TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, February 6, 2015

CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA KAMPASI YA MBEYA CHAJIVUNIA MAFANIKIO, CHA ONGEZA IDADI YA KUDAHILI WANAFUNZI.

Mkuu wa Chuo cha CBE Kampasi ya Mbeya,Dionise Lwanga, akiwa ofisini kwake akiongea na Mwandishi wa Mbeya yetu blog
UONGOZI wa Chuo cha Elimu ya Biashara(CBE) Kampasi ya Mbeya umewashukuru wananchi kwa kuendelea kuwaunga mkono na kuwapa mafanikio makubwa katika kipindi ambacho wanasherehekea miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.

Vijana wa kata ya vingunguti Isyesye jijini Mbeya wajitolea kukarabati barabara

Vijana ambao wametoa muda wao kuhakikisha wanarejesha mawasiliano ya miundo mbinu kati ya vingunguti na gombe kaskazini.

KAMPUNI YA SIMU YA TTCL YAZINDUA MNARA WA MAWASILIANO, WAISHIO VIJIJINI KUNUFAIKA ZAIDI

Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Chunya ambaye pia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Chunya, Sosthenes Mayoka akikata utepe kuashiria ufunguzi wa sherehe za kuzindua mnara wa simu ya kampauni ya TTCL katika kijiji cha Shoga wilayani Chunya.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Chunya ambaye pia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Chunya(DAS), Sosthenes Mayoka akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mnara wa mawasiliano ya simu ya kampuni ya TTCL.

KUHUSU MUINGILIANO WA MASAFA YA EATV NA ITV KUPITIA KING’AMUZI CHA KAMPUNI YA STAR MEDIA KATIKA KITUO CHA KUSAMBAZA MATANGAZO MAKONGO JUU

