TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, June 2, 2016

MAKAMU WA RAIS AHIMIZA VIONGOZI WA NCHI ZA ACP KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI


  Na Mwandishi Maalum
Port Moresby - Papua New Guinea
2 June 2016,
 
Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameanzisha majadiliano kuhusu umuhimu wa kumwezesha mwanamke kiuchumi kwa viongozi wa nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (ACP) wakati wa Mkutano wa Nane wa Wakuu wa Nchi hizo uliofanyika Port Moresby, nchini Papua New Guinea.
 
Katika mkutano huo wa siku mbili uliomalizika jana nchini humo, Makamu wa Rais alikuwa mtoa mada mkuu katika majadiliano ya kumwezesha mwanamke kiuchumi  ambayo yalifanyika sambamba na Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali.
 
Makamu wa Rais ni miongoni mwa wajumbe wa Jopo la Ngazi ya Juu la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon ambalo liliundwa kusaidia kufanya uchambuzi na kutoa mapendekezo ya namna ya kuchagiza kasi ya kuwezesha wanawake kiuchumi kupitia Ajenda ya mwaka 2030 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu. Jopo hilo linakusanya maoni, uzoefu na miongozo kutoka kwa wadau duniani kote kupitia majadiliano.
Mheshimiwa Samia aliuambia mkutano huo kuwa  uwezo mkubwa walionao wanawake kama wazalishaji wakuu bado haujatumika kikamilifu kwa miongo yote katika kuchangia maendeleo ya kiuchumi katika nchi zao licha ya kwamba wao ni takribani nusu ya nguvu kazi ya dunia na kama wakiwezeshwa mchango wao unaweza kufikia zaidi ya trilion 20 ya pato la dunia.
 
Alisema kuna umuhimu wa serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo kuhakikisha kuwa wanawekeza katika kuwezesha wanawake kiuchumi ili kufanikisha Ajenda 2030 jambo ambalo litapelekea kupatikana kwa usawa wa kijinsia, kuondokana na umaskini na hatimaye uchumi kukua.
 
"Pamoja na maendeleo yaliyofikiwa, bado uwiano wa kijinsia umebaki kuwa mkubwa kwa wanawake katika sehemu zote za fursa za kiuchumi na matokeo, katika nchi zote wanachama," alisema Mheshimiwa Samia.
 
Makamu wa Rais alielezea matumaini yake kwamba uchumi imara ambao unaonekana katika nchi za ACP katika miaka ya hivi karibuni utaendelea kukua na kusisitiza umuhimu wa kuondoa tofauti za kiuchumi baina ya wanawake na wanaume ili kujenga uchumi ulio imara.
 
“Mara nyingi juhudi zimefanyika za kuleta usawa wa wanawake, kwa mwanamke mmoja mmoja,  katika familia, na kama mwananchi, dunia yetu imeendelea, na wote tumepata ustawi," alisema na kuongeza
 
"Kwa hiyo, tuwe na uhakika wa elimu bora, ajira za uhakika, upatikanaji wa huduma bora za afya na maisha huru bila ukatili na ubaguzi viwe vinawafikia kwa urahisi wanawake na wasichana ili kuleta usawa miongoni mwa jamii. Hivi vigezo vina muunganiko wa moja kwa moja na fursa za kiuchumi, uwezo wa mlaji wa kufanya manunuzi na hatimaye kukua kwa uchumi."  
 

Matokeo ya majadiliano ya katika mkutano huo yatasaidia kushawishi kazi ya Jopo hilo na kuhakikisha mtazamo wa kikanda unaingizwa katika ripoti ya kwanza itakayowasilishwa na jopo hilo kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwezi Septemba 2016

No comments:

Post a Comment