BAADHI askari wa kike wa Jeshi 
la Polisi nchini (WP), wameulalamikia uongozi wa jeshi hilo 
kutowapandisha  vyeo kwa muda mrefu tofauti na wenzao wa kiume ambao 
wamekuwa wakipandishwa mara kwa mara. 
Hatua hiyo imekuja baada ya 
askari hao kukutana mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam  katika kikao
 cha siri chenye lengo la kutafuta suruhisho la tatizo hilo.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake
 jijini Dar es Salaam jana, mmoja wa askari hao, kwa sharti la kutotajwa
 jina, alisema suala la kutopandishwa vyeo limekuwepo kwa muda mrefu 
bila hatua zozote kuchukuliwa na uongozi wa jeshi hilo.
Alisema anastaajabishwa na 
utaratibu uliopo kwa sababu, licha ya kupewa mafunzo pamoja, bado 
wanagandamizwa pindi wanaporudi kwenye vituo vya kazi, ambapo askari wa 
kiume kupewa upendeleo wakupandishwa cheo haraka.
“Tunashangaa utaratibu huu 
utaisha lini, kwani sheria za jeshi letu zinasema kuwa askari yoyote wa 
kike au wa kiume anapaswa kupandishwa cheo baada ya muda mchache wa 
kumaliza mafunzo” alisema askari huyo.
Askari  huyo aliongeza kuwa 
endapo ikitokea askari wakike kupandishwa cheo kwa muda sitahiki, eidha 
ni kwa kujuana, ukabila na mkubwa fulani au kutoka kijiji kimoja.
Pamoja na hayo, aliivitaja 
baadhi ya vyeo ambavyo wamekuwa wakivilalamikia kutopewa  ni kama 
Msaaidizi wa polisi, Msaidizi wa Inspekta wa polisi, Inspekta wa Polisi,
 na vingine ambavyo wamekuwa wakitaka kupandishwa.
Kwa mujibu wa askari huyo, vyeo 
ambavyo vimekuwa vikitolewa kwa askari hao ni usajenti  na koplo ambavyo
 hukaa navyo hadi kustaafu kazi au kufariki.
Alipoulizwa  Mrakibu Msaidizi wa
 Polisi (ASP), Advera Senso, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Jeshi hilo, 
kuhusu nadai hayo, alisema mfumo wa upandishwaji vyeo katika jeshi hilo,
 ni wakawaida ambapo kigezo kuu ni sifa.
“Hakuna askari 
wakike wala wakiume bali wote ni askari na wako sawa kigezo kikubwa 
kinachoangaliwa katika upandishwaji vyeo hivyo ni sifa”alisema Senso 
Alisema mfumo wa jeshi hilo, 
unawachukulia kuwa askari wote kuwa wako sawa, pale inapotokea askari 
wakiwemo wanawake kama waana sifa zinazostahili kupandishwa cheo 
inafanyika hivyo na si vinginevyo.

No comments:
Post a Comment