TCRA logo

1. Masafa ni rasilimali muhimu katika shughuli za Mawasiliano (simu, wavuti, redio, na utangazaji). Masafa ya Mawasiliano (Spectrum) hugawanywa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) (ikitambuliwa hapa kama Mamlaka) kwa kutoa leseni kwa watoa huduma za mawasiliano nchini kwa mujibu wa sheria na masharti ya leseni. Moja ya kazi za Mamlaka ni pamoja na kupokea na kusuluhisha matatizo ya muingiliano wa masafa kati ya watoa huduma mbalimbali wa mawasiliano kwa kutumia ujuzi na wataalamu na teknolojia ya mitambo maalumu na mahususi ya kisayansi kufanya kazi hiyo. Kazi hizi zimeainishwa katika Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano ya 2003 (TCRA Act of 2003) na Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Electronic and Postal Communications Act (EPOCA) ya mwaka 2010. 2. Mnamo tarehe 29 Januari 2015, Mamlaka ilipokea malalamiko kuhusu ubora wa matangazo ya vituo vya ITV na EATV yanayorushwa na Kampuni ya Star Media (T) Limited ambaye ni msambaza matangazo ya dijitali. ITV na EATV wana leseni ya Maudhui (Content Service Lisence) na Star Media wana leseni ya Miundombinu ya Utangazaji (Network Facility License as a signal distributor) kutoka TCRA. Leseni zote za Mamlaka zina masharti ya kuzingatia. 3. Huduma za Mawasiliano hutumia bendi ya masafa tofauti (Spectrum bands). Huduma za mawasiliano ya setilaiti (satellite) hutumia bendi 3.4 mpaka 4.2 GHz, inayofahamika kama C-Band. Ifahamike kuwa masafa ya setilaiti ya kupokea matangazo (satellite downlink frequency) ya 3.644 GHz yanatumika kupokea matangazo kutoka satelaiti ya Intelsat 906 (TP 10) kwa matangazo ya vituo vya utangazaji nchini kupitia mfumo wa dijitali ambao mitambo yake iko katika kilima cha Makongo Juu area. Hata hivyo, sehemu nyingi duniani, ikiwemo Tanzania, hutumia teknolojia ya WiMAX katika bendi 3.5 GHz. Masafa haya yanafahamika duniani kote kwa uwezo wake wa kutumika kiteknolojia kati ya mfumo wa “Fixed Satellite Services (FSS)” na IMT kama vile mwendo kazi wa intaneti bila waya (Broadband Wireless Access (BWA) transmission) ikiwemopia teknolojia ya WiMAX. 4. Kufuatia malalamiko yaliyopokelewa na Mamlaka, TCRA iliteua timu ya wataalamu Wahandisi wa Masafa kufanya uchunguzi ili kubaini tatizo la muingiliano wa masafa yaliyosababisha ITV na EATV kutokuonekana vizuri katika king’amuzi cha Star Media, kwa kutumia utaratibu na jinsi sheria zinavyoelekeza. Timu hiyo ya wataalamu wa masafa iliwasiliana na Star Media na kutembelea eneo la Makongo Juu kwenye mitambo yao ili kubaini aina ya muingiliano, muda wa muingiliano na maeneo husika. Timu hiyo ilifanya uchunguzi kwa kutumia vifaa maalumu kwenye eneo lenye mitambo ya kurusha matangazo ili kubaini muingiliano wa masafa kupitia watoa huduma wa intarneti za mwendo kasi kupitia teknolojia ya WiMAX katika bendi 3.4 – 3.6 GHz. Aidha timu ilifanya tathmini ya vipimo vya matumizi ya masafa na watoa huduma katika bendi nzima ya C- ya kupokelea matangazo (downlink frequency) kutoka 3.4 GHz hadi 4.2 GHz.
8. Kutokana na vielelezo vya matokeo ya uchunguzi uliofanywa na wataalamu wa masafa kwa kutumia vifaa maalumu, Mamlaka ilitoa maelekezo kwa Star Media ili kutatua tatizo la muingiliano uliokuwepo katika mtambo wake wa urushaji matangazo Makongo Juu. Kwanza, kutumia kifaa kiitwacho IF attenuator/filter katika mitambo yake ya kupokelea mawasiliano ya matangazo ya setilaiti (FSS receiving station); Kutumia LNB converter katika bendi ya masafa 3.7 – 4.2 GHz badala ya kutumia masafa ya (C-band) yote (3.4 – 4.2 GHz); hata hivyo, masafa 3.664 GHz yamehifadhiwa kama wigo unaozuia matumizi kati ya watumiaji wa matangazo ya mitambo iliyosimikwa juu ya ardhi (Terrestrial) – (3.4-3.6 GHz) na yale ya wanaotumia Satelaiti ya kupokelea matangazo (3.7-4.2 GHz). Pili, Mamlaka ingeagiza watoaji wa inteneti ya mwendo kasi katika mitambo yao (BWA) kuwa na nafasi ya kutosha kati ya mitambo ya “FSS” na kufuata utaratibu uliowekwa kulingana na matumizi ya masafa, ikizingatiwa kwamba mawimbi yaliyo mengi katika eneo la Makongo Juu hupokelewa kutoka sehemu mbalimbali kutoka Jiji la Dar es salaam. Tatu, njia mbadala zitumike katika kupokea matangazo ya utangazaji katika kilima cha Makongo Juu kama vile teknolojia ya Mkongo wa Mawasiliano (fiber optic) satelaiti kutumia mfumo wa bendi ya Ku-Satellite band, au “microwave links”.

