Shirilisho
 la Ngumi la Kimataifa (IBF) limepongeza bingwa mpya wa uzito wa Super 
Middle katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki yaa Kati, 
Mtanzania Francis Cheka.
 Katika barua yake aliyomtumia 
Francis Cheka ya tarehe 28/12/2012 Mwenyekiti wa kamati ya Ubingwa wa 
IBF/USBA Lindsey Tucker alisema “Tunachukua fursa hii kukutakia maisha 
na mafanikio mazuri kama bingwa wa IBF na kumhimiza kuishi kama bingwa”.
 Cheka atatakiwa kutetea taji lake katika kipindi cha miezi sita kufikia
 mwezi wa 6 mwakani dhidi ya mpinzani ambaye ana rekodi ya mapambano 
yasiyopungua 15 na mengi awe ameyashinda hususan mapambano mawili ya 
mwisho.
Aidha
 IBF inampongeza bondia Chiotcha Chimwemwe kutoka Malawi kwa ushupavu 
wake na ushindani mzuri katika pambano hilo lililofanyika katika uwanja 
wa Sheikh Amri Abeid katika jiji la Arusha tarehe 26 Desemba, 2012.
CHIOTCHA AONJA MACHUNGU YA CHEKA
 Bondia
 kutoka Jamhuri ya watu wa Malawi Chiotcha Chimwemwe alionja machungu ya
 Mtanzania Francis Cheka katika mpambano wao uliopewa jina na “Vita vya 
Ziwa Nyasa” tarehe 26 Desemba 2012 siku ya Boxing Day jijini Arusha.
 Ulikuwa
 ni mpambano wa mwaka ambao bondia Francis Cheka nusura aupoteze katika 
raundi ya pili wakati konde zito la kushoto la kapteni Usu kutoka katika
 jeshi la jamhuri ya watu wa Malawi, Chiotcha lilipompeleka chini na 
kuinuka kwa msaaada wa kamba za ulingo.
 Konde
 hilo zito lilifungua mpasuko mkubwa katika paji la Cheka na hivyo 
kuleta wasiwasi kwa mashabiki zaidi ya elfu 10 waliofurika katika uwanja
 wa Sheikh Amri Abed kumshughudia Cheka akipambana kiume kwelikweli.
 Raundi
 ya kwanza mpaka ya nne Chiotcha alikuwa anamiliki mpambano huo na 
makonde mazito ya mkono wake wa kushoto kwani anatumia staili ya South 
Paw inayomlazimu kutanguliza mbele mguu wa kulia.
 Ni
 katika raundi ya sita ambako Cheka aliweza kubadilisha mwelekeo wa 
mpambano kwa kuanza kumwadhibu Chiotcha na makonde mazito ya 
kombinasheni yaliyomfanya Mmalawi huyo kumkumbatia bila mafanikio 
Mtanzania huyo asiyepigika.
 Cheka
 aliwanyanyua mashabiki waliojaa uwanjani wakiongozwa na Mstahiki Meya 
wa jiji la Arusha, Mh. Gaudence Lyimo alipompiga bila huruma Chiotcha na
 kumlazimu refarii wa kimataifa wa mpambano huo Nemes Kavishe wa 
Tanzania kumwonya kutomshika Cheka kama vile anapigana mieleka.,
 Juhudi
 za Chiotcha kujisalimisha kwa kumkumbatia Cheka hazikuzaa matunda kwani
 aliendelea kupewa mkong’oto na mwana huyo wa Kitanzania aliyejizolea 
sifa kemkem kwa kuwapiga wapinzani wake.
 Mashabiki
 wengi walinyanyuka katika viti vyao katika raundi ya 12 ya lala salama 
wakati Cheka alipodhihirisha kweli ni bondia asiyepigika kwa kumpiga 
makonde mazito kichwani Chiotcha na kumfanya apepesuke kila mara. 
 Katika
 mchezo huo ulioandaliwa na kampuni ya Green Hills (T) Investment ya 
jijini Dar-Es-Salaam inayomilikiwa na bingwa wa zamani wa taifa Andrew 
George, mabondia wa mapambano ya utanguliizi walikuwa wa ngumi za ridhaa
 kutoka katika jiji la Arusha.
 Mpambano
 huo ulisimamiwa na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi 
na Mashariki ya Kati, Mtanzania Onesmo Ngowi akisaidiwa na Kamishna wa 
TPBC kutoka Jiji la Arusha bw. Roman Chuwa. 
 Refarii
 alikuwa Nemes Kavishe kutoka Tanzania wakati majaji walikuwa: Daudi 
Chikwanje kutoka Malawi, Boniface Wambura kutoka Tanzania na Galous 
Ligongo kutoka Tanzania.

No comments:
Post a Comment