TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, October 25, 2015

TUMEPIGA KURA, NA SASA TUPOKEE MATOKEO KWA AMANI NA UTULIVU, KUNA MAISHA BAADA YA UCHAGUZI.


JUMAPILI ya Oktoba 25, 2015, Tanzania imefanya Uchaguzi Mkuu wa madiwani, wabunge pamoja na kumpata Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Uchaguzi ni nini? Zipo tafsiri mbalimbali lakini mojawapo na iliyo wazi ni kwamba, Uchaguzi  ni njia ya kidemokrasia inayotumiwa na watu katika kuchagua viongozi wa kuwaongoza kwa kipindi fulani kwa mujibu wa Katiba au utaratibu waliojiwekea wenyewe.
Huu ni Uchaguzi Mkuu wa Tano kufanyika tangu mfumo wa vyama vingi ulipoanza tena mwaka 1992, lakini ni wa 11 tangu Tanganyika na Zanzibar zilipoungana mwaka 1964.
Uchaguzi wa mwaka huu ulikuwa na umuhimu wa kipekee kwa sababu kadha wa kadha, mojawapo ikiwa umri wa miaka 23 tangu mfumo wa vyama vingi ulipoanza.


Huu ni umri mkubwa, na kwa hakika vijana wengi waliojitokeza kujiandikisha safari hii ni wenye umri wa kati ya miaka 18-35, ikimaanisha kwamba wengi wao walizaliwa kuanzia mwaka 1992. Hawa wanatengeneza asilimia 57 ya wapigakura wote.


Umuhimu mwingine ni kwamba, kulinganisha na uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995, safari hii demokrasia imekua na kupanuka kiasi cha kushuhudia wapigakura 22.75 milioni, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini tangu tupate Uhuru.
Kwa upande mwingine, hamasa imeongezeka, upinzani umeimarika zaidi na uhuru wa habari umepanuka ukiwamo ukuaji wa sekta ya habari na mawasiliano, hususan mitandao ya kijamii.

Haya yote yanatokea kutokana na kuwapo kwa amani na utulivu, sifa ambazo zimeendelea kuitambulisha vyema Tanzania hata katika jumuiya za kimataifa.
Uchaguzi Mkuu ni gharama kubwa kifedha, rasilimali watu na muda, na kama mambo yatakwenda mrama maana yake nchi itakuwa imeingia hasara kwa kupoteza fedha, lakini pia itaingia kwenye machafuko ambayo yatatowesha amani iliyodumu kwa miaka mingi.
Madhara ya machafuko au vita – kama tulivyoshuhudia kwa majirani zetu Rwanda na Kenya ni vifo, ulemavu wa kudumu, kutengana na familia, ukimbizi na kuvurugika kwa uchumi, jamii na siasa kwa ujumla. Kwa miaka yote tangu Uhuru, licha ya uchanga na umaskini kama taifa, Watanzania hatujazoea maisha ya vurugu na machafuko na ndiyo maana tuna wajibu wa kuhakikisha uchaguzi huu unapita salama. 

Wajibu wa kulinda amani ya nchi yetu ni wa kila Mtanzania bila kujali rangi, dini, kabila ama nafasi yake katika jamii. Tunaposema hivyo tunamaanisha kwamba, vyombo vya dola vinapaswa kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria na kuhakikisha Watanzania wanapiga kura kwa amani kuchagua viongozi wao kwa utaratibu waliojiwekea.
Balozi wa Demokrasia Tanzania's photo.
Kimsingi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ndio wasimamizi wa chaguzi zote, hivyo wana dhamana kubwa kuhakikisha kila aliyejiandikisha na kujitokeza siku hiyo anatumia haki yake ya kikatiba kupiga kura bila kubughudhiwa.

Ili kuondoa utata huo, NEC pia inapaswa kuhakikisha kunakuwa na uwazi kuanzia hatua ya kupiga kura mpaka wakati wa kutangaza matokeo, ambayo pia yanatakiwa kutolewa kwa wakati ili kuondoa mashaka miongoni mwa wagombea na wananchi kwa ujumla.
Wanasiasa, hususan wagombea ama wapambe wao, wanapaswa kutoa kauli za kuhamasisha amani na utulivu kwa siku hizi chache zilizosalia kuelekea uchaguzi mkuu, siku ya uchaguzi na baada ya kutangazwa kwa matokeo.


Bomu ya kiatomiki ilipolipuka mjini Nagasaki
Huku ulimwengu ukiadhimisha miaka 70 tangu ndege za kijeshi za Marekani ilipodondosha bomu la kinyuklia juu ya Nagasaki tazama picha za janga hilo.