JESHI LA POLISI NCHINI LASHIRIKI KUZINDUA MAGARI MAPYA YA KAMPUNI YA ULINZI YA SECURITY GROUP AFRIKA JIJINI DAR LEO

 Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la polisi nchini Inspekta wa Polisi Mussa Mussa akiwa na mkuu wa jeshi la polisi mstaafu Philimon Mgaya akikata utepe wa kuashiria kuzindua magari mapya Zaidi ya ishirini ya kampuni ya ulinzi ya Security Group Africa ambayo yataanza kutumika katika kazi mbalimbali za kampuni hiyo hivi  karibuni.Katikati yao ni mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Eric Sambu.
 Mwakilishi wa Mkuu wa jeshi la polisi nchini Inspekta wa Polisi Mussa Mussa akipokea msaada wa pikipiki mbili aina ya Boxer toka kwa mwenyekiti wa bodi wa kampuni ya Security Group Africa ambae pia
ni mkuu wa  jeshi la polisi mstaafu Philimon Mgaya kwa ajili ya kusaidia jeshi hilo katika oparasheni mbalimbali za kupambana na uhalifu,Katikati yao ni mkurugenzi mkuu wa kampuni ya SGA nchini  Eric Sambu.
 Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya SGA nchini  Eric Sambu akizungumza kwenye hafla ya kuzindua magari mapya Zaidi ya ishirini ya kampuni ya ulinzi ya Security Group Africa ambayo yataanza kutumika katika kazi mbalimbali za kampuni hiyo hivi karibuni.Hafla hiyo imefanyika katika ofisi za kampuni hiyo Mbezi Beach jijini Dar Es Salaam.
 Mwakilishi wa Mkuu wa jeshi la polisi nchini Inspekta wa Polisi Mussa Mussa akikagua gwaride maalum la kuashiria kuanza kwa shuguli ya kuzindua magari mapya Zaidi ya ishirini ya kampuni ya ulinzi ya Security Group Africa ambayo yataanza kutumika katika kazi mbalimbali za kampuni hiyo hivi karibuni.Kulia kwake ni mkuu wa kitengo cha mafunzo cha SGA bwana Rogers Lumwaji.
 Mwakilishi wa Mkuu wa jeshi la polisi nchini Inspekta wa Polisi Mussa Mussa akipeperusha bendera kuashiria kuanza kutumika kwa magari magari mapya Zaidi ya ishirini ya kampuni ya ulinzi ya
Security Group Africa ambayo yataanza kutumika katika kazi mbalimbali za kampuni hiyo hivi karibuni.Katikati yao ni mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Eric Sambu.

BALOZI WA RWANDA AONANA NA DR.K SHEIN ZANZIBAR

MATUKIO YA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO

mre2Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wabunge kwenye jengo la utawala la  Bunge mjini Dodoma Februari 6, 2015. Kutoka kushoto ni Yahya Kassim Issa wa  Chwaka, Jerome Damas Bwanausi wa Lulindi  na  Muhammad Amour Chombo wa Magomeni . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)(Picha na  Ofsi ya Waziri Mkuu) 

KAMATI YA NIDHAMU YAWAADHIBU NYOSO, MORRIS

nyoso
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewafungia kati ya mechi tatu na nane wachezaji Juma Nyoso wa Mbeya City na Aggrey Morris wa Azam kutokana na makosa ya kinidhamu waliyoyafanya wakiwa uwanjani.
Nyoso ambaye alilalamikiwa na TFF kwa kumfanyia vitendo vya udhalilishaji mshambuliaji Elias Maguri wa Simba amefungiwa mechi nane za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL). Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Ibara ya 57 na Ibara ya 11 (f) ya Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012.
Akiwa mbele ya Kamati hiyo jana (Februari 5 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Nyoso alikiri kufanya na kujutia kosa hilo, pia amemuomba radhi mchezaji Maguri kwa kitendo hicho.
Akisoma uamuzi huo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wakili Jerome Msemwa alisema kitendo kilichofanywa na Nyoso ni kosa kubwa, kudhalilisha utu wa mtu, na ni mfano mbaya kwa watoto na jamii nzima ya mpira wa miguu.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AMFARIJI JAJI MSTAAFU AGOSTINO RAMADHANI KWA KUFIWA NA MAMA YAKE MSAZI

