TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 4, 2015

RAIS JAKAYA KIKWETE AMUANDALIA RAIS WA UJERUMANI DHIFA YA KITAIFA YA CHAKULA CHA USIKU, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete(wa pili kutoka kulia) na mgeni wake Rais wa Shirikisho la Ujerumani, Joachim Gauck (wa tatu kutoka kulia) wakifurahia wakati wa dhifa ya kitaifa ya chakula cha usiku aliyomwandalia  kiongozi  huyo jana usiku, Ikulu jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mke wa Rais wa Tanzania, mama Salma Kikwete na Mke wa Rais wa Ujerumani Bi. Daniella Schadt.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete(wa pili kutoka kulia) akiwa na mgeni wake Rais wa Shirikisho la Ujerumani, Joachim Gauck (wa tatu kutoka kulia) wakiwa wamesimama wakati wimbo taifa wa Tanzania na ujerumani ulipopigwa wakati wa dhifa ya kitaifa ya chakula cha usiku aliyomwandalia  kiongozi  huyo jana usiku, Ikulu jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mke wa Rais wa Tanzania, mama Salma Kikwete na Mke wa Rais wa Ujerumani Bi. Daniella Schadt.
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Askofu Gehazi Malasusa (wa pili kutoka kushoto) na viongozi wengine wa Serikali wakiwa kwenye dhifa ya kitaifa ya chakula cha usiku aliyoandaliwa Rais wa Ujerumani Joachim Schadt na Rais Jakaya Kikwete jana usiku jijini Dar es salaam.
Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete na mgeni wake Rais wa Shirikisho la Ujerumani Mh. Joachim Gauck wakielekea sehemu ya nyuma ya ukumbi kutazama Brass bendi ya Jeshi la Polisi iliyokuwa ikitoa burudani wakati wa dhifa ya kitaifa ya chakula cha usiku aliyomuandalia mgeni wake jana usiku Ikulu jijini Dar es salaam.
Mkuu wa wilaya ya Temeke Sophia Mjema (kushoto) akiongea na baadhi ya wageni waalikwa akiwemo Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Diana Melrose (aliyesimama) wakati wa dhifa ya kitaifa ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Rais  Jakaya Kikwete kwa Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck , Ikulu jana usiku.
Rais wa Shirikisho la Ujerumani Mh. Joachim Gauck akitoa ujumbe wake kwa wageni mbalimbali waliohudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Jakaya Kikwete Ikulu.
Rais wa Shirikisho la Ujerumani Mh. Joachim Gauck na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania wakitazama Brass Bendi ya Jeshi la Polisi iliyokuwa ikitumbuiza wakati wa dhifa hiyo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania wakitazama vikundi mbalimbali vya ngoma za asili vilivyokuwa vikitumbuiza wakati wa dhifa ya kitaifa  Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck na mkewe Bi.Daniella Schadt wakati wa dhifa ya kitaifa ya chakula cha usiku aliyowaandalia wageni hao jana Usiku, Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Shirikisho la Ujerumani Mh. Joachim Gauck (wa pili kutoka kulia) akiteta jambo na Rais mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi jana usiku wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam. Kushoto ni mke wa Rais wa Ujerumani Bi. Daniella Schadt na mama Sitti Mwinyi Mwinyi.

No comments:

Post a Comment