TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, February 1, 2015

SIKU YA SHERIA NCHINI ILIVYOSHIRIKISHA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA NHIF

1
Emmanuel Sarakyika wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya akimpima shinikizo la damu mmoja wa watumishi wa Mahakama alipotembelea  kupata huduma hiyo katika banda la NHIF kwenye maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Dar es salaam ambapo Rais Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini zitakazo fabika februari 04 2015 katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Saalam.
2
Afisa Masoko na Elimu kwa Umma wa NHIF Bi Hawa Duguza akimpima urefu Bw. Ben Kigongola wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu katika banda la NHIF kwenye maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Dar es salaam.

3
Afisa Matekelezo wa NHIF, Bi. Shazy Amasha akimsikiliza kwa makini mmoja wa wageni kutoka kundi maalumu aliyetembelea banda la NHIF katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Dar es salaam.
4
Afisa Uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bi. Tamasha Magongo akitoa maelezo ya jinsi ya kujiunga na Mfuko kwa wageni waliotembelea banda la NHIF katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Dar es salaam.
5
Afisa Masoko na Elimu kwa Umma wa NHIF Bi. Catherine Kameka akimsikiliza kwa makini mmoja wa wageni waliotembelea banda la NHIF ili kufahamu huduma zitolewazo na Mfuko huo katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment