TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, December 29, 2012

NEW MPANDA AIRPORT TO PROMOTE TOURISM IN WESTERN

 
Katavi national park is ready for sustainable mass tourism, thanks to the paving and lengthening of the runway and the refurbishing of the Mpanda airport terminal building, only 40km from the Park. The runway can accommodate modern and large airplanes such as ATR72.

Tanzania haiwezi kukwepa maendeleo ya bioteknolojia ya utandawazi duniani

 
Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava akifungua Warsha kwa maafisa wa mipakani kuhusu usimamizi wa mazao na bidhaa zitokanazo na Bioteknolojia ya kisasa. Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Julius Ningu na kushoto ni Afisa Mazingira Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Esta Makwaia. Warsha hii imefanyika leo kwenye Hotel ya La kairo jijini Mwanza
 
Washiriki wa Warsha ya Usimamizi wa mazao na bidhaa zitokanazo na bioteknolojia ya kisasa wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi (katikati) Mara baada ya kufungua warsha hiyo kwenye Hoteli ya La kairo Jiji Mwanza
 …………………………………………….
Lulu Mussa na Ali Meja
Mwanza
 Imeelezwa kuwa Tanzania kama nchi nyingine haiwezi kukwepa maendeleo ya bioteknolojia kutokana na utandawazi na maendeleo duniani kote, kwa kuwa bioteknolojia ya kisasa ni nyenzo muhimu katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini, kuboresha kilimo, uzalishaji viwandani, afya na hifadhi ya mazingira.
 Hayo yamesemwa leo na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Ngosi Mwihava katika warsha ya siku moja kwa maafisa wa mipakani kutoka mikoa ya kanda ya ziwa, warsha iliyolenga kukuza uelewa kwa watendaji wanaosimamia mazao na bidhaa zitokanazo na bioteknolojia ya kisasa.
 Amesema, Serikali kwa kutambua mchango mkubwa unaoweza kupatikana kutokana na matumizi ya bioteknolojia ya kisasa katika sekta za afya, kilimo, viwanda na mazingira, imeridhia Itifaki ya Cartagena ya Mkataba wa Bioanuai mwaka 2003 kwa lengo la kuhifadhi mazingira kwa kuzingatia usalama katika usafirishaji,  kuunda na kupitisha mfumo wa kitaifa wa usimamizi wa matumizi salama ya Bioteknolojia mwaka 2007.
 Eng. Mwihava amewaasa watendaji katika maeneo ya mipakani kuwa na usimamizi madhubuti katika maeneo yao ya kazi kwa kuwa mipaka kati ya Tanzania na nchi nyingine ndiyo njia kuu za uingizaji wa mazao na bidhaa zitokazo nje.
 Pamoja na faida za bioteknolojia hiyo ya kisasa Eng. Mwihava amewataka watendaji hao kuwa makini na athari zinazoweza kutokana na matumizi ya teknolojia hiyo pale itakapotumiwa bila kufuata taratibu za usalama zilizowekwa.
 Warsha hii ya siku moja kwa imewashirikisha maafisa forodha, Maafisa Afya na watafiti wa Mazao kutoka Mikoa ya Mwanza, Mara na Kagera, kutoka Idara , wakala za Serikali na sekta binafsi.

KUTANO WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO TASWA WAFANYIKA BAGAMOYO LEO

Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwan Kikwete  akifungua mkutano mkuu wa chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA unaofanyika kwenye Hoteli ya Kiromo View Bagamoyo mkoani Pwani ambao unajadili mambo mbalimbali ya Maendeleo na changamoto zinazokabili chama hicho.
Waanishi wa habari za michezo ambao ni wanachama kutoka vyombo mbalimbali nchini wanahudhuria mkutano huo ambao ni wa siku moja.
Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA Bw. Juma Pinto akimkaribisha mgeni rasmi ili kufungua mkutano huo leo asubuhi unaofanyika kwenye  hoteli ya Kiromo View Bagamoyo.
 
Katibu wa Chama cha Waandishi wa habari za michezo TASWA Bw. Amir Mhando akizungumza katika mkutano huo, kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa TASWA Maulid Kitenge, Mwenyekiti Juma Pinto, Mgeni rasmi Ridhiwan Kikwete na kushoto ni George John Katibu Msaidizi.
 
Mtaalam wa SACCOS kutoka Manispaa ya Ilala Bw. Luambano akitoa mada kuweka na kukopa kwa waandishi wa habari wanachama wa TASWA waliohudhuria katika  mkutano huo
 
Kutoka kulia ni waandishi wakongwe Mwina Kaduguda, Mzee Wlly Chiwango na Mzee Salim Said Salim kutoka Zanzibar wakiwa katika mkutano huo.
 
Kutoka kulia ni Shafii Dauda, Erasto na Ibrahim Masoud wakiwa katika mkutano huo.
 
Kutoka kulia ni Elizaberth Mayemba , Timzo Kalugira na Crala Alphonce wakifuatilia mada katika mkutano huo.
 
Kutoka kushoto ni Elius Kambili, Alfred Lucas na Salum Jaba wajumbe wa kamati ya utendaji ya TASWA wakiwa katika mkutano huo.
 
Kutoka kulia ni Mgaya Kingoba, Salum Jaba, Richard Mwaikenda na Tulo Chambo wakifuatilia mada katika mkutano huo.
 
Wajumbe mbalimbali wakihudhuria mkutano wa Chama cha Waandishi wa habari za michezo TASWA kwenye hoteli ya Kiromo View mjini nje kidogo ya mji wa Bagamoyo mkoani Pwani .