Benki ya Exim yaadhimisha Siku ya Saratani Duniani na Watoto wenye Saratani Hospitali ya Taifa Muhimbili

exim1Mkuu wa matawi wa Benki ya Exim, Bi. Elizabeth Mayengoh, akikabidhi vitabu kwa mmoja wa watoto waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwenye wodi maalum ya watoto wanaougua ugonjwa wa saratani katika kuadhimisha siku ya saratani duniani. Wanaoshudia ni baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim na wazazi wa watoto hao. Benki hiyo ilikabidhi vifaa mbalimbali vikiwemo vyakula, vifaa vya kuchezea, sabuni, vifaa vya shule nk, lengo likiwa ni kujenga uelewa kuhusiana na ugonjwa wa saratani mpango unaoendana na kauli mbiu ya mwaka huu ya Siku ya Saratani Duniani inayosema kuwa tatizo la saratani “lipo ndani ya uwezo wetu”.
exim2Meneja masoko msaidizi wa Benki ya Exim, Bi. Anita Goshashy akishikana mikono na Dr. Livin Mumbari  Daktari wa watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, muda mfupi baada ya benki hiyo kukabidhi vifaa mbalimbali kwa watoto waliolazwa hospitalini hapo kwenye wodi maalum ya watoto wanaougua ugonjwa wa saratani katika kuadhimisha siku ya saratani duniani. Wanaoshudia ni baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim na wazazi wa watoto hao. Benki hiyo ilikabidhi vifaa mbalimbali vikiwemo vyakula, vifaa vya kuchezea, sabuni, vifaa vya shule nk, lengo likiwa ni kujenga uelewa kuhusiana na ugonjwa wa saratani mpango unaoendana na kauli mbiu ya mwaka huu ya Siku ya Saratani Duniani inayosema kuwa tatizo la saratani “lipo ndani ya uwezo wetu”.

Sitta awapa 5 Tamasha la Pasaka

indexNa Mwandishi Wetu 
 
WAZIRI wa Uchukuzi, Samuel Sitta ameelezea kufurahishwa na waandaaji wa Tamasha la Pasaka na kusema kuwa katika miaka 15 ya tamasha hilo wana mengi ya kujivunia.
 
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam jana na kusainiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa kamati yake imepokea salamu kutoka kwa Waziri Sitta akizungumzia maandalizi ya miaka 15 ya tamasha hilo.
 
“Ni tamasha lenye tija kwa Watanzania, mimi mwenyewe nimekuwa shahidi wa namna mnavyosaidia yatima, wajane na makundi mbalimbali ya kijamii.
 
“Nimesikia mwaka huu mna tamasha kubwa la miaka 15 tangu muanze kufanya Tamasha la Pasaka, niwatakie kila la heri katika maandalizi na naamini litakuwa tamasha la aina yake,” alisema Msama katika taarifa yake akimnukuu Sitta.
 
Alisema wamekuwa wakipokea salamu kutoka kwa wadau mbalimbali wakizungumzia kuhusiana na maandalizi ya Miaka 15 ya Tamasha la Pasaka na wakielezea pia mafanikio mbalimbali yaliyopatikana kwa kipindi hicho.
 
Baadhi ya walioguswa na maandalizi ya tamasha hilo ni waimbaji mahiri wa muziki wa Injili kutoka Afrika Kusini Solly Mahlangu ‘Obrigado’ na Rebecca Malope.
 
 Wasanii hao wamewahi kwa nyakati tofauti kuja nchini katika Tamasha la Pasaka, ambapo mwaka huu waandaji wamepanga kufanya sherehe ya Miaka 15 ya Tamasha la Pasaka.

NFT CONSULT WAPANIA KULETA MABADILIKO TANZANIA

DSC_0252
Baadhi ya washiriki wa warsha ya siku moja iliyoendeshwa na kampuni ya NFT Consult kwa maofisa rasilimali watu na watoa mafunzo kutoka makampuni mbalimbali nchini wakifanya usajili kabla ya kuanza kwa warsha hiyo.

