutano wa 3 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
Baadhi ya Wabunge na Mawaziri wakifuatilia masuala mbalimbali ndani ya ukumbi wa Bunge wakati wa kikao cha 36 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo.
Wageni mbalimbali waliolitembelea Bunge wakifuatilia kikao cha 36 cha mkutano wa 3 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari St. Anne Marie ya Mbezi Beach jijini Dar es salaam wakifuatilia kikao cha 36 cha mkutano wa 3 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.

MADIWANI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA WAUPONGEZA MGODI WA BUZWAGI

Meneja Uendelevu wa Mgodi wa Buzwagi, George Mkanza akifafanua jambo kwa madiwani wa halmshauri ya mji wa Kahama wakati ziara ya kutembelea Mgodi huo. 
Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kahama Abel Shija(mwenye skafu) pamoja na waheshimiwa madiwani na wataalamu wa halmashauri hiyo wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa wataalamu wa Mgodi huo. 

diwani wa mwanga kusini mkoani Kigoma akishiriki shughuli za kijamii

ACT WAZALENDO WATANGAZA SIKU RASMI YA MAPOKEZI YA KIONGOZI WAO ZITTO NA WALE WA UKAWA

 

Katibu wa Itikadi mawasiliano na uenezi wa chama cha ACT WAZALENDO Ndugu ADO SHAIBU akizngumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam kuhusu mapokezi ya kumpokea kiongozi yao na mbunge pekee wa chama hicho ZITTO KABWE ambaye naye amekumbwa na timua timua ya bungeni,mapokezi ambayo yatafanyika Jijini Dar es salaam siku ya Jumapili

Na EXAUD MTEI 

Story ambayo bado ipo maskioni mwa watanzania walio wengi ni mwenendo wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania na mizengwe yake ambayo imesababisha wabunge saba wa vyama vya upinzani kusimamiswa kushiriki shughuli za bunge kwa vipindi Tofauti tofauti akiwemo mbunge kutoka ndani ya chama cha Act wazalendo Mh ZITTO ZUBERI KABWE na wabunge wa vyama vya UKAWA.

Sakata hilo limeendelea kuchukua Headline katika maeneo mbalimbali ambapo asubuhi hii chama cha ACT wazalendo kupitia kwa kiongozi wao ADO SHAIBU wamejitokeza mbele ya wanahabari kueleza msimamo wa chama chao kuhusu sakata hilo.

SHIWATA kumkabidhi Samatta eneo Jumapili


Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Cassim Taalib alisema jana jijini Dar es SAlaam kuwa maandalizi yamekamilika na Mbwana amewasili nchini kwa mechi ya timu ya TAifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Misri utakaochezwa Jumamosi.

Alisema sherehe hizo zitaambatana na ugawaji wa nyumba na misingi ya nyumba kwa wasanii 35 ambao wanafikisha ya wanachama 180 waliokwisha kabidhiwa nyumba zao.

Alisema SHIWATA imemzawadia Mbwana ekari tano ili ajenge kituo cha michezo kwa lengo la kuibua vipaji vya vijana wa Tanzania watakaolitangaza taifa hili kwenye medani ya michezo kimataifa.

Taalib alisema mtandao huo unaomiliki eneo la ekari 300 za kujenga makazi unawakaribisha wadau wa michezo kuwekeza kwa kujenga kumbi za burudani,shule za michezo, studio za kurekodia, viwanda vya kutengeneza vifaa vya michezo na hosteli za kufikia wachezaji.

Alisema sherehe za kugawa nyumba zinafanyika kwa mara ya tano kutoka ujenzi huo uanze katika kijiji hicho ambapo wanachama 185 wamekabidhiwa nyumba zao walizojengwewa kwa njia ya kuchangishana.

Alisema mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa HAbari, Utamaduni na Sanaa, NApe Mnauye ambaye atakuwa waziri wa pili kutembelea kijiji hicho baada ya NAibu WAziri wake, Anna Wambura kutembelea mapema mwaka huu.

SHIMUTA wataka wanamuziki wasio na maadili kupuuzwa









MAKAMU WA RAIS KUZINDUA JUKWAA LA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI,


Wazanzibari wahimizwa kupanda miti

SERIKALI YATOA UFAFANUZI KUHUSU TUHUMA ZILIZOTOLEWA NA MWANDISHI WA " THE ECONOMIST" GAZETI LA KIINGEREZA.






MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZUNGUMZA NA WATANZANIA WANAOISHI NCHINI PAPOA NEW GUINEA

Castle LITE sasa kupatikana kwenye ujazo wa mili lita 440




























=============================

WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM KUNUFAIKA NA MPANGO WA UPIMAJI WA ARDHI KWENYE MAENEO YASIYO RASMI.


