TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, June 3, 2016

AZANIA BENKI YAKABIDHI VIFAA KWA AJILI YA AZANIA KIDS RUN 2016.

 
 Afisa Masoko wa ya Azania, Othman Jibrea (kushoto) ambao ni wadhamini wa michezo hiyo, wakizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo. kulia ni Mratibu Azania BAnki Kids Run 2016, Bw. Wilhelm Sidabuday.kulia Mjumbewa kamati ya Utendaji ya shirikisho la Riadha Tanzania RT, Tulo Chambo
  
   
 Afisa Masoko wa ya Azania, Othman Jibrea (kushoto) ambao ni wadhamini wa michezo hiyo, wakizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo. kulia ni Mratibu Azania BAnki Kids Run 2016, Bw. Wilhelm Sidabuday.
 Afisa Masoko wa ya Azania, Othman Jibrea (kushoto) ambao ni wadhamini wa michezo hiyo, akionyesha moja ya Vifaa vilivyokabidhiwa leo, kulia ni Mratibu Azania BAnki Kids Run 2016, Bw. Wilhelm Sidabuday.
 
Baadhi ya Washiriki wa michezo hiyo,Recho Stivini Mwanafunzi wa Mburahati Sekondari mwenye umri wa miaka 15, Ally Muidini ,Muungano Shule ya Msingi mwenye umri wa 16,wakifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa BMT jijini Dar es Salaam leo.(Picha KWa Hissani ya Miss Demokrasia Tanzania).
==============================

Na: Shaaban mpalule

NAIBU waziri wa habari, utamaduni, sanaa na wasanii Anastazia Wanbura anatarajiwa kuwa mgeni rasmi michuano ya riadha ya Azania Kids Run 2016 zitakazofanyika  Juni 5 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mmoja wa waratibu wa mbio hizo, Wilhelm Gidabuday, alisema kufikia jana mchana, mchakato wa usajili ulikuwa ukiendelea vema, ambako wazazi na walezi wamejitokeza kusajili watoto wao.

Gidabuday alisema kuwa, matarajio ni kusajili watoto wapatao 2,000 walio na umri chini ya miaka 16, ambao watashiriki Azania Bank Kids Run 2016, mbio zilizogawanywa katika kategori tano za kilomoita 5, km 2, km 1, mita 100 na mita 50.

Alibainisha kuwa, fomu za ushiriki zinapatikana katika Matawi ya Azania Bank popote jijini Dar es Salaam, pamoja na Ofisi za Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), pamoja na Ofisi za BMT zilizoko Samora Avenue katikati ya jiji.

Aliwataka wazazi na walezi ambao hawajachukua fomu za ushiriki wa watoto wao, kuchangamkia mchakato huo kwa kufika katika vituo husika na kununua fomu hizo kwa shilingi 2,000 tu, ili kuwawezesha watoto kushiriki na kushinda zawadi.

Naye, Ofisa Masoko Mwandamizi wa Azania Bank inayodhamini mashindano hayo, Othman Jibrea, alisisitiza umuhimu wa wazazi na walezi kusajili watoto wao katika Azania Bank Kids Run, ili kufikia lengo lao la kuibua vipaji vipya vya riadha.
Jibrea alibainsiha kuwa, Azania Bank imejitosa kudhamini mbio hizo kutokana na mlengo wake wa kuibua vipaji vichanga katika riadha, hivyo ili kufikia lengo, wazazui na walezi hawana budi kujitokeza kwa wingi kusajili watoto wao.

Alizitaja zawadi za mbio za Kilomita tano kuwa ni Sh. 200,000 kwa mshindi wa kwanza, Sh. 150,000 kwa mshindi wa pili na Sh. 100,000 kwa mshindi wa tatu, wote wakitarajiwa pia kupata medali, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo (track suit).
Jibrea alibainisha kuwa, mshindi wa kwanza wa mbio za kilomita 2 atajinyakulia Sh. 100,000, mshindi wa pili Sh. 75,000 na mshindi wa tatu Sh. 50,000, pamoja na medali, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo.

Katika mbio za kilomita 1, Jibrea alitaja zawadi za washindi kuwa ni Sh. 75,000 kwa mshindi wa kwanza, 50,000 kwa mshindi wa pili na Sh. 40,000 kwa wa tatu, ambao watapata zawadi ya ziada ya medali, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo.
"Pia, washindi wa nne hadi wa 10 wa mbio hizo, watapata kifuta jasho cha Sh. 15,000, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo. Nia ni kuwafanya watoto watakaoshiriki kutotoka bure mwishoni mwa mashindano," alisema Jibrea.

No comments:

Post a Comment