Na Mwandishi wetu
MOJA ya makampuni makubwa yanayoshughulika na ushauri wa jinsi ya kuongeza ufanisi katika maeneo ya kazi, NFT Consult wameendesha kongamano kubwa la kutambua haja ya mahitaji ya wadau mbalimbali wa maendeleo hapa nchini.
Kampuni hiyo ya kimataifa ambayo imeingia nchini mwaka 2010 ikiwa na matawi Uganda, Kenya, Tanzania, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini imesema kongamano hilo limelenga kuonesha uwezo wao katika kubadili mifumo ya utendaji kazi.
Ofisa Mtendaji wa kampuni hiyo, Badru Ntege amesema kwamba wamekuwa wakiendesha mafunzo mbalimbali yenye kueleza thamani ya mfanyakazi na mdau wowote ambapo uthamini wa wadau ndio unaotoa mwanya wa mabadiliko chanya yanayotakiwa
“Mafanikio ya eneo lolote lile linatokana na wadau kusikiliza wenzao na kisha kufanyia kazi kauli za upande wa pili.” Alisema Ntege.
DSC_0361
Timu ya NFT Consult ikijitambulisha kwa washiriki kabla ya kuanza warsha hiyo. Kutoka kushoto ni Inside Business Partner wa NFT Consult, Aisu Mori, Client Partner wa NFT Consult, Immaculate Mwaluko, Ofisa Mtendaji mkuu wa kampuni ya NFT Consult, Badru Ntege, Meneja biashara mkazi wa NFT Consult/Franklin Covey Tanzania, Joan Ajilong na Client Partner wa NFT Consult, Sophia Shuma.
Alisema katika mafunzo ya kuthamini ,kanuni kubwa inayotumika ni kujipanga katika nafasi husika na kutumia changamoto kama fursa za kubadili mazingira ya kazi na kazi yenyewe ili kupata matokeo yanayotakiwa.

SKYLIGHT BAND WAENDELEA KUTOA BURUDANI YA NGUVU JIJI DAR, NI IJUMAA HII TENA

Binti mwenye sauti ya kumtoa Nyoka pangoni, Ashura Kitenge akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) ndani ya kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar es Salaam Ijumaa iliyopita huku akipewa sapoti na Meneja wa Skylight Band, Aneth Kushaba AK47 pamoja na Kisura mwingine wa Skylight Band anayefamika kwa jina la Baby.
Tukutane baadae tupunguze stress za wiki nzima kwa burudani iliyoenda shule na sehemu ya watu wastaarabu kama kawaida na mtonyo wetu ule ule getini.
Msanii wa Skylight Band Joniko akiendelea kutoa burudani huku vijana wa Skylight Band wakitimua vumbi jukwaani wakiongozwa na Sony Masamba ndani ya kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar

Ujerumani iko tayari kushirikiana na mahakama ya Afrika

index
Immaculate Makilika –MAELEZO ARUSHA
Rais wa  Shirikisho la  Ujerumani amesema Serikali yake iko tayari kushirikiana na Mahakama ya Afrika katika utendaji kazi wake ili kusaidia  kutoa huduma iliyokusudiwa kwa walengwa.
 
Rais huyo ameyasema hayo leo alipotembelea Mahakama ya  Afrika iliyopo  mjini Arusha, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku sita nchini na kusema kuwa angependa kuona utawala wa  sheria ambao unaozingatia demokrasia  unafuatwa na kuheshimiwa.
 Aidha, Rais Ghauck ameipongeza mahakama hiyo kwa weledi wake na hatua nzuri waliyofikia huku akitolea mfano kesi iliyosikilizwa mwaka 2014 huko Adis Ababa, Sudan.
‘Tunaunga mkono maendeleo pia  tungependa kuendelea kushirikiana nanyi, msisite kutuomba msaada  alisema Rais Gauck’.
 
Naye kwa upande wake Jaji Mkuu wa Mahakama ya Afrika Augustino Ramadhani  alisema Serikali ya Ujerumani imekua na ushirikaiano mzuri na Mahakama hiyo kwani ilisaidia pia katika ujenzi wake.
 
Hata hivyo jaji Ramadhani amesema wamemuomba Rais wa Ujerumani asaidie kujenga mahakama ya Afrika ya Mashariki, ombi ambalo Rais huyo amesema atalishughulikia kushirikiana na  viongozi aliongozana nao.
 