Na: Veronica Mwakimi.
 
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini imezitaka halmashauri zote kuacha urasimu katika upatikanaji wa hati miliki ya makazi kwa watanzania waliopo kwenye maeneo mbali mbali  kwa kuwa inachangia kuzolotesha maendeleo ya Wananchi na makazi yanayowazunguka .

Akizungumza na Jambo leo  katika mahojiano maalum wa gazeti hili, Kaimu kamishina msaidizi wa Wizara ya Ardhi, bwana Idriss Kayera, amesema jijini dar es salaam leo kuwa wananchi wapewe elimu ya juu ya viambatanisho muhimu katika hatua ya upatikanaji wa hati hizo kwa watanzania ili kuweza kumiliki ardhi.

Bwana Kayera amesema kuwa Serikali kwa sasa inalenga kuongeza hati miliki ya ardhi kwa watanzania maeneo mbali mbali ya nchini kupitia  halmashauri zinazojishugulisha na maeneo ya upimaji wa maeneo ya makazi ili kuendana na kasi hiyo ya mabadiliko.

hata hivyo ameongeza kuwa, kwa sasa Serikali inao mpango wa kuongeza hati miliki hizo kwa ajili ya kuwaweka watanzania kuweza kujimilikisha  Ardhi tofauti na miaka ya nyuma ambapo watanzania wengi wameishi kwenye makazi yao bila kuwa na hati za umiliki wa ardhi hizo. 
  
Wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi

aidha ameyataja maeneo ambayo yametengwa bila utaratibu maalum kuwa ni pamoja na kimara ambayo unafanyika mpango wa kuweza kuyapima kama yalivyo huku pia akisema kuwa yapo maeneo yaliyojengwa pasipo utaratibu ikiwemo Buguruni, Tandika, Mburahati, Vingunguti ambako wakazi wake watapewa leseni ya makazi kutokana na msongamano walionao.

Mpaka sasa katika mwaka wa 2015/16 tayari wamepima hati miliki 23,000, ikiwa ni kwa maeneo ya mjini,  na kuongea kuwa umuhimu wa hati miliki ni kumuwezesha mwananchi kuweza kujiendeleza yeye pamoja na Maisha yake ikiwa ataweza kuyatumia  vyema makazi hayo pamoja na hati hiyo ambayo anaweza kuitumia kujiwekeza kwenye uchumi mkubwa tofauti na mkazi ambaye yupo kwenye makazi yasiyokuwa kwenye mipango miji.  

Wizara ya ardhi imefikia maamuzi hayo ikiwa ni pamoja na kuwabana Makandarasi feki wanaojenga majumba bila utaratibu au kutokuwa na kibali kutoka kwenye halmashauri husika za mikoa vitendo vinavyopelekea kuhatarisha maisha ya wakazi wa maeneo husika pale majengo yanapokosa sifa na vigezo vya uimara wa ujenzi huo feki, ambapo pia imewataka kuacha mara moja kujichukulia hatua kiholela katika kujihusisha na ujenzi na badala yake wametakiwa kufuata utaratibu husika kutoka kwenye halmashauri hizo.

Mwisho.

AZANIA BENKI YAKABIDHI VIFAA KWA AJILI YA AZANIA KIDS RUN 2016.

 
 Afisa Masoko wa ya Azania, Othman Jibrea (kushoto) ambao ni wadhamini wa michezo hiyo, wakizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo. kulia ni Mratibu Azania BAnki Kids Run 2016, Bw. Wilhelm Sidabuday.kulia Mjumbewa kamati ya Utendaji ya shirikisho la Riadha Tanzania RT, Tulo Chambo
  
   
 Afisa Masoko wa ya Azania, Othman Jibrea (kushoto) ambao ni wadhamini wa michezo hiyo, wakizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo. kulia ni Mratibu Azania BAnki Kids Run 2016, Bw. Wilhelm Sidabuday.
 Afisa Masoko wa ya Azania, Othman Jibrea (kushoto) ambao ni wadhamini wa michezo hiyo, akionyesha moja ya Vifaa vilivyokabidhiwa leo, kulia ni Mratibu Azania BAnki Kids Run 2016, Bw. Wilhelm Sidabuday.
 
Baadhi ya Washiriki wa michezo hiyo,Recho Stivini Mwanafunzi wa Mburahati Sekondari mwenye umri wa miaka 15, Ally Muidini ,Muungano Shule ya Msingi mwenye umri wa 16,wakifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa BMT jijini Dar es Salaam leo.(Picha KWa Hissani ya Miss Demokrasia Tanzania).
==============================

Na: Shaaban mpalule

NAIBU waziri wa habari, utamaduni, sanaa na wasanii Anastazia Wanbura anatarajiwa kuwa mgeni rasmi michuano ya riadha ya Azania Kids Run 2016 zitakazofanyika  Juni 5 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mmoja wa waratibu wa mbio hizo, Wilhelm Gidabuday, alisema kufikia jana mchana, mchakato wa usajili ulikuwa ukiendelea vema, ambako wazazi na walezi wamejitokeza kusajili watoto wao.

