TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, February 2, 2015

Bondia wa kulipwa Farncis Cheka atupwa jela miaka mitatu, familia yapanga kukata rufaa

Na Ripota wetu, Morogoro
 
Bondi wa kulipwa nchini, Francis Cheka ambaye maarufu kwa jina la SMG, amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na faini ya Sh milionai moja kwa kosa la kumpiga meneja waje wa baa, Bahati Kibanda.
 
Cheka alitiwa hatiani Julai 2 mwaka jana kwa kumpiga na kumsababishia maumivu makali Kibanda ambaye alikwenda hapo kudai fedha zake katika baa aliyokuwa anaifanyia kazi  ijulikanayo kwa jina la Vijana Social Hall.
 
Hakimu Mwanamizi wa mahakama ya mkoa wa Morogoro Said Msuya alikubaliana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na kuthibitisha shitaka hilo.
 
Hakimu Msuya alisema kuwa adhabu hiyo ni fundisho kwa mshitakiwa na watu wengine wanaotumia vibaya nguvu zao kwa watu wengine na anatakiwa kumlipa mlalamikaji fidia ya Sh milioni moja.
 
Pamoja na Cheka kupewa nafasi ya kujitetea, bondia huyo hakutoa maelezo yoyote na kuiachia mahakama hiyo kutoa adhabu inayostahili kwa bondia huyo aliyejizolea sifa kemkem katika ngumi za kulipwa nchini.
 
Hata hivyo, taarifa zilizotufikia wakati tunakwenda mitamboni, familia ya Cheka inampango wa kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.

No comments:

Post a Comment