Aidha, Jaji Ramadhani amesema kuwa uwepo wa Mahakama hii Afrika ni jambo la kujivunia  kwani itaweza kusaidia matatizo ya waafrika wote kutoka sehemu  mbalimbali.

BARABARA YA MBWENI – MALINDI YAPATA UFADHILI

 Mbunge wa Bunge kla Afrika Mashariki ambaye pia ni mkazi wa Mbweni, Shy Rose Bhanji akiwa na Mwenyuekiti wa Serikali ya Mtaa Mbweni-Malindi, jijini Dar es Salaam, Bariki wakisimamia ukarabati wa barabara yao leo.
 Mbunge wa Bunge kla Afrika Mashariki ambaye pia ni mkazi wa Mbweni, Shy Rose Bhanji akielekeza jambo kwa mkandarasi.
Barabara ya Mbweni-Malindi inavyonekana baada ya kuanza kufanyiwa ukarabati.

CCM YABOMOA JENGO LA TANU JIJINI DAR ES SALAAM

Wananchi wakiangalia jengo la ofisi ndogo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) la Lumumba, ambapo kilizaliwa chama cha Tanu lililobomolewa kupisha ujenzi wa jengo jipya la chama hicho Dar es Salaam jana
…………………………………………………………………………
Dotto Mwaibale
 
JENGO la ofisi ndogo la Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mtaa wa Lumumba Dar es Salaam ambako ndiko kilizaliwa Chama cha Tanu limebomolewa ili kupisha ujenzi wa jengo jipya la chama hicho.
 
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye alisema jengo hilo limebomolewa kwa ajili ya matengenezo ya kawaida.

NAPE AANZA ZIARA KWENYE VYOMBO VYA HABARI

  Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali,  Bwana Gabriel Lyimo Nderumaki ( wa pili kutoka kushoto) akielezea masuala mbali mbali yanayohusu tasinia ya habari wakati wa mkutano na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye uliofanyika kwenye ofisi za Kampuni ya Magazeti ya Serikali,Tazara jijini Dar es Salaam.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza wakati wa kikao chake na Viongozi na waandishi wa Magazeti ya Serikali alipowatebelea leo ikiwa sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari.

Thursday, February 5, 2015

NI IVORY COAST VS GHANA FAINALI YA AFCON 2015


Ghana imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Mataifa Afrika AFCON 2015 baada ya kuwachapa wenyeji Equatorial Guinea mabao 3-0 katika mchezo wa Nusu Fainali uliomalizika kwa aina yake usiku wa jana.
Magoli ya Ghana yalifungwa na Jordan Ayew dakika ya 42, Wakaso Mubarak dakika ya 45 na Andrew Ayew dakika ya 75.

Kwa matokeo hayo sasa Ghana itakutana na Ivory Coast katika mchezo wa Fainali utakaopigwa siku ya Jumapili Februari 7, 2015.
Ivory Coast walifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuwatoa Congo DR kwa mabao 3-1 juzi.

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAMHURI YA KIISLAMU YA IRAN.

she`1Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya  Kiislamu ya Iran Mohammed Javad  Zarif alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na ujumbe aliofuatana nao,[Picha na Ikulu.]
shei2Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)  akizungumza na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya  Kiislamu ya Iran Mohammed Javad  Zarif (wa pili kulia) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na ujumbe aliofuatana nao,[Picha na Ikulu.]

NAPE AANZA ZIARA KWENYE VYOMBO VYA HABARI

  Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali,  Bwana Gabriel Lyimo Nderumaki ( wa pili kutoka kushoto) akielezea masuala mbali mbali yanayohusu tasinia ya habari wakati wa mkutano na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye uliofanyika kwenye ofisi za Kampuni ya Magazeti ya Serikali,Tazara jijini Dar es Salaam.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza wakati wa kikao chake na Viongozi na waandishi wa Magazeti ya Serikali alipowatebelea leo ikiwa sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari.