Gidabuday alisema kuwa, matarajio ni kusajili watoto wapatao 2,000 walio na umri chini ya miaka 16, ambao watashiriki Azania Bank Kids Run 2016, mbio zilizogawanywa katika kategori tano za kilomoita 5, km 2, km 1, mita 100 na mita 50.

Alibainisha kuwa, fomu za ushiriki zinapatikana katika Matawi ya Azania Bank popote jijini Dar es Salaam, pamoja na Ofisi za Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), pamoja na Ofisi za BMT zilizoko Samora Avenue katikati ya jiji.

Aliwataka wazazi na walezi ambao hawajachukua fomu za ushiriki wa watoto wao, kuchangamkia mchakato huo kwa kufika katika vituo husika na kununua fomu hizo kwa shilingi 2,000 tu, ili kuwawezesha watoto kushiriki na kushinda zawadi.

Naye, Ofisa Masoko Mwandamizi wa Azania Bank inayodhamini mashindano hayo, Othman Jibrea, alisisitiza umuhimu wa wazazi na walezi kusajili watoto wao katika Azania Bank Kids Run, ili kufikia lengo lao la kuibua vipaji vipya vya riadha.
Jibrea alibainsiha kuwa, Azania Bank imejitosa kudhamini mbio hizo kutokana na mlengo wake wa kuibua vipaji vichanga katika riadha, hivyo ili kufikia lengo, wazazui na walezi hawana budi kujitokeza kwa wingi kusajili watoto wao.

Alizitaja zawadi za mbio za Kilomita tano kuwa ni Sh. 200,000 kwa mshindi wa kwanza, Sh. 150,000 kwa mshindi wa pili na Sh. 100,000 kwa mshindi wa tatu, wote wakitarajiwa pia kupata medali, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo (track suit).
Jibrea alibainisha kuwa, mshindi wa kwanza wa mbio za kilomita 2 atajinyakulia Sh. 100,000, mshindi wa pili Sh. 75,000 na mshindi wa tatu Sh. 50,000, pamoja na medali, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo.

Katika mbio za kilomita 1, Jibrea alitaja zawadi za washindi kuwa ni Sh. 75,000 kwa mshindi wa kwanza, 50,000 kwa mshindi wa pili na Sh. 40,000 kwa wa tatu, ambao watapata zawadi ya ziada ya medali, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo.
"Pia, washindi wa nne hadi wa 10 wa mbio hizo, watapata kifuta jasho cha Sh. 15,000, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo. Nia ni kuwafanya watoto watakaoshiriki kutotoka bure mwishoni mwa mashindano," alisema Jibrea.

CHAMA CHA KUTETEA ABIRIA TANZANIA (CHAKUA) KWA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA SAFARI INDOOR DIGITAL (SID) WAZINDUA MPANGO MPYA WA KUTOA ELIMU KWA ABIRIA KUPITIA TELEVISHENI ZILIZOPO KATIKA MABASI YAENDAYO MIKOANI NA MASAFA MAREFU.

Mwenyekiti wa Chama cha Kutetea Abiria TAnzania(CHAKUA), kulia akifafanua jambo kuhusiana na Ushirikiano na KAmpuni ya Safari Indoor Digital (SID) wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa kutoa Elimu kwa Abiria kupitia Televisheni (Screen) Zilizopo katika Mabasi Yaendayo Mikoani na MAsafa Marefu.Wengine kutoka kulia ni Innocent Malethowa kutoka Safari Indoor,(pili kulia),Mkurugenzi wa Utawala wa kampuni ya Usafiri ya Safari Indoor, Doreen Chamberlain wa pili kutoka kushoto na Lulu Masawe kutoka Kilimanjaro Express, hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Idara Habari Maelezo jijini Dar es Salaam leo. (PIcha Kwa Hisani ya Miss Demokrasia Tanzania).

Na: Shaaban Mpalule- Maelezo.

Chama cha Kutetea Abiria Tanzania (CHAKUA), kwa kushirikiana na Kampuni ya Safari Indoor Digital (SID) na Kampuni ya Mabasi ya Kilimanjaro ExPress , imezindua mpango wa mpya na wa Kisasa katika kutoa Elimu kwa abiria kupitia Televishen zilizopo katika mabasi yaendayo Mikoani na Masafa Marefu na nje ya nchi.

