TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, February 5, 2015

Kamati ya utalii ya wilaya ya wete yaagizwa kuzungumza na wananchi wa kisiwa cha Fundo

cuf 

Waziri wa Habari , Utalii , Utamaduni na Michezo  Said Ali Mbarouk ameiagiza kamati ya utalii ya wilaya ya wete kurejea katika mazungumzo na wananchi wa Kisiwa cha Fundo na kuwaelimisha faida na umuhimu wa Sekta ya Utalii katika kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla .
Amesema kuwa bado wananchi wa Kisiwa hicho wanahitaji elimu zaidi na kuongeza kwamba kamati ya utalii ya Wilaya ndiyo yenye dhamana ya kuhakikisha kwamba wakaazi wa Kisiwa hicho wanatambua faida ya Sekta hiyo .
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na wajumbe wa kamati ya Utalii ya Wilaya hiyo pamoja na Viongozi wa kutoka Taasisi zinazohusika na masuala ya Uwekezaji ikiwemo ZIPA , Kamisheni ya Utalii na  Idara ya ardhi  na kuwataka kuongeza uhamasishaji wa wawekezaji kuwekeza ili kuitangaza wilaya hiyo kupitia sekta ya utalii .
Amesema kuwa kitendo cha baadhi ya wananchi wa Kisiwa cha Fundo cha kutoshirikiana na mwekezaji kunaweza kuitoa dosari sekta hiyo ambayo imekuwa tegemeo la taifa katika kuimarisha uchumi wake ambapo suluhisho lake ni kamati kuwaelimisha wananchi hao .
“Pamoja na elimu mnayoitoa lakini iko haja kwa kamati  kurejea kwenye meza ya mazungumzo na wakaazi wa kisiwa hicho ili kuwaelimisha umuhimu wa sekta na kuwataka kushirikiana na mwekezaji ambaya ana nia ya kuboresha uchumi wa nchi ” alieleza .
Aidha mesema kuwa  kamati hiyo inajukumu la kuwasikiliza wananchi pamoja na kuchukua changamoto zao na kisha kuzifikisha kwa mwekezaji ili kutafuta ufumbuzi kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla .
Hata hivyo Sheha wa Shehia ya  Fundo Khamis Abeid amesema kuwa mgogoro huo wa wananchi wa Kisiwa hicho pamoja na mwekezaji unachangiwa na wanasiasa ambao wamekuwa wakipita na kuwashawishi wananchi kutokubaliana na mradi huo .
Amesema kuwa iwapo wanasiasa watakuwa tayari kufika katika Kisiwa hicho na kisha kuzungumza na wananchi juu ya mradi huo na umuhimu wake wananchi wako tayari kutoa ushirikiano kwani wanatambua faida za Sekta ya Utalii .
“Mgogoro huu unachangiwa na wanasiasa , kwani wananchi wanasema kuwa Viongozi wao wa Jimbo ndio wanaowaambia kuukataa mradi huu na hapa mimi biko tayari tufuatane nao hadi kwa wananchi wakawaambie  faida ya mradi huu ” alifahamisha .
 Mapema mwenyekiti wa kamati hiyo  Hassan Khatib Hassan amemhakikishia waziri kuwa mradi wa ujenzi wa hoteli katika Kisiwa hicho utatekelezwa vyema kwani kamati inaendelea kutoa elimu kwa wakaazi wa Kisiwa hicho .
Amesema kuwa kamati yake imeshafika katika kisiwa hicho na imewahai kufanya vikao na wananchi wa Kisiwa hicho na katika vikao hivyo mazungumzo yao yameonyesha kukubalika kwa mradi .
Katika Kisiwa cha Fundo jumla ya miradi miwili ya ujenzi wa Hoteli inatarajia kujengwa ambapo mmoja kati ya hiyo ni mradi wa mwekezaji mzalendo .

No comments:

Post a Comment