Kuingia kwa sekta ya afya katika BRN kunaleta matumaini mapya

 kip1
Mtendaji Mkuu wa PDB Bw. Omari Issa akielezeaumuhimu wa sekta ya Afya kuingia BRN kuungana na sekta nyingine zilizotangulia zinazoendelea kuzaa matunda
kip2
Dr Linda Ezekiel ambae ni Mkurugenzi wa sekta za jamii (Afya, Elimu na Maji) PDB akiwasilisha mada kuhusu malengo ya kipaumbele sekta ya afya kwa miaka

SERIKALI KUDHIBITI UJANGILI WA BIASHARA HARAMU MAZAO YA MALIASILI

mgi
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mahmoud Mgimwa akijibu swali bungeni.
……………………………………………………………………………………
Na Lorietha Laurence-Maelezo,Dodoma SERIKALI imejidhatiti katika kudhibiti ujangili na biashara haramu ya mazao ya maliasili kwa kuridhia na kutekeleza mikataba minne ya kudhibiti ujangali wa tembo na unaovuka mipaka na kulinda mapori ya akiba.

Serikali yatenga kiasi cha shilingi bilioni 3 kukuza ajira

anne
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Anne Kilango Malecela
…………………………………………………………………………………..
Na Lorietha Laurence-Maelezo ,Dodoma
SERIKALI kupitia Wizara ya kazi na Ajira imetenga kiasi cha shilingi bilioni 3 kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015 kwa ajili ya kutekeleza mpango wa kukuza ajira kwa vijana.
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Anne Kilango Malecela, akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Susan Lyimo kuhusu mkakati wa serikali kuwakopesha vifaa wahitimu wa mafunzo ya Veta ili kujiajiri.

Serikali kuwasilisha Muswada wa Sheria ya Habari bunge la Aprili

MTA
Hussein Makame-MAELEZO,Dodoma
SERIKALI inatarajia kuwasilisha Muswada wa Sheria ya Habari katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la mwezi April mwaka huu ili kujadiliwa na kupitishwa kuwa Sheria kamili.

KIKAO CHA KWANZA CHA BODI YA MRADI WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI GEREZA KIGONGONI – BAGAMOYO KATI YA SHIRIKA LA MAGEREZA NA KAMPUNI YA TARBIM CHAFANYIKA LEO MJINI BAGAMOYO

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI DODOMA LEO

Kamati ya utalii ya wilaya ya wete yaagizwa kuzungumza na wananchi wa kisiwa cha Fundo

cuf 

Waziri wa Habari , Utalii , Utamaduni na Michezo  Said Ali Mbarouk ameiagiza kamati ya utalii ya wilaya ya wete kurejea katika mazungumzo na wananchi wa Kisiwa cha Fundo na kuwaelimisha faida na umuhimu wa Sekta ya Utalii katika kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla .
Amesema kuwa bado wananchi wa Kisiwa hicho wanahitaji elimu zaidi na kuongeza kwamba kamati ya utalii ya Wilaya ndiyo yenye dhamana ya kuhakikisha kwamba wakaazi wa Kisiwa hicho wanatambua faida ya Sekta hiyo .
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na wajumbe wa kamati ya Utalii ya Wilaya hiyo pamoja na Viongozi wa kutoka Taasisi zinazohusika na masuala ya Uwekezaji ikiwemo ZIPA , Kamisheni ya Utalii na  Idara ya ardhi  na kuwataka kuongeza uhamasishaji wa wawekezaji kuwekeza ili kuitangaza wilaya hiyo kupitia sekta ya utalii .

wakulima 7 wakabidhiwa matrekta leo

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akikabidhi
funguo za trekta kwa Mwalimu wa Shule ya msingi Kwadelo Bw. Hamza Haji,matrekta saba yalikabidhiwa leo kwa wakulima chini ya usimamizi wa Diwani wa Kwadelo Alhaji Omari Kariati.(Picha na Adam Mzee)
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akikabidhi funguo za trekta kwa Dk. Edmund Mndolwa ambaye ni Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa ikiwa sehemu ya matrekta saba yaliotolewa na Alhaji Omari Kariati Diwani wa Kwadelo.