TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, February 3, 2015

Msanii wa Muziki Juma Nature, Aomba Msaada Wa Kuwanusuru Wasanii

Nyota na msanii mkongwe wa muziki wa bongo flava nchini Tanzania, Juma Nature amesema kuwa wasanii wakongwe wa muziki huo watapotea kabisa katika ramani ya muziki kama wadau wa muziki pamoja na vyombo vya habari havitawapa nafasi ya kutosha kama wanavyopewa wasanii wengine wa sasa.
Nature amesema kuwa zamani kipindi yeye yupo Bongo Records wasanii wote walikuwa kitu kimoja na kazi zao walikuwa wanafanya kwa kushirikiana na kwa umoja kitu ambacho kilifanya wote kuwa na mafanikio sawa kwani hata maonesho yao walikuwa wanagawana fedha sawa kitu kisichowezekana kwa sasa.
Nature amesema kuwa kwa sasa wasanii kama yeye watapotea kutokana na wadau wa muziki kuwatumia wasanii wachache katika shughuri zao za kila siku huku akitolea mfano jinsi Diamond anavyopewa kipaumbele katika maonesho na kazi nyingine huku wasanii wazuri kama Rich Mavoko na Ali Kiba wakisahaulika kitu kinachosababisha kuwa na matabaka kwani wanaopewa nafasi ndio wanaofanikiwa.
Katika hatua nyingine Juma Nature amewaasa wadau wa muziki kutowasahau wakongwe wa muziki nchini kwani wao ndio walioufikisha muziki huu hapa ulipofika.

No comments:

Post a Comment