Flightlink yawaandalia chakula cha jioni wafanyakazi wake na familia zao katika kuuaga mwaka

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege ya Flightlink,Munawer Dhiren akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha usiku kilichokuwa kimeandaliwa maalum kwa ajili ya kukutana kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo pamoja na familia zao ikiwa ni sehemu pia ya kuuaga mwaka iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege ya Flightlink,Munawer Dhiren akiendelea kuzungumza.
 Sehemu ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Ndege ya Flightlink pamoja na familia zao wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo,Munawer Dhiren (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza nao wakati wa hafla ya chakula cha usiki iliyokuwa imeandaliwa maalum kwa ajili ya kukutana kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo pamoja na familia zao ikiwa ni sehemu pia ya kuuaga mwaka iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana. 
 Mazungumzo ya hapa na pale kwa wadau wa Kampuni ya Flightlink yakiendelea wakati wa hafla hiyo.
 Wakati wa Chakula uliwadia na kila mmoja alipita kuchukua chakula akipendacho.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Flightlink wakipozi kwa picha wakati wa hafla ya chakula cha usiki iliyokuwa imeandaliwa maalum kwa ajili ya kukutana kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo pamoja na familia zao ikiwa ni sehemu pia ya kuuaga mwaka iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.
 Picha ya pamoja kwa wafanyakazi wote wa Kampuni ya Ndege ya Flightlink.
Wakurugenzi wa Kampuni ya Flightlink wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa.(Picha zote na Othman Michuzi).

Unique Model 2012 Mrembo wa Apatikana

Mwanamitindo bora wa mwaka 2012
Catherine Masumbiga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Unique
Model Photogenic Elizabeth Pertty (kushoto) na Unique Model Talent
Vestina Charles mara baada ya kutangazwa kwa mshindi.
Mwanamitindo
wa mwaka 2012 Catherine Masumbiga (katikati) amepatikana jana usiku
kwenye shindano lililofanyika kwenye Klabu ya New Maisha
jijini Dar es Salaam akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa pili
Cesilia Michael (kushoto) na mshindi watatu Amina Ayubu.
Washiriki waliongia tano bora.
Washiriki waliongia tano bora.
Majaji wa shindano hilo kutoka kushoto ni Gymkhana Hilal kutoka Paka Wear , Asia Idarous na Martine Kadinda.
Unique Model Talent of the year 2012 Vestina Charles akionyesha uwezowake wa kucheza jukwaani.
Wakitumbuiza mashabiki mapema kabla ya kuingia kuonyesha mavazi ya aina mbalimbali.
Washiriki 12 wa shindano hilo wakiwa wamejipanga tayari kusubiri kutangazwa mshindi.

ARUSHA KUWA MAKAO MAKUU YA CHAMA CHA NGUMI ZA KULIPWA AFRIKA YA MASHARIKI NA KATI (ECAPBA).

 Chama cha Ngumi za Kulipwa Cha Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA) kimepata nyumbani baada ya Mstahiki Meya wa jiji la Arusha  Mh. Gaudence Lyimo kuomba kihamie Arusha ili kiweze kukaa karibu na “Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, EAC”Rais wa ECAPBA Onesmo Ngowi alimhakikishia mstahiki meya kuwa ECAPBA itahamishia makao yake makuu katika jiji la Arusha. Kwa sasa ECAPBA ina makao yake makuu katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.
 Juhudi za Mstahiki Meya Gaudence Lyimo za kukuza michezo na kukuza utalii katika jiji la Arusha ni moja ya sababu zilizomfanya rais wa ECAPBA kuamua kuhamishia makao makuu katika jiji la Arusha.
 Uamuzi huo uliungwa mkono na mmoja wa wanachama wa  ECAPBA bw. Daudi Chikwanje ambaye ndiye Katibu Mkuu wa Chama Cha Ngumi za Kulipwa Cha Malawi!
 Nchi ya Malawi ni mwanachama wa ECAPBA pamoja na Kenya, Zambia, Ethiopia, Burundi, Sudan ya Kusini, DRC, Rwanda, Uganda na Sudan.
 ECAPBA inaratibu ubingwa unaojulikana kama ECAPBF ambao unawapa mabondia wa ukanda huu kuwa mabingwa imara wa ngumi Afrika.

Friday, December 28, 2012

MATUKIO KATIKA PICHA

 Kutokana na Hali ya Maisha Kuwa Ngumu, wakazi wa Manspaa ya  mji wa Moshi wakiwa katika harakati na Biashara ya kuuza Matunda, katika kipindi hiki kuelekea Mwisho wa Mwaka (1)
Soko la Bidhaa za watu wenye imani ya Rasta inazidi kushamili huku bidhaa hizo pia zikizidi kuwekewa ubunifu kama inavyoonekana , Mkazi wa Manspaa ya Mji wa Moshi akiingia kupata moja ya Bidhaa hizo (1)

Matukio Mbali Mbali katika Picha

 Mabango ya barabarani yanaendelea kuujaza mji wa Moshi kitendo ambacho kinakuwa kero, baada ya kujazana  kila kona (2)
 Mafundi wajenzi wa Manspaa ya mji wa Moshi wakiendelea za Ukarabati wa Mitalo katika Kipindi hiki cha Mwisho wa Mwaka (1)
 Mjasilia Mali akiendelea na Pilika pilika wakati wa kutafuta chochote kitu
 Mjasilia Mali(Mama Ntilie wa Migamoni Mama Lishe)wakiwajibika kuandaa chakula kwa ajili ya wateja wao (6)
Pamoja na kuwa na sifa ya Usafi Mji wa Moshi, Lakini Bado ustaarabu kwa watu wengine si kurizisha, hapa wakiendelea na usafi Watu wa Halmashari (Picha Mchimati@faceboo.com)