 Akizungumza kwenye Ukumbi wa Idara habari Maelezo leo, Mkurugenzi wa Utawala wa kampuni ya Usafiri ya Safari Indoor, Doreen Chamberlain, amesema kuwa mpango huo utawawezesha abiria kupata na kujifunza masuala mbali mbali.
aidha Safari Indoor Digital wakiwa kama wadau wakubwa wa usafiri kwa kushirikiana na jeshla polisi, SUMATRA wametengeneza kipindi maalum ambacho ambacho kitaandaliwa na kampuni ya SAFARI INDOOR DIGITAL (SID).

kutokana na hali hiyo CHAKUA inawataka abiria wote kuitumia fulsa hiyo vizuri kusogezewa huduma ya elimu ili kujitetea au kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika ikiwemo polisi , Sumatra na chakua pindi wanapofanyiwa manyanyaso katika vyombo vya usafiri kwani wakati elimu ikitolewa katika Screen kutatolewa pia na namba za simu kwa ajili ya malalamiko.
 

SERIKALI KULICHUKULIA HATUA ZA KISHERIA GAZETI LA ECCONOMICS LA UINGEREZA KWA UPOTOSHAJI WA TAARIFA DHIDI YA SERIKALI YA UTAWALA WA AWAMU YA TANO.

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kimetoa Ufafanuzi kuhusu Taarifa iliyotolewa na Gazeti la kiingereza ikihusisha juu ya Utendaji wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa John Pombe Magufuli.kwamba Wawekezaji wa nje wameendelea kusuasua ya kuingia Madarakani ukilinganisha na Utawala wa Awamu ya nne.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo Zamaradi Kawawa, amewataka Wanahabari kutumia Kalamu zao na vyombo vya habari kuandika habari zilizo sahihi ili kuepusha upotoshwaji wa taarifa mbali mbali kwa wananchi, "ndugu zangu na wenzangu wandishi wa habari, kumekuwepo na wimbi kumbwa la vyombo na wanahabari kuandika habari za upotoshaji, kwa kweli kitendo hiki siyo kizuri na inavyoonekana ivi sasa kuna vyombo ama kama siyo watu binafsi wenye nia mbaya ya kuitakia mabaya tanzania, kama ambavyo mwandishi wa habari la Economics la nchini Uingereza alivyofanya katika taarifa yake ya kwamba Tanzania ivi sasa inayumba kwenye suala la Uwekezaji kwa wawekezaji" amesema Zamaradi. 

 Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara Habari Maelezo jijini DAr es salaam leo Daudi Riganda amesema kuwa ni taarifa za uzushi zinazoenezwa na baadhi ya vyombo vya nje kuhusiana na kuitakia mabaya Tanzania na kwamba si kweli kuwa Wawekezaji wengi wamesitisha kuingia nchini kuwekeza.

aidha amewahakikishia watanzania kuwa takwimu zilizopo zinaonyesha kwamba Tanzania mpaka sasa bado inaendelea kuwa na mahusiano mazuri na wawekezaji wengi na wanaendelea kuwapokea wawekezaji bila Ubaguzi wa aina yoyote.

Na kwamba Tanzania aina vikwazo vyovyote ilivyoviweka kwa wawekezaji kuja kuwekeza kutokana na kwamba tanzania ni nchi yenye Amani na kuhusiana na taarifa hiyo tayari Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza umetaarifiwa ili kufuatilia gazeti hilo amabapo taratibu za kisheria zinaendelea kupitia Mwanasheria wa Serikali ili kuwachulia hatua Stahiki wahusika wa Taarifa hizo za Upotoshaji dhidi ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo Zamaradi Kawawa(kushoto),Meneja Uhusiano kituo cha Uwekezaji TAnzania (T.I.C) Daudi Riganda, akifafanua Taarifa ya Upotoshaji iliyoandikwa na Gazeti la Econonic na Mwanahalisi.katika Idara habari maelezo jijini Dar es Salaam leo( Picha na Raymond Urio).

  

John kitime atambulishwa kuwa katibu mkuu wa shirikisho la muziki tanzania



 
raisi wa shirikisho la muziki tanzania ado novemba (watatu kulia) akiongea na waandishi wa habari jijini dar es salaam leo wakati wakumtambulisha katibu mkuu wa shirikisho hilo john kitime (wanne kulia)Mkutano huo umefanyika kwenye Ukumbi wa Idara Habari maelezo jijini Dar es Salaam Leo.(Picha kwa Hissani ya Miss Demokrasia Tanzania).

Thursday, June 2, 2016

WAZIRI WA MALIASILI PROF. JUMANNE MAGHEMBE AIOMBA JUMUIYA YA KIMATAIFA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KWA VITENDO KATIKA VITA DHIDI YA UJANGILI